Napenda kuchukua nafasi hii kuwaomba radhi wote walioathirika na post yangu niliyopost trh 02/11/2013 yenye kichwa cha habari '' Rushwa Ngome ya CCM Bagamoyo.Nakiri ya kwamba wakati naandika post hiyo jazba na hasira vilitawala akili yangu.Hii baada kuona harufu ya rushwa na upendeleo ktk idara mbalimbali hasa idara ya elimu kwa kupendelea baadhi ya walimu kupewa kazi maalum zenye posho mara kwa mara miaka yote huku wengine wanazikosa nafasi hizo hata kwa miaka sita,ukizingatia malupulupu ya kazi ya ualimu ni madogo mpk uteuliwe kusimamia mitihani au kusahihisha na semina,hivyo kwa wale wanaokosa hizi nafasi kila mwaka wanajikuta wanachukia kazi ya ualimu ( baadh wafikiria kuacha kazi) kupunguza molari yao ya kufanya kazi (baadhi yao wakiishi maisha magumu kwa kutegemea mikopo kutoka kwa baadhi ya watumishi,mikopo hii ina riba kubwa mpk asilimia 50 kwa mwezi,mtu akikopa laki moja analipa 150,000) huku wengine wkt wote mifuko yao imejaa pesa kwa kutokosa kuteuliwa ktk kazi hizi za posho kwa kuwa wananetwork na wakubwa wa idara ya elimu.Hali hii hujenga matabaka,kushusha molari ya kazi,kuchukia kuitumikia serikali na migogoro kazini.SHETANI ALITAWALA AKILI YANGU.HAKIKA NILIPATA MAJARIBU MAKUBWA YA IBILISI.Nachelea kusema tuhuma zote nilizoelekeza kwa idara ya Elimu Wilaya,TRA,Ardhi,mahakama,Kikosi cha usalama barabarani na jeshi la polisi zimejaa upotoshaji wa hali ya juu.TRA na askari na wa check point ya Dunda sekondari wamekuwa na uhusiano nzuri na wafanyakazi wa jumuia ya Dunda,kwani wanadiriki mpk kuwasimamishia magari wapande.Askari hawa wamekuwa wanahakikisha usalama wa wanafunzi unazingatiwa.Shukrani kwa afande Ashura na Machiwa kwa kazi yenu nzuri TUKO PAMOJA.MUNGU AWABARIKI MUISHI MIAKA 200,100 kila mmoja.Natambua mchango mkubwa wa idara hizi ktk kuwaletea Watanzania maendeleo.Nani asiyejua jinsi gani idara ya ardhi ilivyotuletea maendeleo Bagamoyo kwa kushirikiana na serikali kuu kwenye zoezi la upangaji na upimaji wa ardhi kwa maendeleo ya Bagamoyo na Tanzania kwa ujumla.Idara hii imekuwa kiungo muhimu ktk utekelezaji wa mkakati wa serikali ya mh.Rais JK wa matumizi bora ya ardhi yetu kutuletea maendeleo hapa Bagamoyo na Tanzania kwa ujumla.Nikizungumzia idara ya mahakama,tunaona jinsi gani idara hii inavyofanya kazi ya kutatua migogoro mbalimbali na kusikiliza mashauri mbalimbali kisha kuyatolea maamuzi ya haki.Nao TRA wanafanya kazi ngumu ya kukusanya mapato kwa ustawi wa taifa letu tukufu.Kwa upande wa jeshi la polisi,nachelea kusema jeshi hili likishirikiana na vyombo vingine vya usalama kama idara ya usalama wa Taifa linafanya kazi nzito sana kuwatumikia Watanzania kwa kulinda raia na mali zao.Amani,utulivu na mshikamano ni matunda ya kazi nzuri ya jeshi la polisi na idara ya usalama wa Taifa pamoja na vyombo vingine vya usalama.Ktk suala la amani,utulivu.Napenda kutambua michango ya marais wa awamu zote ktk kudumisha amani,utulivu,upendo na mshikamano ktk Taifa letu.Marais waastafu na Rais wa sasa mh.Jakaya Mrisho Kikwete wamefanya kazi kubwa kututumikia Watanzania kwa kuliongoza Taifa kwa kutumia hekima,weledi,uzalendo,upendo,uchapa kazi wa hali ya juu..Napenda pia kuiomba radhi idara ya elimu kwa kuhitumu kujihusisha na vitendo vya RUSHWA.Tuhuma hizi sina uhakika nazo ni maneno tu ya mitaani.Natambua mchango mkubwa wa idara ya elimu sekondari ya wilaya ya Bagamoyo ktk kusimamia elimu hapa Bagamoyo.Napenda kumuomba radhi rafiki yangu Chilipweli kwa kumtuhumu anapewa rushwa ya ngono kutoka kwa walimu wa kike.Natambua mchango wa Chilipweli ktk kutunza rikodi za shule zote za Bagamoyo kwa kutumia ujuzi wake wa IT uliotukuka.Hapa nilighafilika kwa kusikiliza maneno ya mitaani yaliyojaa uzushi na majungu.Napenda pia kumwomba radhi mwl.Mazoko kwa kumuhusisha kutoa rushwa ya ngono kwa Chilipweli ili apate upendeleo.Mwl.Mazoko namuheshimu sana kwa upendo,ucheshi na uchapakazi wake.Nakiri vilevile hapa nilipotoka.Naomba radhi pia kwa walimu wafuatao ; mwl.Masimbi na mkewe,mwl.Mtawa na mkewe,Mwl.Eddy,Mkumbae,Hoza kwa kuwahusisha na vitendo vya rushwa ktk idara ya elimu ili wapate upendeleo wa kupata nafasi mbalimbali zinazohusisha malipo ya posho.Naomba radhi pia kwa Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri (W) Bagamoyo,Afisa Elimu wa Wilaya,Afisa wa Afya (W) Bagamoyo,Meneja wa TRA (W) Bagamoyo,Afisa Ardhi,mkuu wa jeshi la polisi (W) Bagamoyo,Mkuu wa Wilaya,Katibu Tawala wa wilaya kwa kuwakwaza na post yangu iliyojaa jazba ktk mtandao wa Jamii Forums.Hata hivyo ukweli wa tuhuma nilizotaja unaweza kujulikana iwapo uchunguzi wa kina ukifanyika.HALI HII HAITAJIRUDIA TENA.Hata hivyo ninyi mliopewa dhamana ya kuwa wakuu wa idara mbalimbali TENDENI HAKI KWA KILA MTU.OFISI YA ELIMU SEKONDARI YA BAGAMOYO ACHENI UPENDELEO WA WAZIWAZI KWA BAADHI YA WALIMU MARAFIKI ZENU.NI KINYUME CHA SHERIA YA AJIRA NA MAHUSIANO KAZINI MWK YA 2007. NNapenda kuwasilisha.