DuaZaMama
JF-Expert Member
- Jun 2, 2025
- 1,882
- 4,152
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Richard Abwao, amesema kuwa wananchi wa mkoa huo ndio walinzi wa kwanza wa amani na amewapongeza kwa ushirikiano mzuri na jeshi la polisi, hasa katika kipindi hiki cha kampeni kuelekea uchaguzi mkuu.
Soma pia GE2025 - RPC Marko Chilya: Hakuna anayeweza kuzuia uchaguzi
Akizungumza katika mahojiano kwenye Kipindi cha Jambo Tanzania cha TBC1 leo Septemba 19, 2025, Kamanda Abwao ameeleza kwamba Mkoa wa Tabora uko katika hali ya utulivu, ambapo shughuli za maendeleo zinaendelea kufanyika kwa amani kutokana na utulivu wa wananchi wake.
Kuhusu masuala ya ukatili wa kijinsia, Kamanda Abwao ameeleza kwamba Jeshi la Polisi linaendelea kutoa elimu kwa jamii ili kupunguza au kumaliza kabisa tatizo hilo, na kuongeza kuwa jamii inaendelea kupokea elimu hiyo na kuifanyia kazi ipasavyo.