Roger Milla aitabiria makubwa Taifa Stars | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Roger Milla aitabiria makubwa Taifa Stars

Discussion in 'Sports' started by BAK, Jun 23, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jun 23, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,609
  Trophy Points: 280
  Date::6/23/2008
  Roger Milla aitabiria makubwa Taifa Stars
  Na Angetile Osiah, Yaounde
  Mwananchi

  GWIJI wa soka wa Cameroon, Roger Milla ameshangazwa na kiwango kilichoonyeshwa na Taifa Stars wakati ilipocheza na nchi hiyo Jumamosi, akisema kuwa Tanzania itakuwa na timu bora katika miaka miwili ijayo.

  Stars ilifungwa mabao 2-1 na Cameroon katika mechi hiyo iliyofanyika Jumamosi kwenye Uwanja wa Ahamadou Ahidjo jijini hapa, lakini uamuzi mbovu ulichangia wenyeji kupata ushindi huo mfinyu, ukiwemo ule uliompa mwanya Samuel Eto'o kufunga bao la pili.

  Eto'o alifunga bao hilo kwa kiki ya chini baada ya kuunawa mpira wakati akihangaika kutuliza mpira na refa kutopiga filimbi. Tukio hilo lilikuwa ni hitimisho la uamuzi mbovu uliofanywa wakati mwingi wa mchezo huo wa michuano ya awali ya Kombe la Dunia/Mataifa ya Afrika.

  "Hivi mmeanza kupanda juu lini," alisema mchezaji huyo wa zamani wa taifa wa Cameroon, ambaye aliibuka kwenye hoteli ya Mont Febe baada ya mechi hiyo.

  "Nimeiona mechi ya leo na nimeona kuwa mna timu nzuri ambayo katika miaka miwili ijayo itakuwa tishio barani Afrika. Mnachohitaji ni kuendelea hivi. Nimeona timu ina wachezaji wengi vijana na ambao wataweza kufanya vizuri baadaye. Wana maumbile madogo, lakini wana kasi sana.

  "Mnahitaji miaka miwili au mitatu kuwa timu kubwa barani Afrika."

  Eto'o alifunga bao la kwanza katika dakika ya 65 wakati mpira ulipomponyoka kipa Ivo Mapunda alipokuwa akijaribu kudaka krosi ya Geremi Njitap na kumfikia mshambuliaji huyo wa zamani wa Barcelona aliyefunga kwa kiki ya mguu wa kushoto.

  Mshambuliaji huyo, ambaye ni mshindi wa tuzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika kwa miaka mitatu, alifunga bao la pili lililokuwa na utata baada ya kuunawa mpira kabla ya kupiga shuti kabla ya wenyeji kuanza kupoteza muda kusubiri mchezo uishe. Bao la Stars lilifungwa katika dakika ya 77 na Danny Mrwanda.

  Maoni ya Miller hayakutofautiana sana na mashabiki wengi wa Cameroon walioona mechi hiyo. Wengi waliishangilia Stars wakati ikirejea hotelini baada ya mechi hiyo na baadhi walisifu jitihada za kipa Ivo Mapunda.

  "Sina shaka kuwa mna kipa bora sana," alisema shabiki mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Soulemane. "Ilikuwa kama mna nyani golini kwa jinsi alivyokuwa akiokoa mipira. Kwa kweli bila ya kipa yule, mngeweza kufungwa mengi."

  Cameroon ilishindwa kabisa kupenyeza mipira kwenye ngome ya Stars na kuamua kutumia mipira ya krosi, huku ikilazimisha kona kwa muda wote wa dakika tisini, lakini ni mpira mmoja uliozaa bao wakati Ivo alipoudondosha mpira wa krosi kutoka kwa Geremi Njitap.
   
 2. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #2
  Jun 24, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Wabongo kwa ku-spin!

  Kufungwa twafungwa lakin' chenga twawala!
   
 3. Gang Chomba

  Gang Chomba JF-Expert Member

  #3
  Jul 11, 2008
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 8,790
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  wabongo mtabakia hivyo hivyo, wenzenu haoooo wanakwenda kushiriki mashindano ya ukweli...
   
Loading...