katima
Member
- Aug 22, 2012
- 99
- 59
Katika hali ya kusikitisha Rushwa imetawala uchaguzi wa Tarime vijijini na imeshindwa kuthibitiwa na vyombo husika vilivyopo nchini kisheria kupambana na adui rushwa anaenyemelea kura za vuguvugu la madiliko ya wanaTarime vijijini. Mdudu huyu anasambazwa na mgombea wa CCM Ndg Christopher Kangoye. Taarifa hizi zimetolewa kwa malalamiko na wananchi wa maeneo mbalimbali wa jimbo hilo, miongoni mwa wananchi hao ni wale wa kata ya Nyakunguru ambao wanadai kuwa mgombea wa Chama cha mapinduzi Ndg Christopher Kangoye amekuwa akihonga wapiga kura wa kata hiyo zaidi ya shilingi 5000, kofia, kanga na tisheti za CCM ili wamchague yeye. Wananchi hao wamelalamikia hali hiyo na kudai kuwa wameachwa nyuma kimaendeleo kwa kukosa wawakilishi wazuri kimaendeleo,kwani kwa miaka ya nyuma na ya hivi karibuni rushwa ilitumika kununua kura zao kwa kupewa hongo ya kofia na tisheti, chumvi na pesa hali inayopelekea wabunge kuwasahau kiuwakilishi kutokana na hali ya kununua kura zao. Matumizi ya rushwa yamelalamikiwa pia na wananchi wa kata ya mbogi, kwa kudai kuwa mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM Ndg Christopher Kangoye kwa kushirikiana na Mgombea Udiwani wa Kata ya Sirari kupitia tiketi ya CCM Ndg Sagara wanatoa pesa za rushwa katika kata hiyo kwa kupitia kada wa CCM anaezisambaza kwa watu kwa kushirikiana na familia yake,baadhi ya wananchi wamedai na kubaini kuwa pesa hizo kutoka kwa Ndg Kangoye zilipelekwa Mbogi usiku wakuamkia kampeni kwenye kata hiyo na gari ndogo nyeusi inayojihusisha na kampeni za mgombea udiwani kata ya Sirari kupitia CCM kwa lengo la kumsaidia Kangoye. Pia kofia,tisheti zinazogawiwa bure hutumika kama kivutio kwa wananchi kuhudhuria kwenye mikutano ya kampeni za CCM, hali hii imelalamikiwa hasa na wananchi wa kata ya Mbogi walipewa shilingi 5000 kama rushwa ya kumchagua Ndg Kangoye na kupewa pia kofia, vilemba na tisheti.
Pia baadhi ya matajiri akiwemo Peter Zakaria na Christopher Gachuma,wamekuwa wakitoa vitisho kwa mgombea wa CHADEMA Ndg John Heche,hii ni kutokana na ubia walioingia na mgombea wa CCM Ndg Christopher Kangoye kuwa wamsaidie ashinde na aje kuhakikisha wanakuwa na gawio kutoka mgodi wa north mara ( Nyamongo), mgodi ambao mara nyingi hupiganiwa na wagombea wa CHADEMA wanapobahatika kupata ridhaa ili uwe sehemu ya msaada kwa jamii ya wanatarime.
Uchaguzi huo pia umegubikwa na siasa za koo zinazofanywa na mgombea wa CCM Ndg Christopher Kangoye, kwa kuwaomba Wanainchage (anakotokea) Ndg Kangoyeyeye kuwa wamchague yeye na sio mgombea wa CHADEMA au mgombea mwingine anaetokea kwenye koo yeyote, kwani koo zingine kamwe hazitawaongoza wanainchage na hazina historia ya kutoa mbunge kwa kuzitaja majina Inchugu,Nyamongo,Wanchali,Warenchoka.
Mgombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA ndg John Heche ametoa rai kwa DC wa Tarime kuwa ahakikishe analinda amani ya wanatarime vijijini mda huu wa uchaguzi kwa kuweka kando tofauti zao za zamani za kurumbana mara kwa mara kuhusu haki kwa wanatarime ambao mara kadha wamekuwa wakinyanyaswa na vyombo vya dola kupitia kwa mamlaka ya DC.