Roho wa Mungu yuko pamoja na Lowassa

Roho wa Mungu yuko pamoja na Lowassa

Paul Alex

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2012
Posts
4,344
Reaction score
9,845
Yohana 11
⊙41 Basi, wakaliondoa lile jiwe. Yesu akatazama juu mbinguni, akasema, "Nakushukuru Baba kwa kuwa wewe wanisikiliza. 42 Najua kwamba unanisikiliza daima. Lakini nimesema hayo kwa ajili ya watu hawa waliopo hapa ili wapate kuamini kwamba wewe ndiwe uliyenituma." 43 Alipokwisha sema hayo, akaita kwa sauti kubwa: "Lazaro! Toka nje!"

Hapo juu ni sala aliyoifanya Yesu kabla ya kumfufua Lazaro,rafiki mkubwa wa Yesu!

Ukimuangalia sana Lowassa utagundua kuna jambo kubwa ndani yake tena la maajabu, karibu la kimiujiza hivi!

Angalia safari yake ya kisiasa ,angalia upendo wake kwa watu, angalia busara,upole na unyenyekevu wake kisha waangalie maadui zake, walio hai na wanaoendelea kutoweka kwenye uso wa dunia kila uchao na utagundua kuwa roho wa Mungu yuko juu ya Lowassa.

'Ugonjwa huu hautaleta umauti ila ni kwaajili ya utukufu wa Mungu'.
Haya ni maneno Yesu Kristo aliyowaambia Maria na Martha dadaye, wote dada wa Lazaro ,familia Yesu aliyoipenda sana, pale walipomfikishia Yesu habari za Ugonjwa wa Lazaro.

Tumejionea wenyewe juu ya wale walioigeuza afya ya Lowassa kama agenda ya kisiasa 2015. Mzee wa watu aliwajibu kwa kifupi kabisa kuwa afya ni majaliwa ya Mungu.

Huyo waliyesema hawezi kuongea leo hawataki aongee na watanzania,
Huyo waliyesema ni mgonjwa sana leo hawataki afanye mikutano ya siasa.

Sijui kama hila na vitisho vya Sizonje vitafanikiwa kuzuia utukufu wa Mungu usijidhihirishe 2020.
Ila nachojua kwa hakika ni kuwa Mungu wa Lowassa yu hai.
 
chadema wanadai Kenya kuna demokrasia ila procedure za kutangaza matokeo ukweli zinatia Mashaka! je hii ni demokrasia tunayoiamini wote? naamini hili ni kosa la pili kubwa la chadema kutoka kwa chanzo kilekile.
mkija kufanyiwa nyie msilalamike Kabisa.
 
Back
Top Bottom