Riwaya Tamu: Historia Batili Sehemu ya 03

Riwaya Tamu: Historia Batili Sehemu ya 03

Mdharuba

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2011
Posts
824
Reaction score
521
STORY: HISTORIA BATILI(Fake History)
MTUNZI: Jumaa Khatib Mdharuba

+255 718 274 130

Season 01-Episode 03
★★★★★★★★★★★★★★
Kitu ambacho kiliwashangaza wengi juu ya Mr.Khatib ni ule uharaka wake katika kujibu messages katika simu yake.. iwe ni meseji ya kawaida(sms), iwe kupitia whatsapp, au hata e-mail, alikua anajibu haraka sana pindi tu meseji inapomfikia..Mambo mengi aliyokuwa nayo na uharaka ule katika kujibu meseji, viliwafanya wengi wabaki midomo wazi sana..bado walishindwa kumtambua vizuri Khatib ni mtu wa namna gani!!.
Akiwa ndani ya Atlantic Superstore, ndani ya Mji wa Vancouver alisikia tone katika simu yake kuashiria kuna meseji..
Akatoa simu yake iliyokua mfuko wa jeanz yake nyeusi na kuisoma msg ile ambayo ilitumwa kupitia whatsap..
"Toka hapo Supermarket haraka Sarah ametumwa na dada yake akufuatilie" Ilikuwa ni msg iliyotumwa na Mama Mdharuba katika namba maalum ambayo alijua lazima itakua hewani kwa muda huo!! Khatib hakupoteza hata sekunde moja pale Supermarket na kupotelea anakokujua yeye..
"Dada, nimezunguka Supermarket yote ila sijamuona shem.., labda atakuwa ameshatoka.." Aliongea Sarah baada ya kupiga simu Tanzania na dada yake Sauda kupokea..
"Duuh!! Haya sawa..ila umehakikisha kweli kuwa hayupo?" aliuliza Sauda akiwa hajui chochote kuhusu Atlantic Superstore kuwa ilikua ni Supermarket kubwa sana ambayo kama mtu ataizunguka yote kwa haraka haraka kama alivyokua anafanya Sarah ilihitaji zaidi ya masaa mawili, alichofnya Sarah ni kuzunguka sehemu za mwanzoni tu za Supermarket ile na alitumia dakika 15 tu ili kumridhisha dada yake ili amruhusu aende chuoni kwake maana alihisi kuchelewa sasa kwani alikua akikaa mbali kidogo na eneo la chuoni.
"Nimezunguka kote dada, sijamuona"
"Ok sawa,wewe wahi chuo ukimaliza mambo yako tutaongea"
★★★★★★★★★★★★★★
Ni siku ya 20 sasa tangu Khatib aondoke nyumbani katika mazingira ya kutatanisha..Sauda alishabadilika na kukonda sana, alikua anakula mara chache sana tena kidogo mno, kutokana tu na msukumo wa Mama Mdharuba..
Aliwaza mambo meengi saana.."Kwnn mume wng asafir mpka Canada na asinipe taarifa?", "kama kweli Canada kuna baba yake mzazi kwanini hataki Sarah apajue??", "Kwanini hataki kumpeleka Sarah kwa baba yake hyo?", "Kwanin lakin mimi asiniage wakt ni mkewe halali wa ndoa?", "Au nimemkosea nini jamani?". Sauda alikua na maswali mengi sana kichwni kwake, lkin hakuwa na mtu wa kumpa majibu..
Akiwa katika hili dimbwi la mawazo, simu yake iliita!! Akaitazama na kuangalia mpigaji alikuwa amemsave "Lovely Husband". akashangaa sana..akaamua kutokupokea kwani alikua na hasira sana hakujua ataongea nini na msaliti huyu mjeuri anayeondoka na kusafiri bila kuaga..
Simu ikaita mpaka ikakata, mara ikaanza kuita tena..ila safar hii kwa namba ambayo ilisomeka "Sarah", akaamua kupokea..
"Haloo..uko wapi mke wangu??, mi niko nyumbani hapa mbona sikuoni?" Sauda alishikwa na kigugumizi baada ya kusikia sauti ya mumewe badala ya Sarah kama alivyotegemea..akashindwa kujibu chochote..akakata simu ili aihakikishe vizuri ile namba. Ilionekana kuanza na +255 kuonyesha kuwa ni namba ya Tanzania lakini hakuwahi kuiona kabla, akajaribu kuchunguza vizuri simu yake akagundua kuwa kuna namba mbili zilizoseviwa kwa jina moja.."Sarah". Moja ni ya yule mdogo wake lakini hii nyingne ndo anaiona leo..Mashaka juu ya Khatib yakaongezeka..
Simu ikaita tena kwa mara ya tatu.."Lovely Husband" ndiye alikua mpigaji.. akapokea.."Mke wangu, uko waapi? mbona unanikatia simu?" aliongea Khatib kwa upole saana..
"Niko Mbezi" Alijib Sauda kwa mkato maana ilikua si kawaida yake..
"Mbeziii?? kwa mama??" Alijidai kushangaa Khatib kama vile mtu ambaye hajui kuhusu uwepo wa Sauda pale Mbezi..
"Ndio, nipo kwa mama, sasa ntabaki na jinyumba lote hilo peke yangu niingie kichaa bure" Sauda aliongea katika hali iliyoonesha jazba za waziwazi kabisa.
"Kwanini umeamua kwenda Mbezi bila kunipa taarifa?" aliuliza swali gumu sana Khatib ilhali akijua kuwa simu yake haikuwa hewani..
"Aaaah eeeh..Mbezi ndo unaona mbalii? Na ww uliyeenda Canada? Ulinipa taarifa??" Alihoji bi Sauda na kumfanya Mr.Khatib apandwe na hasira.
"Now, it's 10:43 a.m, make sure you come back home before 2 p.m" Aliongea Mr.Khatib na kukata simu..
Pamoja na majibu ya kuchukia aliyoyajibu Sauda, lakini alikuwa hajasahau principles za hyu bwana.. Na hapa alishaanza kupata picha nini kingetokea kama asingefika Morogoro kabla ya muda uliotajwa..
Maana Khatib aliongea kwa kiingereza..huo ulikua ni msisitizo katika alichoongea..kingereza kwake ni lugha ya kusisitiza.
★★★★★★★★★★★★★
"Mume wangu, naomba sana unisamehe kwa kuondoka bila kukupa taarifa, lakini ni kuwa nilishindwa kuvumilia kukaa hapa ilhali sijui ww ulikua wapi??"
Alijaribu kujitetea Sauda baada ya kufika Moro na kukutana na Mr. Khatib ambaye alishamgeuzia kesi tayari..Alitumia akili zake nyingi kumuendesha Sauda atakavyo..alishamshinda katika hoja tayari licha ya kuwa yeye Khatib ndo mwenye makosa!!
"Sawaa..lakini ni mara ngapi nakwmbia kuwa simu yangu isipokuwa hewani unitumie e-mail?" Alihoji Khatib na kumfanya Sauda azidi kupoteza points.
"Mume wangu, hivi ni halali kweli ww utoke ukijua umemuacha mkeo ndani halafu wategemea hyo mkeo ndo akutumie msg kukuuliza umeenda wapi?? ww hujui majukumu yako?? Au wataka kunambia umesahau kuwa una mke?" Hayo ni maswali mfululizo aliyoyauliza Sauda kwa hyu bwana Khatib lakin msimamo wa Khatib bdo ni ule ule tu..
"Mi nilivyoona hunitumii e-mail, nkajua huna waswasi labda unajua niko wapi!" Aliongea kwa kejeli bwana Khatib akiwa hajui kuwa anaumiza moyo wa mwenzie..
"Haya niambie sasa..ulikuwa wapi?" Alijaribu kuwa mpole Sauda ili ajue undani wa tukio hili la kupotea kwa hyu bwana kwa siku 20!!
"Wewe si umesema mi nimeenda Canada bila kukuaga? Sasa unauliza nilikua wapi ili iweje? Si unajua nilipokuwa?" Aliendeleza majibu yake yasiyo mema bwana Khatib bila kujali kuwa Sauda anaumia..
"Kwakweli Khatib nakupenda lakini mmmh ntashindwa kukuvumilia mwenzangu.."
"Hapana, wewe unakua hivi kwa sababu tu huna kazi inayokufanya uwe busy..but....." Aliongea Khatib na kuweka kituo..akaonekana kufikiria kitu.. kisha akaendlea.."Naomba tuelekee pale ofisini kwetu, maana sijafika siku nyingi.."
