Riwaya: Sahii ya kifo

Riwaya: Sahii ya kifo

Willy Gamba 1

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2015
Posts
352
Reaction score
377
RIWAYA; SAHIHI YA KIFO
MTUNZI; ISSA MBAGA

SEHEMU YA KWANZA

Jua lilikuwa likiaga upande wa mashariki na
kwenda kuungana na magharibi ili kukamilisha
siku, huku likisindikizwa na hali ya hewa yenye
ubaridi kwa mbali. Ndege pia walipeperusha
mbawa zao kutafuta makazi ambayo yatawafanya
walione jua la kesho hata baadhi ya nyumba za
jirani zilionekana kufuka moshi kama ishara ya
maandalizi ya chakula cha usiku. Sauti za wakina
mama pia zilisikika zikiwaita watoto wao kurudi
nyumbani ili kuepukana na dhoruba za giza
litakapo kuwa kubwa, wengine wakiwatuma
wakubwa kwenda kununua mafuta ya taa na
mishumaa ili waweze kupata mwanga.
Lakini nyumba ya kina David ambayo ndio ilikuwa
ikionekana yenye thamani katika kijiji hicho cha
Gairo mkoani Morogoro ilikuwa tofaauti baada ya
kuzongwa na huzuni pamoja na mabishano ya
hapa na pale juu ya swala la David kutaka kwenda
mjini baada ya kumaliza elimu yake ya kidato cha
sita katika shule ya sekondari Gairo.
Familia ilikuwa imekusanyika katika kitanda cha
mama yao mzazi, ambaye alikuwa hoi kutokana na
maradhi ya moyo yaliyokuwa yakimsumbua kwa
muda mrefu. Yaliyo sababishwa na mshtuko
alioupata baada ya kupata taarifa juu mbaya,
kuwa mumewe kahukumiwa kifungo, kutokana na
ubadhirifu wa fedha uliotokea katika benk ya NMB
tawi la magomeni. Tawi alilokuwa akifanyia kazi
miaka ya nyuma huko kwenye jiji la maraha na
uchafu wote Dar es saalam.
“swala hili halitowezekana hata kidogo. Ni bora ya
hawa wadogo zako ndiyo wangelilia kwenda mjini
lakini sio wewe. Kwani kumbukumbu unazo za nini
kilichotokea huko unakotaka kwenda, mimi Mzee
Kazinge baba yako nasema kauli ya mwisho baki
hapa kijijini”
Baada ya kumaliza kuongea kwa jazba na hasira
mzee Kazinge alitoka nje.
“Baba!! Baba!!...”.David alimuita baba yake kwa
sauti ya unyenyekevu lakini mzee huyo hakugeuka
nyuma.
David alimwangalia mama yake kwa huzuni sana
kisha akamueleza,,,,
“Mama safari hii ni kwa sababu yako huenda
nikafanikiwa kupata pesa huko zitakazo saidia
kufanikisha kufanyiwa upasuaji”
“Najua mwanangu kama unanipenda mama yako.
Unatamani niendelee kuishi. Lakini fikiria pia kama
utaondoka hapa hakuna wa kunihudumia, wewe
ndio tegemeo langu , baba yako mwenyewe hali
yake ndio hiyo unayoiyona tangu ametoka jela
amechanganyikiwa pombe ndiyo imekuwa furaha
yake, nakuomba ubaki baba yangu kama Mungu
amepanga niiishi nitaishi lakini kama hakupanga
basi kazi yake haina makosa”
Mama yake aliendelea kumsisitizia;
“…Lingine wadogo zako atawahimiza nani kusoma
na kuwatunza pia”?
Lakini David hakujibu swali hilo, badala yake
alibaki kimya tu anamuangalia mama yake
aliyekuwa anazungumza kwa shida kitandani.
Maneno hayo yalimuumiza sana David machozi
yakamtoka lakini alijikaza kiume. Hasa baada ya
kuona wadogo zake wamenyong’onyea na kukosa
amani ndani ya mioyo yao. Kutokana na maneno
aliyoyasema mama yao na malumbano yaliokuwa
yakiendelea hapo ndani, ndipo alipo wavuta na
kuwapakata na kuongea nao.
”Msijali wadogo zangu mimi sitaondoka na wala
mama hatokufa alikuwa anatania tu sawa Dason ?
“Ndiyo” Dason aliyekuwa mdogo wake wa mwisho
alijibu
“Nishaaa?”
“Abee
“Haya nendeni jikoni mkaandae mimi nakuja kupika
sawa”?
“Sawa kaka”.alijibu Nisha mdogo wake wa pili
Mzee Kazinge alivyotoka alielekea kilabuni ambako
wanauza pombe za kienyeji ili kukamilisha furaha
yake. Alirudi usiku akiwa amelewa chakari,
alipokuwa njiani aliropoka maneno ambayo
yalionekana kuendana na ukweli wa maisha yake.
”Elimu yangu mwenyewe imenipeleka gerezani!
Nimekosa nini katika nchi hii, kipi bora kuwa
mjinga au kuwa na elimu? Ama kweli Serikali ina
siri kali!!!”
Aliongea maneno hayo njia nzima mpaka alipofika
nyumbani kwake. Familia yake ilikuwa imesha lala
baada ya kupata chakula cha usiku ambacho
kiliandaliwa na David, wakati huo ilikuwa yapata
kama mishale ya saa nane usiku hivi. Kijiji kizima
kilikuwa kimya, sauti yake iliweza kuamsha baadhi
ya majirani. Aligonga mlango wa nyumbani kwake
zaidi ya mara nne lakini hakuna alieitika. Ndipo
alipozunguka nyuma ya nyumba na kumgongea
David dirishani.
”David, David”
”Naam” sauti yenye usingizi iliitika.
”Mimi nagonga we husikii eeh?”
“Nakuja baba”
Ndipo alipo nyanyuka kitandani na kwenda
kufungua mlango. Ghafla David alijikuta akipokea
kipigo kutoka kwa baba yake,,,,
” Mimi na wewe nani baba humu ndani eeh?”
Alimuliza David huku akiendelea kumpiga.
”Haiwezekani mimi nigonge mara zote hizo wewe
upo ndani kama ndiye mwenye nyumba hii”
Hasira hizo pia ziliendana na swala la David
kutaka kwenda mjini maana alilihusisha pia wakati
kipigo kikiendelea,,,,,,
“Unataka nikuzike mapema huko unakotaka
kwenda?”
”Unajifanya hujui kilicho mfanya mama yako aje
huku kijijini wakati niko gerezani?”
Bila kujibiwa aliendeleza kipigo ambacho kilimfanya
David aanze kuhisi maumivu mpaka kufikia hatua
ya kulia kwa sauti kubwa kama mtoto mdogo
wakati ni dume linalo kimbilia miaka ishirini na
ushehe.
Kilio cha David, kiliwatoa majirani majumbani
kwao. Mama yake alipokisikia kilio cha mwanae,
alijitahidi kwenda kumuamulia japo alikuwa hoi,
kama ilivyo misemo ya Waswahili samaki mmoja
akioza wote wameoza mama yake naye
akajumuishwa katika kipigo hicho bila kujali afya
yake.
Hali ilizidi kuwa mbaya kwa mama David mpaka
majirani walipo wasili eneo la tukio na kumshika
mzee Kazinge.
”Jamani muwaisheni hospitali haraka huyu mama.”
Sauti za watu zilisikika huku wengine
wakimbembeleza David.
”Mwenye namba ya gari la hospitali apige upesi
bila hivyo tutachelewa” wazo lilitolewa na
kufanyiwa kazi haraka iwezekanavyo na baada ya
muda gari likaletwa.
Nisha na Dasoni pia waliamka baada ya zogo
kuwa kubwa. Walijikuta wakilia bila kujua kinacho
endele kutokana na umri wao, japo Nisha alikuwa
kigoli na Dason ni mdogo asiye pungua miaka tisa.
Mwana mama Muksini ambaye alikuwa wa
makamu alipowaona aliwafuata na kuwachukua
kisha kumuongezea kanga nyingine. Kwani Nisha
maumbile yake yalikuwa yameanza kuonekana
hasa nyonga na chuchu zilizo chongoka kwa kuwa
alitoka na kanga aliyo lalia tu. .
”Sasa jamani huyu mzee Kazinge tumpeleke kwa
mwenyekiti wakati mkewe akiwaishwa hospitali”
Alizungumza mzee Nyomolage.
Safari ikaanza baada ya kujigawa makundi mawili.
ambayo ni mzee Nyomolage, na mama Muksini
akiwa na kina Dason na mzee Mtepa pamoja na
mzee Kazinge mwenyewe wao walielekea njia ya
kwa mwenyekiti lakini kwa kumshikiria mzee
kazinge asije akawakimbia na pombe zake alizo
kuwa nazo kichwani.
David,Stallone,Junior na mama coolin wao
walielekea hospitali kumpeleka mama David.
Safari ya kwa mwenyekiti haikuchukua muda
maana hapakuwa mbali sana na kwa kina David
ndani ya dakika kadhaa wakawa wamewasili na
mzee Nyomolage ndie aliyegonga mlango......
”mwenyekiti,,mwenyekiti” sauti mbili tu zilitosha
kumuamsha mzee maige ambaye ndie alikuwa
mwenyekiti.
Mwenyekiti aliamka na kutoka nje akiwa amebeba
taa ya chemli iliimsaidie kuona kutoka na kuto
kuwa na umeme nyumbani kwake.
”Vipi jamani mbona usiku na mkusanyiko mkubwa
kuna nini!!? Aliuliza mwenyekiti kwa mshangao,
Mzee Nyomolage alionekana kuwa kiongozi wa
msafara kwasababu alikuwa jirani sana na mzee
kazinge hivyo swali hilo alijibu yeye,,,,,
”tumemleta mzee Kazinge alikuwa anawafanyia
vulugu familia yake na hivi tuna vyoongea mkewe
amewaishwa hospitali hali yake si nzuri ndugu
mwenyekiti”.
”Mzee Kazinge tatizo nini mpaka unaleta vulugu
kwa familia yako eeh? Mwenyekiti aliuliza
”umesha sema familia yangu nyinyi inawahusu nini
mbona mnakuwa wa mbea kuingilia mambo yasio
wahusu? We mwenyekiti si umelala na familia yako
nani aliyekuja kuku uliza kwa nini umelala eeh ni
jibu sasa”?
Majibu ya mzee kazinge yalionekana dhahiri
kutoeleweka kutokana na pombe aliyokuwa
amekunywa iliyo mlewesha kufikia hatua ya
kutojua anazungumza nini na mbele ya nani.
” Mzee Nyomolage na wenzio embu mfungeni
kamba kisha muingizeni ndani mpaka kesho
panapo majaaliwa pombe ikiwa imemusha
kichwani tutaendelea na mshauri haya”alizungumza
mwenyekiti.
Zoezi hilo likafanyika kwa haraka.
”Ndugu mwenyekiti basi na mimi naomba watoto
hawa wa mzee kazinge nikalale nao maana kwao
hakuna mtu kaka yao pia ameelekea
hospitali”.mama Muksini alionesha huruma kwa
watoto hao Nisha na Dason
”Hakuna shida mama ila kesho mjitahidi kuwahi
ilitujue tunafanya nini juu ya tatizo hili.
”Sawa na shukuru tutajitahidi” alijibu mama
muksini kwa heshima.
Muda huo huo mzee Nyomolage na wenzie
walielekea majumbani kwao na ilikuwa yapata
kama saa kumi kasoro hivi,njia nzima mazungumzo
yalikuwa juu ya swala hili.
*************
Watu walionekana wakipisha barabarani baada ya
kusikia king’ola cha gari la wagonjwa lililokuwa
mwendo kasi likiwasili katika eneo la hospitali ya
wilaya Gairo,pilika pilika za manesi zilifanyika kwa
haraka, kitanda chenye matairi kiliandaliwa
hatimaye mama David alishushwa kwenye gari na
kulazwa kwenye kitanda hicho,mbiombio
kilikimbizwa kuelekea icu (chumba cha wagonjwa
mahututi) maana hali yake ilionekana kuwa mbaya
zaidi.
.David hakuwa mbali nae alijipa majukumu ya
kusukuma kitanda hicho, macho ya David yalikuwa
kwa mama yake na sala nyingi zilimtoka ndani ya
moyo wake,
Kwakuwa moyo wake ulikuwa na uchungu usio
stahimilika kinywa chake kilitoa maneno ya
majonzi mbayo huweza kupekecha mwili na moyo
wa mtu yeyote yule mwenye roho ya kibina
adamu.
”Dokta jitahidini kuokoa maisha ya mama yangu
jamani”
”mama usituache wenyewe,tutakuwa kimbilio la
nani sisi”?
”Nisha na Dason wana kusubiri nyumbani nitakuwa
sina cha kuwaeleza ukiondoka”
Maneno hayo aliyokuwa anaya zungumza David
kwa sauti ya kuchoma moyo, yaliwafanya watu
waliyo yasikia kushika vifua vyao na kutingisha
vichwa vyao kusikitika kwa huruma
Baada ya mwendo wa mita kadhaa wakawa
wamefika kwenye chumba cha wagonjwa
mahututi .
Mmoja kati ya wauguzi alimzuia David asiingie
katika kile chumba na kumwambia,
”kijana usijali tutajitahidi kuokoa maisha ya mama
yako hivyo subiri kwenye benchi.” Aliketi lakini
aliendelea kulia kilio cha kwikwi hata maumivu ya
kipigo akawa hayasikii zaidi ya uchungu uliokuwa
ukitapatapa ndani ya moyo wake juu ya mama
yake.
Muda huo huo jamaa zake ambao walibaki kwenye
dirisha la mapokezi kutoa maelezo pia walifika
eneo alilokuwa David na kumfariji.
***************
.
Ndani ya chumba cha matibabu mama David
alionekana kupoteza fahamu hivyo ikabidi
wamshutue na kifaa maalumu, mipigo mitatu tu
ilitosha kurudisha fahamu yake hata vidole vyake
vilivyokuwa vimejikunja vilianza kutikisika na
kujikunjua taratibu,
Dokta aliyekuwa anaongoza jopo hilo la madaktari
walio kuwa wamevaa nguo sale zenye rangi ya
kijani na vikofia kichwani na kujifunga vitambaa
midomoni , alishusha pumzi baada ya kuona
graphu ya mapigo ya moyo inasoma ipasavyo
kwenye komputa , hata wenzie pia walishusha
pumzi juu ya zoezi hilo gumu la kumrudishia
fahamu mama David
”mungu mkubwa jamani” sauti ya dokta wa kike
ilisikika.
Lakini hata hivyo upumuji wake ulikuwa sio wa
kawaida ilibidi awekewe mirija maalumu
iliyounganishwa na hewa safi ya oksijeni ambayo
itamsaidia kupumua kwa muda mpaka hali yake
itakapo kuwa nzuri.
madaktari walipo maliza wakawa wanakusanya
vifaa vyao na kuhakikisha mgonjwa anaachwa
katika hali inayo ridhisha na chini ya uangalizi wa
manesi kisha kwenda kuendelea kutoa huduma
kwa wengine.
************
Sauti za Ndege zilianza kusikia na kijua chenye
miale myembamba iliyokuwa inapigana
kufukuza giza la alfajri kilianza kuchomoza, watu
wengi walio lala kwenye mabechi ya hapo hospitali
walianza kuamka,na wengine wakipishana kwenda
kwenye vyumba vya wagonjwa wakiwa wameshika
vitafunwa na chupa za chai,.wafagizi pia
waliendelea na usafi.ilikuwa yapata majira ya saa
kumi na mbili asubuhi ,
David alikuwa amejiinamia chini kwenye benchi
ambalo lipo kaaribu na chumba alicho kuwa mama
yake, majirani walio msindikiza walikuwa
wamepitiwa na usingizi kutokana na uchovu.
Kama ilivyo ada uchungu wa mwana ana ujua
mzazi hivyo David hakuwa na budi kujua uchungu
wa mama yake pia, uchungu huo ndio ulimfanya
kukosa hata lepe la usingizi,
.kichwa kilicho kuwa kimeinama chini kilinyanyuka
baada ya kushtuliwa na mlango wa chumba alicho
lazwa mama David, miguu ya David ilichanganya
kumfuata yule daktari aliye toka mle ndani na
kumshika koti lake na maneno yalio kuwa yana
muelemea moyoni mwake yaka mtoka,,,,,,,
”Daktari mama yangu anaendeleaje? tafadhali
usinifiche,,
Daktari alimtoa mikono David kisha kumshika
begani na kumueleza........
”hali ya mama yako inaridhisha kiasi ila kuna
mambo inabidi tukazungumzie ofisini kwangu”
Walifuatana mpaka ofisini na dokta alianza kumu
uliza baadhi ya maswali,,,
”kijana tatizo lilikuwa ni nini mpaka mgonjwa
anafikia hali ile mnaendelea kukaa naye nyumbani?
Swali hilo lilionekana ni kama kusifiwa na kipofu
umependeza, hivyo David alikaa kimya kutafakari
huku mawazo yalio kuwa yanaelea kichwani
mwake ni kwamba,,,
ITAENDELEA
 
SEHEMU YA PILI
Daktari alimtoa mikono David kisha kumshika
begani na kumueleza........
”hali ya mama yako inaridhisha kiasi ila kuna
mambo inabidi tukazungumzie ofisini kwangu”
Walifuatana mpaka ofisini na dokta alianza kumu
uliza baadhi ya maswali,,,
”kijana tatizo lilikuwa ni nini mpaka mgonjwa
anafikia hali ile mnaendelea kukaa naye nyumbani?
Swali hilo lilionekana ni kama kusifiwa na kipofu
umependeza, hivyo David alikaa kimya kutafakari
huku mawazo yalio kuwa yanaelea kichwani
mwake ni kwamba,,,
”kama nikimueleza kilichotokea baba anaweza
kuwa katika wakati mgumu”
wakati akiendelea kutafakari daktari alimuuliza kwa
mara ya pili na David akajibu,,
”matatizo ya kifamilia tu daktari” ila macho yake
yalionekana kuogopa hivyo yalimfanya daktari
kuhisi kuwa anamdanganya ndipo alipo mchimba
mkwara kutaka kujua ukweli,,
” Kijana haya ni maisha ya mama yako ukifanya
mchezo unaweza ukayapoteza huku unajiona, mimi
natakiwa kuandika taarifa juu ya mgonjwa huyu
unafikiri nitaandika nini? Mama yako ameonekana
ana majeraha sehemu za usoni, hali ambayo hata
wewe unayo hivyo basi mama yako hatopata
huduma nyingine mpaka taarifa zake zitakapo
kamilika pia kumbuka kwamba kwa sasa
ametibiwa kutokana na hali yake kuwa mbaya
lakini bila hivyo tusinge weza kumpokea bila
maelezo kutoka kituo cha polisi na baada ya wiki
mbili anatakiwa kufanyiwa upasuaji wa moyo wake
ukichelewa inabidi asafilishwe kwenda india
gharama zitakuwa juu yenu serikali haito changia
chochote kwa kuwa huu ni uzembe uliofanyika”
Daktari aliongea kwa hasira na kuhamaki.
Maneno hayo yalizidi kumpa wakati mgumu David
maana akifikiria baba anaumuhimu kwake na
mama ana umuhimu kwake nini afanye? Akajikuta
yupo njia panda na chozi jembamba likaanza
kumtoka mtoto wa kiume.
Baada ya mpigano wa mawazo kichwani mwake
akaona bora amueleze tu juu ya tatizo ambalo
limemkuta mama yake ili kuokoa maisha yake.
Daktari akawa anaendelea kuandika maelezo hayo
kwenye faili lake na alipo maliza akamruhusu David
aende nyumbani warudi mchana na chakula
huenda mgonjwa akawa anauwezo wa kupeleka
japo kitu mdomoni.
Daktari alipogeuza macho aliona tangazo lililo
bandikwa ukutani likisema ,,,,,,,
”PINGA UNYANYASAJI KWA WANAWAKE NA TETEA
HAKI ZA BINAADAMU” TANGAZO HILI LIMELETWA
KWENU NA WIZARA YA AFYA IKISHIRIKIANA NA H
ISANI YA WATU WA MAREKANI” Daktari alipo
maliza kulisoma alimwangalia David
ambaye pia macho yake yalilenga kwenye tangazo
lile, Tangazo hilo lilimfanya Daktari kupata wazo
nini afanye juu ya mzee kazinge.
David aliondoka ofisini kwa daktari akiwa na
huzuni huku akifikiria hatima ya wazazi
wake,alifika kwa wenzie ambao walikuwa wa
mesha amka , na macho yao yakigeuka huku na
kule ni dhahiri yalikuwa yana mtafuta David
hatimaye walimuona ameegemea ukutani akiwa
amewapa mgongo,wote walijikuta wakimuita kwa
pamoja David..........!!!!!!
Ndipo mama Coolin alipo nyanyuka kutoka kwenye
benchi na kwenda kusimama karibu naye.,,,
”ulikuwa wapi maana tulikuwa na wasiwasi kuto
kuwepo kwako” aliuliza mama Coolin
David alijikaza na kujitahidi kumjibu japo alikuwa
na kazi ya kuubembeleza moyo wake ambao una
majonzi,alivuta pumzi ya ndani na kumwambia,,,,
”nimetoka kwa Daktari”
”kasemaje ”? Mama coolin aliuliza kwa hofu,
“hali ya mama inaridhisha kiasi tofauti na alivyo
kuja pia anatakiwa kufanyiwa upasuaji ambao
unagharimu kiasi ki kubwa cha pesa kama kita
chelewa ugonjwa ukizidi atatakiwa asafirishwe
kwenda india kwa matibabu zaidi”
Kisha akakaa kimya kwa muda na mboni za
macho yake yakielekea kwenye chumba alicho
mama yake ukimya huo ulimfanya azidi kuduaa
mpaka alipo shtuliwa na kina Stallone ambao nao
walimsogelea,
“Vipi jamani mbona kimya kimezidi kuna
usalama”? aliuliza Junior,
“Kiasi chake upo” mama Cool alijibu,
Baada ya maongezi hayo David aliwaambiwa
waelekee nyumbani huku yeye akianza kujongea.
Na wenzie wakimfuata na safari hiyo iliyoanzishwa
ya kuelekea nyumbani wakiwa kwa miguu ikawa
inasindikizwa na maongezi ya hapa na pale kama
mama Coolin kuwa eleza wenzie kilichojiri kwa
Daktari kama yeye alivyo elezwa na David .
Walichukua muda wa masaa mawili mpaka kufika
njia panda ya mtaani kwao ambayo ndio iliyo
onekana kutaka kuwatenganisha kabla ya kuagana
ili kila mmoja akaendelee na shughuli zake ikiwemo
kupumzika kutokana na uchovu wa usiku kucha,
Davidi alipo taka kuelekea kwao taswira zilianza
kuelea kichwani mwake kwamba kitendo
anachotaka kuki fanya si cha kiuungwana cha
kutaka kuondoka bila kutoa shukrani zake kwa
wema alio fanyiwa na majirani zake alipo kumbuka
usemi mmoja kutoka kwa mwalimu wake
uliosema,,,,,,,
“mwenye busara hujifunza kwa mateso yake” ndipo
alipo thubutu kunyakuwa kinywa chake na kutoa
tabasamu la kirafiki lililosindikizwa na maneno ya
upole yalio mfanya mama Coolin kutoa chozi lenye
mchanganyiko wa furaha na huzuni huku wakina
stallone na junior midomo yao kuonekana kutaka
kusema neno,,,,
“Akili yangu iliyokuwa na upeo mdogo wa kufikiria
leo imeweza kuongezeka baada ya kufikishwa
katika ulimwengu wa faraja ndani ya masaa saba
ya shida, ambayo yalio nifanya niweze kumjua
mwalimu wa maisha na kujua nini maana ya
tatizo, huenda maneno yangu yasisadiki moyoni
kwenu ila naomba mzipokee shukrani zangu za
dhati mimi na familia yangu akiwemo mama yangu
kipenzi,ninyi ni binaadamu mnao stahili kuishi
katika hii dunia”
David alizungumza maneno hayo kwa unyenyekevu
sana ili walio msaidia mpaka mama yake kufika
hospitali wajue kuwa msaada wao unamuhimu na
ameujali kuliko ambavyo wao wangeweza kufikiria
maana wema ni akiba.
Junior nae alizidi kumpa moyo wa ujasiri
kukabiliana na tatizo ambalo lipo mbele yake,,,
“David, thamani ya mtu inakuja pale yeye
mwenyewe anapo jithamini hivyo hatukuwa na
budi kuonesha ushirikiano wetu kwako juu ya
tatizo lako isitoshe sisi ni vijana ambao tuna
tarajia kuja kuwa wazazi wa baade tusipo pendana
na kujaliana matatizo yetu hata watoto zetu
hawato pendana hizi ni changamoto katika maisha
tupo pamoja mpaka mwisho wa tatizo hili.
Upendo huo ulio oneshwa hapo ulimfanya kila
mmoja kujiona ni miongoni mwa watu wema sana
katika dunia maana kila mmoja alitambua thamani
ya mwenzie.
mama Coolin pia aliweza kuahidi kuandaa chakula
cha mgonjwa hivyo aliomba aruhusiwe awahi
kukipika, basi wote wakakumbatiana na kila mmoja
kuelekea kwake.
*****************
Ukimya ulio tanda kwenye nyumba ya kina David
ulimuogopesha sana na akiangalia milango yote
imefungwa jukumu la kuanza kuita lika chukua
nafasi mdomoni mwake,,,
Baba!!!!!!? Baba!!!!..,? nisha !!!!!? Lakini bila
mafanikio zaidi ya sauti zilizo kuwa zinajirudia
rudia kumkera tu maskioni mwake ghafla alishtuka
alipo vutwa shati kwa nyuma na shingo yake ilipo
geuka kumbe alikuwa ni Dasoni hakuwa na budi
kuitoa ile sura yenye mikunyanzi usoni mwake na
kumbeba mdogo wake kipenzi,
Alipo taka kumuuliza nisha yuko wapi macho yake
yaliweza kumuona kwa mbele Nisha akija huku
akiambatana na mama Muksini, walipo wasili
karibu yake mama Coolini alimueleza,,,,,
“milango niliifunga jana baada ya nyie kwenda
hospitali baba yako tulimpeleka kwa mwenyekiti
hivyo alilala huko kutokana na pombe alizo
kunywa na huu mguu tulikuwa tunaelekea huko ila
Dasoni ndiye alie wahi kukuona wakati ukija hapa
ndio maana akakukimbilia”
Alipo maliza aliuliza hali ya mgonjwa na jibu likawa
lilelile alilo wapa wakina mama Coolin.
“Basi tuongozane twende wote huko”David
alimueleza mama Muksini,
“David jihurumie na wewe ungeoga kwanza kisha
uendee nyumbani kwangu Yule masichana wangu
wa kazi akupatie chai ndio uje maana hiyo kesi
haiwezi kuendeshwa bila wewe kuwepo”mama
Muksini alimueleza David baada ya kumuhurumia
lakini kwa David haikuwa hivyo,,
“nashukuru sana kwa ukarimu wako lakini kiukweli
sina hata hamu ya kula kitu chochote kile kwa
sasa ni vyema tuwahi huko kwa mwenyekitini ili
tujue kinachoendelea huenda hata yeye Baba
akawa na wasi wasi juu ya hali ya Mama”
Mama Muksini kutokana na maelezo ya David
akawa hana kipingamizi ikabidi waongozane
kuelekea kwa mwenyekiti na walipo anza kuiona ile
bendera ya chama cha mapinduzi (ccm) iliyo
chakaa ikipepea juu ya mlingoti David alifanikiwa
kumuona Baba yake akiwa na mwenye kiti
wakitoka ndani kwenda kwenye mabenchi ambayo
wakina mzee Nyomolage walisha wasili kitambo
huku akiwa amesha funguliwa zile kamba alizo
fungwa usiku na pombe zilisha kwisha kichwani.
Moyo wa hasira ulimshika David alipo kumbuka
hali ya Mama yake kule hospitalini lakini alijikaza,,,
Miguu yao ilipo kanyaga eneo lile macho makavu
ya David yalionza kubadilika rangi kutaka kuwa
mekundu kutokana na hasira yalipo gongana na
mzee Kazinge ana kwa ana na moyo wa mzee
kazinge ukionekana kuteseka na aibu kwa kitendo
alicho kifanya maana Alisha elezwa yote yalio
tokea na mwenyekiti wakati walipo kuwa
wanajibizana akiwa anafunguliwa zile kamba alizo
fungwa.
Bila kuchelewa ndugu mwenyekiti akaanzisha kikao
na swali kwa David juu ya hali ya mgonjwa
kwanza.. Jibu alilo toa David lilizidi kuchokonoa
aibu iliyo jificha kwa mzee kazinge kufikia hatua ya
kuinama chini lakini mwenyekiti aliendelea kuuliza
maswali mengi mengi ambayo yalichukua muda
mwingi mzee Kazinge kuya jibu mpaka ilipo timia
saa saba kasoro hakuna jibu wala sababu ya
msingi ambayo iliyomfanya mzee kazinge kumpiga
David na mkewe.
Mwenye kiti ndipo alipo amua kutaka kukata shauri
kwa kuruhusu mzee Mazinge apelekwe kituo
kidogo cha polisi kwa matatizo aliyo msababishia
mkewe mpaka kulazwa.
Kutokana na hatua aliyofikia mwenyekiti ilimtisha
mzee Kazinge alipofikiri kuiacha familia yake kwa
mara ya pili tena kwa ujinga , na yeye kwenda
gerezani, kilimuumiza sana na kuleta mlipuko
mkubwa wa mamumivu mwilini mwake na chozi la
kujilaumu likaanza kumtoka hali ambayo ilileta
huzuni kubwa kwa kina Dason na Nisha,.
Ali watazama na kufikiria kama mkewe atakufa
hospitali ni zahiri safari hii ataukumiwa kifungo
cha maisha.ndipo macho yake yalipomtazama
David kisha kugeukia upande wa kina Nisha na
Dason ambao walipakatwa na mama Muksini kisha
kuanza kusema,,,,,
“Mwenyekiti kwanza naomba radhi kwa niliyo
yafanya naamini kwangu ni hasira na pombe
ambazo ndizo zilizo nifanya nitende hivi, pia familia
yangu ambayo naipenda sana najua ni vigumu
kuomba radhi kwenu lakini naomba mnisamehe pia
mkaniombee msamaha kwa mama yenu maana
nikienda kituoni huenda nisionane na nyie tena
wala mama yenu.
“ Kikubwa ni kwamba familia hii sio maskini ila
kuna mambo ambayo yamejificha leo ninge penda
kuwa eleza zile kumbukumbu ambazo niliapa
hazito saulika katika maisha yangu yote David
najua unajua ulicho kiona kwa macho yako ila
chanzo hukijui. Tega sikio ili ujue kwanini
nilikukataza usiendee mjini kwa wakati huu. Wote
walijikuta kukaa kimya huku macho na maskio ya
David yakikaa kiudadisi kutaka kujua chanzo
Mzee kazinge anaanza kuwa simulia,, ilikuwa
mwaka 2002
Ilikuwa mwaka 2002 ndani ya jiji la dar es saalam
nikiwa mfanyakazi katika NMB banki iliyopo tawi la
magomeni katika kitengo cha mikopo, kitengo
hicho kilinifanya nifahamiane na watu wengi sana
na wenye tabia tofauti kutokana na ukalimu nilio
nao.
Japo niliiamini kuwa hata uwe mwema kiasi gani
lazima utakuwa na maadui wanao kuzungua, hao
pia nili jitahidi kuishi nao.kila ofisi utakayo kwenda
kama ikiwa na wafanyakazi thelathini basi kumi na
watano lazima walikuwa wanalifahamu jina la
Alfred Kazinge
Miaka ilivyozidi kwenda huku nikiwa tayari nina
watoto wa wili David na Nisha, jina langu
lilijulikana zaidi ndani na nje ya jiji la dar es
saalam hasa na wafanya biashara waliokuwa
wanaingia na kutoka. nilikuwa na pokea simu
nyingi sana kiasi ambacho zingine zikawa zinaleta
ugomvi kwa mke wangu magrety .(mama david)
Umaarufu huo ulianza kuniletea dosari katika kazi
yangu baada ya kumpata rafiki Helman ambaye
ndio nikamfanya ndugu yangu wakaribu baada ya
kuhamia hapo jijini dar es salaamu kutokea mkoani
Tanga ambapo ndipo walipo baadhi ya ndugu
zangu. Na makaburi ya wazazi wangu yalipo.
Bwana Helman alianza kunifanya nichelewe kurudi
nyumbani kwangu kwa kunipitisha sehemu nyingi
za anasa na kunikutanisha na marafiki zake ambao
wengi walionekana ni wenyeji wa Arusha,.kila
walipo kaa walikuwa wanazungukwa na wasichana
ambao nilikuwa nashindwa kuwaangalia kwa mara
ya kwanza kutokana na nguo zao za anasa walizo
kuwa wanavaa.
Hivyo sehemu hizo za starehe zilinifanya
kumgeuza mke wangu magrety kuwa mlinzi wa
nyumba na mtunza muda kwa kuangalia saa ya
ukutani ni saa ngapi narudi na alipo sikia honi ya
gari majukumu ya kufungua mlango pia aliyabeba
na alinivumilia sana hata nilipo amia dunia
nyingine yenye utembeaji wa kupepesuka( ya ulevi)
ITAENDELEA
 
Hongera na angalizo kama una uhakika hadithi itafika mwisho tujuze mapemaa coz imekuwa kama daladala jioni hazikawii kukatisha luti ila ni kwa nia njema mleta uzi maana hii ni khatari sana kuwaacha watu na kiu bila kujua khatma ya kitu.
 
Hongera na angalizo kama una uhakika hadithi itafika mwisho tujuze mapemaa coz imekuwa kama daladala jioni hazikawii kukatisha luti ila ni kwa nia njema mleta uzi maana hii ni khatari sana kuwaacha watu na kiu bila kujua khatma ya kitu.

usiwe na shaka mkuu hapa ni mwanzo mwisho
 
SEHEMU YA TATU.
Bwana Helman alianza kunifanya nichelewe kurudi
nyumbani kwangu kwa kunipitisha sehemu nyingi
za anasa na kunikutanisha na marafiki zake
ambao
wengi walionekana ni wenyeji wa Arusha,.kila
walipo kaa walikuwa wanazungukwa na
wasichana
ambao nilikuwa nashindwa kuwaangalia kwa
mara
ya kwanza kutokana na nguo zao za anasa
walizo
kuwa wanavaa.
Hivyo sehemu hizo za starehe zilinifanya
kumgeuza mke wangu magrety kuwa mlinzi wa
nyumba na mtunza muda kwa kuangalia saa ya
ukutani ni saa ngapi narudi na alipo sikia honi ya
gari majukumu ya kufungua mlango pia aliyabeba
na alinivumilia sana hata nilipo amia dunia
nyingine yenye utembeaji wa kupepesuka( ya
ulevi)
Nakiri kuwa sikuwahi kumpiaga mke wangu hata
nilivyo kuwa katika hali hiyo. Ilifika kipindi nikawa
na kosa hata muda wa kuzungumza na watoto
wangu vipenzi japo kwa wakati huo David ndiye
aliye kuwa na akili ya kunijibu na kunielewa nini
na
zungumza pia kwa utoto wa Nisha wa kuzunguka
zunguka na kupiga kelele pale subuleni wakati wa
mazungumzo ya hapa na pale ili kuendelea
kujenga amani na upendo niliukumbuka pia;
Namshukuru sana mke wangu siku ya jumamosi
majira ya saa tatu usiku nikiwa tayari
nimejiandaa
kutoka ndipo alipo niweka chini na kunikumbusha
mateso niliyo yapitia wakati na soma shida ngapi
nili pata na leo na tumia fedha bila kujali kuwa
kuna watu wenye shida duniani pia hata upande
wa penzi lake, baba yake alikuwa na fedha kiasi
ambacho yeye aliweza kuniibia na kunipatia ili
niweze kuendeleza masomo yangu na kujikimu
kwa
mahitaji madogo madogo.
Hakika jambo hilo lili niingia kichwani na kuona
kuwa Helman sio rafiki mzuri kwangu
sikuchelewa
niliingiza mkono mfukoni na kutoa nokia yangu
kisha kubonyeza vitufe 0654000092 na kupiga
sekunde kadhaa simu ikaanza kuita na muda huo
huo ikapokelea nilicho anza kukisikia ni kelele
nyingi za mziki na sauti za wanawake
tofauti ,hivyo nilijua tayari wamesha wasili baa na
wenzie wanakunywa pombe tu, akanzaa
kuongea,,,
“hallo uko wapi wewe mbona tunakusubiri
hutokei”? Aliuliza Helman kwa sauti ya juu ili
aweze kusikika kutoka na eneo alilopo
“Helman naomba usogee sehemu yenye utulivu
kidogo ili tuzungumze”nilimwambia
“Eeh uko wapi sasa? maana huku warembo
wanakusubiri kwa hamu uje kuwa mwagia pesa”
sauti hiyo aliyo ongea Helman, Magrety aliweza
kuisikia alizidi kujua vitendo alivyo kuwa na
vifanya
mme wake,Alfredy, aibu ikamshika Alfred ndipo
alipo zungumza kwa ukali,,,,,
”Sikia Helman kuanzia sasa urafiki wetu mimi na
wewe umeisha siwezi kutelekeza familia yangu
sababu yako na hata ukija ofisini nita kuhudumia
kama wateja wengine na sio kama rafiki yangu
pia
nyumbani kwangu sikuhitaji”
kisha akakata simu. upande wa Helman akawa
anaendelea kulalamika,,,,,
“hallo?,hallo? Lakini bila mafanikio alipo itazama
simu yake akagundua kuwa ilisha katwa muda
mrefu , oooh shit!!! Ndio neno li lilo mtoka.Helman
Akaondoka kwa mwendo wa haraka kuelekea
walipo wenzie walio kuwa wanajiburudisha na
warembo alifika huku akihema na kuzungumza
kwa
jazba…
“Jamani mpango wetu unaanza kuharibika yani
kama huyu jamaa ameotea dili vile au kuna mtu
kamvujishia huyu eeh?
Wote walihamaki! Na mmoja wao kuuliza kwanza
kafanyaje kwasababu leo si ndio tumepanga akija
tumalize kila kitu na tujue mchongo tuna useti
vipi?
“Alfred amekataa kuja na kasema kuwa hataki
urafiki na mimi maana mimi sio rafiki mzuri kwa
maneno haya huoni kama kanishtukia? Helmani
alizungumza na kuendelea kusema kwa hasira
huku akipigapiga mikono yake kwenye meza.
wakataka kuharibiana wenyewe ndipo walipo
kubaliana wafanye jambo.
****************
Nilipo kuwa naomba radhi kwa mama David
ghafla
muito mfupi kwenye simu yangu uliita nilipo
angalia nikakuta ni namba ngeni imenitumia
ujumbe nilishikwa na woga nilipo ona ujumbe ulio
andikwa,,,
“KAZI YETU KWAKO HAIJAISHA MPAKA LENGO
LETU LITA KAPO TIMIA”
kisha mbele akaandika maneno yalio ashiria
kucheka,,,
”hahahaha!!!!!!!”
Nilipigwa na butwaa hali iliyo mfanya mke wangu
mama David kuwa na wasiwasi naye akaichukua
ile simu na kusoma ujumbe ule, kabla hajamaliza
ghafla hodi ikawa inagongwa kwa nguvu sana
wote
tulizidi kushikwa na woga kila mmoja aliwaza
huenda ni Yule aliye tuma ujumbe ule wa vitisho?
lakini hatukuwa na uhakika tukajikuta
tumesogeleana na bahati nzuri Nisha na David
kila
mmoja alikuwa chumbani kwake hivyo
hawakuweza kujua kile kilichoendelea pale
sebleni.
Ikabidi nijikaze na kumwambia mama David
alekee
chumbani maana hatujui nani anaye gonga majira
yale ya usiku na hatukuwa na mazoea ya ugeni
wa
usiku bila taarifa na getini amepita vipi mtu huyo
anaye gonga mlango nilitazama huku na kule
nikakuta mchi wa kinu kidogo nika uchukua
nakuelekea mlangoni hakika sikuamini nilicho
kiona
mbele ya macho yangu
Nguvu ziliniishia na ule mchi mdogo nilio ushika
ulianguka chini kisha nikashusha pumzi ndefu,
kumbe alikuwa ni Sagu kijana ambaye alikuwa
anasimamia ujenzi wa nyumba yangu hii ninayo
ishi sasa hapa gairo ambayo niliamua kuijenga
kwa siri na huku mbali kwa sababu kama
kampuni
ingejua najenga wangeanza kunifuatilia na kuhisi
huenda nikawa naihujumu.
Basi nilimkaribisha japo aliuliza maswali ya hapa
na pale mbona na hema kiasi kile na nimeshika
mchi kama navizia kitu fulani cha hatari lakini
nilimpa majibu yalio mlizisha na hakujua kilicho
kuwa kina endelea kwa muda huo, hivyo tuliketi
na
kuanza mazungumzo,,,,,
“Sagu mbona usiku na bila taarifa? Nilimuuliza
”aisee bosi samahani kwani nilijaribu kupiga simu
yako ila mtandao ulikuwa unasumbua” alinijibu
Nikamtazama kwa makini lakini kila nilipo taka
kumuliza swali getini aliingiaje mdomo wangu
ulikuwa mzito niliwaza mambo mengi kichwani
mwangu kwa muda mchache nilio kuwa na
mtazama mpaka sauti ya mke wangu Magrety
iliposikika kutokea chumbani ,,,,,
”Eeh shemeji umekuja saa ngapi? Alimuuliza Sagu
kwa kuzuga
“Muda mrefu shemeji yangu wazima hapa? sagu
Alijibu na kuuliza hali
“Sisi wazima mnatunyima nini huko?Magrety
aliuliza huku akiweka kisura cha kujichekesha
asishtukiwe kama alitoka kwenye hofu
“huko tuta wanyima nini zaidi ya mvua
zinazoendelea kunyesha na viazi kuzidi
kunawaili”?
Baada ya mazungumzo hayo mafupi Magrety
alinyanyuka na kwenda kumuandalia chakula
Sagu
nasi tukawa tunaendelea na mazungumzo,,,,
“Mmh Sagu niambie ujio wako kama unautofauti
na siku nyingine?nilimuuliza
“hapana bosi ni ulele tu vifaa vya ujenzi
vimepungua hivyo nime ona bora nije ili
nimalizane
na wewe ukabidhiwe nyumba yako baada ya
muda
mfupi”alinijibu
“basi hakuna shida kesho nitakupatia fedha ili
ukaendelee na ujenzi” nilipo mjibu nikanyanyuka
na
kumuaga na kumtakia usiku mwema wakati yeye
akielekea kula na kwenda kwenye chumba cha
kumpumzika maana alikuwa sio mgeni.
Usiku nilipata usingizi wa mang’amu ng’amu
sana
niliwaza kila neno ambalo mke wangu aliniambia
na kuufikiria zaidi ule ujumbe nilio tumiwa, mke
wangu alizidi kunionea huruma kwa hali ilivyo
badilika ghafla kutoka kwenye furaha mpaka
kufikia huzuni ambao hata yeye hakutegemea kwa
muda ule kama ungeweka makazi ndani ya mioyo
yetu, ila kinywa chake hakikusita kutamka
maneno
haya ambayo yalimpendeza mungu,,
“mme wangu kesho tukiamka salama tuelekee
kanisani tuka fanye maombi maana hali ina anza
kuwa tete”
Hakika nilijikuta nikimporomoshea mvua nyingi ya
mabusu usoni mwake kisha nikamueleza,,
“mke wangu wewe ni mwanamke ambaye
umetumwa kuja kunibadilisha mimi katika dunia
hii
na kunipa faraja ambayo wengine wanaikosa
nakushukuru sana mama David” nilizungumza
maneno hayo huku uso wangu ukionesha
masikitiko makubwa kwa yote niliyo yafanya
nyuma.
Mke wangu akanisogelea taratibu na kuniangalia
kwa sekunde kadhaa usoni kisha akaachia
tabasamu la kimahaba na kulaza kichwa chake
juu
ya kifua changu ,
kutoka kwenye tabasamu lile niliweza kuhisi
alichofikiria huenda hakuamini kama nimeamua
kubadilika kwa muda mfupi kiasi kile.
kule kumisi kulala mapema na mimi kulimfanya
apitiwe na usingizi mapema lakini kwangu ilikuwa
tofauti mpaka kulipo kucha baada ya kumshwa
na
jogoo la kwanza.
Tuliamka wote tukajiandaa na kuibeba familia
yangu kwenye gari yangu aina ya BMW230 safari
ikawa kuelekea kanisani kama mke wangu alivyo
nishauli lakini kabla hatuja fika nilimshua Sagu
njiani ambaye pia tuliongozana nae kutoka
nyumbani na kumpatia kiasi cha fedha kwa ajili
ya
vifaa vya ujenzi na nauli ya kurudi Morogoro.na
baada ya muda tukawa tumefika kanisani ibada
iliendelea vizuri ila tulikaa mabenchi tofauti mimi
na mke wangu, na watoto wetu walienda kukaa
na
watoto wenzao kwa kuwa tulikuwa tumechelewa
hivyo mabenchi mengi yalikuwa na nafasi chache.
Wakati ibada ikiendelea nilihisi kutekenywa na
kitu
mfukoni nilipo toa ilikuwa ni simu yangu ambayo
niliweka muito wa kimyakimya ili isipige kelele
tukiwa ibadani, macho yangu yalipigwa na
bumbuwazi kuona tena namba ngeni ikiwa
imetuma ujumbe ambao nilianza kuwa na
mashaka
nao, ujumbe wenyewe ulisomeka hivi,,
“TUKO NJE TUNA KUSUBIRI UKITOKA UJE
KUCHUKUA MZIGO WAKO”
Maneno hayo kwa kweli yalizidi kuniogopesha
maana nikagundua kuwa kuna watu wameanza
kunifuatilia kama ni swala la kwenda kanisani
mawazo tulipata usiku mimi na mke wangu ndipo
tukaamua kuwaanda na watoto wetu tukaja
kanisani sasa wamejuaje kama tupo kanisani
moyo
ukaanza kuingiwa na wasiwasi juu ya Sagu.
Nilishindwa kuvumilia kukaa ndani ya kanisa
hivyo
nikatoka kwa mwendo wa haraka hali iliyo
wafanya
walio karibu nami kunishangaa maana
nilionekana
kama mtu aliyechanganyikiwa huku nikiwa na
bonyeza vitufe kutafuta namba ya Sagu nilivyo
fika
tu nje ikawa tayari inaonekana mbele ya mboni
zangu hapo mkono wangu ukaanza kubonyeza
kile
kitufe cha kijani kumpigia sagu na kuweka simu
sikioni nilizidi kushikwa na hasira baada ya
kujibiwa,,,,
”Ndugu mteja namba unayopiga kwa sasa
haipatikani jaribu tena baadae”
Nilipiga zaidi ya mara nne na jibu likawa lile lile
na
mawazo ya ule ujumbe wa kwanza ukawa kama
umenitoka kwa muda kichwani baada ya
kuchanganywa na muhudumu aliye nijibu wakati
nikiwa na mpigia Sagu, sikuwa na jinsi ilinibidi
nichukue maamuzi ya kutaka kurudi tena ndani
ya
kanisa,nilivyo piga hatua tatu kabla sijaukalibia
mlango wa kanisa ujumbe mwinigine ukaingia
hapo ulinifanya nigeuke nyuma na kupepesa
macho
yangu pande zote kama nitamuona yoyote
ambaye
anafahamiana na mimi huenda nikamjua huyu
anaye nitumia ujumbe usio eleweka kama huu
uliongia na kunieleza kuwa……..
“VIPI IBADA IMEISHA MBONA UMEWAHI
KUTOKA?”
Hapo sikuchelewa tena nikapiga haraka namba
hiyo iliyo nitumia ujumbe bahati nzuri ikawa
imepokelewa mdomo ukawa na kihere here cha
kuongea,,,
”Hallo? Hallo?
Hallo?hallo?
nikajikuta naongea peke yangu, nilipo toa sikioni
kuingalia ilikuwa bado ipo hewani nilizidi
kuchanganyikiwa mpaka nikaanza kujuta kwanini
nilienda kanisani na familia yangu maana
imeshaonekana ni hatari inayo taka kunikumba
lakini ghafla nikasikia sauti kwa mbali ikiongea
ndipo nilipo weka tena simu sikioni,
Hallo? Nilizungumza na bahati nzuri muhusikia
naye alianza kuzungumza ila nilishtuka baada ya
kusikia ananza kutaja jina langu tena ilikuwa ni
sauti ya kike,,,
“Hallo mr.Alfred kazinge”? alizungumza nami
sikutaka kupoteza muda nikamjibu kwa sauti ya
ukali bila kujali eneo nililopo
“Wewe ni nani na unataka nini toka kwangu”?
Nilihamaki
”hahahahaha” alicheka kwa dharau kisha
akaendelea kujitambulisha
”haina haja ya kunijua jina maana haito saidia
cha
msingi toka hapo ulipo na sogea mbele utakuta
kuna gari aina ya range nyekundu imepaki uje
kuchukua mzigo wako.
Nami nilifanya kama walivyo niagiza ilinibidi
nielekee mahali nilipo elekezwa, mwendo wa
hatua
kadhaa tu ulinifanya niwe nimewasili eneo lile na
nilipokuwa nashanga shanga mara kioo cha gari
lile aina ya range kikashushwa na mkono
ukaonesha ishara ya kuniita nikasogea mpaka
kwenye dirisha lile lakini aliyetoa kichwa chake
nje
huku uso wake ukiwa umefichwa na miwani meusi
hakua mwanamke kama sauti niliyo isikia kwenye
simu, alikuwa mwanaume tena aliye kuwa
amekomaa sana kwa mtazamo.
Nilipotaka kujua kama kuna mwanamke mle ndani
iliniweze kumuuliza anashida gani na mimi, nafasi
hiyo nilinyimwa baada ya kukabidhiwa bahasha
kubwa ya kaki iliyo kuwa imetuna kiasi kisha gari
hilo kuondoka kwa mwendo kasi sana lakini nilipo
taka kuifungua bahasha hiyo ilinijue kuna nini
nilishtushwa na breki iliyo kuwa imebanwa ghafla
kama vile dereva anayetaka kukwepa ajali ya
kugonga, hivyo uso wangu ulibidi utazame
kwenye
gari lile ila nilicho kiona ni yule jamaa aliye
nikabidhi ule mzigo akitazama nyuma yangu huku
akitingisha kichwa chake kama amegundua kitu
fulani hivi.
ITAENDELEA
 
SEHEMU YA NNE
Nilipotaka kujua kama kuna mwanamke mle ndani
iliniweze kumuuliza anashida gani na mimi, nafasi
hiyo nilinyimwa baada ya kukabidhiwa bahasha
kubwa ya kaki iliyo kuwa imetuna kiasi kisha gari
hilo kuondoka kwa mwendo kasi sana lakini nilipo
taka kuifungua bahasha hiyo ilinijue kuna nini
nilishtushwa na breki iliyo kuwa imebanwa ghafla
kama vile dereva anayetaka kukwepa ajali ya
kugonga, hivyo uso wangu ulibidi utazame
kwenye
gari lile ila nilicho kiona ni yule jamaa aliye
nikabidhi ule mzigo akitazama nyuma yangu huku
akitingisha kichwa chake kama amegundua kitu
fulani hivi. Nilipogeuka alikuwa
Ni mama David na David hapo akili yangu ikabidi
ichekeche kwa haraka na jibu nililo pata ni
kwamba
yule jamaa atakuwa amejua kuwa hii ni familia
yangu na nilipo mgeuzia shingo kwa mara ya pili
nilizidi kuogopa baada ya kumuona
ametengeneza
umbo la bastola kwa kutumia kiganja chake cha
kulia na kuonesha ishara kuwa atawashuti, kisha
gari hilo likaacha vumbi na kuishia zake,hata
hamu
ya kutaka kujua kilichopo kwenye ile bahasha
sikuwa nayo nilicho kifanya ni kwenda kumshika
mkono David na kumwambia Magrety
akamchukue
Nisha tuondoke nyumbani ila kwa hasira nilitaka
kumchapa vibao Magrety kwa maneno aliyo
niambia,,,,,,,,
”mume wangu tatizo nini mbona ibada haija
isha”?
“fanya kama nilivyo kuambia kamchukue nisha
haraka macho huna hata sauti husikii?
Niilizungumza kwa sauti ya ukali bila kujali kuwa
baadhi ya watu walikuwa wana tutazama
Magrety hakukaidi agizo hilo, walipo wasili tu
niliwasha gari safari ikawa kuelekea nyumbani
hakika mwendo nilio kuwa naenda nao kama
askari wa barabarani wangeniona wasingee sita
kunikamata niliwakosakosa kuwagonga watoto
wenye tabia za kucheza barabarani lakini
nilimshukuru mungu baada ya kufika salama.
Mimi na mke wangu tukaelekea chumbani huku
nikiwa nimeshika ile bahasha mkononi na kina
David kuwaacha sebuleni baada ya kuwa
nimemuonya David asithubutu hata kunyakua
mguu wake kuutoa nje pia amuangalie Nisha
asicheze mbali naye nilifikia kukaa juu ya kitanda
huku mama David akiwa ana lalamika mwenyewe
“maisha gani haya tunayoanza kuishi?
”Hatuna amani nayo kabisa au kuna mtu
umemkosea mme wangu? Aliniuliza .
”Hakuna mtu niliye mkosea wala kumdhulumu
haki
yake mimi mwenyewe na shangaa haya yanayo
tokea ghafla hivi!!! ila yote ni mitihani tu katika
maisha mke wangu inabidi tupambane nayo sio
wote watakao kupenda wengine ni wanafiki”
Ilibidi niwe mpole na kusimama kama mwanaume
kwenye nyumba maana mke wangu asije
kupoteza
dira kabisa hata ya kutoa mawazo kama na mimi
ningeamua kunyong’onyea.
Baada ya kumuona kidogo anaanza kutulia
nikaichukua ile bahasha na kuanza kutaka
kuifungua ila mke wangu akauliza,,
” kuna nini humo”?
”Ngoja tufungue kwanza ili tujue kuna nini”
nilimjibu
Nikatoa gundi iliyo kuwa imebandikwa kama
kufuli
ya bahasha na kilichokuwa ndani kila mmoja
alishika mdomo, tulitazamana kwa mshangao
kisha nikaingiza mkono ndani ya ile bahasha
nilicho anza kutoa yalikuwa ni maburungutu ma
tano ya fedha mpya na kila burungutu lilikuwa na
kiasi cha milioni tano hivyo jumla yalikuwa yana
thamani ya milioni ishirini na tano
”Nilijiuliza fedha hizi ni za nini? Wakati huo mke
wangu alizidi kupagawa na macho yalimtoka na
kuendelea kutazama ile bahasha.
Nilipo ingiza mkono mara ya pili nikatoa karatasi
iliyo kuwa imeviringisha kitu fulani kigumu na
nilipoikunjua mapigo ya moyo yaliongeza kasi na
mke wangu alinyanyuka pale kitandani tulipo
kuwa
tumeketi kwa mshtuko na kusema kwa sauti ya
mshangao,,,,
”aaah bastola”? Yesu kristu balaa gani hili mume
wangu? Aliuliza maswali yasiyo kuwa na majibu.
Niliishika bastola ile kisha kuigeuza geuza zaidi
ya
mara mbili baadae nikagundua kuwa karatasi ile
iliyoviringisha bastola ilikuwa na maandishi yalio
nipa maelekezo juu ya ile bahasha,,,,,,,,
”HIZO FEDHA NI KIASI CHA AWALI KABLA YA
KAZI
TUNAYO TAKA KUKUPA, NA KAZI ITAKAPO
KAMILIKA UTAMALIZIWA KIASI KAMA HICHO PIA
HIYO BASTOLA SIO KIFAA KITAKACHO TUMIKA
KATIKA KAZI YAKO ILA UTAKITUMIA KUIMALIZA
FAMILIA YAKO KWA MKONO WAKO MWENYEWE
KAMA UTAKAIDI AGIZO LETU.
ITAKAPO FIKA SAA 4:30 USIKU NJOO TUKUTANE
PALE LANDMARK HOTELI YA RIVERSIDE
UBUNGO.KWA MAZUNGUMZO ZAIDI BILA
KUSAHAU
HIYO BASTOLA ”0768606510 NDIO NAMBA
UTAKAZO TUMIA KUTUTAFUTA UKIFIKA.
Ujumbe huo nilio kuwa na usoma kwa sauti ili
mke
wangu pia asikie ukazua taflani kwa muda huo
baada ya mke wangu kupandwa na hasira na
kuanza kunipigapiga na mikono yake kifuani huku
akilia na yote hayo ni kwasababu ya upendo
alionao kwa watoto wake,,,,
”sitaki mimi Alfred hayo mambo yako kama
ulikuwa unafanya na wenzio mmalizane wenyewe
sio kutuingiza na sisi watoto wangu nawapenda
sana”
Alilalamika kwa muda kisha kuondoka chumbani
kwa hasira na kwenda kwa watoto wake nami
nilibaki chumbani nikiendelea kufikiria ni kwanini
yanatokea haya kuna nini nilicho kifanya kwa
mtu?
Japo mawazo yakawa yananijia na kuanza
kumshtumu pia Helman lakini kila nikijiuliza mara
mbilimbili ni kipi nilichomkosea sikupata jibu na
kama kukataa mimi na yeye tusiwe marafiki ndio
anifanyie hivi mbona mambo yanayo nitokea ni
makubwa kuliko hilo la urafiki? Hayo ndio
mawazo
yalio kuwa yana zungukazunguka ndani ya
kichwa
changu.
Magrety alishinda na watoto wake siku nzima bila
kurudi chumbani wala kuniita kwenye chakula
japo
hata kama angeniita nisinge weza kula maana
yalio nikuta kwa muda mfupi nilihisi kushiba,
nami
nilishinda ndani mpaka kiza kika ingia nilipo
tazama saa yangu ikawa inaniambia ni saa 3:30
usiku hivyo nikaona muda huo unanifaa sana
kujiandaa ili kwenda kuonana na wapuuzi nisio
wajua. Maana kutoka magomeni mpaka maeneo
ya ubungo ningeweza kumudu foleni kwa muda
huo.wa usiku.
Nilipo maliza tu kujiandaa nikachukua biblia
yangu
kisha kupiga magoti chini ya kitanda na kuanza
kumuomba mwenyezi mungu..
.
”eeh Mungu baba mimi kijana wako nina nyoosha
mikono yangu kwako kwa kuwa wewe ndio unaye
jua vinavyo onekana na visivyo onekana naomba
unilinde mimi na familia yangu,umlinde mke
wangu
kipenzi na huko niendako naomba nirudi salama
maana sijui ninacho endea ila ni katika hali ya
kuilinda familia amin,
Baada ya sala hiyo fupi nilirudiaha biblia yangu
kabatini kisha kuchukua ile bastola na kuiseti
vizuri.
wakati naendelea na kitendo hicho Magrety
akaingia, alishtushwa na kitendo nilicho kuwa
nakifanya maana usoni mwangu nilisha tengeneza
v na kama alijua nilichokipanga vile kwamba
kama
kuna mtu atanilitea ujinga na muua hapo hapo.
Magrety alinisogelea na kunieleza
”Nakuomba mume wangu usiende huko tafadhali
tupige simu kituo cha polisi kwanza kama kwenda
basi uende na maaskari”
kipindi hicho wakati anazungumza hasira zake
zilikuwa zimemuisha na kwa bahati mbaya
kukasirika kwake kwa mara ya kwanza ndiko
kuliko
nifanya nijitolee maisha yangu kwenda huko kama
kufa ni kafe maana najua nitakufa kishujaa kwa
kuilinda familia yangu kama baba anaye jali na
kuipenda familia.
Nilipo kuwa nataka kutoka Magrety akawa
ananikataza nisiondoke nilicho, kifanya nika
msukumia kitandani huko na kumpa onyo asipige
simu kituoni maana hatuwezi jua kuwa hao jamaa
wana nia gani na wameweka mitego gani hivyo
tuna weza kuongeza tatizo badala ya
kulipunguza.
kisha nikatoka mle chumbani na kumuacha
Magrety akilia kilio cha kwikwi nami nikaanza
safari ya kuelekea huko,
wakati nimeshika komea la mlango wa kutokea
nje
nikakumbuka kitu kichwani ilinibidi nielekee
chumbani kwa Nisha nikambusu shavuni wakati
akiwa amelala kisha kwenda na chumbani kwa
Davidi pia alikuwa amesha lala nilimshika
kichwani
na kumuambia maneno ya kiume,,,,
”David wewe ndio kidume changu cha baadae na
kiongozi wa famila hii mungu aendelee kuku kuza
na ukuwe salama ili baadae uje kulinda familia
yako kama mimi leo ninavyo jitolea maisha yangu
juu yenu”
Nilirudi vyumbani kwao kuwaaga maana sikujua
huko ninako kwenda kama nitaweza kurudi hai
au maiti, baada ya hapo safari yangu ikawa
imeiva
sasa nilitoka na kuwasha BMW230 yangu
kuelekea huko na ndani ya dakika kadhaa nikawa
nimefika eneo husika nikatoa simu yangu na
kuanza kubonyeza vile vitufe husika kama namba
ilivyo kuwa inajieleza 0768606510 nika piga na
simu ikaanza kuita na baada ya sekunde tu
nikasikia sauti niliyo ifahamu kabisa
Ikisema hallo??!!
Nilipo mjibu kuonesha kwamba ninamskia
alinipatia maelezo,,,
”Alfred subiri hapo hapo nimeshakuona”
Nilitamani kumuita jina lake ili nijue kama ni yeye
au nimefananisha sauti, tatizo simu ikakatika
ghafla,nilipo itazama ilikuwa imekatwa kusudi,
Niliendelea kusubiri kama alivyonielekeza huku
kichwani na mimi nikipanga maarifa yangu
nifanyeje kama litatokea tatizo juu ya uhai
wangu.
Baada ya dakika kupita sauti za viatu zikawa
zinasikika zikinisogelea nilipotazama mbele
nikaona warembo wa wili walio panda kiasi,wenye
shingo ndefu na nyembamba zilizo pambwa na
mikufu ambayo ni ghari kununua pia hata miili
yao
ilikuwa ni myembamba japo kuanzia kiunoni
walitenga kiasi kwa vijana wa sasa wanawaita
umbo namba nane.
walivaa nguo zilizo fanana, makoti mafupi yenye
rangi nyeusi pamoja na vimini, .mikono yao
ilivalishwa gropsi zilizo fanana na rangi ya
makoti
yao sura, zao zenye weusi uliong’a
uliwatambulisha kuwa wao ni waafrika halisi,
sura
hizo ni kazi kuzitofautisha kama huja zizoea.
Nilishangaa walivyo jigawa, mmoja akakaa
upande
wangu wa kulia na mwingine kushoto hapo
uvumilivu ulinishinda ikabidi niwaulize kwa ukali
ili
kujihami,,,,,
”nyie ni wakina nani”?
Twin killers(mapacha wauaji) walinijibu huku
wakiwa wameweka sura ya ukatili
”Kwa hiyo mnataka nini sasa”? niliwauliza nami
kwa ukatili maana nilijua wanawake ni waoga
hivyo wanaweza kutishika lakini kumbe ndio
nikawa nime wachochea, wakanishika mikono
yangu yote wakiwa wamegawana kila mmoja na
upande wake.
Nilipojitikisa kwa nguvu zangu zote ili waniachie
kumbe bastola yangu niliyokuwa nimeiweka kwa
nyuma walisha itoa bila mimi kujua na kuniwekea
kichwani,,, moja alizungumza,,
”Songa mbele haraka we kijana”
Kutokana na jinsi alivyo zungumza kile kiswahili
chake nikaanza kuhisi kuwa hawa si watanzania,
wakanikukusa hivyo hivyo huku nikiwa na weka
hali ya ubishi mpaka tulipo fika nyuma ya ile
hoteli
ambapo kulikuwa na meza moja iliyo jitenga
kwenye maua mengi marefu na mwanga hafifu
wa
taa zenye rangi tofauti,na kulikuwa na bwawa la
kizungu pembeni(swimming pool)
Meza hiyo ilikuwa imezungukwa na watu wapatao
saba walio shiba vilivyo wote wakiwa wame
simama kumzunguka mtu moja ambaye yeye
aliketi kwenye kiti nikahisi huenda huyu ni bosi
wao nikaanza kuogopa,
Sauti ya kofi ilisikika kutoka kwa yule jamaa aliye
keti na kuwaambia wale madada kwa lugha nilio
weza kuitambua kuwa ni kinyaruanda, ila siku
bahatika kujua maana ya yale maneno.
baada ya ishara hiyo ya kofi wakaniachia kisha
nika sogezewa kiti nami nika keti pamoja nae.
Alinitazama kwa dharau halafu akachukua simu
yake iliyo kuwa juu ya ile meza na kupiga, sikujua
ni nani aliye kuwa ana mpigia ila alisema,
”hallo? eeh tumesha muandaa” kisha aka kata
simu
Ndani ya muda mchache nilishtuka baada ya
kuguswa bega kwa nyuma nilipo geuka alikuwa ni
Helman, nilinyanyuka kwa kuhamaki nikarudia
kumuita tena,
”Helman ni wewe unae nifanya kukosa furaha
mimi
na familia yangu?
Alicheka kisha akasema,
”Alfred raha unajinyima mwenyewe wewe na
familia yako mbona tulivyo kuwa marafiki
haukukosa amani”?aliniuliza lakini sikumjibu.
ITAENDELEA
 
Kuhusu hilo gamba sina shaka kasi yako ya usein bolt naijua once again hongera
.
 
SEHEMU YA TANO
Alinitazama kwa dharau halafu akachukua simu
yake iliyo kuwa juu ya ile meza na kupiga, sikujua
ni nani aliye kuwa ana mpigia ila alisema,
”hallo? eeh tumesha muandaa” kisha aka kata
simu
Ndani ya muda mchache nilishtuka baada ya
kuguswa bega kwa nyuma nilipo geuka alikuwa ni
Helman, nilinyanyuka kwa kuhamaki nikarudia
kumuita tena,
”Helman ni wewe unae nifanya kukosa furaha
mimi
na familia yangu?
Alicheka kisha akasema,
”Alfred raha unajinyima mwenyewe wewe na
familia yako mbona tulivyo kuwa marafiki
haukukosa amani”?aliniuliza lakini sikumjibu.
Naye akaja aka kaa kwenye kiti, yule jamaa niliye
mkuta amekaa pale mezani mara ya kwanza
wakati naingia akawaruhusu wale mabaunsa
pamoja na wale madada mapacha waondoke
hivyo
tukawa tumebaki watatu pale mezani na Helman
akanzaa kuniambia lengo la mimi kuwepo pale,,
”Alfred kwanza unatakiwa ujue duniani kuna watu
na viatu, sasa leo nakuweka wazi kuwa mimi si
katika watu ila ni kiatu, kuunda urafiki na wewe
sio
bure ila ni kwa maana ili nitengeneze pesa kupitia
mgongo wako hivyo kazi ninazo taka kukupa ni
mbili ya kwanza,
” nataka uwe unanipa taarifa kila gari la fedha
linapo kuwa linasafirisha fedha kutoka benki moja
kwenda nyingine ili tuweze kuchukua chetu
mapema”.
Na kazi ya pili,
”Unatakiwa uni pambe kwa meneja wako kuwa
mimi ni mteja mzuri sana katika swala la mikopo
ili niweze kuwa naye karibu na aniamini hata siku
mambo yakibuma achukue muda kujua kama ni
mimi ndiye na husika atakapo sikia tetesi juu
yangu”
Jicho lili nitoka na kutetemeka baada ya
kugundua
maelezo yake yana maanisha kuwa yeye ni
jambazi
na ndio kazi iliyo kuwa inamuweka dar es salaam
hata hivyo hakuishia hapo aliniangalia kisha
akamuangalia yule jamaa mwingine na
kunitambulisha,
”huyu jamaa anaitwa Cholo yeye ni mtu wa
Rwanda ninafanyanae kazi hii kwa muda wa
miaka
mingi sana na yeye ndiye anaye nichoresha dili
nyingi sana za kwao na wale mapacha amekuja
nao huku tanzania kwa kuwa kule nchini kwao
wameshashtukiwa na wana tafutwa na polisi”
Maneno yake yalinifanya nizidi kumchukia Helman
maana alikuwa anataka kunishirikisha katika kazi
ambazo hata cheti chake sina nilinyanyuka kwa
gadhabu na kumwambia,
”hiyo kazi yako fanya na hao hao wakimbizi
wenzio lakini sio mimi, siwezi kuwa kama
kunguru
wako hawa mapacha walio kimbia nchi yao
wakati
ni raia halali wa Rwanda naenda kutoa taarifa
kituoni”
Nilipo maliza kuzungumza niligeuza mwili wangu
na kuanza kupiga hatua kuondoka, zilipofika
hatua
tano mbele Helmani akaniita nilisimama kwa
sekunde bila kumgeukia kisha ndio nikageuza
shingo yangu,
miguu ilitaka kuishiwa nguvu nilipo muona
baunsa
mmoja akimleta Sagu huku nguo zake zikiwa
zimeloa damu na kisha kumtupa chini pale
pembezoni mwa bwawa la kizungu(swimming
pool)
nilirudi haraka haraka na kumsogelea Sagu.
nikagundua kuwa walimchoma kisu dakika
kadhaa
nyuma baada yakuona tundu lililo kuwa lina toa
damu nyingi na yule baunsa akiwa ameshika kisu
kilicho lowa damu ila alikuwa bado anapumua
nikaanza kumuuliza kwa sauti iliyo kuwa
inakaribisha mchozi,,
”Sagu imekuaje mdogo wangu umefanya nini na
hawa wamekujuaje wewe eeh? Wakati huo
nilikuwa
nimepiga magoti na kujaribu kumuinua nikimshika
mabega yake,
ndipo alipo anza kunieleza.,,,,,
”hawa jamaa waliwahi kutuona mimi na wewe
nilipo kuja mara ya kwanza kununua vifaa vya
ujenzi siku za nyuma kule karia koo na
inavyoonesha walianza kukufuatilia muda sana
kabla hata ya Helman aja kufuata moja kwa moja
na kuanzisha urafiki na wewe na tulipo achana
walinifuata na kuniuliza kuwa nina uhusiano gani
na wewe, nili waambia nakusaidia tu kubeba vifaa
vyako maana sikujua wanalengo gani na nilikuwa
siwajui hivyo ilinipa ugumu kujitambulisha moja
kwa moja, ndipo walipo nipatia pesa na namba
zao za simu niwe na wapa taarifa zako, kiufupi
mimi ndiye niliye rahisisha Helman kuanzisha
urafiki na wewe”
Maneno ya Sagu yalinipandisha hasira lakini
huruma ilinijia kila nilipomtazama na hali aliyo
nayo kwa wakati ule, lakini sikujua bado sababu
ilio wafanya waamue kmchoma kisu mpaka nilipo
muuliza swali hilo Sagu na kunijibu,,
”walipo nipatia zile namba na pesa hawakujua
kama mimi sikai hapa dar es saalam na walipo
kuwa wana hitaji taarifa zako nilikuwa nakupigia
na kuzua jambo lolote lile kuhusu ujenzi halafu
nikawa na kuuliza swali ambalo walilo kuwa
wanataka kujua huku nikijichekesha chekesha ili
ujue kama ni utani”
” sasa kumbe mdogo wake na Helman alikuwa
anasoma chuo kikuu cha mzumbe aliniona siku
moja Morogoro mjini ndipo alipo mpigia simu
kaka
yake na kumueleza kuwa ameniona,
baada ya muda Helman alinipigia na kuniuliza
niko
wapi na mimi nikamdanganya kuwa nipo dar es
saalam, na neno alilo niambia ni kuwa anataka
kuonana na mimi.jumapili”
” hapo sikuwa na jinsi zaidi ya kuelekea stendi ya
mabasi msamvu na kuchukua gari kuja huku ili
asijue kama nilikuwa Morogoro ndio sababu ilio
nifanya nije usiku ule wa jumamosi bila taarifa
nyumbani kwako na jumapili ile nilivyo wapa
taarifa kuwa nipo na wewe wenzie waliamini
kuwa
nipo hapa dar na ulivyo nishusha pale ndipo nilipo
kuja kuonana na Helman,”
”kwakuwa Helman anamuamini sana mdogo wake
ilibidi anipeleleze kwa kunipa kipigo mpaka nilipo
kubali kuwa nilikuwa Morogoro na kisu hiki
wamenichoma nilipo kataa kuwaeleza ni kitu gani
na fanya kule Morogoro hivyo hawajui kama
unajenga, siri yako mimi ndio nakufa nayo”
Mpaka Sagu anamaliza kunieleza njama nzima
waliokuwa wanaifanya ya kunizunguka mimi
mchozi ulikuwa umesha lowesha shavu langu
lote,
kimya kweli kilitawala kwenye kinywa cha Sagu
kumbe alisha kata roho, hasira zilinipanda ,nilipo
geuka kwenye meza walio kuwa wameketi kina
Helman ilikuwa nyeupe kumbe wakati walivyo
mtupa Sagu pale chini wakakimbia maana
walijua
hato weza kupona na ile ni kesi ya mauaji na
ghafla maskio yangu yakaanza kusikia ving’ola
vya
polisi
Ndipo nami nilipo pata akili ya kukimbia,
niliongoza
moja kwa moja mpaka kwenye
BMW230 na kuiwasha na mwendo wa kasi
ukachukua nafasi barabarani, nilipishana na
magari
yasiyo pungua matatu ya polisi yakielekea land
mark hotel kwenye tukio japo sikujua ni nani aliye
wapa taarifa, hilo si kujali kwa wakati huo kilicho
kuwa akilini mwangu ni kutoka eneo lile maana
kama ningeonekana wange hisi kuwa ni mimi
nahusika na mauaji kwa ushahidi wa nguo zangu
kulowa damu nilizozipata wakati nime mpakata
marehemu Sagu,
kila nilipo kuwa na simama kwenye foleni hofu
ilizidi kunielemea moyoni mwangu mpaka nafika
getini kwangu sikuamini kama nimeweza kujitoa
kwenye eneo lile la hatari, nilichukua simu yangu
na kumpigia Magrety(mama David) aje
kunifungulia geti lakini simu yake ikawa
haipatikani
na usiku ndio ulikuwa unazidi kuwa mnene japo
siku angalia saa ila nili hisi yaweza kuwa ni kama
saa nane hivi.
Nilishuka kwenye gari na kwenda kuluka ukuta
kisha nikaenda kumgongea dirishani aniletee
funguo za geti, alipo kuwa analeta funguo
akataka
kupiga kelele baada ya kuziona damu kwenye
shati
langu akijua labda mimi ndiye nilie jeruhiwa
nikamtuliza na kumwambia tuta yazungumza
chumbani, nikafungua geti na kuingiza gari ndani.
Magrety alikuwa amesimama kwenye kizingiti cha
mlango akinisubiri nilimsogelea na kumshika
kiunoni ili asiwe na hofu na kwenda naye
chumbani. Huko ndipo kimbembe kilipo anza
baada
ya Magrety kushindwa kuniamini juu ya damu
nilizo nazo aliongea kwa wasiwasi huku
akinipapasa maeneo ya tumboni kama angeweza
kuliona jeraha lakini haikua hivyo, baada ya
kulikosa ndipo sauti ya ukali na yenye kuogopa
ikamtoka,,,,,
”Alfred umeua mume wangu?
”sijaua mke wangu? Nilimjibu
“Mbona umelowa damu zimetoka wapi kumbuka
uliondoka na ile bastola huku ukiwa na hasira
balaa gani hili lina ikumba nyumba yangu!!!!!!!!!!!”
alizungumza Magrety
Nikachua akili kichwani, kwamba kama nita
mwambia Sagu amefariki litazuka jambo lingine
usiku ule ili nibidi ni mbembeleze tuzungumze
kesho ili hofu na jazba alizo nazo zipungue,
nilimshika kwenye paji lake la uso na kumtazama
kwa jicho la huruma kwenye mboni za macho
yake
kwa dakika kadhaa bila kumwambia chochote
kisha nikamuacha chumbani nami nikaelekea
bafuni kuoga ili kutoa taka mwili pamoja na zile
damu.
Wakati natoka bafuni huku nikijifunga funga taulo
vizuri nikashangaa kumuona mama David
amekasirika vibaya yani na akiwa ameshika simu
yangu mkononi nilipo muuliza nini tatizo alinijibu
kwa kuniuliza swali,,,
“Kati yako na Helman nani ameusika na mauaji
ya
Sagu”?
Moyo ulinipasua ghafla, amejuaje huyu? Ndio
swali
nililojiuliza kichwani mwangu nilipo itazama ile
simu nikaona mwanga kwenye kioo hauja zimika
nika hisi huenda kuna mtu amepiga au ametuma
ujumbe,nikampokonya ile simu kwa nguvu na
nilipo
itazama nikaona ujumbe ulio kuwa umefunguliwa
muda si mlefu aliye tuma alitumia namba ngeni
hivyo sikumjua muhusika ni nani na alisema,,,,,,,
”ukijifanya mjanja naenda kutoa taarifa kituoni
juu
ya mauaji ya Sagu”
Sikuwa na jinsi ilinibidi nimueleza ukweli tu mke
wangu kwa kilicho tokea kule nilipo toka, hapo
kidogo akawa kanielewa, akanyanyuka na kwenda
kuchukua biblia kabatini na tukamuomba
mwenyezi
azidi kutuepusha na mabalaa. Tulipo maliza
nikamuomba ni lale maana asubuhi natakiwa
kuwahi kazini kama mambo mengine
tutazungumza kesho na kujua nini kitaendelea.
Asubuhi na mapema nikaamka nikajiandaa huku
moyo wangu ukiwa na hofu maana sikujua nini
hatima ya tukio lile baada ya polisi kwenda pale
hotelini,nika toka nje kuelekea kwenye gari langu
ili
ni wahi kazini lakini sikuweza kufanya hivyo
kutokana na kuona damu kwenye siti niliyokuwa
nimekalia jana usiku hivyo ilinilazimu ni pande
bodaboda mpaka kazini.
Wakati naendelea na kazi pale ofisini kwangu
akaja mfanya kazi mwenzangu akiwa na gazeti
lililo andikwa ,,,,
”mtu mmoja auwawa na watu wasio julikana
usiku
wa kuamkia leo katika hoteli ya landmark iliyopo
maeneo ya river side ubungo na jeshi la polisi
linaendelea na uchunguzi kuwa baini wauaji hao”
huku gazeti hilo likiwa limewekwa picha kubwa
kwa mbele ya marehemu Sagu iliyo pigwa
kwenye
tukio hilo.
Hali ilizidi kuwa tete kwa upande wangu siku hiyo
nilijikuta kukosa amani kabisa tangu nilipo ona
picha ile kwenye lile gazeti, ufanisi wangu wa kazi
ulipungua ilipofika mishale ya saa saba mchana
ilinibidi niombe ruhusa kwa meneja kuwa naumwa
ili nikapate muda wa kupumzika kutokana na
hekaheka za jana na kujadili swala lile na mke
wangu.
Mchana huo nilipanda daladala kurudi nyumbani
huko pia walizidi kunichanganya maana kulikuwa
hakuna jambo walilo kuwa wanazungumza zaidi
ya
tukio lile la mauaji ya Sagu
”jamani duniani kuna watu wa katili sana
unawezaje kutoa uhai wa mwenzako kama kuku”
Utazani wao hawajaumbwa au hawato kufa” hizo
zilikuwa sauti za abilia walio kuwa nyuma yangu
wakionesha kusikitika juu ya tukio lile.
Daladala ilipofika kwenye kituo changu nilishuka
nakuongoza njia ya nyumbani kwangu, baada ya
kupita nyumba kadhaa kabla sijafika kwenye
nyumba yangu nilistaajabu kumuona Cholo yule
jamaa wa kinyaruanda niliyetambulishwa na
Helman akitokea maeneo ya nyumbani kwangu
nilisimama kuhakikisha kama ni yeye au
kupagawa
kwangu tu, lakini alivyo sogea alikuwa ni yeye
kweli, naye alipo niona alishtuka pia aliningalia
kwa jicho la shari kisha akaongeza mwendo wa
kutembea.
Kitendo kile kilinifanya nianze kukimbia kuwahi
familia yangu ili nijue kama ipo salama nilifika
nyumbani na kukuta geti lipo wazi nikaelekea
sebleni nikakuta makochi yamesogezwa na vitu
vipo katika mpango usio eleweka nili nibidi niite
kwa hofu,,
”Magrety Magrety?
”Abee mume wangu”aliitika kisha kuja pale
sebuleni kutokea chumbani kwa David akiwa
ameshika kifaa cha kudekia kisha kuniuliza,,,
“Mbona mapema Alfred kuna usalama kweli
huko?
”Usalama upo kiasi ila habari za kifo cha Sagu
ndio limekuwa gumzo la jiji huko nje”
”kuna mtu aliye kuja hapa” nilimuuliza
”hapana hajaja mtu”alijibu
”Kwanini umeuliza hivyo”?aliniuliza
”Maana geti lipo wazi”
”Ooh walikuja wazoa taka watakuwa walisahau
kufunga lakini huja nijibu kwanini umewahi
kurudi?
alijibu na kuniuliza nami nikamueleza sababu iliyo
nifanya niwahi kurudi.
****************
ITAENDELEA
 
SEHEMU YA SITA
Kitendo kile kilinifanya nianze kukimbia kuwahi
familia yangu ili nijue kama ipo salama nilifika
nyumbani na kukuta geti lipo wazi nikaelekea
sebleni nikakuta makochi yamesogezwa na vitu
vipo katika mpango usio eleweka nili nibidi niite
kwa hofu,,
”Magrety Magrety?
”Abee mume wangu”aliitika kisha kuja pale
sebuleni kutokea chumbani kwa David akiwa
ameshika kifaa cha kudekia kisha kuniuliza,,,
“Mbona mapema Alfred kuna usalama kweli
huko?
”Usalama upo kiasi ila habari za kifo cha Sagu
ndio limekuwa gumzo la jiji huko nje”
”kuna mtu aliye kuja hapa” nilimuuliza
”hapana hajaja mtu”alijibu
”Kwanini umeuliza hivyo”?aliniuliza
”Maana geti lipo wazi”
”Ooh walikuja wazoa taka watakuwa walisahau
kufunga lakini huja nijibu kwanini umewahi
kurudi?
alijibu na kuniuliza nami nikamueleza sababu iliyo
nifanya niwahi kurudi.
****************
Miaka kama mitatu ilipita mke wangu akapata
ujauzito ambao mtoto ndio huyu dason na
uchunguzi ulifanyika juu ya kifo cha sagu ila
wakafanikiwa kumkamata cholo yule mnyaruanda
ilisemekana kuwa helman alihonga pesa nyingi
sana mpaka yeye hakuhusishwa katika ile kesi.
Mpaka siku moja nikiwa nimetulia na magrety
nikapokea ujumbe kutoka kwenye namba ambayo
alijitambulisha moja kwa moja kuwa yeye ni
helman na kunipa vitisho,,,,
”NAJUA KUWA WEWE NDIYE ULIE TOA TAARIFA
KITUONI MPAKA CHOLO AMEKAMATWA NA KAMA
ISINGE KUWA PESA ZANGU LEO NA MIMI
NINGEKUWA GEREZANI SASA UTAKIONA
KILICHOMFANYA NYOKA KUKOSA MIGUU KAMA
SIO KUFA WEWE BASI FAMILIA YAKO ITAKUWA
KWENYE MATATIZO NA HIVYO VIKISHINDIKANA
UTAMFUATA CHOLO GEREZANI KWA GHARAMA
YOYOTE ILE”
Huo ndio uliokuwa ujumbe wa mwisho kutumiwa
na Helmani kabla ya kuundaa mpango wake
ulionifanya mpaka nikaenda gerezani
Vitisho kutoka kwa Helman ndio ikawa sehemu
ya
maisha yangu kwa kipindi chote hicho japo tangu
tukio la mauaji ya marehemu Sagu sikuwahi
kumtia machoni zaidi ya kupata ujumbe huo nami
sikutaka kujua yuko wapi maana kwa kiasi fulani
hali iliaanza kuwa shwari kutokana na jeshi la
polisi nchini kuwa makini na matukio kama hayo.
Nami umakini ukazidi kwa familia yangu na
kuzidisha upendo kwa wanangu na kumngojea
kwa
hamu kiumbe kilicho kuwa tumboni kwa Magrety
na ufanisi wangu wa kazi ukawa umerejea kama
kawaida hivyo amani kwa ujumla ikawa imerejea
nje hata ndani ya moyo wangu ikawa nikitoka tu
kazini sina sehemu ya kwenda zaidi ya kuelekea
nyumbani,
Jumatano moja iliyo pambazuka na hali ya
mvuamvua kulikuwa na watu wengi nje walio
kuwa
wana subiri kuingia ofisini kwangu kwa ajili ya
kusaini fomu za mikopo ili wakaendeleze biashara
zao na wale walio kuwa ndio wanaanza kuchukua
mikopo walikuja na kopi za hati za nyumba zao
pamoja na picha baada ya taratibu zote kufuatwa
kama wasaidizi wangu kwenda kuhakiki nyumba
hizo na sahihi kuwekwa na mdhamini kama mtu
alizaminiwa nyumba.
Kazi ilikwenda vizuri wengi niliwakamilishia
huduma walizo kuwa wanahitaji lakini hofu ilirudi
tena baada ya kupata mteja aliyetambulika kwa
jina la Khaji Kipeneko baada ya kunionesha fomu
yake iliyokuwa na sahihi yake na ya mdhamini ila
ile ya mdhamini nilikuwa na ifananisha na ya
Helman alipo nionesha na picha ya nyumba
nikahakiki kuwa ni kweli ni ya Helman macho
yalipepesuka marambili mbili kisha ni kamtazama
yule jamaa kwa makini na kumuuliza kwa
dhihaka,,,,,
“aliyekudhamini nyumba hii ya thamani ni nani
yako maana anaonekana ana moyo sana”
“ni bosi wangu” alinijibu
Mdomo wangu ukapata kigugumizi kidogo na
wala
sikuta kuendelea tena maana anaye kuwa mfanya
kazi wa Helman lazima watakuwa wanashirikiana
katika maswala yao ya ujambazi tu nikamsainia
haraka haraka na kumueleza siku ya kuja
kuchukua mkopo wake na kumruhusu aondoke
maana alisha niharibia siku. Na bahati yeye ndiye
aliyekuwa wa mwisho hivyo nami sikuchelewa
ilinibidi niondoke kwa kuomba ruhusa ya uongo.
Nikiwa njiani ndani ya gari langu BMW230 huku
mvua ya rasharasha ikiwa inaendelea na kifaa
maalumu cha kusafishia kioo kikiwa kinabadilisha
upande kwenda kulia na kushoto iliniweze kuona
vizuri hakika macho yangu yalimuona yule jamaa
mwenye jina la Khaji Kipeneko akiwa na Helman
kwenye mgahawa mmoja ambao haukuwa mbali
sana kutoka pale benki na kama kuna jambo
walikuwa wana lijadili hivi, ilinibidi nisimame na
kuwaangalia vizuri walipo liona gari langu
walinyanyuka na kuondoka.
Nilifikiri kwa muda pale huku kichwa changu
nikiwa
nime kiinamisha kwenye usukani,
“ kwamba maisha haya nitaishi mpaka lini na kwa
nini niwe mtumwa wa elimu yangu mwenyewe?
“Helman yeye ni nani kwangu mungu ? Hapana,
sasa kwanini nimuhofie? nilijiuliza maswali mengi
na kujijibu mwenyewe, ilinibidi nichukue maamuzi
ya kumfuata anieleze kama kuna sababu nyingine
inayo mfanya aendelee kunifatafata maana ni
miaka mitatu imepita lakini bado anataka
kuendelea kuwa kikwazo kwangu.
Nilifungua mlango wa gari kwa hasira bila kujali
mvua iliyo kuwa inaanza kuchanganya na
kumfuta
Helman kule waliko kuwa wanaelekea na yule
kibalaka wake Khaji Kipeneko nilifika mpaka
maeneo yale lakini njia ilikuwa nyeupe sikujua
waliingilia upande gani, ilinibidi nirudi kwenye ule
mgahawa na kutulia kidogo kushusha pumzi
kidogo mpaka muhudumu alipo kuja na
kumuagiza
aniletee bia ya Kilimanjaro ya moto.
Nilikunywa bia ile taratibu mpaka nikamaliza japo
nilihisi inaweza ikanipunguzia mawazo lakini
haikuwa hivyo, nikatoa waleti yangu mfukoni na
kumuita muhudumu ili nimpatie fedha yake cha
ajabu alicho nijibu alinifanya nimpatie maneno
yasio stahili kuambiwa binaamu,,,
“ mbona umeshalipiwa hicho kinywaji’? aliniambia
“Na nani”?
“Amesema ni kwambie mgomvi wako” alinijibu
yule
muhudumu
“Wewe dada unakichaa? Utawezaje kupokea pesa
toka kwa mtu mwingine wakati kinywaji
nimekunywa mimi na isitoshe umeniona nimekuja
peke yangu hapa embu nitokee usoni mwangu”
nilimjibu na kumtupia pesa usoni naye akainama
akaziokota na kuniomba radhi ambayo sikumjibu
kisha akaondoka, jibu lile alilo nijibu kuwa
mgomvi
wako ndiye aliye kulipia nilijua yawezekana kuwa
Helman bado yupo maeneo yale nilinyanyuka na
kutaka kuweka waleti mfukoni baada ya kuitoa
nilipokuwa nataka kumpatia fedha yule
muhudumu,
lakini kumbe kutokana na zile papala niliangusha
pale chini badala ya kuweka mfukoni kama
ilivyokuwa nia yangu.japo kwa muda huo sikujua.
Nilimfuata yule muhudumu na kumuuliza aliye
nilipia yuko wapi alinionesha sehemu ambayo
aliyo
kuwepo mwanzoni lakini baada ya kwenda mimi
sikumuona yule dada allisema
“ alikuwa hapa mida sio mirefu wakati mimi
nakuja
kwako” nilikasirika sana ilinibidi niondoke zangu
nyumbani.
Nilipofika nilimkuta Magrety pamoja na Nisha
wamejipumzisha kwenye makochi kutokana na
mzigo aliokuwa nao tumboni mwake. Nilielekea
mezani na kujiandalia chakula mwenyewe, nilipo
kuwa naanza kula tu David naye alikuwa anarudi
kutoka shuleni basi nikaungana naye pamoja
tukala wote, kisha nikaelekea chumbani kutafakari
mpaka Magrety naye alipo amka nakunikuta nipo
chumbani
“eeh mme wangu umerudi saa ngapi tena”?
aliniuliza
“Muda mrefu mpaka nimekula we ulikuwa bado
ume lala na Nisha wako pembeni sikutaka kuwa
sumbua”
Basi baada ya maongezi hayo mafupi ilinibidi
nimueleze kilicho nikuta siku hiyo naye alinipa
wazo,
“Baba David mme wangu swala hili sasa naona
linazidi kuelekea pabaya zaidi maana huyu
Helman
inaonekana ni sugu na anaweza akakusababishia
matatizo makubwa maana haiwezekani kipindi
chote hiki awe bado anakufuatilia halafu bila kosa
lolote lile cha msingi hapa kesho twende tukatoe
taarifa kituoni hata kama kuna jambo lita tokea
basi polisi lisiwe geni kwao”
“Nimekuelewa mke wangu mpendwa nitafanya
hivyo kweli hali hii inazidi kuniogopesha sana
hasa
nikifikiria usalama wa familia yangu”
Tuliweza kukubaliana maamuzi yetu mimi na mke
wangu kilicho baki tulikuwa tunaomba uzima kwa
mwenyezi mungu tufike salama siku inyofuata ili
tuelekee kituoni;
Waswahili wana sema mwenye nacho
huongezewa
kwangu usemi huo ulichukua nafasi baada ya
kuongezewa matatizo niliyo kuwa nayo,
Asubuhi na mapema wakati nikiendelea kujiaanda
ili nieleke kituoni na baada yapo ndio niende
kazini,
sikujua kilicho nisukuma kuwasha luninga yangu
ya chumbani ambayo ilikuwa inatangaza habari
mpya,,
“ndugu watazamaji wa kipindi chetu cha ”
matukio
yetu” siku ya leo tunaamka na habari ambayo
imeshika katika habari zote tulizo nazo,
“Gari lililo kuwa linasafirisha fedha jana jioni
kutoka Dar es salaam kwenda Tanga lilivamiwa
na
majambazi wasio julikana na kuwajeruhi baadhi
ya
maaskari waliokuwa wana linda gari hilo ila kwa
bahati nzuri kuna baaadhi ya vielelezo ambavyo
vimeweza kuonekana eneo la tukio ni pamoja na
waleti iliyokuwa na vitambulisho ambavyo
vinasemekana ni vya mmoja wa wafanyakazi wa
benki ya NMB akitambuliwa kwa jina la Alfred
kazinge pamoja na bastola moja ambayo
ilionekana kutumiwa katika tukio hilo na kwa
taarifa tulizo nazo ni kwamba polisi wanaelekea
kumkamata mtuhumiwa baada ya kuthibitisha
kuwa vifaa hivyo ni vya muhusika wa tukio hilo
kwa uthitisho ulio tolewa na meneja wake wa tawi
la magomeni”
Nilizima luninga ile haraka na kusimama kwa
muda bila kujua cha kufanya na kutoamini
nilichokiona na kukisikia kwa masikio yangu
mawili,mpaka nilipo kumbuka mazingira ambayo
nitakuwa nimeangusha ile waleti ndipo nilipo
gundua kuwa ni pale mgahawani niligeuka nyuma
kumtazama Magrety aliye kuwa kitandani nika
mkuta kashika kichwa na mdomo ukimtetemeka
kwa hofu, nilitupa macho yangu chini kisha
kuyainua na kupiga hatua kumsogelea na
kumwambia,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
“ Magrety mke wangu hapa sina njia nyingine ya
kukwepa kesi hii maana ile waleti ni kweli yangu
na vile ni vitambulisho vyangu pia kama
unakumbuka ile bastola nilisha wahi kuishika
tena
bila gropsi na wale mapacha walikuwa na grops
walivyo ichukua kwangu yawezekana huu mpango
ulikuwa endelevu ulioandaliwa
“ pia kwa kipindi chote hicho yawezekana ikawa
haikutumiwa na kama ilitumiwa basi watumiaji
walivaa gropsi ili zile alama za mikono zikipimwa
zionekane ni za kwangu Helman namjua anaakili
sana ya kijambazi japo mimi sio muhusika
inanibidi nikimbie tu ilibaadae nije kulea familia
yangu nakuomba usiwaambie chochote hawa
watoto maana wanaweza kuishi kwa hofu sana
katika maisha yao nami napenda wawe na amani”
Nilibusu tumbo la mke wangu na kukiomba radhi
kiumbe kilichopo ndani..,,,,,,,,,
“ewe malaika usiye jua chochote kinacho endelea
naomba unisamehe sana kwa uwamuzi ninao
uchukua wa kuondoka bila ya wewe kuzaliwa
maana utakosa upendo wangu kwa muda na sina
ninachoweza kukuachia kwa sasa zaidi ya
kumbukumbu za maumivu utakazo kuja kuzikuta
utakapo zaliwa na kujitambua.
Maneno hayo niliyo kiambia kiumbe kilichopo
tumboni yali mchoma sana Magrety alisikia
uchungu usio na mipaka, machozi yalianzisha
ujirani na mashavu yalitililika vyakutosha acha
makamasi yalio kuwa yana toka kwa kupiga hodi
hata kile kilio cha kwikwi kikachukua nafasi
kinywani mwake. Nami sikutaka kupoteza muda
zaidi ya kuingia kwenye droo na kuchukua kiasi
kidogo cha fedha ambacho nilikiweka kama akiba
na kingine kumuachia Magrety kwa ajili ya familia
yangu na kuhusu hati za mali alikuwa anajua
wapi
zilipo.
nikampiga busu la mwisho na yeye ambalo
lilimfanya azidi kutoa machozi na kutaka kunizuia
nisiondoke lakini sikutaka kumuendekeza nikatoka
kwa nguvu mpaka nje kisha nikafungua geti na
kurudi kwenye BMW230 na kuiwasha na kutoka
mpaka nje ya geti
wakati najaribu kunyoosha matairi vizuri ilinianze
kuondoka ghafla nikaona vikofia vya polisi
vikibembea kwa nyuma ya gari lao walikuwa ni
wengi waliobebwa nyuma ya gari hilo huku mitutu
ya bunduki ikiwa mbele ya vifua vyao ilinibidi
nijisalimishe mwenyewe tu.,
walishuka hata kabla gari lao halija simama vizuri
na kunivamia moja kwa moja walinijua baada ya
kuoneshwa na meneja wangu ambaye ndiye alie
waleta nyumbani kwangu.
Walikamata mikono yangu na kunifunga pingu
kwa
nyuma baada ya kuigeuza mikono yangu kisha
kunirudisha mpaka ndani kwangu askari wengine
walijigawa kwenye vyumba vingine wakikagua
kama kuna siraha au zana zingine amabazo zina
husiana na ujangili kiukweli nilijisikia vibaya sana
nilipo waona watoto wangu pamoja na mke
wangu
walivyo kuwa wananililia lakini askari hao
hawakujali lolote walishindwa hata kumuhurumia
mke wangu kwa hali aliyo nayo, walikuwa
wakimsukuma kila alipo kuwa ananisogelea na
kunililia,
Sikuweza kujikaza katika hali hiyo nami machozi
yakawa yananitoka kila nikiwatazama familia
yangu ikitapatapa kwa kukosa msaada hata wa
kubembelezwa, maaskari hao walipo maliza
ukaguzi wao walinitoa nje huku nikiwa bado nina
pingu mikononi jambo ambalo lilinifanya nione
aibu
kutokana na wingi wa watu hasa majirani zangu
walivyo kusanyika kushuhudia tukio hilo,
nilipandishwa kwenye gari lao kama ng’ombe
wanao pelekwa mnadani kisha kuondoka kuelekea
kituoni.
ITAENDELEA
 
