RT inahitaji maoni yako kuhusu riadha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

RT inahitaji maoni yako kuhusu riadha

Discussion in 'Sports' started by Kibunango, Sep 5, 2008.

 1. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #1
  Sep 5, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Chama cha Riadha Tanzania (RT), limesema baada ya Rais Jakaya Kikwete kusema anataka kusaidia mchezo huo kwa kutafuta kocha wa kigeni, chama hicho kimesema hakitakurupuka badala yake hivi sasa wanakusanya maoni ya wadau mbali mbali kuhusu nini cha kufanya.

  Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa RT, Suleiman Nyambui alisema wao hawawezi kufanya mapendekezo yoyote juu ya kauli ya Rais Kikwete pekee yao, lazima wapate maoni ya wadau mbali mbali wa mchezo huo.

  ''Hili jambo ni la kitaifa na sio RT pekee yao wapange, hapa ni lazima kwanza tukusanye maoni ya wadau wa mchezo kisha tuyajadili, inawezekana tatizo ikawa si kocha, hivyo kupitia maoni hayo tunaweza kupata kitu tofauti na mawazo ya kutafuta kocha,'' alisema Nyambui.

  Alisema kwa sasa kikubwa wanachofanya ni kukusanya maoni ya wadau na watayapeleka katika Kamati ya Ufundi kisha wataitisha kikao cha Kamati ya Utendaji kujadili mapendekezo hayo.

  Alisema baada ya kupitisha mapendekezo hayo ndipo watakutana na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo kwa mambo mengine zaidi.

  Source: Majira
   
 2. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #2
  Sep 6, 2008
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Ni hatua nzuri waliyochukua. Hata hivyo ni muhimu watoe maelezo kuhusiana na Waziri wa michezo kubaki huko China kwa wiki mbili zote... alikuwa anafanya nini na ni kiwango gani cha pesa kilitumika kumu-accomodate huko?

  Kingine ni kwamba, je walienda na malengo gani katika upataji wa medali? waliweka kigezo chochote au hawakuwa na target yoyote?... kila kitu kwenye mambo kama haya lazima pawe na target, kama hawakuwa nayo walienda kufanya nini sasa huko Beijing tena wakisindikizwa na Mh. Waziri?

  Uwajibikaji ndicho kilio changu hapa. Makosa mengi yanafanyika hapa nchini na utatuzi wake unakuwa kuunda tume tu, ambapo wala hatuoni mabadiliko. Katika michezo napo lazima tuulize....kama kulikuwa na target ya medali kabla ya kwenda Beijing kwanini target hiyo haikufikiwa? Na kama haikufikiwa nani amewajibishwa kwa makosa yaliyosababisha kutofikia target hiyo? Kama hatukuwa na target kwanini tulijihangaisha kwenda kujumuika huko... (maana tungeliweza kabisa kupeleka mtu mmoja au wawili tu wa kupeperusha bendera na siyo msululu wa watu wasio na malengo wakiongozwa na waziri).

  Nang'ang'ania hili swala la uwajibikaji maana kuna mifano hai ya kuigwa. Na ndiyo maana wenzetu wanaendelea. Huko Uingereza kiongozi wa michezo ameachishwa kazi baada ya wanariadha kushindwa kufikia target yao ya medali 5.... medali walizopata ni nne tu!!! Siye ni sifuri 0000 na bado watu wanapeta!! Inakera kwa kweli. Tafadhali someni kwenye link ifuatayo kuona wenzetu walivyo serious na maswala yao: http://www.timesonline.co.uk/tol/sport/more_sport/athletics/article4653228.ece

  SteveD.
   
 3. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #3
  Sep 8, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Maoni yanazidi kutolewa......

  JK aelezwe ukweli, tatizo la riadha Tanzania si kocha  MCHEZO wa riadha una historia ya pekee hapa nchini kutokana na rekodi yake ya kufanya vema kimataifa na hivyo kuiweka Tanzania katika ramani ya kimataifa.

  Hivi karibuni Tanzania ilishiriki michezo mikubwa kabisa duniani ya Olimpiki, ambako katika timu hiyo ilikuwa na wanariadha wanane na waogeleaji wawili, lakini haikuweza kufanya vema na hivyo kurejea mikono mitupu.

