Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe
Robert Mugabe ameukejeli uamuzi wa Marekani
kuhalalisha ndoa za mashoga katika majimbo yote 50
kwa kuahidi kusafiri hadi White House na
kumchumbia Barack Obama.
Wakati wa mahojaino ya kila wiki na kituo cha redio
cha taifa, rais wa Zimbabwe alitania kwamba
amepanga kwenda Washington DC kupiga goti moja
na kuomba kumchumbia.
Rais Barack Obama wa Marekani
Mugabe, ambaye anajulikana kwa kupinga vikali
mahusiano ya jinsia moja, alikuwa akijibu kuhusiana
na marekebisho ya kifungu cha 14 cha Marekani.
Katiba inawahakikishia mashoga na wasagaji kuwa
na haki sawa kuoana kama walivyo watu wengine.
Mahakama Kuu ya Marekani
Akizungumzia hilo siku ya Jumamosi, Mugabe
alisema: Nimeshahitimisha kuwa tangu Rais
Obama aidhinishe ndoa za jinsia moja, kutetea watu
mashoga na kufurahia kukubalika kama vile ni
jambo la lazima, nitasafiri hadi Washington, DC,
kumchumbia.