Rushwa na ufisadi nchini na hatima ya nchi yetu.

Rushwa na ufisadi nchini na hatima ya nchi yetu.

aminiusiamini

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2011
Posts
3,577
Reaction score
2,226
WanaJamii,

Mara nyingi tumekuwa tukisikia kuhusu ufisadi,na wizi kutokea katika mashirika ya umma na serikali huku wahusika waliochukua dhamana ya nchi,wakicheka kana kwamba ni jambo la kawaida, na muda mwingine wakubwa hawa wa nchi kuhusika katika maovu haya;Kucheka huku ni sawa na kuchekea tabia mbovu kwa mtoto bila kumwonya na ambayo itakuja kutuangamiza sisi watanzania wote bila kujali hali zetu.

Nchi yetu kwa muda wa miaka kumi imekuwa kama haina raisi au kiongozi anayesimamia mustakabli mnzima wa nchi na hali za wananchi.Nchi iligeuka sehemu au kitovu cha wanya'nganyi,wala rushwa na mambo mengine mengi,kiasi kwamba mambo yalitokea TRA TPA ni sehemu ndogo sana ya ufisadi uliokithiri nchini.Hawa viongozi walioguswa ni kweli wanahusika kwa njia moja au nyingine lakni je,ndio wezi tu waliopo hapa nchini? je wailiba pekee yao?

Ninakubaliana na wengi wetu ambao wanasema bado Raisi asiiishie hapa,hajaenda kwenye utalii,miradi ya maji,madini,na nishati nk.Tanzania ina mali nyingi sana na rasilimali nyingi kiasi kwamba hatuhitaji kwenda kuomba hela nje kuendeshea serikali wala mipango ya maendeleo.Vitega uchumi tulivyonavyo kama vikipata watu wabunifu na wachapa kazi tunauwezo wa kufika mbali bila kutegemea sumuni ya mkoloni na mikopo isiyojenga nchi bali kuivuruga.

Swali ni nani tumlaumu kwa kufika mahali hapa ? Mimi nathani tujilaumu wenyewe sisi watanzania.Pamoja naweza kusema kwa kujiamini kwamba tunaye raisi baada ya Nyerere kutokea,lakni hatima ya nchi yetu iko mikononi mwetu na sio raisi magufuli.
Leo hii,vijana kwa wazee na wamama wanalalamika kuhusu huduma za jamii mbovu,kutowajibika kwa viongozi na mambo mengi lakni wanasahau kuwa wao ndio chachu,wenye hatamu na nguvu kubwa kuliko viongozi.

Nathani imefika wakati tupige vita rushwa kwa pamoja,na vitendo vyote vya ufisadi na wizi.Wengi wanaolalamika kuhusu vitendo vya wengine kufanya ufisadi ni kwamba wao wenyewe hawakupata fursa hio na wanalalamika kwasababu hawana.Lakni leo hii,kijana mtanzania utasikia akiwaza maisha ya anasa bila kutaka kufanya kazi kwa bidii,kutegemea vya kunyonga Zaidi kuliko jitihada na kazi .

Kuwalaumu viongozi kwa rushwa nathani tusiishie hapa.Rushwa na ufisadi imekuwa sehemu ya maisha yetu sisi watanzaniaKila mtanzani kwa nafasi yake na uwezo wake,ametumia ufisadi na rushwa kujipatia haki na pengine sio haki ilimradi kupata kile anachotaka kwa njia sio halali,na udanganyifu lakni inapokuja kumuhusu mtu Fulani kwa moja kwa moja tunabadilika na kunyoosheana vidole.

Kuna watu,nyumba waliuziwa pale osysterbay,masaki kwa bei za kutupa.Viwanja na mambo mengine mengi kwa njia sio sawa.Wengine wameshinda kesi kwa kuhonga hakimu,Wako wale kwenye madirisha ya malipo wanaochukua ten percent hata kama ni hela ndogo swala ni kwamba unapokea rushwa kwa nafasi yako;Mbuzi hula kwa urefu wa Kamba yake.Kwahiyo tusijidanganye kuwa viongozi tu ndio wezi na wala rushwa,hata wewe mwenyewe hapo ulipo ulishwahi kupokea au unapokea rushwa na kutoa rushwa na uko fisadi.Je fisadi ni nani hasa TANZANIA? naomba tujiulize hilo swali na tutajikuta tunanyoosheana vidole huku vidole vitatu vyote vikiturudia.

Rai yangu kwenye watanzania ni kumpa support kubwa sana raisi Magufuli katika vita hii,na ujenzi wa taifa letu kwa upya kabisa.Ni matumaini yangu tutaendelea kupata wazalendo Zaidi katika kazi za serikali katika kuwatumikia wananchi na kama sio mfanyakazi serikali basi mfanyabishara mzalendo unayetii sharia na kuipenda nchi yako..

Tanzania itajengwa na kubomolewa na sisi wenyewe na sio rais Magufuli .


Idumu nchi yetu TANZANIA.
 
Mungu zidi kumpa afya njema na nguvu JP Magufuli maana ni mkombozi wetu .
 
Back
Top Bottom