  Kufanya vibaya huko kwa Tanzania, hususan kwa wanariadha ambao Watanzania walikuwa wakiwapa upatu mkubwa wa kurejea na medali, kulitokana na mambo mengi ambayo kimsingi huwezi kuyagundua mapema.

  Nikiwa kama, mdau mkubwa wa riadha na mwenye utaalamu kwa mtazam o wangu Tanzania ilifanya makosa kadhaa yaliyochangia kwa namna moja ama nyingine kupata matokeo tuliyoyapata.

  Moja maandalizi yalikuwa duni, mfano kambi ambayo tulikuwa tukiambiwa kuwa ilikuwa jijini Arusha, huwezi kusema ni kambi kwani ni kama wachezaji walikuwa majumbani, hususan wengi wao walikuwa ni wakazi wa mjini Arusha, ambako mara nyingi walikuwa wakikaa majumbani mwao na kuendelea na shughuli zao mbalimbali, na kutokea wakati wa mazoezi tu.

  Hapo ilitakiwa wangetengwa kwa kuweka kambi nje ya jijini la Arusha, kama vile Karatu, Babati, Moshi na kwingineko.

  Pili kiufundi, kilichochangia wanariadha kutofanya vema katika michezo hiyo hasa wale wa mbio zaa Uwanjani, ni namna ya maandalizi vilevile ambako, huwezi kufanyia mazoezi uwanja wa vumbi halafu ukaenda kukimbia kwenye uwanja wa kisasa wenye zulia maalumu ‘Tartan’.

  Sasa nini tufanye ili tufike ambako tunataka, kikubwa ni uwezeshwaji ili kuhakikisha programu za kifundi zilizopangwa zinafanikiwa.

  Pia suala la viwango kwa wachezaji wetu, linabidi liangaliwe kwa undani zaidi, kwani viongozi wahusika wa Tanzania hawafanyi ipasavyo.

  Zoezi hili hapa nchini linasimamiwa na Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), ambako mchezaji akifikia kiwango tu, anahakikishiwa asilimia 100 kushiriki. Mfano wachezaji wengi waliokuwa katika timu walifikia viwango kati ya Juni 28 mwaka jana na Julai 28 mwaka huu, huku wale wa Marathoni wakiwa wamefikia viwango mwaka jana.

  Kutokana na hilo, tumekuwa hatuna programu endelevu mara wachezaji wanapofikia viwango. Kigezo cha kufikia tu kiwango na kupewa nafasi ya kushiriki si muhimu sana bali ni sehemu ya mchezaji kuelekea kushiriki. Wahusika hawakai chini kutafakari baada ya mchezaji kufikia kiwango.

  Tatizo jingine ni viongozi kutokuwa na uongozin wa pamoja, bali matabaka kutawala. Kumekuwa na samaki wakubwa na wadogo. Tuache hizi hadithi za majina za akina Nyambui, Bayi, Ikangaa na mengineyo. Hatuko katika kukuza majina.

  Utasikia enzi zetu sisi, tulikuwa hivi, mbona watu hao ndio watawala hivi sasa na hawaleti hizo enzi zao?.

  Hivi karibuni Rais Jakaya Kikwete aliatangaza azma yake ya kujikita katika kuuinua mchezo wa Riadha. Hapa napenda Mheshimiwa Rais aelezwe ukweli na wahusika. Mchezo wa riadha hapa nchini hauna tatizo la makocha.

  Mfano Tanzania tuna makocha wa hali ya juu, ‘First Class’ wengi, wako akina Filbert Bayi, yupo Tupa ambaye ni daraja la kwanza na yuko nje nchi akifanya kazi hiyo, wakiwamo akina Mosi Ally, Begashe ambaye ana ‘Masters’ ya riadha, Suleiman Nyambui ambaye ameishafanya kazi hiyo nchini Marekani na Barhain, kina Juma Ikangaa na wengineo, hivyo suala la kocha si tatizo za riadha Tanzania, bali uwezeshwaji.

  Tunahitaji serikali iweke sera safi na kisha Riadha iwezeshwe. Mifano hai Kenya, Ethiopia haina ‘Ma TX’, lakini imepiga hatua katika mchezo wa riadha kutokana na serikali zao kuwekeza kwenye mchezo huo.

  Mfano Mkoa wa Manyara, ndio unaoongoza kuwa na bajeti kubwa katika upande wa michezo, lakini je inasaidia vilivyo michezo. Serikali ndio mitaa, sasa kama halmashauri hazitekelezi sera ya michezo, maendeleo kutoka ngazi za chini yatatoka wapi.

