Roboti wa Microsoft amtusi Obama! #Teknolojia

the great wizard

JF-Expert Member
Dec 21, 2015
1,482
887
Microsoft walizindua akaunti ya Twitter kwaajiri ya roboti yao inayojulikana kama Tay ambayo inatumia artificial intelligence kujibu tweets na kujichanganya na vijana, lakini masaa machache baada ya Tay kuanza kutweet akasema mambo yaliyo ashiria kumtusi raisi wa Marekani Obama na pia kauli hizo tata zilionesha kwamba Tay anaubaguzi wa rangi.

Tay ambaye alifunguliwa akaunti Twitter kwaajiri ya kuchati kupiga gumzo na vijana, kabla hajaanza kutoa kauli za kibaguzi na kauli za kashfa Tay alionekana kuimudu kazi yake huku akiweza kuongea lugha ya vijana na maneno ya vijana.
Roboti huyo ambaye alitengenezwa na watafiti pamoja na wanasayansi wa Micrososft anajifunza maneno na tabia kutokana na tabia ambazo watu wanae piga naye gumzo wanazo hivyo jinsi ambavyo unachati naye ndivyo na yeye anajifunza mambo mengi zaidi.

Kwa inavyoonekana ni kwamba watumiaji wa mtandao wa Twitter walimlisha Tay mambo mengi juu ya ubaguzi pamoja na propaganda za kinazi, hii ilisababisha roboti hiyo kuwa na mawazo ama fikra za kibaguzi na pia za kinazi na ilipelekea kutoa maoni ambayo baadaye yalifutwa Twitter.

Tay alifutiwa baadhi ya tweets zake twitter baada ya kusema kwamba Bush ndiye aliye tekeleza shambulio la 9/11 marekani na kwamba Hitler angeweza kufanya kazi bora kushinda aliyofanya nyani alie madarakani sasa na pia katika tweet nyingine roboti hiyo ilisema kwamba mgombea wa uraisi kupitia chama cha republican Donald Trump ndiye tumaini pekee tulilo nalo.

Tay bado yupo twitter hadi mda huu ila tu zile tweets za utata zimefutwa na anatumia tweet handle ya @tayandyou hivyo kama wewe pia upo twitani basi ungana na maelfu ya watu ambao wanaifuata akaunti hiyo maarufu.
 
huyo ni jike
tay-picture.jpg
 
Back
Top Bottom