RPC Mtwara: Wananchi kaeni mkijua ya kwamba hizo vurugu mnazozipanga kesho sisi tumejipanga vilivyo



Kwa kweli na kama tunajali kweli na pia km Serikali inakitakia mema chama chetu kilichopewa ridhaa kwenye uchaguzi (CCM), basi busara, akili na utashi wa hali ya juu ni lazima utumike. Wasi wasi tu ni pale Wassira alipokiri hivi karibuni (akihojiwa juu ya bomu la kanisani Arusha) kuwa wakati mwingine Serikali huchelewa kuchukua maamuzi muafaka kwa wakati. Govt must do something positive to arrest the maturing tension, if it all can!
 
Mmmmmmm? Sasa wanaipiku Arusha?

Nahisi,ili kuwepo kwa ahadi mbalimbali za kuwapa matumaini watu wa kusini zitaendekea kutolewa katika kila Wizara yenye miradi kusini ya nchi;

Mfano Wizara ya ujenzi wanasema kipande cha barabara kilichobaki kitakamilika Disemba mwaka huu,na
Wizara ya Nishati watatoa ahadi zao kama bajeti iliyopita,na

Kubwa zaidi Mtwara inaweza kutangazwa kuwa jiji wakati wa uchaguzi ujao,kwani hata Arusha ilitangazwa jiji,lakini baada ya uchaguzi ikasemekana kwamba vigezo havikukamilika ili wapewe hadhi ya jiji.!!!
 
kama nimemuelewa sawasawa THE BIG SHOW ni kuwa kesho ni Passive resistance ( kwa tafsiri yangu ni "mgomo") hakuna huduma za kijamii usafiri na kadhalika. Wewe hayo maandamano yanatoka wapi ?

MpigaKelele
Uko sahihi,hakuna atakaendamana wala kuleta vurugu,duka langu nina lipa kodi vizuri tuh,nimeamua kesho kutofungua wao wanakimbilia kwenye vyombo vya habari kutangaza wamejipanga,wamejipanga kitu gani??kunilazimisha nifungue au wamejipanga kitu gani??

I will tell you something,sisi ndio waasisi wa hii passive resistance kama utakuwa unakumbuka historia vema,

Mjerumani kuna kipindi alijenga reli huku enz hizo na kuanzisha kilimo cha karanga maeneo ya nachingwea na kanda zingine za kusini,pia alianzisha na kilimo cha pamba pia,lakini wananchi wa huku asilimia kubwa kilimo cha pamba walikuwa hawakitaki na kutumikishwa tuh kwa ujumla walikuwa hawapendi,mjerumani msimu ulivyofika alivyokuja kuwaambia watu waandae mashamba,watu hawakupinga,walilima vizur na kuandaa mashamba,ilipofikia kipindi cha kupanda mjerumani alipogawa mbegu za pamba wananchi walizichukua na kwenda kuzichemsha hadi zikatokota kisha kesho yake wakaenda kuzipanda tena kwa ustadi wa hali ya juu sana,wajerumani wakashangaa sana,yani hawa jamaa wanalima,wanapanda bila kushurutishwa bila bakora??

Kivumbi sasa kikaanza miez ilivyoanza kukatika miche haichomozi,hadi kikafikia kipindi cha kuanza kutengeneza maua ardhi kimyaaa,haitoi chochote,walichofanya wajerumani ni kujaribu kuchimba baadhi ya mbegu na kwenda kuzipima ili waone kama zina hitilafu ama la,walichokiona hawakuamin macho yao..!,kumbe wale washenz hizi mbegu walizichemsha kwa makusudi??

Msimu umeisha na wao wameshapata hasara..!

Hiyo ndiyo passive resistance mkuu,wamakonde wana msemo mmoja unasema ya kwamba TUKOSE WOTE..!

Usifanye mchezo na wamakonde mpiga kelele,tumevurugwa sana..!!
 
Last edited by a moderator:


Kwa kweli na kama tunajali kweli na pia km Serikali inakitakia mema chama chetu kilichopewa ridhaa kwenye uchaguzi (CCM), basi busara, akili na utashi wa hali ya juu ni lazima utumike. Wasi wasi tu ni pale Wassira alipokiri hivi karibuni (akihojiwa juu ya bomu la kanisani Arusha) kuwa wakati mwingine Serikali huchelewa kuchukua maamuzi muafaka kwa wakati. Govt must do something positive to arrest the maturing tension, if it all can!
 
kwa hiyo heshima ni kuwaua raia wanaodai haki zao?
 
We are tired of that slogan we need action and not trailer everyday bana. BIG SHOW tell em to kick the RPC ass kufa uku unarusha ngumi kuluko unauliwa uku umepiga magoti tunataka li move tumechoka na trailer
 
I hope upepo utapita bila ya kuitaja Chadema kama chanzo huko Mtarwara.
 

Acha ujinga wewe! tena kwa namna ulivyoandika kishabiki,inaelekea wewe ndio unayesambaza vipeperushi vya uchochezi! watu wakijeruhiwa au kuuana we unapata faida gani! Basi ukae mbele kabisa ktk maandamano hayo sio kwenye laptop eboo!
 
Acha ujinga wewe! tena kwa namna ulivyoandika kishabiki,inaelekea wewe ndio unayesambaza vipeperushi vya uchochezi! watu wakijeruhiwa au kuuana we unapata faida gani! Basi ukae mbele kabisa ktk maandamano hayo sio kwenye laptop eboo!


Vp mbona mapovu mengi saana??
Nani kakuambia wananchi wamehasishwa kufanya fujo??umesoma kwanza au umekurupuka??
Au una 10 percent za wazee wako unazozitetea??
Kukaa nyumbani na kufanya shughuli zao za kawaida nazo ni fujo?
Pole sana,lakini kazi mtaijua mwka huu,kila kona ya nchi hapashikiki...
 
Mtwara muwe makini serikali hii inawatumikia mafisadi msije kuta mashimo gesi ikawa imeisha changamkeni kabla hawajaanza kuchimba vinginevyo so
 
Siku zote ubabe hauwezi saidia kutatua mgogoro, njia sahihi ni kusikiliza kilio cha wana Mtwara na kukifanyia kazi na hapo gesi itaondoka kirahisi.

Kinyume cha hapo ni hujuma kila siku katika bomba lenyewe.

Hongera wana Mtwara.

Polisi wao hufikiri kwa kutumia nguvu tu,hata jambo la kutumia busara wao hutumia nguvu.Sijui watajigawa vipi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…