Mashaxizo
JF-Expert Member
- Jun 13, 2013
- 6,707
- 3,360
Za hapa wanabodi?
Hope muwamaridadi,
Na hapa kwangu baridi,
Kwa amaani napumua.
Poleni kwa masimanzi,
Ya maisha na mapenzi,
Kwa waso kazi na penzi,
Mola atawaongoa.
Nisiwachoshe w'body,
Kwanza naweka midadi,
Hapa kuna ka zawadi,
Napenda kuwagaia.
Maisha fanya ni chungwa,
Likate vinne viungwa,
Robo moja ya kiungwa,
Ni penzi kiromantikia.
Tatu zilosalia,
Kuna mambo kama mia,
Yote yakusubiria,
Maamuzi kutolea.
Tatu zipo kwenye kichwa,
Ubongo wako chekecha,
Usije ukaendeshwa,
Na robo iloanzia.
Ukiuvaa ujuba,
Utapita kwenye miba,
Kwa kale ka kisiriba,
Ka chabo ulozoea.
Chabo 1 jicho waziba,
Yanini kujipa shida?
Chakuokota si cha kwiba,
Ndio rule ya dunia.
Siku nitaoa mwali,
Mwenye kujua ukweli,
1 na 1 ni mbili,
Aelewe sio kujikariria.
Chuo si lazima kwa kweli,
Napenda asokalili,
1 na 1 ni mbili,
Ajue kuzitumia.
Sipendi wa kushindana,
Hakuna wa kufanana,
Maisha mafupi sana,
Skendo sijazoea.
Baraka nawatakia,
Kwa wote waloelewa,
Na hata wasoelewa,
Zawadi tawafikia.
...
Source: Mashaxizo.
Hope muwamaridadi,
Na hapa kwangu baridi,
Kwa amaani napumua.
Poleni kwa masimanzi,
Ya maisha na mapenzi,
Kwa waso kazi na penzi,
Mola atawaongoa.
Nisiwachoshe w'body,
Kwanza naweka midadi,
Hapa kuna ka zawadi,
Napenda kuwagaia.
Maisha fanya ni chungwa,
Likate vinne viungwa,
Robo moja ya kiungwa,
Ni penzi kiromantikia.
Tatu zilosalia,
Kuna mambo kama mia,
Yote yakusubiria,
Maamuzi kutolea.
Tatu zipo kwenye kichwa,
Ubongo wako chekecha,
Usije ukaendeshwa,
Na robo iloanzia.
Ukiuvaa ujuba,
Utapita kwenye miba,
Kwa kale ka kisiriba,
Ka chabo ulozoea.
Chabo 1 jicho waziba,
Yanini kujipa shida?
Chakuokota si cha kwiba,
Ndio rule ya dunia.
Siku nitaoa mwali,
Mwenye kujua ukweli,
1 na 1 ni mbili,
Aelewe sio kujikariria.
Chuo si lazima kwa kweli,
Napenda asokalili,
1 na 1 ni mbili,
Ajue kuzitumia.
Sipendi wa kushindana,
Hakuna wa kufanana,
Maisha mafupi sana,
Skendo sijazoea.
Baraka nawatakia,
Kwa wote waloelewa,
Na hata wasoelewa,
Zawadi tawafikia.
...
Source: Mashaxizo.