RPC, OCD wagongana kuhusu CHADEMA

RPC, OCD wagongana kuhusu CHADEMA

Candid Scope

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2010
Posts
11,897
Reaction score
6,933
FFU_at_the_Embassy_500x370.jpg

Picha: Januari 10, 2012 picha ya pamoja Balozi wa Marekani nchini na
wakufunzi wa FFU baada ya kuhitimisha mafunzo
katika ubalozi wa Marekani, Dar es Salaam


CHAMA cha Demokarasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Chato mkoani Geita, kimemshukia Mkuu wa Polisi wilayani humo, Leonard Nyaoga kwa madai kuwa anatumiwa na CCM kutaka kudhoofisha jitihada zao. Tuhuma hizo zimekuja kufuatia OCD huyo kuualifu uongozi wa CHADEMA kwa njia ya simu kuwa amesitisha mikutano yao ya hadhara kwa madai tayari walikwisha kukaa kikao cha pamoja na viongozi wa vyama vya siasa na dini na kukubaliana kuisitisha.


Hata hivyo sababu hizo zilipingwa vikali na CHADEMA kwa madai kuwa katika kikao cha pamoja na jeshi hilo Nevemba 7 mwaka huu, ilizuiliwa mihadhara ya kidini na wala si mikutano ya vyama vya siasa. Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Katibu wa CHADEMA wilaya ya Chato, Mange Ludomya, alisema kitendo cha OCD kuzuia kuendelea na mikutano yao kinaonyesha wazi jinsi anavyoweza kuwa anatumiwa na chama tawala kuwadhoofisha.
"Tunamshangaa sana huyu OCD wetu...sisi tulipeleka barua ya kumtaarifu kuwa tutakuwa na mkutano wa hadhara kwenye kijiji cha Nyarututu kata ya Bwanga Desemab 16 kama sheria inavyotuagiza lakini amenipigia simu ananieleza kuwa mkutano huo usitishwe kwa kuwa tulikubaliana,” alisema.


Kufuatia hali hiyo, Katibu huyo alisisitiza kuwa mikutano ya CHADEMA itafanyika kama kawaida na kama ni nguvu za jeshi la polisi ni bora zikatumika kusaka majambazi wenye silaha zinazoangamiza maisha ya wananchi.


Akizungumza kwa njia ya simu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Leonard Paulo alikana kuwepo kwa zuio hilo na kudai kuwa zuio kama hilo hufanyika kwa maandishi si kwa njia ya simu. Aidha, aliwataka viongozi wa vyama vya siasa kunapotokea mkanganyiko kama huo ni vema wakawasiliana na wenzao ngazi ya mkoa kwa lengo la kumfikia ofisini kwake na kufanya mazungumzo ili kuondoa dosari zinazoweza kujitokeza.
 
Mjasiria tumbo km huyo OCD sijui kwa nini aliumbwa binadamu. Bora angeumbwa Mchicha vijana wakapata Vitamin C
 
Mjasiria tumbo km huyo OCD sijui kwa nini aliumbwa binadamu. Bora angeumbwa Mchicha vijana wakapata Vitamin C

Kuna kitu ambacho kinaonekana kuanza ku-change ndani ya jeshi la polisi ingawa si kwa kasi ila kwa mwendo wa kinyonga.
 
huyo OCD ni dhahiri kuwa anatumiwa kudhoofisha harakati za ukombozi, ni mchumia tumbo tu na huenda hata huo u-ocd amepewa kimagumashi!
Pongezi zangu za dhati zimfikie huyo RPC,HONGERA SANA KAMANDA.
 
Kama kungekuwepo Marpc wengi wenye busara kama za Rpc huyu mauaji yanayofanywa na polisi kwenye mikutano ya Chadema yangeepukwa.
 
Hivi hata kwenye polisi kuna u OCD wa chupi!???? nauliza tu
 
Hivi hata kwenye polisi kuna u OCD wa chupi!???? nauliza tu.........

Upo mkuu sana tena sana kama ulivyo u IGP wa chupi jamaa anakula dada wewe unazawadiwa
 
Kama kungekuwepo Marpc wengi wenye busara kama za Rpc huyu mauaji yanayofanywa na polisi kwenye mikutano ya Chadema yangeepukwa.
RPC huyo kaongea vizuri. Tatizo kesho utasikia karudishwa makao makuu.
 
huyo OCD ni dhahiri kuwa anatumiwa kudhoofisha harakati za ukombozi, ni mchumia tumbo tu na huenda hata huo u-ocd amepewa kimagumashi!
Pongezi zangu za dhati zimfikie huyo RPC,HONGERA SANA KAMANDA.

Tatizo kubwa ni mfumo mbaya wa uongozi ambao hauna check and balance, inabidi amri yeyote ya polisi basi ipitiwe na chombo kingine huru ili kujiridhisha kuwa ni sahihi au ni ya kimagumashi na polisi anapata jeuri hii kwa kuwa anajua kuwa hakuna chombo kingine kitakachom hold accountable kutokana na kauli hiyo.
cha kufanya ni kuwa katika katiba mpya Polisi waendelee kupewa taarifa kuhusu kutoa ulinzi kwenye mikutano na sheria iwalazimishe kufanya hivyo na kama kuna tatizo wanalo hisi linahatarisha usalama basi itabidi waende kwa jaji wa mahakama ya kimkoa ili waweze kumshawishi ili aweze kukubaliana nao kwa kuhalalisha zuio bila hivyo ni kumuachia mhuni mmoja kuamua anachotaka huo ni ukichaa.
 
Unashangaa OCD kutumika na CCM,yawezekana ww hufuatilii matukio muhimu mbona rais alisema mwenyewe kwamba CCM itakwama ikiendelea kutegemea police kwan unadhan alimaanisha nn?
 
Kama kungekuwepo Marpc wengi wenye busara kama za Rpc huyu mauaji yanayofanywa na polisi kwenye mikutano ya Chadema yangeepukwa.
mirembe panakufaa sana. wewe unaona ni mikutano ya chadema tu ndo yenye haki? you are too bias na hufai, nyoka wa mndimu mkubwa wewe.
 
Back
Top Bottom