  Wahusika wamshauri rais, hatuna muundo, sera ya michezo inatekelezwa majukwaani huku vitendo ikiwa ni ndoto.

  Mfano mwingine Chuo cha Michezo Malya, kinazalisha wataalamu wengi, je serikali inajua wanakokwenda, ina takwimu? Serikali ndio wahusika, hivyo inatakiwa ijipange.

  Pia tujiulize je michezo kweli ipo? Zamani kulikuwa na michezo mbalimbali, mfano majeshi yalikuwa na michezo mbalimbali, lakini hebu jiulize michezo ya Jeshi la Polisi iko wapi hivi sasa? Magereza nao lini wameendesha mashindano yao.

  Zamani majeshi haya yalikuwa na michezo yake hiyo, ambayo ilikuwa ikiibua nyota kadhaa ambao walikuwa wakiwekwa Chuo cha Polisi Moshi na kuendelezwa na baadhi yao waliibuka na kulitangaza vema taifa.

  Mfano, wanariadha wengi wanaoing’arisha Kenya ni wanajeshi, hivyo uwepo wa sera na muundo makini katika michezo, Tanzania itarejea katika ramani yake ya kutesa katika medani ya michezo kimataifa.

  Kwa mtazamo wangu, Rais aelezwe ukweli katika kuelekea kusaidia mchezo wa riadha hapa nchini, lakini suala la kocha si tatizo la mchezo wa riad ha hapa nchini. Na huu ndio mtazamo wangu.

  Source: Tz Daima
   
 4. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #4
  Sep 13, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  RT kuadhimisha Siku ya Michezo kwa mbio

  CHAMA cha Riadha Tanzania (RT), kinatarajiwa kuadhimisha Siku ya Michezo Duniani kwa kuandaa mbio maalumu zitakazofanyika kuanzia Septemba 19 hadi Septemba 21 mwaka huu.

  Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa RT, Mujaya Suleiman Nyambui, alisema kuwa, mbio hizo zitafanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

  Nyambui alisema kuwa, ni kawaida kwa wanamichezo wote duniani, kufanya maandalizi kabla ya kilele cha maadhimisho, hivyo wameamua kufanya maandalizi kwa mbio hizo maalumu.

  Alisema kuwa, kila mwaka Septemba 21, ni siku ya michezo Duniani, ambako wanamichezo wanaadhimisha siku hiyo kwa kushiriki michezo mbalimbali, ambako kwa riadha watakimbia umbali tofauti, kuruka vihunzi, kurusha mkuki, kisahani na mingineyo.


  Source: TZ Daima
   
 5. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #5
  Sep 13, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Wanariadha kuweka kambi Arusha, Moshi


  KATIKA kuhakikisha timu ya Tanzania inafanya vema katika mashindano ya riadha ya dunia yajulikanayo kama ‘Greatest Race on Earth’ (GROE), 2008/09, Benki ya Standard Chartered imetoa sh 6,420,000 kwa ajili ya maandalizi ya timu hiyo.

  Ofisa Mtendaji wa benki hiyo, Hemed Shah, alisema jijini Dar es Salaam jana, katika hafla ya kukabidhi hundi ya fedha hizo kwa Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha Tanzania (RT), Suleiman Nyambui kwamba, fedha hizo ni kwa ajili ya kuweka kambi kwa timu ya Tanzania, itakayokuwa mkoani Arusha na mji wa Moshi kwa kushirikisha wanariadha nane.

  Shah alisema, benki hiyo imekuwa ikisaidia wakimbiaji wa Tanzania kila mwaka, lengo ikiwa ni kuhakikisha wanafanya vizuri katika mashindano wanayoshiriki na hivyo kuiletea sifa nchi.

  Kwa upande wake, Nyambui aliishukuru benki hiyo kwa kusaidia kuinua mchezo huo, kutokana na fedha hizo za maandalizi na kuomba makampuni mengine kujitokeza kusaidia.

  Mbio hizo za dunia, zimepangwa kufanyika katika nchi mbalimbali, ambako zaidi ya nchi 600 duniani zitashiriki na mshindi kujinyakulia dola milioni moja za Kimarekani, huku benki hiyo ikidhamini mashindano hayo kwa miaka mitano sasa.

