Rushwa inaweza kuwa katika makundi makuu mawili. Aina ya kwanza ni ile inayomuhusisha mtu mmoja mmoja hususan pale anapotumia madaraka yake na ofisi ya uma kwa manufaa yake binafsi. Katika mfumo huu, watu katika jamii huwa hawahusishi maisha ya mtu binafsi na ya utumishi wake katika ofisi za uma. Anaweza akawa mtu anayepokea laki tano kwa mwezi lakini akawa anaishi maishi ya kimilionea na jamii ikaona sawa. Hapa kuwa na mipaka dhahiri kabisa kati ya utumishi na maisha binafsi hivyo watu hawaoni sabab ya kuhoji.
Aina ya pili ya rushwa ni ile iliyopo kimfumo ambapo jamii huona rushwa ni sehem katika mfumo wa maisha yao ya kila siku, tena ndo njia rahisi ya kufanya mambo yao kimkato. Katika aina hii mto rushwa na anaepokea hakuna yeyote kati yao anayeona kuwa kuna dhambi au kosa lolote kwa lile walifanyalo, bali ni tamaduni ya kawaida tu ambayo ishazoeleka.
Swali la msingi hapa je sheria zetu na sera kuhusu rushwa zinalenga kupambana na rushwa ya aina gani katika hizo mbili? Kwa nchi ambayo tayari rushwa ishakuwa sehem ya jamii, sera zenye mlengo wa kupambana na rushwa katika ngazi ya mtu binafsi haziwezi fanikiwa kwa sabab zitafanikiwa kuondoa sehemu ya tatizo tu na sio kutatua tatizo kuu. HAPA TUNAWEZA KUSEMA RUSHWA IMEZIDI UZALENDO.
Kwa mfano mtanzania gani atakapokamatwa kwa kosa la barabari atakubali mara moja kuandikiwa risiti na kulipa faini badala ya kuomba kutoa rushwa? Ni wachache sana, na tena hukasirika zaidi hata kufoka, lakini akitoa rushwa anakuwa na amani zaidi ataondoka huku anamuaga trafiki.
JPM hatofanikiwa kuiono rushwa kwa hisia na maona aliyonayo tu, bali anahitaji kupambana na rushwa kwa njia mbadala, leo kama mtumishi analalamika njaa, hajapndishiwa mshahara mwaka mzima, unamshawishi achukue rushwa, tena sabab jamii ndio chachu kubwa ya rushwa inakuwa kwake ni rahisi kufanikiwa. Sheria pekee haitoshi, watu wanapambana na rushwa kubwa lakini rushwa ndogo ndo zina athari kubwa kwa jamii kubwa, rushwa katika elimu, afya zina madhara makubwa ya kila siku.
Unapoendelea kubana hela unachochea rushwa, unapofanya watumishi waishi kama mashetani unachochea rushwa. Njia mbadala ni kuhakikisha jamii inapata inachotaka kwa wakati, jamii inaishi kwa amani sio kwa stress. Jamii inaihitji kuridhika.
RUSHWA MWENZAKO KESHACHUKUA NAFASI YA UZALENDO, TENA KAMFUTILIA MBALI KAMA TULIVYOMFUTILIA MBALI NDULI IDI AMIN DADA UGANDA. KUMRUDISHA MZALENDO UNATAKIWA UWE NA MBINU KALI SANA ZA UTONGOZAJI KUMFANYA MTANZANIA AMUACHE RUSHWA ARUDI KWA MZALENDO, SIO KWA SURA ILIYOKASIRIKA AU SAUTI KALI BALI KWA NJIA NA MIENENDO SAHIHI ITAKAYOMFANYA AKUAMINI.
"MBUZI KAFIA KWA MUUZA SUPU"