Ruby Ruby, nini hiki unafanya?

STUNTER

JF-Expert Member
Dec 15, 2015
13,075
17,237
Mwanzo ulivyojing'atua clouds watu tulikupongeza sana kwa kukuona jasiri,
ila kipindi hiko hiko ukatoa diss track kwenda kwa clouds iitwayo Wale Wale,
Ok, tukasema labda umeamua kujiponya nafsi kwa kulitema dukuduku lililokusakama rohoni,

Hayo yakapita na maisha yakaendelea.
Chakushangaza leo umetoa wimbo mpya uitwao 'KWI KWI' ambao kwa mwenye akili timamu akiuskiza atajua waziwazi kwamba ni Disstrack nyengine kwa clouds hasahasa Boss wao Ruge,

Huu ujio wako kusema kweli umenidissapoint sana,
nilitegemea umewamwaga clouds na utaendelea na maisha mengine lakini kwa jinsi mchezo unavyokwenda unaonyesha Inferiority ya wazi wazi kabisaaa,
Ruby umekosa msimamo, unawaaibisha watu waliokukingia vifua,

unawaaibisha wanawake wenzako kwa ujumla, yani unareact kama mwanamke aliyepewa talaka kuutwaa mafumbo, Ina maana Ruge Mutahaba ndio anakutia jamba-jamba mpaka unakosa utulivu kabisa?
Na sitoshangaa kesho nikaskia umekwenda kuwapigia magoti Clouds,
shame on you.!
 
Walikuwa na ukaribu sana na ruge naamin ruge alimla maana kuna watu wanaamin ili mwanmke akazin akuheshim lzma umle. Nilikuwa nawaona sana wakingozana wakat ule so lbda rubby ana zaid ya hilo
 
Walikuwa na ukaribu sana na ruge naamin ruge alimla maana kuna watu wanaamin ili mwanmke akazin akuheshim lzma umle. Nilikuwa nawaona sana wakingozana wakat ule so lbda rubby ana zaid ya hilo
Haha, kumbe??
 
Fresh tu Acha awachane.

Sugu na wenzie waliimba zaidi ya nyimbo 30 zote za kuwachana Ruge na Clouds media.

Huyo ndio kwanza mbili unalalamika....namshauri aendelee kukaza uzi mpaka zitimie 10.
 
Fresh tu Acha awachane.

Sugu na wenzie waliimba zaidi ya nyimbo 30 zote za kuwachana Ruge na Clouds media.

Huyo ndio kwanza mbili unalalamika....namshauri aendelee kukaza uzi mpaka zitimie 10.
Tatizo ni kuwadiss watu wasiokuwa na muda na wewe, matokeo yake anaishia kuumiza moyo wake bure..
Kama anajichoresha ki-design flani hivi...
Bora angekausha akapiga mzigo kama Jide alivyoamua kufanya mpaka Leo anafanya vizuri..
Akiwekeza kwenye kudiss hatofika mbali kwani muda mwingi ataishi na donda ndugu lisilopona na maadui zake watajua anaumia, wataishia kufurahi tu.
 
Ye anawakilisha ujumbe wake, sasa Clouds hawana muda nae vipi, au ulitaka na wao waimbe wimbo wa kumjibu Ruby?
 
Back
Top Bottom