Russians Say Soviet Rule Was ‘Closer to People’ Than Current Regime

Russians Say Soviet Rule Was ‘Closer to People’ Than Current Regime

FRANC THE GREAT

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2016
Posts
5,500
Reaction score
8,067
Russians Say Soviet Rule Was ‘Closer to People’ Than Current Regime

1565281445738.png

Andrei Nikerichev / Moskva News Agency

More people in Russia view the late Brezhnev era of the Soviet Union as “close to the people” than they do President Vladimir Putin’s Russia, according to a survey by the independent Levada Center pollster.

Russians have expressed increasingly positive opinions about the Soviet Union over the years, with nostalgia toward the U.S.S.R. and Stalin hitting record highs in recent months. Putin’s popularity has meanwhile been lagging amid widespread poverty and controversial pension reforms.

According to Levada’s results published Monday, 29% of Russian respondents described late 1970s-early 1980s Soviet rule as “close to people” when offered a list of choices.

A quarter of the respondents said Soviet rule was “strong and enduring,” 22% called it “just” and 20% “legitimate.”

When asked to characterize Russia's current leadership, 41% called it “criminal and corrupt” and 31% called it “distant from the people and alien.”

Another 24% called the regime “bureaucratic,” 19% “shortsighted” and 15% “inconsistent.”

The poll’s methodology of giving multiple choices makes it less likely for respondents to provide the answer they think is expected from them, Lev Gudkov, the head of Levada, said in comments to the Vedomosti business daily.

Levada conducted the survey among 1,608 respondents between June 27 and July 4. Levada did not provide a breakdown of those surveyed by age.

Source: The Moscow Times
 
Levada ni foreign agent. Inajulikana hivyo Russia. Mimi siyo Pro Putin lakini Putin anafanya vizuri kama unafuatilia habari za tv kuhusu Russia. Na Putin utawala wake upo wazi na karibu sana na wananchi.

Russia ni Taifa ambalo lilifeli likanyanyuka likafeli likanyanyuka. Miaka ya 90's ya Yeltsin Russia lilifeli Taifa lao. Yeltsin alikuwa ni dhaifu mno na alikuwa ni asiyekuwa na maono, kwa hiyo Taifa la Russia licha ya kufeli ila liliwekwa mfukoni kwa kiasi chake na Marekani(west). Yeltsin ndiye aliyempendekeza Putin awe rais wa Russia.

Kwa vile Yeltsin alikuwa ni softly na asiyekuwa mwenye kuweka mbele maslahi ya Russia na kwa vile ndiye aliyempendekeza Putin kuwa kiongozi wa Russia wamagharibi walidhani Putin naye ni boya kama Yeltsin. Ndiyo maana kipindi kile Putin alikuwa karibu na Amerika ya Bush, kwa sababu walidhani Putin is equal to Yeltsin.

Putin alipoanza kuzungumzia maslahi ya Urusi, wakaona aaaah! Huyu jamaa siyo. Ndipo drama zote juu ya Russia na Putin zikaanza tena. Putin alikabidhiwa Russia ni dhohofulhal ijapokuwa Russia ni Taifa kubwa na kongwe. Ila alipoifikisha hapa Russians wanamkubali na ndiyo maana wanaendelea kumkubali wengi wao kwani mtu huwezi kupendwa na wote. Ni sawa sawa na raia wanaom' criticize Trump au Boris Johnson ndiyo kusema hawakubaliki Marekani au Uk?

Mfano hai ni yale maeneo yaliyokumbwa na mafuriko huko Russia, Putin alikwenda huko kuwajulia hali. Itafute hiyo clip then utajua ukaribu uliyopo baina ya Putin na raia na Serikali yake.
 
When asked to characterize Russia's current leadership, 41% called it “criminal and corrupt”and 31% called it “distant from the people and alien.”

Halafu we bwana mkubwa bhana! Haya matango pori karne hii hayafanyi kazi. Kaangalie walichokifanya kaka zako Us. Wamezuia meli iliyosheheni vyakula ya Venezuela kisa Maduro. Sasa meli inakwenda kwa Maduro au kwa raia?
 
Umetangulia kwa kujihami kuwa wewe si Pro-Putin. Well! Hakuna ulazima wowote wa kusema hivyo na michango na maoni ya pande zote zenye ufahamu juu ya hili hayazuiliwi ndiyo maana nikaileta hii taarifa hapa kama ilivyo na bila kupunguza wala kuweka maneno yangu ili pia tupate kulijadili hili hapa jukwaani.

Umezungumza kuhusu taasisi iliyohusika na utafiti huo ijulikanayo kama Levada Center na ukasema kuwa hiyo taasisi ni foreign agent. Unasema hivyo kwa maana gani na kwa sababu zipi kwamba hiyo taasisi ni foreign agent?

Pia umesema kuwa Putin anafanya vizuri kwa mujibu wa habari za TV. Sikatai kuhusu hilo lakini Je! Tunaweza kupata uthibitisho wa utendaji kazi wa Putin kupitia habari za TV pekee. Na Je! ni taarifa za TV zipi hizo? Na anafanya vizuri kwa muktadha gani?

Umezungumzia utawala wa Boris Yeltsin na ukaulinganisha na wa Vladimir Putin na ukasema kwamba Yeltsin alikuwa 'softly' n.k.
Sasa, hicho ulichokizungumza kinaendana na utafiti uliofanyika hapo?

Huoni kuwa unachokizungumzia hapo ni kitu tofauti kabisa na kile kilichopo mezani? Ahsante!
 
Ndugu, huu ni utafiti na siku zote utafiti kama huu katika maswala hususan ya kisiasa unaweza usimpendeze kila mtu na si kazi ya utafiti kumpendeza kila mtu.

Umewaita US kaka zangu, umezungumzia Venezuela na meli ya vyakula...

Narudi palepale. Je! Hivyo vina uhusiano gani na utafiti unaozungumziwa hapa?
 
Ndugu yangu tafiti nyingi uwa haziendani na ukweli wa mambo kutokana na jinsi ya utafiti ulivyofanywa.Mara nyingi tafiti uwa si za kweli kutokana na ushilikishwaji wa watu wa kila upande.

leo hii ukienda mtwara ukiwauliza kati ya utawala uliyopita na utawala huu uliyopo upi upo karibu na wananchi,watakwambia utawala uliyopita.na ivyo ivyo ukija Dar ukiwauliza napo watakwambia tu utawala uliyopita.

Sasa toka nenda mkoa wa Dodoma,kirimanjaro,morogoro alafu waulize ivyo,watakwambia ni utawala huu.sasa hapo kupata utafiti mzuri ni lazima ujue mkoa una watu wangapi,wangapi wanasema utawala uliyopo na wangapi wanasema utawala uliyopita.hapo unaitaji mabilioni ya dola kufanya utafiti
 
Kwanza kabisa, umesema kuwa tafiti nyingi huwa haziendani na ukweli wa mambo. Mpaka hapo kwa mujibu wa kauli hiyo utakubaliana na mimi kuwa zipo pia tafiti zinazoendana na ukweli wa mambo.

Pia umeeleza sababu ni jinsi utafiti ulivyofanywa na jinsi gani unavyoshirikisha watu. Sawa, lakini sababu kubwa ya utafiti kukosa uhalisia ni kukosekana kwa 'Weledi' ama Skills/Professionalism.

Kwa taasisi imara ambayo inafanya kazi kwa weledi ikizingatia kanuni na misingi ya kiutafiti, haiwezi kushindwa kushughulikia maswala kama hayo ya ushirikishwaji wa watu kuendana na aina ya utafiti wanaoufanya.
 
Watu wa Urusi lazima waione USSR ilikuwa bora kuliko Urusi ya Sasa kwa sababu hiyo Soviet iliipendelea zaidi Urusi kuliko majimbo mengine yaliyokuwa yanaunda USSR Kama Ukraine, Georgia,Chechneya ambayo hayakupewa kipaumbele jambo lililochochea hisia za kujitenga.
 
Waliofanya utafiti huu inabidi wamuombe kwanza msamaha Bwana PUTIN maana ni kama vile kumzalilisha kufananisha ukaribu wa Serikali yake na ule kwa Soviety.

Neno (ukaribu) lina maana kubwa sana katika utawala wa Nchi na hapo uwa kuna changamoto kubwa sana.Tawala nyingi zimeanguka kwa sababu ya kutokuwa na ukaribu na Wananchi wake.

