roho

Victor Mlaki

JF-Expert Member
May 1, 2016
4,151
4,275
KWA NINI NI MUHIMU KUJARIBU KILA ROHO.
Kujaribu ninakotaka kukujejengea msingi hapa ni "Kupima au kadiria",fasiri hiyo imetoka kwenye neno "jaribu"test"kwa mujibu wa Kamusi ya Kiswahili Sanifu toleo la Pili ukurasa wa128.
Biblia ya Kiingereza(English Standard Version"ESV") In the Book of 1John4:1-3(page1023) "Beloved do not believe every spirits but #test#the spirits to see whether they are from God,for many false prophets have gone out into the world.2By this you know the Spirit of God:every spirit that confesses that Jesus Christ has come in the flesh is from God.3And every spirit that does not confessJesus is not from God.This is the spirit of antichrist, which you heard was coming and now is in the world already.
Katika Biblia ya Kiswahili"The Holy Bible in Kiswahili Union Version iliyochapwa kama BIBLIA "Maandiko Matakatifu" iliyochapishwa na Bible Society of Tanzania kwa kushirikiana na Bible Society of Kenya mwaka1997 Kitabu cha Waraka wa Kwanza wa Yohana4:1-3(Ukurasa wa250)"Wapenzi msiiamini kila roho bali #zijaribuni#hizo roho,kwamba zimetoka kwa Mungu,kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani.2Katika hili mwajua Roho wa Mungu.Kila roho ikiriyo kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili yatokana na Mungu...................
Lengo la Andiko hili ni kukuwezesha kutambua kuwa upo umuhimu mkubwa
sana wa kushuku na kuchunguza kabla ya kuamini au kukubaliana na jambo au suala lolote lile.
SIYO KILA JAMBO LINALOFANYIKA CHINI YA JUA LINAFANYIKA KWA NGUVU"ROHO"SAHIHI YAPO PIA MAZINGAOMBWE YANAYOIGA NGUVU YA ROHO SAHIHI.
Biblia imeujenga msingi imara sana wasomaji kujifunza kutokana na mifano hai inayoakisi utendaji katika maish yetu ya kila siku.
HAYA NITAKAYOYAANDIKA HAPA CHINI NI MANENO YANGU NA SIYO BIBLIA
Maneno hayo ni" .......Nyuma ya kila jambo na kila tukio kuna msukumo hai wa kitendaji unaofanya jambo litokee na huo msukumo hai wa Kitendaji kwa uelewa mdogo sana nilioutumia ni sawa na "roho"
Nilishawahi kuandika"NYUMA YA KILA KITU KUNA KILA KITU"kumaanisha ili kitu kifanyike huwa kuna kani tendaji iliyo hai inayokisukuma kuwa kilivyo na kuendelea"continuity"
Ili kuweza kuondoa kabisa utendaji au tukiaji wa hali jambo au tukio lolote lile ni vyema sana kuangalia nyuma ya hilo tukio kuna roho gani na kufanikiwa kuidhibiti roho ni kufanikiwa kutawala mkunjuo w jambo au hali inayokusibu.
LEO WATU WENGI WANAISHI MAISHA AMBAYO YANATAWALIWA NA ROHO AMBAZO WAKATI MWINGINE WAO HUJIKUTA KATIKA HALI NA MWENDELEZO WA HALI AMBAZO HATA KUZIELEZEA WAO WENYEWE WANASHINDWA.
Sijalenga uamiani au kubaliane na Andiko hili nililoliandika kwa Makusudi kabisa ila natamani sana tupende kusoma Biblia na kumuomba Mungu atuwezeshe kuelewa.
Biblia ni Kitabu kinachoigusa moja kwa moja kila kona ya Maisha ya Mwanadamu yeyote yule tangu kuzaliwa hadi kufa.
Your Spiritual Friend
Victor Mlakimtoto Wa Wilbard
Thank You.
 
Back
Top Bottom