Rumande kwa mauaji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rumande kwa mauaji

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Apr 30, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Apr 30, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  MKAZI wa Keko Dar es Salaam, Noel Mwapula (24), anayedaiwa kuwa mlinzi, amefikishwa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, akikabiliwa na mashiatka yapatayo matano likiwemo la mauaji ya watu wawili katika maeneo tofauti.
  Amesomekwa mashitaka yake na mahakimu wanne tofauti na awali alisomewa mashitaka Mbele ya Hakimu Karim Mushi, na Wakili wa Serikali , Alice Mtulo na kudaiwa kuwa, Agosti 21 mwaka jana, majira ya saa 3 usiku, katika eneo la Mchikichini, Dar es Salaam, mshitakiwa alimuua Omary Juma kwa makusudi


  Pia imedaiwa kumuua Yassini Ramadhan Februari 23 mwaka huu, majira ya saa 2 asubuhi, katika eneo la Sharrif Shamba,jijini Dar es Salaam.

  Pia Mbele Hakimu Janeth Kaluyenda imedaiwa kuwa, Machi 13 mwaka huu saa 12 jioni, katika eneo la Mchikichini, mshitakiwa alipanga njama ya kuiba kiasi cha shilingi 300,000na kabla ya alitumia vitisho ili apewe fedha hizo.

  Ilidai kuwa kabla ya kuiba fedha hizo, mshitakiwa ambaye alirudishwa rumande alitumia kisu kumtishia Bena Kimaro ili ampe fedha hizo.

  Kutokana dna sheria za Jamuhuri waMuungano wa Tanzania mshitakiwa hakutakiwa kujibu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kuendesha kesi za mauaji na mshitakiwa alirudishwa rumande hadi Mei12 .
   
Loading...