SEHEMU YA SABA
Walikamata mikono yangu na kunifunga pingu
kwa
nyuma baada ya kuigeuza mikono yangu kisha
kunirudisha mpaka ndani kwangu askari wengine
walijigawa kwenye vyumba vingine wakikagua
kama kuna siraha au zana zingine amabazo zina
husiana na ujangili kiukweli nilijisikia vibaya sana
nilipo waona watoto wangu pamoja na mke
wangu
walivyo kuwa wananililia lakini askari hao
hawakujali lolote walishindwa hata kumuhurumia
mke wangu kwa hali aliyo nayo, walikuwa
wakimsukuma kila alipo kuwa ananisogelea na
kunililia,
Sikuweza kujikaza katika hali hiyo nami machozi
yakawa yananitoka kila nikiwatazama familia
yangu ikitapatapa kwa kukosa msaada hata wa
kubembelezwa, maaskari hao walipo maliza
ukaguzi wao walinitoa nje huku nikiwa bado nina
pingu mikononi jambo ambalo lilinifanya nione
aibu
kutokana na wingi wa watu hasa majirani zangu
walivyo kusanyika kushuhudia tukio hilo,
nilipandishwa kwenye gari lao kama ng’ombe
wanao pelekwa mnadani kisha kuondoka kuelekea
kituoni,
Mama David japo na hali yake ile alijaribu
kulikimbiza gari lile kama mwanamke mwenye
kichaa lakini hata hivyo hatua zake
hazikumchukua
mbali na kudondoka chini hiyo ndio ilikuwa mara
ya mwisho kuiona famila yangu na kuwaona kina
David wakimlilia mama yao pale alipo dondoka
chini hata mahakamani hawakuja si kujua
walipatwa na nini huko nyuma.
Mahakama ikatoa hukumu ya mimi kuhukumiwa
kifungo na mali zangu zote kutaifishwa na
kupigwa
mnada ndipo familia yangu ikawa imekuja huku
katika nyumbaa hii niliyo ijenga kwa siri na Dason
alizaliwa huku na hakuweza kunijua baba yake
mpaka nilipo toka gerezani kwa msamaha wa
Rais.
Hata hivyo wakati natoka gerezani nilikutana na
mwanamke mmoja aliyekuwa rafiki wa mke
wangu
ambaye alikuwa anaijua familia yangu vizuri
aliniambia kuwa ana ushahidi kuhusu tukio lililo
kuwa limetokea ambao unaweza ukanisaidia pia
kulipwa fidia au kurudishiwa mali zangu lakini
kikubwa alicho kisema ni kwamba.
“ushahidi huo Helman amesikia kuwa ninao mimi
baada ya kutonywa na mafanyakazi mwenzangu
hivyo ananitafuta kwa hudi na uvumba na mimi
pale hotelini kwetu nilipo kuwa nafanya kazi
nimeacha kwa kuona maisha yangu yata kuwa
hatalini”
lakini kabla hajamaliza maongeza nilimuona
katanua mdomo kwa kupigwa na butwaa na
macho yake yakiangalia eneo ambalo mimi nili
lilipa mgongo nilipo geuza shingo nilimuona
Helman ambaye alikuwa ananifananisha hivi na
yawezekana hakuamini kama ningeweza kutoka
jela kwa wakati ule na alionekana
kuchanganyikiwa
baada ya kuniona mimi na yule mama rafiki wa
mke wangu mwenye ushahidi hivyo hatukuwa na
jinsi zaidi ya kukimbia na huko mbele
tukapotezana kila mmoja akapita njia ya peke
yake
ndipo nami nilipo fanya haraka kwenda ubungo
na
kupanda abood ya kuja huku Morogoro.
Hofu yangu iliyo kuwa inanifanya ni mkataze
David
asiende mjini ni kwamba Helman yaweze kana
anajua kuwa mimi huo ushahidi nilichukua kwa
yule mama ambaye anaitwa Magdalena hivyo
japo
si rahisi kumkumbuka David kwa kuwa miaka
mingi imepita na David amekuwa sana lakini
dunia
haina siri yawezekana tu akajulikana na akapata
matatizo makubwa sana zaidi ya haya niliyo
yapata mimi. Hayo ndiyo matukio yaliobadilisha
maisha yangu.
***************************************
Baada ya mzee kazinge kumaliza yalio mtokea
mpaka kufikia katika hali ile aliyokuwa nayo sasa
kila mtu alichoka kwa kweli wengi walidondosha
machozi na kumuhurumia hata David akawa
amejua ukatili alio fanyiwa baba yake japo
kumbukumbu ya machache alikuwa nayo akili
mwake lakini kiini cha matatizo alikuwa hakijui
sasa ndio amejua mtoto wa kiume hata Nisha
naye aliye kuwa mdogo kwa wakati ule ameweza
kujua alicho fanyiwa baba yake na Dasoni yeye
ndio amekuwa kama Nisha wazamani asiye jua
chochote zaidi ya kuona kama watu wanasimulia
hadithi za bibi na babu tu,
Ndugu mwenyekiti alivyo taka kuongea neno
alikatishwa na sauti ya mama Coolin ambaye
alikuwa amebeba chakula alicho enda kukiandaa
kwa ajili ya mgonjwa,,,
“jamani tumechelewa kupeleka chakula cha
mgonjwa na sasa yaelekea saa tisa kasoro na
kule
ilikuwa ni saa saba ndio tulitakiwa twende tatizo
kufuata mahitaji sokoni mpaka kuandaa na mikaa
yenyewe ya siku hizi hii ndio imenichelewesha
Davidi mwanangu twende haraka tukaombe
tuingie
hata kama tumechelewa wanaweza waka
tuelewa”
David alinyanuka akawa anaelekea kule alipo
mama Coolin ili ampokee kikapu cha chakula na
mzee Kazinge naye akaona si vibaya kwenda
kumuona mkewe japo uso wake ulikuwa bado una
aibu kwa alicho mfanyia mkewe,
Waliongozana wale watatu mpaka barabarani na
kuchukua bajaji kuelekea Hospitali huku wakijadili
ni jinsi gani wanaweza wakalipa ile bili ya
mgonjwa kule Hospitali maana walifanyiwa
msaada kutokana na hali yake kuwa mbaya,
maongezi hayo walienda nayo mpaka yalipo
wafikisha hospitali,
Walifika getini na kumuomba mlinzi awarusu
waingie kutokana na hali walio muacha nayo
mgonjwa halafu alibaki mwenyewe, kwa kuwa
mlinzi naye binaadamu aliwaruhusu na walipo
ruhusiwa tu mama Coolin akawaomba watangulie
maana alisahau hata kununua maji ya kunywa
mgonjwa hivyo akaelekea kwenye duka lililopo
karibu na Hospitali hiyo ya gairo,
David akawa yupo na baba yake mzee Kazinge
akimuelekeza njia za kupita ili waweze kufika
kwenye chumba ambacho mama yake alikuwa
amelazwa, na ndani ya dakika kadhaa wakiwa
wanakaribia chumba kile na David alimwambia
baba yake,
“ Baba inabidi nionane na daktari kwanza maana
chumba hicho hawaruhusiwa kuingia kama hodi
zingine za wagonjwa wa kawaida”.
Akamuacha baba yake pale akiwa amesimama na
yeye kuelekea kwa Daktari lakini alipo fika
hakumkuta ofisini mwake ilimbidi arudi kule alipo
baba yake sasa wakati ana mkaribia tu baba
yake,
aliona mlango wa chumba alicho lazwa mama
yake kitanda kilicho kuwa na mtu aliye funikwa
kuanzia kwenye miguu mpaka kichwani
kinatolewa
na yule daktari akawa anatoka kwenye kile
chumba
Daktarialipo muona David na yule mzee macho
ya
Daktari yalionekana kumkazia sana mzee Kazinge
kwa muda kisha kumuangalia David aliye duwaa
kukiangalia kile kitanda kilicho kua kinasukumwa
kupelekwa asiko kujua, Daktari alipo maliza
kuwangalia alisikitika
Kusikitika kule kwa daktari kulimpa wasiwasi
mzee
kazinge hakuelewa kwanini Daktari alifanya vile
hivyo alibaki akishangaa tu,
Miguu ya David ilianza kupiga hatua ndogo ndogo
kuelekea kwenye kile kitanda, kadri alivyo kuwa
anazidi kusogea ndivyo mwendo ukawa
unaongezeka na baadae mbio zikachukua nafasi.
Alifika kwenye kile kitanda na kuwasukuma
baadhi
ya manesi walio kuwa upande wake na kuufunua
ule mwili uliokuwa umefunikwa, maskini wa
mungu
macho ya David yalianza kuwa na chemchem za
machozi alipo hakiki kuwa mama yake ndio
ameaga dunia,
Dokta alimpa pole sana David na baadhi ya
manesi
wakawa wanambembeleza na kumshika
alivyokuwa
anajitupa tupa chini kwa kumlilia mama yake
kipenzi, uchungu alio kuwa anausikia David alihisi
yupo kwenye mpaka wa uhai na umauti,
Mzee Kazinge naye akawa kajisogeza eneo lile
kwa
aibu kubwa iliyo mjaa usoni mwake japo ni kweli
alikosea kwa kitendo kile cha kumpiga mkewe
