mdhalendo
JF-Expert Member
- Dec 14, 2011
- 282
- 273
Msajili wa vyama vya siasa nchini Mheshimiwa John Tendwa amekuwa mstari wa mbele kutoa kauli kali dhidi ya vyama mabalimbali vya siasa kwa kile anachokiita "kwenda kinyume na taratibu za kidemokrasia". Mfano mzuri ni kipindi Tendwa alipokuwa mkali dhidi ya CHADEMA kuwa chama hiko kimekuwa hakifuati sheria zilizopo nchini.
Lakini tangu kuanza kwa chaguzi za ndani katika chama cha mapinduzi CCM hatujasikia kauli yoyote ya karipio kutoka kwa msajili huyu wa vyama vya siasa nchini. Rushwa hizo zimeshuudiwa wazi kuanzia katika chaguzi za mikoani, UWT, UVCCM na hata mwelekeo wa jumuiya ya wazazi. Jana Mheshimiwa Zungu amekamatwa na TAKUKURU lakini tendwa bado yupo kimya. Sasa Tunajiuliza kazi kubwa ya Tendwa ni kukemea na kuvitisha vyama vya upinzani pekee?? Kwanini anafumbia macho rafu zinazofanyika ndani ya chama tawala? u kwavile mwajiri wake yupo kwenye chama hicho? Dhambi ya unafiki itammaliza Tendwa