DOKEZO RTO Rukwa akwamisha masomo ya madereva wa mabasi na malori

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Husika na kichwa hapo juu,
Mimi ni dereva wa mabasi ya abiria Mkoa wa Rukwa. Nimeshindwa ku-renew leseni yangu kutokana na kukosa cheti cha PSV C PLAIN.

Hivyo, nilipata taarifa kuwa Chuo cha VETA Mpanda kimekuja Rukwa kutoa mafunzo ya udereva wa Public Service Vehicles (PSV) na Heavy Duty Vehicles (HDV). Nikalipa ada na kusoma kwa takribani wiki 4 hadi 5.

RTO Rukwa alihitimisha mafunzo kwa kutoa mafunzo ya usalama barabarani, baada ya hapo tukapewa mtihani. Katika watu 92 wa PSV, walifaulu 31 na mimi nikiwemo. Hata hivyo, RTO aligoma kuendeleza mchakato wa mtihani wa vitendo (practical test) kuanzia mwezi wa tisa 2025 hadi sasa, tarehe 29 Januari 2026, takribani miezi 6.

Baada ya kuhangaika bila mafanikio, tukaona twende Mkoa wa Katavi, kilipo chuo, kufanya practical test ya kuendesha ili tupate vyeti. Ila kilichotokea ni kwamba:

RTO Rukwa alipiga simu Mpanda ili tusisaidiwe kwa sababu anazozijua yeye. Na kweli, wanafunzi wa udereva takribani PSV 92 na HDV 100 walikwamishwa. Achilia mbali hilo, kuna wengine walizuiwa kufanya mtihani wa nadharia kwa sababu hawakubeba leseni siku ya mtihani.

Naomba kupaziwa sauti: je, Polisi yupo kwa ajili ya kutusaidia au kutuangamiza? Sina kazi kwa muda sasa kwa sababu ya hali hii.

SIHITAJI KUBEBWA KUPATA CHETI. Nimelipa ada, nimesoma, na nimefaulu mtihani wa kuandika, ila RTO amegoma kuendeleza mchakato wa mafunzo kwa sababu zake binafsi, akidai kwamba madereva wa Rukwa wana viburi, hivyo anafanya hivyo ili kutukomesha.

Nimekosa uthibitisho wa kuweka. Naomba mjiridhishe na taarifa hii ili tutendewe haki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…