Ukaribu na Wananchi sio kwenda kukaa nao bali kuzisikiliza kero zao na kuzifanyia kazi pasipo kuangalia kabila wala chama.PUTIN kaweza kuwasikiliza Wanachi wake,viongozi wake na wasomi wake ili kufanikisha kujenga Nchi na kuleta maendeleo ndani ya URUSI.kaweza kuweka ukaribu kati ya viongozi wake na Wananchi na pia kawapa eshima kubwa sana wasomi wa ndani ya URUSI.

Tatizo kubwa lilikosababisha kuanguka kwa SHIRIKISHO la SOVIETI ni uchumi.uchumi wa SHIRIKISHO ulikumbwa na changamoto ya elimu,ajira na pato la taifa kuwa chini.

* AJILA*ELIMU*PATO LA TAIFA

Wananchi wengi walikosa ajila katika Shirikisho kutokana na ushindani wa mfumo wa viwanda kati ya mataifa ya magharibi(EU na Marekani)na Shirikisho.Shirikisho lilishindwa kuwekeza katika sekta ya elimu na kutoweza kutoa nafasi na eshima kwa wasomi wa ndani.Technologia ya magharibi ilikuwa juu kushinda ya Shirikisho ivyo ikapelekea kushindwa kwa Shirikisho katika soko la viwanda.

Pia Serikali ya Kisovieti ilishindwa kuwapa nafasi wawekezaji ikawa ndo msimamizi mkuu wa makampuni yote na mwenye hisa zote za kila kampuni kubwa katika Sovieti.
Serikali ya Kisovieti ilijikuta inakusanya kiasi kidogo kwenye Pato la taifa kutokana na rushwa iliyokisiri kila sehemu na kufa kwa baadhi ya makampuni makubwa ya Sovieti.Wananchi waliona ndani ya Shirikisho maisha ni magumu sana na wengi waliamua kwenda kwenye nchi za magharibi kutafuta maisha,hata wasomi wengi walikimbia katika shirikisho na kwenda kufanya kazi sehemu nyingine.

sehemu kubwa ya Shirikisho maisha yalikuwa magumu sana mpaka ikafika mahali baadhi ya sehemu zikafanya mabadiliko ya uwongozi na kuanza kuomba uhuru wao.

Hii inaonyesha kabisa jinsi gani Serikali ya Shirikisho haikuwa karibu na Wananchi wake
 
Umetangulia kwa kujihami kuwa wewe si Pro-Putin. Well! Hakuna ulazima wowote wa kusema hivyo na michango na maoni ya pande zote zenye ufahamu juu ya hili hayazuiliwi ndiyo maana nikaileta hii taarifa hapa kama ilivyo na bila kupunguza wala kuweka maneno yangu ili pia tupate kulijadili hili hapa jukwaani.

Umezungumza kuhusu taasisi iliyohusika na utafiti huo ijulikanayo kama Levada Center na ukasema kuwa hiyo taasisi ni foreign agent. Unasema hivyo kwa maana gani na kwa sababu zipi kwamba hiyo taasisi ni foreign agent?

Pia umesema kuwa Putin anafanya vizuri kwa mujibu wa habari za TV. Sikatai kuhusu hilo lakini Je! Tunaweza kupata uthibitisho wa utendaji kazi wa Putin kupitia habari za TV pekee. Na Je! ni taarifa za TV zipi hizo? Na anafanya vizuri kwa muktadha gani?

Umezungumzia utawala wa Boris Yeltsin na ukaulinganisha na wa Vladimir Putin na ukasema kwamba Yeltsin alikuwa 'softly' n.k.
Sasa, hicho ulichokizungumza kinaendana na utafiti uliofanyika hapo?

Huoni kuwa unachokizungumzia hapo ni kitu tofauti kabisa na kile kilichopo mezani? Ahsante!
Nimejibu kwa historia: Kuonesha kabla ya Putin Russia ilikuwa wapi na baada ya Putin Russia imekuwa wapi. Kisha nikaelezea uhalisiya wa hizo takwimu asili yake ni wapi na nini. Putin anachukuliwa baada ya Stalin ni yeye Putin. Stalin aliwaonyesha wananchi jinsi ya ku' survive lakini Putin anawaonyesha wananchi jinsi gani ya kuishi siyo kusurvive. Uzuri wa nchi kama Russia unakwenda kwa historia. Takwimu ya Levada inasema;

When asked to characterize Russia's current leadership, 41% called it “criminal and corrupt” and 31% called it “distant from the people and alien.”

Kwa kujibu swali hili iangalie Russia ilipotoka kabla ya Putin na ilipo baada ya Putin. Viongozi wengi wa nchi ya Russia wanafahamika walikuwa wanaongoza kwa mkono wa chuma. Kwa madaraka aliyokuwa nayo Putin kwa nchi kama ya Russia sidhani hao wafanya tafiti wangekuwepo na hao raia wanaotoa mawazo sidhani kama wangeyatoa kama tawala ya Russia ingelikuwa ilivyo kama tafiti ya Levada inavyodai.

Russia vyama vya upinzani vinamiliki vituo vya radio, runinga, forums mbalimbali n.k Licha ya hivyo unazungumza utakavyo na wala hautodhurika.
Uhalifu na ubadhilifu wa Putin ni upi? Laiti kama Russia's current leadership, 41% are “criminal and corrupt” uhuru hata huo wa kufanya tafiti na uhuru wa raia kutoa maoni usingekuwepo ungeminywa. 41% ni kubwa usiifanyie masihara.

Anachokifanya Levada kulinganisha tawala ya soviet na ya sasa( ya Putin) kwa Russia ni divide and rule. Na utawala wa Russia wanaifahamu hiyo Levada kwamba ni NGO inayofadhiliwa na wahisani wa nje ya Russia.
 
Mwaka 1990 kaya zilizokuwa zinaishi chini ya mstari wa umaskini ndani ya Urusi ilikuwa 30%

mwaka huu kaya zinazoishi chini ya mstari wa umaskini ni 13%

Putin kapunguza gape la kaya maskini zinazoishi chini ya dollar 13.warusi kwa sasa wengi wamerudi makwao maana maisha ya Urusi yamekuwa bora kuliko ya nchi za ulaya
 
Utafiki fake huo.....wanaufuatilia historia ya Soviet Union wanajua tofauti ya kipindi kile na sasa.....
 
Ukitaka uwe Bora machoni mwa taasisi na serikali za magharibi popote duniani kuwa pro west Kama alivyokula Yeltsin..Putin alionekana kuwa pro west lakini baadae aliwageuka hii Ni kwasababu Putin Ni mzalendo no 1 ..
Malengo ya Putin Ni kuijenga Russia yenye nguvu internationally kijeshi, kiuchumi, na kisiasa..
Na hili limefanikiwa Leo Russia Ni nchi ya kuogopwa Sana na Western.. ingia issue ya Georgia, Ukraine, na Syria..
 
Uchumi wa Russia hauwezi kuwa juu kihivyo kwani hauwezi kukua in isolation labda kijeshi.

NB: Uchumi wa Russia unazidiwa na uchumi wa jimbo la Texas ambalo ni la pili kwa ukubwa nchini Marekani.
 
Ukitaka uwe Bora machoni mwa taasisi na serikali za magharibi popote duniani kuwa pro west Kama alivyokula Yeltsin..Putin alionekana kuwa pro west lakini baadae aliwageuka hii Ni kwasababu Putin Ni mzalendo no 1 ..
Malengo ya Putin Ni kuijenga Russia yenye nguvu internationally kijeshi, kiuchumi, na kisiasa..
Na hili limefanikiwa Leo Russia Ni nchi ya kuogopwa Sana na Western.. ingia issue ya Georgia, Ukraine, na Syria..
Hahaha! Na je ukitaka uwe bora machoni mwa Serikali za 'Mashariki' kwa akina 'Kiduku' unatakiwa uwe Pro nani?

Unauzungumziaje uzalendo wa mtu? Je! Ukishajenga uadui na Western basi wewe ndiyo mzalendo no.1?

Tujadili pia na hili;
Malengo ya Rais Putin yameweza kufanikiwa kwa kiwango gani? maana umetaja hapo kwamba kijeshi, kiuchumi na kisiasa.

Mwishoni umezungumza kwamba leo Russia ni nchi ya kuogopwa sana na Western lakini hujaweka sababu za msingi na zina manufaa gani kwa Warusi wenyewe kuliko hiki wanachokilalamikia kipindi hiki kuhusu rushwa, ufisadi n.k.?

Maana kama ni nchi kuogopwa tu inawezekana kabisa na zipo nchi nyingi tu zinaogopwa na Western. Mfano tu hata Africa kuna nchi zinaogopwa kutokana na sababu mbalimbali.
 
Back
Top Bottom