Rushwa ya CCM katika kinyang'anyiro cha Ubunge wa EALA ni aibu

Daniel Mbega

JF-Expert Member
Mar 20, 2013
338
180
Kesho Bunge linakutana kwa vikao vyake vya Bajeti mjini Dodoma, lakini agenda ya moto zaidi ni uchaguzi wa wabunge watakaoiwakilisha Tanzania kwenye Bunge la Afrika Mashariki (EALA).

Yapo mengi yanayoendelea kuanzia kwenye mchakato wa ndani ya vyama vya siasa hadi katika kuomba kura kwa wabunge.

Lililo kubwa ni kwamba, rushwa ndiyo inaonekana kushika kasi kwenye kinyang'anyiro hicho, zaidi ikiwa inaendeshwa na wanamitandao ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambacho kina wagombea wengi japokuwa kikanuni nafasi zake ni sita.

Ni kuwepo kwa wagombea hao wengi, na msuguano mkubwa ndani ya chama unaoendelea kuzaa makundi ndani ya wabunge wa CCM, ndiko kunakoelezwa kuchochea rushwa ambapo taarifa zinazsema mamilioni ya shilingi yanagawiwa kwa baadhi ya wajumbe watakaopiga kura.

Mbaya zaidi ni kwamba, mgawanyiko wa wabunge wa CCM unaelekea kuchochea mambo kwenye uchaguzi huo kukiwa na mikakati ya kuhakikisha wanapita hata watu ambao 'hawakutarajiwa', kwa maana ya wale ambao hawako kwenye duru za siasa za siku zote.

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) iko wapi jamani? Hivi kweli hawajasikia, hawajui ama hawayaoni yanayotendeka Dodoma? Au ndiyo funika kombe mwanaharamu apite?

Tusubiri tuone hali itakuwaje.

=============
rushwa ccm.jpg
 
Unauliza mpemba kuvaa msuli?! Mbona hiyo ni jadi yao!!
 
Bashite angekua mgombea mkwala ungepigwa kulazimisha ashinde!
Daudi Bashite weka vyeti mezani!
 
Hiyo ndiyo desturi zao za rushwa. Acha wafu wazikane. Na mwaka huu ccm inaelekea kufa, ila nawajua wazee wa puchu a.k.a punyeto (bao la mkono) watasurvive tu lkn kwa shida sana.
Hapo makund tayar yasheundwa. Pro and ant group
 
Back
Top Bottom