jaji anaelekea kuthibitisha uhalali wa Kauli ya Rostam.Asante Rostam
Ndugu Rostam alipotosha. Kivipi? Alichokisema hakitumiki kisutu pekee, hata huko kimataifa uingiliaji wa mikataba na sheria na mahakamni unafanyika.
Mifano ipo:
1. HUWAWEI na tenda za teknolojia marekani,.Wachina hawa walishindwa kukamilisha.kazi zao kwa Viongozi wa Marekani kuwawekea ngumu wasifanyebiashara nchini humo kwa visingizio visivyokuwa na ushahidi.
2. Ufaransa ilifuta takwa lake la kimkataba kupeleka bidhaa (manoari ya kivita) Russia kwa kutishwa na NATO. Russia ilishalipa hela yalibaki makabidhiano.
3. Ujeruman ilivunja makubaliano ya kununua gesi kutoka Russia wakati tayari kampuni za nchi hizo zimeishaingia makubaliano.
4. Iran imezuiwa kufanya biashara ya mafuta na gesi wakati ina mikataba halali na kampuni za nchi nyingine za kimataifa, pia ilizulumiwa hela zake za Amana.
5. Venezuela iliibiwa Dhahabu zake zilizokuwa zimehifadhiwa kwenye Vaults za Uingereza tena kwa makubaliano ya sheria za kimataifa. Uingereza iligoma kuzitoa kwa mmiliki halali Venezuela.
6. Russia ilizuia mashirika ya Ndege ya ulaya yasitumie anga lake wakati mashirika hayo yalikuwa na mikataba na kampuni za nchi hiyo. Pia Ulaya na marekani zililazimisha kampuni za nchi zao kuondoka Russia wakati kampuni hizo zina uwekezaji huko.
7. Kwa sheria za baharini US hana uhalali wa kuzuia tankers za Iran kupitisha mafuta bahari ya Hindi Lakini kaweka kizuizi hicho. Na Iran hatakiwi kuzuia meli zisipite mlango wa Hormuz lakini kazizuia hasa zile za nchi waliomchokoza.
8. Marekani ilizuia askari wake waliofanya uhalifu na Netanyahu wasikamatwe na ICC, na US ikatishia kumkamata Mkuu wa Mahakama hiyo tena mahakama ya KIMATAIFA. Katika hali hii Ndugu Azizi anatushawishije tuwe na imani na huko kimataifani?
Kwa hiyo, hata huko Kimataifa, kuingilia maamuzi ya mahakama, wanasheria majaji ni kawaida. Hakuna cha kisutu ama cha kimataifa. Vinginevyo nielezwe sikuelewa sawa sawa hoja ya Mtanzania mwenzetu na ndugu Yetu Mheshimiwa Rostam Aziz.
Nakaribisha kukosolewa kwa hoja yangu na kwa kutumia lugha na kauli yoyote itakayokufanya uwe na amani moyoni mwako.
Karibu.