Roma Mkatoliki usiposema ukweli kesho, wakatoliki halisi tutausema Jumanne

Status
Not open for further replies.

Tomito Tomato

Senior Member
Feb 11, 2017
167
444
Kesho tunataka kusikia yafuatayo..wale watu wawili waliokuja kukuhoji kwanini walikuwa hawakujui je walielekezwa na nani kwako?..mlipoingia ndani ya ile Noah kwanini nyote mlifungwa vitambaa vichwani na mkaja kufunguliwa mlipoingizwa katika nyumba ya kwanza Mikocheni na siku mbili baadae mkahamishiwa katika nyumba iliyopo Oysterbay..

Kwanini kati yenu wote ni wewe tu ndiyo uliyepigwa sana na virungu magotini huku ukikanyagwa kila mara mbavuni mwako na kuna wakati ukawekewa bastola kichwani ndipo ukaanza kunywea...?

Ni kiongozi gani ambaye juzi usiku alikuja katika hiyo nyumba na kuzungumza nanyi kisha akawatishieni nyote?

Yule dada aliyekuwa akiongoza mateso yenu huku akiwa anawahoji na kuwarekodi anatoka katika taasisi gani?

Kiongozi gani aliomba kuongea na wewe jana asubuhi kabla hamjaondoshwa hapo Oysterbay na kupelekwa Polisi?

Ole wako usiseme huu ukweli kesho.
 
Wewe ndio utuambie ukweli umejuaje alipigwa virungu? ulikuwepo

Sasa umejuaje hatosema ukweli wakati yeye ndio anajua ukweli? Tatizo lenu tayari mna majibu yenu mfukoni sasa mnalazimisha Roma aseme hayo.
Ukweli ni ukweli tuu hata kama hauto wafurahisha kwa hiyo mtulie msilazimishe aseme myatakayo
 
Kwa jana kuachiliwa kwa masharti ilihali yeye sio mhalifu,ni dalili tosha atapindisha ukweli,akipindisha ukweli basi kajiweka rehani kwani atakuwa mhanga wao ama watakuja kumtumia then kumpoteza,salama yake ni kuweka bayana then aombe hifadhi ama msaada kwa mashirika ya kutetea haki ili achore mstari kabisa baina yao na wao wabaki ndio watuhumiwa kwa lolote litakalokuja kutokea mbeleni.
 
Sifikirii kama atasema bayana ya yaliyomkuta.Kutishiwa uhai kubaya.
Aliimba .."leta defender!,leta wajeda !leta wagambo!..Roma nimejitoa muhanga...!"
Wamepeleka Noah tu,karudi ameufyata.Eti hawezi kuzungumzia tukio,utafikiri kuna kesi inayosikilizwa.
 
Kwa jana kuachiliwa kwa masharti ilihali yeye sio mhalifu,ni dalili tosha atapindisha ukweli,akipindisha ukweli basi kajiweka rehani kwani atakuwa mhanga wao ama watakuja kumtumia then kumpoteza,salama yake ni kuweka bayana then aombe hifadhi ama msaada kwa mashirika ya kutetea haki ili achore mstari kabisa baina yao na wao wabaki ndio watuhumiwa kwa lolote litakalokuja kutokea mbeleni.

maelezo mazuri kabisa haya mkuu na anatakiwa kesho aseme ukweli wa hayo maelezo hapo juu na siyo mengineyo.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom