Rushwa yawafukuzisha kazi askari saba

Rushwa yawafukuzisha kazi askari saba

Efendi

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2016
Posts
315
Reaction score
438
Rushwa yawafukuzisha kazi Askari saba

Jeshi la Polisi Tanzania leo, Januari 11, 2019, limewasimamisha kazi askari saba (7) wa vyeo mbalimbali kwa kutenda kosa kinyume na mwenendo mwema wa Jeshi la Polisi na tayari wamefikishwa mahakamani kusomewa mashitaka yanayo wakabili.

Hatua hii imechukuliwa, baada ya askari hao kuomba rushwa ya bilioni moja na baadae kupokea rushwa ya milioni mia saba toka kwa mfanyabiashara wa dhahabu aitwaye Sajid Abdalah Hassan ambaye walimkamata akiwa na dhahabu kiasi cha kilogramu 319.59, yenye thamani ya mabilioni ya shilingi za kitanzania.

Askari hao waliosimamishwa kazi ni;

1. E.4948 CPL Dani Isack Kasala
2. F.1331 CPL Matete Maiga Misana
3. G.1876 PC Japhet Emmanuel Lukiko
4. G.5080 PC Maingu Baithaman Sorrah
5. G.6885 PC Alex Elias Nkali
6. G.7244 PC Timoth Nzumbi Paul
7. H.4060 PC David Kadama Ngelela.

Aidha, kuhusu Afisa SSP: Moris Okinda ambaye alikuwa kiongozi wa askari hao walioomba na kupokea rushwa ya kiasi hicho cha fedha, mamlaka yake ya kinidhamu tayari imemsimamisha kazi na tayari amefikishwa mahakamani pamoja na askari hao.

Pamoja na askari hao, pia wamefikishwa mahakamani watuhumiwa wengine wa nne waliokamatwa huko Kigongo feri Wilayani Misungwi wakitorosha madini hayo ya dhahabu kutoka Tanzania kwenda Nchi jirani ya Rwanda.

Watuhumiwa waliokamatwa wakitorosha madini hayo ya dhahabu ni;

1. Sajid Abadalah Hassan, miaka 28, mfanyabiashara wa dhahabu, mkazi wa Ilala Dar es Salaam na Mwanza mtaa wa pamba ‘A’.

2. Kisabo Kija @ Mkinda , miaka 55, mfanyabiashara wa dhahabu, mkazi wa mwatulole –Geita

3.Emmanuel Ntemi, miaka 63, dereva, mkazi wa kijiji cha mwatulole –Geita

4. Hassan Sadiq Hassan, miaka 28, Mhindi, Raia wa Pakistani, mkazi wa Mwanza mtaa wa Pamba ‘A’, Mfanyakazi wa duka la kuuza vito.

Kufuatia sakata hili, Jeshi la Polisi Tanzania kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na wanaendelea na uchunguzi wa kina ili tuweze kuwakamata watuhumiwa wote waliohusika kwa namna moja au nyingine katika sakata hili.

(KILA BINADAM NI MFUNGWA MTARAJIWA, MWENYEZIMUNGU ATUEPUSHE)
 
Rushwa yawafukuzisha kazi Askari saba

16 minutes ago

Sent using Jamii Forums mobile app
Tungepata picha za hao police ingelikuwa poa kabisa make lazima kutakuwa na raia wengi ambao wameishaathirika na utendaji wao.Make hakuna kitu kizuri kuona mtu aliyekufanyia unyanganyi kwa kutumia chao chake halafu unamsikia lupango

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba kufahamu; Kichwa cha habari kinasema "Rushwa yawafukuzisha kazi Askari saba", lakini ndani ya habari nimesoma kwamba, askari hao wamesimamishwa kazi na kufikishwa mahakamani.

Sasa, polisi akisimamishwa kazi na kufikishwa mahakamani ndiyo tayari anakuwa amefukuzwa kazi? Naomba kufahamu tafadhali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jina la Mchungaji Siku halijaonekana mbona??ili hali kwenye zile dhahabu kuna tofali kadhaa zmeandikwa jina lake
 
Huyo PC maingu dogo alikuwa muonevu na mjuaji Sana hapa jijini Sasa sijui anaenda kuishi vp na watu aliowafanyia hujuma na kuwabambikia kesi Hapo butimba? Tujifunze kuwa na kipato halali ili tuishi maisha yenye kumpendeza Mungu na I we fundisho kwetu sote
 
Kwnn wasiwamiminie tu risasi. Kesi ya kazi gani hao majambazi?
 
Kuna aliyeshtuka kapigwa kanzu hapo akaamua kuchoma utambi. Lilivyolipuka yeye yuko mbaaaaaali saa hizi
 
Dah!!!

Jamaa walikuwa wanatoka kudadadeki!nawapa pole sana wajue tu ni sehemu ya mchezo kushinda na kukosa vinaambatana.

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
 
Back
Top Bottom