  Mbio za kwanza zitafanyika Nairobi, Kenya Oktoba 26 mwaka huu, kabla ya nyingine kufanyika Singapore, Desemba 7 mwaka huu, huku Januari 18 mwakani zitafanyika Mumbai, India na mbio za mwisho zitarindima Februari 8 mwakani huko Hong Kong.

  Wanariadha wa Tanzania na sehemu watakazoshiriki ni Melkiadi Bino Bayo, Flora Charles Kagali, (Nairobi), Paul Marmo Sumaye, Tea Anthony Mushi (Singapore), Jumanne Boki Tluway, Sarah Maja Selli (Mumbai), Andrea Silvin Mathiya na Banuelia Brighton Katesigwa (Hongkong).

  Source: TZ daima


  Btw.. Nijuavyo duniani kuna nchi 195 na Zenj ikimwemo humo...:D sasa nchi 600 zipo katika dunia gani?
   
 6. Shedafa

  Shedafa JF-Expert Member

  #6
  Sep 14, 2008
  Joined: May 21, 2008
  Messages: 802
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Nami naungana na wachangiaji waliotangulia kuwa tatiza la riadha Tz si kocha, ingawa kuwa na kocha mwenye utaalamu wake kunaweza kuinua kwa kiasi fulani kiwango. Tatizo tulilonalo kwenye riadha ni tatizo hilo hilo kwenye michezo yote, kwa nchi changa kama yetu hatujafikia kiwango cha kutengeneza wachezaji, wenzetu mchezaji huyo huyo anaweza kushughulikiwa mapaka akafikia viwango, tunategemea vipaji. Wakati huo huo wigo wetu wa kupata wachezaji umekuwa finyu kuliko ulivyokuwa miaka ya 70, ingawa idadi yetu ni kubwa mara dufu kuliko ilivyokuwa miaka ya 70. Si wote wenye vipaji wanaojijua kuwa wana vipaji, wengine ni mpaka waambiwe na watu wengine. Lakini wataambiwaje wasipoonekana?, tulionao sasa hivi ni aidha wamependa kuwa wanamichezo au wameishi karibu na wanamichezo nao wakapenda au wamekuwa vinara toka ktk idadi ndogo ya wale walionekana kwa hivyo inakuwa vigumu kupata wenye kufikia viwango vya juu vya kimataifa. Zamani kulikuwa na mashindano mashuleni, kwenye mashirika, taasisi za umma n.k. Hata kama mtu alikuwa hajijui kuwa anakipaji wanaomuona, wanamwambia na kumtia moyo kuwa akijitahidi ataweza. Je? hawa tulionao sasa hivi wanapatikanaje?, ni kweli hawa ndio bora zaidi?. Kwa hali inavyoenda hovyo sasa hivi inawezekana hatuna tena utaratibu utakaotuwezesha kugundua vipaji na kuvitia moyo, kwa mawazo yangu ni mpaka pale tutakapoweza kupanua wigo wa kupata wanamichezo ndio ndoto zetu zinaweza kurudi ktk mafanikio ya miaka ya 70 au hata kuendelea. Hii iwe riadha, soka, ngumi na michezo mingine.
   
 7. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #7
  Sep 17, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  MWANARIADHA wa Tanzania, Dickson Marwa alikumbushwa machungu ya michezo ya Olimpiki baada ya kujikwaa na kuanguka na kisha kumaliza katika nafasi ya 11 ya mbio za nusu marathon zilizofanyika mjini hapa.

  Marwa, ambaye alionyesha kila dalili kuwa angefanya vizuri alijkwaa katika mbio hizo zmbazo washindi wake ni Wakenya, Patrick Makau Musyoki kwa wanaume na Lydia Cheromei,


  Mbio hizo zilidhaminiwa na Shirikisho la Riadha la Kimataifa (IAAF).


  Mbio hizo kwa upande wa wanaume zilikuwa kivutio tangu mwanzo hadi mwisho, baada ya Makau kutimka kwa kasi na kumpita Mkenya mwenzake, Evans Cheruiyot, ingawa wote walimaliza kwa muda wa 59:29, wakati kwa upande wa wanawake, Lydia Cheromei hakuwa na mpinzani.


  Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 31 alimaliza kwa muda bora na rekodi mpya wa 68:35. Muda bora ambao pia ulikuwa wa kwake, aliposhinda kwa mara ya kwanza mbio hizo, Septemba 12, 2004 ulikuwa 69:13.


