Rufaa Majimboni

Rufaa Majimboni

Kapo Jr

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2011
Posts
1,000
Reaction score
292
Wakuu,

Ingekua vyema tuorodheshe majimbo yaliyokatiwa rufaa baada ya uchaguzi wa okt.25, ni idadi kubwa ya wabunge wa CCM ktk majimbo 264, je wameshinda halali na wale wa CHADEMA/ UKAWA wameridhika? Mfano jimbo la Nyamagana/Ilemela-wenje na kiwia wamekata rufaa!

Tajeni majimbo mengine
 
wakuu ingekua vyema tuorodheshe majimbo yaliyokatiwa rufaa baada ya uchaguzi wa okt.25,ni idadi kubwa ya wabunge wa ccm ktk majimbo 264,je wameshinda halali na wale wa chadema/ukawa wameridhika? hivyo mods msiunganishe uzi huu.mfano jimbo la nyamagana/ilemela-wenje na kiwia wamekata rufaa! tajeni majimbo mengine

yaani wenje na kiwia wanajisumbua tu wameshindwa kihalali kabisa
sema kibongo bongo hamna kushindwa ukishindwa umehujumiw
ukifa basi umerogwa
 
yaani wenje na kiwia wanajisumbua tu wameshindwa kihalali kabisa
sema kibongo bongo hamna kushindwa ukishindwa umehujumiw
ukifa basi umerogwa

Aliyeshindwa kihalali ni Kiwia tu, Wenje alikuwa amepiga mtu alichokosea Wenje ni kukubali kuhesabu kura kwa kutumia masanduku ambayo yalilala kwa Mulongo (hapo lazima upigwe).
 
Wenje alishinda toka tarehe 25 usiku hadi asubuhi alikuwa anamzidi Stanslaus Mabula kura 4000, tatzo ni Mawakala wa CCM feki walio kuwa wanaingia vituoni wamevaa sare za Tume ya Uchaguzi na Mabox mapya yenye kura kuanzia mida ya saa5 usiku.

Pia Wenje alijisahau sana, huku akijiamini kuwa atashinda kwa kishindo na kutolipa kipaumbele suala la ulinzi wa kura vituoni (Redbriged) na mawakala vituoni. Magari tena tinted yalikuwa yanaingia vituoni muda wote.

Kosa kubwa ni mabox kulala Vituo vya Polisi au kusombwa hovyo hovyo kwenye Toyota Carry usiku na kupelekwa Halmashauri ya Jiji bila uangalizi chini ya Mawakala wa vyama, na yy kukubali kuhesabu upya asubuhi (Mara 4). Huku zimekwisha kuchakachuliwa.

Pia kuna tetesi kuwa hawa Wabunge wa CCM na diwani mmoja wanaimani za kishirikina, walimtumia mganga mmoja wa kienyeji kutoka Geita-sijui kama alisaidia ama vipi?
 
kuna taarifa kuwa jimbo la rungwe mgombea wa chadema amekata rufaa baada ya utata wa kuchelewesha kutangaza matokeo jambo lililosababisha polisi kutumia mabomu ya machozi
 
kuna taarifa kuwa jimbo la rungwe mgombea wa chadema amekata rufaa baada ya utata wa kuchelewesha kutangaza matokeo jambo lililosababisha polisi kutumia mabomu ya machozi

kipenzi cha watu john d mwambigija alishinda lakini figisu figisu za mkurugenzi zilisababisha ashinde sauli,ila ukiangalia karatasi za mawakala Mzee wa Upako anaongoza.
 
Wakuu,

Ingekua vyema tuorodheshe majimbo yaliyokatiwa rufaa baada ya uchaguzi wa okt.25, ni idadi kubwa ya wabunge wa CCM ktk majimbo 264, je wameshinda halali na wale wa CHADEMA/ UKAWA wameridhika? Mfano jimbo la Nyamagana/Ilemela-wenje na kiwia wamekata rufaa!

Tajeni majimbo mengine

Jimbo la kyela , Mh Abraham Mwanyamaki anasubiri kupewa ubunge wake mahakamani .
 
kipenzi cha watu john d mwambigija alishinda lakini figisu figisu za mkurugenzi zilisababisha ashinde sauli,ila ukiangalia karatasi za mawakala Mzee wa Upako anaongoza.
Tutahakikisha john mwambigija anapewa ubunge wake alionyang'anywa .
 
Ni hivi , baadhi ya majimbo hakutakuwa na kurudia uchaguzi bali wabunge walionyang'anywa ushindi watarudishiwa . Hatutapoteza muda wa kurudia uchaguzi mahali ambapo mshindi halali anajulikana .
 
Ni hivi , baadhi ya majimbo hakutakuwa na kurudia uchaguzi bali wabunge walionyang'anywa ushindi watarudishiwa . Hatutapoteza muda wa kurudia uchaguzi mahali ambapo mshindi halali anajulikana .

katika majimbo yaliyotajwa je tayari kesi zipo mahakamani?
 
kipenzi cha watu john d mwambigija alishinda lakini figisu figisu za mkurugenzi zilisababisha ashinde sauli,ila ukiangalia karatasi za mawakala Mzee wa Upako anaongoza.

vipi amefungua kesi kupinga ushindi wa s h amon?
 
Aliyeshindwa kihalali ni Kiwia tu, Wenje alikuwa amepiga mtu alichokosea Wenje ni kukubali kuhesabu kura kwa kutumia masanduku ambayo yalilala kwa Mulongo (hapo lazima upigwe).

Ni kosa kubwa kurudia kuhesabia kura.The best thing ni kutumia karatasi za mawakala
 
Ni kosa kubwa kurudia kuhesabia kura.The best thing ni kutumia karatasi za mawakala
Hicho ndo kimemgharimu Wenje na wengine wengi ambao tunawasikia wanalia kama Ngurumo naye kwa Prof. Milioni 10 ya Mboga.
 
wakuu ktk majimbo mengi yaliyowekewa pingamizi baada ya uchaguzi mkuu oct.25 kuna taarifa za majimbo mawili kesi zinaendelea,kuhusu majimbo mengine taarifa zake kwa alienazo wakuu tuwekeeni hapa jamvini,ila majimbo ya rungwe na kwa kafulila kesi zinaendelea mahakamani
 
taarifa zilizopo ni kwamba kesi ya kupinga matokeo yaliyompa ushindi s h Amon mahakama imeamuru uhakiki wa kura kwa kutumia fomu namba 21B mbele ya mawakili wa pande zote mbili,zoezi lilianza jana na linaendelea kwa fomu zote za vituo zaidi ya 400!ni wakati wa kusubiri wana rungwe kujua yupi ndie anastahili kuwa mbunge wenu
 
Back
Top Bottom