Uchaguzi 2020 Robert Amsterdam na Sheikh Ponda ndio watakaomuangusha Lissu

IDEGENDA

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
4,505
5,333
Yani kabisa wewe ni Muafrika na unapiganiwa na beberu ili uwe Rais? Utapingwa na Waafrika wote popote duniani walipo. Hivi mnaona hata wale diaspora aliokuwa anawahutubia Lisu akiwa Ulaya wanaonekana sasa hivi? Wameona huyu jamaa hana nia njema kabisa na tz.

Kitendo cha Amsterdam kuingilia mambo ya ndani ya tz tena nyeti kama uchaguzi ili tu kumsapoti Lisu kuna watu wengi sana wameahirisha kumpigia kura Lisu. Watanzania siyo wajinga linapokuja suala la maslahi ya taifa letu, nafikiri manakumbuka sapot aliyokuwa anapata Magu wakati wa janga la corona aliooamua kupambana jino kwa jino na wakenya kupitia wakuu wa mikoa.

Watu wanajiuliza Lisu atatoa wapi mabilioni ya kumlipa Amsterdam kwenye hii kazi yake aliyompa?

Ponda hawezi kusimama kwenye mkutano wa Lisu na kusema waislamu tumpigie kura Lissu na Lissu nae kuchekelea kama zuzu!
Je, Lissu amejiuliza maamuzi ya wakristo kufuatia matamshi hayo ya Ponda kwenye mikutano yake.

#magu 5 tena.
 
Ponda hujui nguvu aliyonayo kwa waislamu, sisi waislam ndio tunajua kwa nini Ponda anasema tumpigie kura Lissu. Maadam Shekhe Ponda kasema nanikiongozi wetu basi tutatekeleza.

Kama huamini subiri uone maeneo yenye waislam wengi kama Magufuli atachomoka, nasababu nikuwa tunamsikiliza kiongozi wetu Shekhe Ponda. Hata wanaccm lilia kama Pohamba watampigia kura Lissu, kwa maana watamsikiliza kiongozi wetu Shekhe Ponda.
 
Yani kabisa wewe ni Muafrika na unapiganiwa na beberu ili uwe Rais? Utapingwa na Waafrika wote popote duniani walipo. Hivi mnaona hata wale diaspora aliokuwa anawahutubia Lisu akiwa Ulaya wanaonekana sasa hivi? Wameona huyu jamaa hana nia njema kabisa na tz...
Mimi mkrito na ninaona sawa Sheikh Ponda kumpigia kampeni Lissu. Udhalimu wa Jiwe umeathili wote si waislamu, si wakristo. Wakristo na Waislamu tumeona Jinsi Jiwe wenu akishirikiana na Ndugai walivyomnyanyasa Prof Assad kwa sababu tu anasimamia uislamu wake. Wakristo na waislamu tumeona jinsi Askofu niwemugizi alivyoteswa na vyombo vya usalama vya magufuli kwa kuambiwa sio Raia na kunyang’anywa passport kwa sababu tu alisimamia kweli yake katika ukristo

Kuhusu Robert Amsterdam wala hatushangazi na zaidi tunamfurahia. Kama mawakili wa ndani wanaompigania Lissu kina Fatma Karume mnalipua ofisi zao na kuwafuta uwakili sasa mnategemea Lissu aendelee kutumia mawakili wa ndani Tanzania???

Mtu mnataka kumuua na mmemsababishia ulemavu kwa marisasi yenu alafu hata mawakili wa ndani wanaomtetea mnawanyanyasa na kuwavua uwakili alafu ndo aendelee kutumia mawakili wa ndani??? Thubutu yenu.

Mwaka huu Ccm mmeshikwa vibaya sana na lazima muachie madaraka mwaka huu mtake msitake.
 
Ponda hujui nguvu aliyonayo kwa waislamu, sisi waislam ndio tunajua kwa nini Ponda anasema tumpigie kura Lissu. Maadam Shekhe Ponda kasema nanikiongozi wetu basi tutatekeleza.

Kama huamini subiri uone maeneo yenye waislam wengi kama Magufuli atachomoka, nasababu nikuwa tunamsikiliza kiongozi wetu Shekhe Ponda. Hata wanaccm lilia kama Pohamba watampigia kura Lissu, kwa maana watamsikiliza kiongozi wetu Shekhe Ponda.
Sawa Ponda kawaambia waislamu mfanye hivyo na Lisu atashinda sehemu yenye waislamu wengi kwa mujibu wako!

Likini umeshajiuliza ni vipi Wakristo nao maamuzi yao baada ya taarifa za Ponda?
 