  Kivutio zaidi kilikuwa ni washiriki watano kwa upande wa wanaume walioweza kumaliza chini ya muda wa sekunde 60.00. Baada ya kilometa 10, Joseph Maregu aliongeza kasi na kuwapita wenzaket. Kufikia kilometa 13, Makau aliyekuwa amejificha katika kundi lao alichukua uongozi wa wenzake 14 .


  Hadi kufikia kilometa 15, Wilson Chebet, aliongeza kasi na kuwapita wnezake huku muda ukionyesha kuwa 42:41/42:42. Hapo, ndipo Dickson Marwa Mkami, alipojikwaa na kuanguka, kiasi cha kuachwa.


  Waliomaliza katika nafasi za juu tano ni, Makau Musyoki, Evans Cheruiyot, Chebet, Paul Kosgei na Charles Munyeki.


  Bingwa wa mwaka jana, Cheruiyot alitumia muda wa 59:12 huku Musyoki akiwa nyuma yake kwa sekunde tano, lakini mwaka huu, hakukuwa na tofauti baada ya wote kumaliza kwa muda wa 59:29.


  Lakini, Makau Musyoki, akitangazwa bingwa kwa kutumia muda bora zaidi. Pia, ni mshindi wa mbio za nusu marathon za Ras al Khaimah, Reading, The Hague (Fortis City-Pier-City) na Berlin.

  Source: Mwananchi
   
 8. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #8
  Sep 17, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  ^^ MMhm kaazi kweli kweli, hebu soma vizuri maoni ya waliotangulia na hasa kuhusu makocha, then ujadili
   
 9. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #9
  Sep 17, 2008
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Sisi tunahitaji chakula cha kutosha mezani kwa wananchi wetu kwanza.Hatuwezi kula michezo.Hayo Mungu atatusaidia kuyafanya baadae.Lakini tushibe kwanza.
   
 10. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #10
  Sep 17, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  ^^ Kamanda unataka serikali ikuwekee chakula mezani sio?
   
 11. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #11
  Sep 17, 2008
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Maana yangu ni kwamba, 'priorities' za serikali ziko 'distorted'.Tunataka ifanye kwanza yale mambo ambayo yatafanya maisha ya wananchi wetu yawe bora .Hizo blaa blaa za michezo baadaye,hatukatai, lakini sio muhimu sana kwa sasa.
   
 12. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #12
  Sep 17, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Wanamichezo ni sehemu ya jamii, na ni sehemu ya ajila vilevile. Kama ni kuboresha sekta zote, sioni mantiki yako kwa nini wanamichezo wawekwe kando.
   
 13. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #13
  Sep 17, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Udhaifu wa viongozi unaua michezo

  Ibrahim Mkamba Septemba 17, 2008

  LEO natanguliza kwenu wasomaji wa safu hii ombi la msamaha kwa kuanza na maelezo yanayoonekana hayahusiani na michezo.Naomba uvumilivu wenu, tutaelewana tu.Viongozi wetu wengi wa sasa ni dhaifu wa kuzidi kiwango.Hebu tazama udhaifu wa mmoja wao.

  Anatetemeshwa kidogo na maandamano ya vitoto vyetu vya shule ya msingi na sekondari kuhusu suala la ongezeko la nauli ya daladala toka shilingi 50/= kwenda 100/= anavipooza vitoto hivyo kwa kuvipa ukubwa wa kukaa kwenye viti vya mabasi vikishalipa hiyo shilingi 100/= vinavyopewa na watu wanaolingana na wale wanaovigomea viti kwenye mabasi!

  Matokeo yake, zaidi ya uhasama wa makondakta wa daladala na wanafunzi, umezuka uhasama mwingine wa ndani kwa ndani baina ya wanafunzi hao na watu wazima unaodhihirishwa na wao (watu wazima) kuacha kuwa watetezi wa wanafunzi pale wanaponyanyaswa na makondakta, tofauti na ilivyokuwa wakati maadili ndani ya daladala yalipokuwa yanaheshimiwa kwa wakubwa pekee kukaa vitini.

