Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 2,450
- 5,279
Mwanachama wa Chama cha Wananchi (CUF), Rose Kahoji amekuwa mwanamke wa tatu nchini kutangaza nia ya kugombea urais katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.
Kwa hatua hiyo, Kahoji anaungana na Rais wa sasa, Samia Suluhu Hassan wa CCM, ambaye tayari amepitishwa na chama chake kuwania nafasi hiyo.
Rais Samia alipitishwa rasmi na Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM uliofanyika Januari 19, 2025, kuwa mgombea urais wa Jamhuri kupitia tiketi ya chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.
Mbali na Rais Samia, Kiongozi wa Chama cha ACT- Wazalendo, Dorothy Semu, naye alichukua fomu Aprili 22, 2025, kuomba ridhaa ya kuteuliwa kuwa mgombea urais wa Jamhuri kupitia chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.
Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu, hadi sasa wanawake watatu wamejitokeza kuwania nafasi hiyo kupitia vyama tofauti vya siasa, hatua inayoashiria kuimarika kwa ushiriki wa wanawake katika uongozi wa kitaifa.
Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Akizungumza leo Julai 12, baada ya kukabidhiwa fomu ya kugombea urais, Rose Kahoji mkazi wa Mbeya amesema ameamua kujitosa katika uchaguzi huo ili kupigania masilahi na maisha bora ya wananchi katika huduma mbalimbali.