Usingemalizia kama Mataga wengine na magu 5 tena, ningetafuta point kwenye ulichoandika. Ila mimi ni mkristo na nitampigia Lissu kura. Hao diaspora unaowasema hawapigi kura.
Diaspora wameona Lisu ni kibaraka ndio maana wako kimya
 
Sawa Ponda kawaambia waislamu mfanye hivyo na Lisu atashinda sehemu yenye waislamu wengi kwa mujibu wako!

Likini umeshajiuliza ni vipi Wakristo nao maamuzi yao baada ya taarifa za Ponda?
Ingekua shekhe Ponda anampigania muislamu ingekuwa na athari, lkn kuonesha alivyo mpenda haki anampigania mkristo mpenda haki, kwahiyo naamini wakristo nao pia watamchagua Lissu kwa sababu nimpenda haki.
 
Lisu yeye mabilioni ya kumpa Amsterdam atayatoa wapi?

Hivi kila mgombea akiweka mtu wake kutoka nje awe anampigania patakuwa na taifa tena?

Lisu kashafeli
Kwani kila anaetetewa na Wakili anatoa hela? We wazungu kila siku wanakupa misaada kuwajengea hospitali, barabara na vyoo vya mashule kwani mnawapa hela?

Kwenye sheria kuna kitu kinaitwa Probono fuatilia ujue maana yake we kilaza wa Lumumba. Sio kila mwenye Wakili lazima amlipe. Unategemea kwa marisasi mliyommiminia mkitaka kuumua dunia ingekaa kimya tu asipate hata mtu wa kmtetea??? Imekula kwenu
 
Ponda hujui nguvu aliyonayo kwa waislamu, sisi waislam ndio tunajua kwa nini Ponda anasema tumpigie kura Lissu. Maadam Shekhe Ponda kasema nanikiongozi wetu basi tutatekeleza.

Kama huamini subiri uone maeneo yenye waislam wengi kama Magufuli atachomoka, nasababu nikuwa tunamsikiliza kiongozi wetu Shekhe Ponda. Hata wanaccm lilia kama Pohamba watampigia kura Lissu, kwa maana watamsikiliza kiongozi wetu Shekhe Ponda.
Tundu lisu hamjui ponda, ponda hatalidhika na uongozi wa Lisu hata siku moja, na baada ya kuitoa CCM ponda ataanza kumtoa Lisu na ndio atajuta kumjua ponda na ajenda zake.
 
Kwani kila anaetetewa na Wakili anatoa hela? We wazungu kila siku wanakupa misaada kuwajengea hospitali, barabara na vyoo vya mashule kwani mnawapa hela?..
Hata uniite mimi kilaza hao kina Amsterdam wamechangia sana, kuna kundi halitampigia Lisu kura sababu yao.

Huwezi wewe mbelgiji unataka kutupangia sisi watz wa kumchagua. Utaanguka tu
 
Hata uniite mimi kilaza hao kina Amsterdam wamechangia sana, kuna kundi halitampigia Lisu kura sababu yao.

Huwezi wewe mbelgiji unataka kutupangia sisi watz wa kumchagua. Utaanguka tu
Sema kilaza wewe wa Lumumbaendo hutampigia kura. Watanzania wengi kwa mamilioni tunampigia kura za kishindo Tundu Antiphas Lissu na kuzilinda
 
Ponda ni Shekhe Mtetezi wa Waisilamu dhidi ya Uonevu wa taasisi za CCM haswa Bakwata.

Bob Amsterdam ni Wakili wa Lissu na ndiye aliemwambia Lissu aje Nchini ili hao waliokuwa wanasema Watamshambulia tena wamguse ili awafungulie mashtaka

Sasa neno Kuangusha litakuwa limepoteza maana kwenye kamili ya ccm
 
Ingekua shekhe Ponda anampigania muislamu ingekuwa na athari, lkn kuonesha alivyo mpenda haki anampigania mkristo mpenda haki, kwahiyo naamini wakristo nao pia watamchagua Lissu kwa sababu nimpenda haki.
Wewe hujui siasa za tz,! Ndio maana ccm itaendelea kutawala.

Lisu sijui hana washauri, kaenda Zanzibar alafu anatamka eti sisi chadema hatuna maslahi na Zanzibar. Kiufupi Lisu hajui siasa ya tz ili uungwe mkono wakupe urais unapaswa kuwaje.
 
Ponda ni Shekhe Mtetezi wa Waisilamu dhidi ya Uonevu wa taasisi za CCM haswa Bakwata.

Bob Amsterdam ni Wakili wa Lissu na ndiye aliemwambia Lissu aje Nchini ili hao waliokuwa wanasema Watamshambulia tena wamguse ili awafungulie mashtaka
Anatetea waislamu kuhusu nini??
 
Back
Top Bottom