  Miongoni mwa watu wazima wanaonyimwa viti kwenye mabasi na vitoto ni wazee sana, kina mama wajawazito na wanaobeba watoto pamoja na wagonjwa.Watu kama hao wakiachiwa viti kwenye mabasi,wanaofanya hivyo ni wakubwa waliopata viti lakini si vitoto vyetu vinavyokaa,vilivyosababishwa na viongozi wetu dhaifu visiwe na adabu.Viongozi wetu hao wanaosahau hata maadili yetu kwa udhaifu wao huo uliopitiliza!

  Sababu ya kuanza na maelezo hayo ni kuonyesha wazi kuwa, kwa aina ya viongozi dhaifu kama hawa, tusitegemee ikawekwa mikakati madhubuti ya kuinua michezo yetu na ikitokea mikakati hiyo ikawapo,viongozi dhaifu kama hawa hawawezi kusimamia na kuhimiza utekelezaji wake. Kama kiongozi anatishwa na vitoto, anagwaya na kuviambia vikae kwenye viti vya mabasi na wazazi wao wasimame,ataweza kweli kuchachamalia viongozi wa chini yake walioharibu mipango ya maendeleo ya michezo?

  Hoja hii imenijia kichwani baada ya kusikia majibu ya jeuri ya walioiongoza timu yetu ya Olimpiki, Beijing, China, ya viongozi wa Kamati ya Olimpiki nchini(TOC) na ya viongozi wa Chama cha Riadha nchini (RT) kila walipohojiwa kuhusu matokeo mabovu mno kwenye mashindano hayo.

  Viongozi hao walikuwa jeuri hivyo kwa kujua kuwa hakuna kiongozi yeyote wa Serikali juu yao angechachamalia madudu yao kwa kuutambua udhaifu wa viongozi wetu. Udhaifu huo katika suala hilo ulijionyesha katika kikao cha Bunge kilichopita, pale kiongozi mmoja wa serikali alipolieleza Bunge kuwa matokeo mabaya tuliyoyapata Beijing hayakuwa ya aibu kwa Taifa! Kama huyo anayetarajiwa kuwajia juu waliovurunda katika maandalizi na mipango mingine ya ushiriki huo anautangazia umma kwamba matokeo hayo hayakuwa ya aibu, haishangazi mahojiano kati ya wanahabari na wavurundaji hao yaonekana kama wanahabari ndio waliokuwa wanahojiwa kutokana na kiburi cha wavurundaji hao!

  Mwanahabari atauliza,"kwa nini tumefanya vibaya namna hii?" Mvurundaji atasema,"Kwani ni Tanzania peke yake imekosa medali katika mashindano hayo?" Atajibiwa na Mwanahabari,"yapo mataifa mengine yamekosa medali lakini kuna yaliyopata,kwa nini nasi tusipate?" Mvurundaji huyo atasema "Sisi tulipeleka wanariadha wangapi na hao waliopata medali nyingi walipeleka wanariadha wangapi?"

  Mwanahabari atapuuza swali hilo kwa kusema"lakini hayo ya wengine hayatuhusu, ninakuuliza kuhusu matokeo mabaya ya timu yetu inayotuhusu". Mvurundaji atasema zaidi,"Nani anasema matokeo hayo ni mabaya?" na mazungumzo ya swali-kwa-swali yanaendelea hivyo bila kujulikana anayetakiwa kujibu maswali ni nani kati ya Mwanahabari na Mvurundaji huyo anayeonekana kutojutia kuharibu kazi ya Watanzania! Jeuri.Kwa nini asifanye jeuri wakati anajua hakuna wa juu yake wa kumpa kashkash?

  Ili nchi yoyote iendelee kimichezo inapaswa iwe na sera nzuri za kuwatengeneza wanamichezo wa michezo mbalimbali tangu wakiwa wadogo, ziwe za klabu au za kiserikali kutegemeana na tofauti za nchi kiuchumi, kiutamaduni na kijamii.Vile vile,inapaswa itengeneze majukwaa ya kuvionyesha na kuviimarisha vipaji hivyo kama mashindano ya UMISHUMTA(baadaye UMITASHUMTA), UMISSETA, michezo ya majeshi na SHIMIWI yaliyokuwapo zamani.

