youngsharo
JF-Expert Member
- Jan 8, 2015
- 2,491
- 500
Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) imezitoza faini kampuni tano za simu za mkononi nchini, kwa kushindwa kutekeleza wajibu wao wa kuhakikisha uwepo wa usalama wa kiufundi na kisheria kwenye masuala ya taarifa zinazopitia kwenye mitandao yao.
Kampuni hizo ambazo kila moja imetozwa faini ya Sh milioni 25 ni Benson Informatics Limited yenye mtandao wa Smart, Mic Tanzania Limited (Tigo), Airtel Tanzania Ltd, Viettel Tanzania Ltd (Halotel) na Zanzibar Telecom Ltd (Zantel).
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa TCRA, Dk Ally Simba alisema kampuni hizo zinatakiwa kutoa faini hiyo kabla ya Januari 29, mwaka 2016 na kwamba kila kampuni imetakiwa kujenga mazingira wezeshi yatakayoweza kuziba mianya ya uharibifu wa mawasiliano kwenye mitandao yao.
Alisema ni vema kampuni hizo zikakumbuka kwamba zinapaswa kufuata Sheria ya Mawasiliano ya mwaka 2011 na kushindwa kutimiza matakwa ya sheria ni kutoa mianya ya wahalifu kujipenyeza, kuingilia mawasiliano ya watu, hivyo kuleta matatizo kwa watumia huduma za mawasiliano.
“Tumepokea malalamiko kutoka kwa wateja kuhusu usalama wa mawasiliano ya simu, ambayo mitandao hiyo inaruhusu wahalifu kuweza kuingilia mitandao hiyo na kutuma ujumbe mfupi wa simu unaopotosha umma”, alisema Dk Simba.
Alisema mamlaka hiyo na Polisi wamepokea malalamiko 42 katika kipindi cha miezi miwili iliyopita na kwamba katika matukio hayo, kila moja linaweza kusababisha hasara ya Sh milioni 25.
Alisema kampuni hizo, zinatambua wajibu wao wa kulinda usalama wa mawasiliano ya wateja na kwamba TCRA iliwakumbusha jambo hilo Oktoba mwaka huu, na kwamba hadi Desemba 2015 hakuna kampuni hata moja kati ya hizo iliyochukua hatua kutekeleza jambo hilo.
Alisema adhabu hiyo, imechukuliwa kutokana na matakwa ya sheria inayosimamia kampuni za mawasiliano na kwamba kama wakishindwa kutekeleza wajibu na mambo yaliyoambiwa kuyafanyia kazi, hatua zaidi zitachukuliwa dhidi yao, zikiwemo za kusitisha leseni zao.

Last edited by a moderator: