Ndo nani mkuu?Wampige zaiko
“Miziki ya kigodoro ni miziki ambayo ukiangalia namna inavyochezwa na hata washiriki wake ni vijana ambao wanatumia kama sehemu ya maficho kwaajili ya kufanya uhalifu’’ amesema Benedict.
Hata hivyo Kamanda Benedict ameongeza kuwa hakutakuwa na ruhusa yoyote ya kufanya Vigodoro katika eneo lolote na wananchi wanatakiwa kulinda utamaduni kwa njia nzuri na sio miziki inayovunja maadili.
Nadhani unazungumzia vigodoro vilivyo boreshwa ambavyo tunaona matangazo eg "Usiku wa bunyero ndani ya Club X" nk..tafsiri anayo zungumzia RPC ni zile party zisizo rasmi zinazo kesha uswahili..shughuli kama 40 ya mtoto nk! Huenda RPC akawa sahihi kwa kiwango kikubwa tu!Nadhani RPC amekosea... Vigodoro huchezwa ndani ya club au nyumba kubwa za ukumbi au nyumba za watu wakati wa sherehe au kuburudika, mm sioni tatizo hata kidogo, waacheni watu waburudike jamani, kama kuna mtu atafanya uhalifu ndio ashughulikiwe.. Ila vigodoro ni utamaduni wa watu kama vile ngoma zilivyo au Dar kuna singeli.. Hizi ni burudani za watu, ni busara kuwaacha waburudike ila wahalifu washughulikieni..
Kwa hiyo vigodoro ndio uchafu tu.Safi sana kamanda.
Tena mwenye nyumba afungwe kabisa iwe fundisho.
Wafurahi kwa njia zingine lakini sio kwa uchafu huo