  Tuko chini sana kimichezo kwa sababu, kwa sasa, tumekosa yote hayo. Ninaposema viongozi imara ndiyo msingi mkuu wa mafanikio kimichezo ninamaanisha kwamba sera nzuri za kutengeneza wanamichezo zitatengenezwa na kutekelezwa kiuhakika chini ya uongozi imara. Majukwaa ya kuonyesha na kuinua vipaji, yatajengwa chini ya uongozi imara. Maaandalizi ya uhakika ya mashindano nayo yatafanikishwa chini ya uongozi imara na inapotokea waliopewa dhamana ya kusimamia ushiriki wa mashindano ya kimataifa wakavurunda, uongozi imara huchukua hatua kali kwa watu hao ili wao au wengine wasirudie kuboronga siku za usoni.

  Kwa udhaifu wa viongozi wetu, nani ndani ya TOC na RT ametetemeshwa kutokana na matokeo mabaya ya Beijing na hivyo atazamiwe kujiweka sawa kuanzia sasa asivurunde tena London mwaka 2012? Kwani hata mwaka huo akiwa madarakani na akivurunda tena nani atamfanya nini cha kumtisha!

  Wenzetu wanaojali hawafumbii macho ujinga ujinga.Kwa mfano,baada ya timu ya soka ya Express ya Uganda kufungwa na Yanga ya Tanzania magoli 4-0 kwenye mashindano ya klabu bingwa ya Afrika Mashariki na ya Kati, Zanzibar mwaka 1975, aliyekuwa Rais wa Uganda wakati huo, dikteta Idd Amin Dada, aliamuru msafara mzima wa timu hiyo ulioshiriki mashindano hayo, isipokuwa wachezaji ambao hawakucheza mechi hiyo,upewe adhabu ya viboko vinne kila mmoja, idadi ya magoli waliyofungwa na Yanga.Walichapwa idadi hiyo ya viboko hadharani! Hata kama Idd Amin alizidisha kiwango, lakini hivyo ndivyo anavyopaswa kutendewa aliyeharibu kazi ya nchi hata kama si viboko vya hadharani.

  Kama viongozi wetu wasingekuwa dhaifu kiasi cha kuwagwaya watoto wetu na kuwaelekeza wawavunjie heshima wakubwa kwenye mabasi ya daladala,wangewasimamia vizuri Maafisa Utamaduni na Michezo katika kuwekwa kwa mikakati ya kuendeleza michezo kwenye maeneo yao ya uongozi badala ya kusubiri mafanikio yanayoletwa na wadau tofauti na kuwa mbele kwenye shamra shamra za kushangilia mafanikio hayo na kuyatangaza kuwa ni matokeo ya sera nzuri za michezo za serikali ya chama cha siasa kinachotawala. Si tuliona jinsi sera za CCM zilivyohusishwa na ushindi wa Big Brother Africa 2(BBA2) wa Mtanzania Richard Bezuidenhout mwaka jana mwishoni?

  Ni vizuri viongozi wetu wa leo wangejifunza toka kwa Dk.Lawrence Gama na Abubakar Mgumia walioshughulikia sana maendeleo ya michezo katika kila mkoa walioongoza kama wakuu wa mikoa.Waliagiza utekelezaji,waliukagua na kukosoa utekelezaji huo,wakiwawajibisha wazembe na matokeo yake yakawa mazuri kimichezo kwenye mikoa hiyo iliyokuwa nyuma kimichezo kama Ruvuma na Tabora kwa Dk Gama na Lindi na Kigoma kwa Mgumia.

  Wanachopaswa kufanya viongozi wetu wa sasa ni kuwabana kweli kweli Maafisa Utamaduni na Michezo,kama walivyofanya viongozi makini waliotajwa,wawape mipango yao ya kuendeleza michezo.Mipango hiyo iwe madhubuti na waonyeshwe utekelezaji wake.Wote wakifanya hivyo, si kwa kucheka cheka, lazima tutakwenda juu kimichezo.

  Litakuwa jambo jema sana pia endapo viongozi wetu wa sasa watajifunza mbinu za uongozi za wenzao wa awamu ya kwanza ambao kila mmoja alikuwa imara katika kutimiza wajibu aliopewa ambapo kwenye michezo kina Jenerali Mirisho Sarakikya,Chediel Mgonja na wengine walisimamia vizuri na kwa nguvu maendeleo ya michezo na matokeo yake nchi yetu ilikuwa juu sana kimichezo. Ni katika awamu hiyo ndiyo kulikuwa na majukwaa ya UMISHUMTA, UMISSETA, Michezo ya Majeshi na kadhalika. Viongozi wetu wa leo wangekuwa na mipango mizuri kama wao,tungekuwa hata na mashindano ya michezo ya vyuo vya elimu ya juu,ikizingatiwa wingi wa vyuo hivyo kwa sasa na umri mdogo,wa kimichezo, wa wanaoingia vyuoni humo miaka hii.