Ndivyo alivyokatisha maongezi na kupotezea lile jambo Mr Khatib kisha wakatoka mpaka katika uwanja mkubwa wa nyuma hiyo..
"Umebeba funguo za gari? Nataka tutumie gari yako" Alihoji Mr Khatib na kumfanya Sauda kurudi ndani. Akarud baada ya dakika mbili kisha wakaingia kwenye gari Sauda akiwa dereva moja kwa moja hadi Morogoro mjini mtaa wa Boma palipokuwa na yard aliyomiliki kijana hyu mdogo wa miaka 27.
"Oooh boss, karibu sana..Habari za siku?, naona hatimaye umetokea tena ofisini.." Ndivyo alivyomkaribisha boss wake Mr Nira Saire ambaye alikua na umri mkubwa kuliko Khatib..lakini pesa zilimfanya asione shida kunyenyekea kwa mtoto mdogo aliyemuacha miaka 6 kwa kuzaliwa..yeye akiwa na miaka 33.
"Yaah nimerudi kaka"
"Sawa boss karibu ofisini, naona leo upo na shem" Alikaribsha bwana Nira na wote wakazama ofisini mwa yard hiyo!!
"Sasaaa..kazi nzuri sana mnafanya, Nira na wenzako wote niwapongeze kwakweli..Nilipata e-mails zako juu ya maendleo ya hapa kipindi hki nlichokua sipo.." Alianzisha maongezi moja kwa moja bwana Khatib baada ya kukaa pale ofisini..na hii ndio ilikua tabia yke., hakuwa na mda wa kupoteza..
"Na napenda kukufahamisha kuwa Saukhat Investment Company inakabiliwa na mabadiliko madogo kuanzia leo, kwahyo naomba ukubaliane nayo mabadiliko hayo" Alizidi kuongea bwana Khatib na kumfanya Nira asikilize kwa makini.
"Kuanzia leo utakua chini ya Sauda-mke wangu, badala ya mimi..kwahyo hyu ndiye atakuwa manager wenu kuanzia sasa.." Hapo aliweka nukta bwana Khatib na kumfanya Sauda ashangae sana juu ya tukio lile huku akimwangalia Nira kutaka kujua atasema nini!!
"Sawa boss, hakuna shida, your wish is my command!!" alijibu Nira kisha kumpa nafasi aendelee..
"Sauda, karibu ofisini kwko, wewe ndio boss hapa kuanzia sasa..Nira atakupa maelekezo yote ya kazi na naomba ushirikiane nae vizuri sana, Nakutakia kazi njema!" Alimalizia kukabidhi majukumu Mr Khatib kisha akasimama kama anayetaka kutoka..
"Sasa..njoo tuongee kidogo kisha utarudi kuendlea na majukumu yako" Alimwita Sauda wakaenda pembeni kidogo ya ofisi wakaonekana kukubaliana jambo kisha Khatib akawasha gari akatoka na Sauda akarudi ofisini.
Khatib alitoka moja kwa moja mpaka maeneo ya Msamvu ambapo alipack gari yake katika packing ya hotel kubwa ya ghorofa nane iliyosomeka kama "Euler Hotel", akazama moja kwa moja mpaka ndani ambapo alipita reception na kusalimiana na wahudumu wa hapo ambao walionekana kumtambua vyema kwani alikua mteja wa kudumu wa hoteli hiyo, kisha akapanda mpaka ghorofa ya tano ambapo kulikuwa na ofisi ndogo ya hoteli hiyo. Akaingia na kukutana na bwana mmoja wa kipemba, mweusi lakin mwenye asili ya kiarabu.
"Karibu boss, nipo kwa ajili yako na nakusikiliza" Alikaribishwa bwana Khatib na bwana hyu ambaye kwa hesabu za haraka haraka alikua ana umri kati ya miaka 40 had 43..
"Haroun..naomba unipe hesabu kamili za siku zote 20 ambazo sikuwepo" Aliongea bwana Khatib akimtizama Haroun Rashid usoni.
"Sawa boss, kila kitu kimeandikwa humu" Alijibu Haroun na kumkabidhi Khatib bahasha ndogo iliyokuwa na karatasi ndani yake.
★★★★★★★★★★★★★★
Don't Miss Episode 04


Mawasiliano:-
+255 718 274 130
 
Riwaya nzuri. Hapa Mapengo jr.atakuwa kapigwa bao la kisigino !
 
Back
Top Bottom