  Kutokana na mipango ya kisayansi ya viongozi wa zamani na usimamizi wao madhubuti,mwaka 1974 tulibeba makombe yote ya soka kwa ukanda wa Afrika Mashariki na ya Kati. Januari: Simba ya kina Abdallah "King" Kibaden, bingwa Afrika Mashariki, Dar es Salaam. Mei: Timu ya vijana, matunda ya UMISSETA, ya kina Mwinda Ramadhani "Maajabu", bingwa wa Afrika Mashariki, Kampala.

  Oktoba: Timu ya Taifa ya wakubwa, chini ya kocha Marijan Shaaban,bingwa wa Challenge,Dar es Salaam. Kwa mipango mizuri iliyokuwapo,wengi wa wachezaji wa timu hiyo ya wakubwa iliyobeba kombe la Challenge walitoka timu ya vijana, matunda ya UMISSETA.

  Baadhi ni Mwinda, Lucas Nkondola, Jellah Mtagwa, Godfrey Nguruko na wengine. Novemba: Simba ilifika nusu fainali ya klabu bingwa Afrika na kutolewa kwa vitisho na Mehalla el Kubra ya Misri kwa penelti.

  Kwenye michezo mingine, mwaka huo Filbert Bayi alivunja rekodi ya mbio za meta 1500 kwenye mashindano ya Jumuiya ya Madola kule Christchurch, New Zealand na kuleta nchini medali ya dhahabu. Rekodi hiyo ya mbio za meta 1500 ilikuwa ikishikiliwa na mwanariadha John Walker wa New Zealand kwa miaka saba! Kipindi hicho tulikuwa na wanariadha wa kujivunia kama Bayi,Suleiman Nyambui,Claever Kamanya, Juma Ikangaa, Gidamis Shahanga, Nzael Kyomo, Mwinga Mwanjala na wengineo.

  Kulikuwa na wanamasumbwi wazuri kama Titus Simba na Habibu Kinyogoli.Hata michezo mingine inayopondwa sasa ilithaminiwa na ndiyo maana tulikuwa na wachezaji bora kama Zakayo Marekwa kwenye kutupa mkuki na Nancy Mtawali kwenye kutupa kisahani huku mpira wa pete ukawa na timu kali nyingi za kutosha kutengeneza ligi zenye msisimko mkubwa za madaraja hata matatu!

  Litakuwa jambo jema pia endapo viongozi wetu wa sasa watajifunza mbinu za uongozi wa wenzao wa awamu ya kwanza ambao kila mmoja alikuwa imara katika kutimiza wajibu aliopewa kiasi cha nchi kuwa juu sana kimichezo kufikia hatua ya timu yetu ya soka kucheza fainali za mashindano ya mataifa huru (wakati huo) ya Afrika nchini Nigeria mwaka 1980.

  Hayo yalikuwa ni matunda ya kuwa na viongozi imara na wakali kwenye kuhimiza utimizaji wa wajibu kwa kila aliyehusika na utekelezaji fulani wa kimichezo.Bila wengi wa viongozi wetu wa leo kuacha kuwa dhaifu kama walivyo,tusiote ndoto ya kupata maendeleo kimichezo.Sera nzuri za kuibua,kuinua na kutunza vipaji vya wanamichezo haziji zenyewe, ni kazi yetu chini ya viongozi wetu.

  Jukwaa la kuonyeshea na kuimarishia vipaji halijijengi bali hujengwa na viongozi wetu.Maandalizi ya uhakika ya ushiriki wa mashindano hayaji yenyewe, ni kazi yetu chini ya viongozi wetu na kuwakaripia waliovurunda dhamana ya kuongoza timu za mashindano ni kazi ya viongozi wetu.

  Kwa udhaifu wao, nani leo atathubutu kuwaambia TOC na RT "nataka maelezo ya kuridhisha kwa nini msichukuliwe hatua kwa kushindwa kutimiza wajibu wenu"? Kama yupo, afanye hivyo sasa kabla aibu hiyo haijapitwa na wakati.


  Source: raia mwema
   
Loading...