wakati anaumwa ila chozi la upendo mpevu
lilimtoka wakati kitanda kile alicho bebwa
marehemu Magrety kikipelekwa kwenye nyumba
ya
kuhifadhia maiti.
Mama Coolin alipo fika naye alikuta hali si shwari
pale, hata maji yenyewe alio kuwa amefata aliya
dondosha chini na kujumuika katika kilio hicho,
baadhi ya watu walio kuwa wema
waliwabembeleza na Daktari aliwaomba waelekee
ofisini kwake akawape utaratibu na sababu za
kifo
cha mama David
Wakati wakielekea kwenye chumba cha Daktari,
David alilia sana kumlaumu baba yake kwa
kitendo
alicho kifanya mpaka mama yake kupoteza uhai
wake.ila hakuwa na jinsi ndio imesha tokea
ilimbidi
aendelee kulia kimyakimya tu kama mwanaume.
Walipofika tu ofisini kwa dakatari walikaribishwa
na Dokta akaanza kuwa eleza,,
“Kwanza poleni sana kwa msiba ulio wapata ila
hii
ni sehemu ya maisha ya binaadamu hivyo hatuna
budi kulikubali hili ambalo lipo mbele yetu lakini
pia tumejitahidi kwa kila tunavyoweza kuajribu
kuokoa maisha ya mgonjwa wetu lakini
tumeshindwa maana mungu ndio mwenye uwezo
zaidi”
“Lakini kikubwa kilicho sababisha kifo chake
mbali
na maradhi ya moyo aliyo kuwa nayo inaonekana
alipigwa huyu marehemu maana damu imevia
kwenye ubongo na hii ni hatari sana kwa uhai wa
binaadamu”
“Na swala hili hatuwezi kulifumbia macho hata
kidogo kwa sababu kila siku vyombo vya habari
vinatangaza juu ya matatizo kama haya na
serikali
ina mikakati migumu sana juu ya kesi kama hizi”
Daktari alipo maliza kuongea David alimwangalia
baba yake kwa jicho la hasira sana na uso uliojaa
udhia wa fadhaa mpaka Daktari alipo tia neno
“Bila shaka wewe ndie mume wa marehemu”aliuli
za Dokta
“ndio mimi Daktari” mzee Kazinge alijibu lakini
swali hilo lilimfanya ateseke kwa aibu
“Najua wewe ndie muhusika wa kipigo cha
marehemu mkeo kwa maelezo niliyo nayo hivyo
hatuna budi kukuchukulia hatua maana kama
nitakuacha na maelezo ya kifo cha mkeo niliyo
andika na weza nikafungwa mimi”Daktari
alizungumza na alipo maliza alichuku simu yake
ya
mezani na kupiga,
“hallo afande nakuomba uje hapa ofisini
kwangu”?
alimpigia simu askari ambaye huwa alikuwa getini
na bila kuchelewa alifika ofisini kwa Daktari na
kupewa maelezo kisha akamfunga pingu mzee
Kazinge na kuanza kumpeleka kituoni kwa kosa
alilo fanya la kukiuka haki za binaadamu kwa
kumsababishia mkewe kifo,
Huzuni ilizidi kutawala moyoni mwa Davidi kilio
kiliongezeka moyoni mwake akawa anajilaumu
kwa
kumueleza Daktari ukweli ile asubuhi alipo muhoji
maana alijua shida na mateso yataanza kuomba
makazi katika familia yake,
Dakatari aliwapa utaratibu jinsi watakavyo weza
kuchukua maiti yao kwa ajili ya mazishi,
Basi hapo hawakuwa na jinsi zaidi ya kuelekea
nyumbani na kuwapa taarifa wengine juu ya
msiba
huo ulio wafika,
D avid alikuwa anajiuliza ni jinsi gani wadogo
zake
wata upokea msiba huo maana ndio wanabaki
yatima mama ameaga dunia na baba gerezani
kwa
mara ya pili.
Ujio wao tu pale mtaani watu wazima
walishaanza
kuhisi kuwa kuna tatizo, David jicho lilikuwa
jekundu na kilio cha kugugumia kiliendelea, mama
Coolin naye ndala zake mkononi kanga iliyojikaza
ikawa mkanda kwenye kiuno chake acha kile
kilemba alicho jifunga kichwani kilicho timka
timka,
mwendo wa haraka uliwafikisha kwenye nyumba
ya kina David,. Mayowe yakaanza kwa masikitiko
ya majonzi kwa kuondokewa na mama yake,
majirani wakaribu wakawa wanavutika na kilio
kile
amabacho kiliashiria kuwa ni msiba.
Ndani ya muda mchache tu taarifa za kufariki
Magrety mama yake na David zikawa
zimesambaa
kijijini hapo Gairo, mama muksini naye aliposikia
hakutaka kuwaambia kina Nisha pamoja na
Dasoni
alichokifanya ni kuwa shika mikono na kuelekea
kule msibani,
walipo kuwa wana karibia walishtushwa na sauti
za vilio ambavyo vilikuwa vinatokea nyumbani
kwako, nisha alipo taka kuuliza kuna nini ghafla
akamuona kaka yake david aki wakimbilia na
huku
akitoa machozi nao wakapokonyoka mikononi
mwa
mama muksini na kumkimbilia kaka yao.
walipokutana kati david akapiga magoti ili
alingane
nao urefu kisha kuwa kumbatia, aliwaangalia
huku
akivuta makasi ndani, hali ile ya huzuni aliyo
onesha kwa wadogo zake ilizidi kuongeza simanzi
kwao hasa alipo ongea maneno ambayo hata
kama
dasoni alikuwa mdogo aliweza kuelewa kuwa
sasa
ni yatima wa mzazi mmoja,,,,,,
“nisha mdogo wangu mama ameatucha wenyewe
hatuna kimbilio sisi wadogo zangu, baba nae ndio
hivyo…….” Aliongea maneno hayo kwa sauti
ambayo lazima utadondosha chozi kama
ukimsikia
mpakashindwa kumalizia baba yake amefanya
nini.
Mama muksini alimnyakuwa david pale alipo
kuwa
amepiga magoti na baadhi ya wazee wengine
wakaja kumsaidia kisha waka mchukua david na
kwenda kumbembeleza mama muksini nae
hakuwaacha nisha na dasoni hivyo nae alienda
kuwa bembeleza, kiukweli mama muksini alitokea
kuwa penda sane watoto hao.
Maturubai yaliweza kufungwa watu wakawa
wamejigawa wanawake upande wao na wanaume
upande wao, stuli iliwekwa njia panda ya kwenda
sehemu ya wanawake na wanaume hao kisha
kiungo kidogo maarufu kama kitunga kiliwekwa
juu
yake kikiwa na picha nyingi za marehemu mama
david ambazo zilipigwa alama x kumaanisha
kuwa
huyu ndie marehemu aliye fariki,
ITAENDELEA
 
SEHEMU YA NANE
Mama muksini alimnyakuwa david pale alipo kuwa
amepiga magoti na baadhi ya wazee wengine
wakaja kumsaidia kisha waka mchukua david na
kwenda kumbembeleza mama muksini nae
hakuwaacha nisha na dasoni hivyo nae alienda
kuwa bembeleza, kiukweli mama muksini alitokea
kuwa penda sane watoto hao.
Maturubai yaliweza kufungwa watu wakawa
wamejigawa wanawake upande wao na wanaume
upande wao, stuli iliwekwa njia panda ya kwenda
sehemu ya wanawake na wanaume hao kisha
kiungo kidogo maarufu kama kitunga kiliwekwa juu
yake kikiwa na picha nyingi za marehemu mama
david ambazo zilipigwa alama x kumaanisha kuwa
huyu ndie marehemu aliye fariki,
wengi wasio mjua marehemu walipita kwenye stuli
hiyo na kutazama picha hizo wengi walisikitika na
maneno mengi kuwatoka mdomoni mwao hasa
walipo oona picha aliyo piga na familia yake
ambayo aliyo wakumbatia watoto wake vipenzi,,,
“maskini watoto wake hawa wawili wadogo kweli
sijui watakuwa kwenye mazingira gani? Alikuwa
anajisemea mmama moja ambaye alikuwa
akitazama picha hizo.
Muda ulivyozidi kwenda mkusanyiko ulizidi kuwa
mkubwa hasa kwa habari zilizo zidi kusambaa
kuwa amefariki kwa kipigo japo wengine
walizungumza mengi ambayo yasio na ukweli
kama vile, alifumaniwa ndio sababu ya kupigwa,
lakini hayo yalikuwa ni maneno ambayo hutokea
kwenye mkusanyiko wa watu au jambo ambalo
lina utata. Ila walio jua walitulia tu wakitafakari
msibao huo na nini cha kufanya.
Wazee wakaribu na marafiki wa mzee kazinge
waliitana na kuweka kikao kutaka kujadili taratibu
za mazishi bila kumsahau david pia alijumuishwa
katika kikao hicho maana alishakuwa mtu mzima
na alikuwa na uwezo wa kutoa maamuzi au
kupinga jambo ambalo ataona si bora kufanyika,,,,
“Ndugu zangu tumekusanyika hapa ili tuweze kujua
tunafanya nini juu ya msiba huu ambao umemfika
mwenzetu wa kufiwa na mkewe na matatizo
ambayo yeye yamemkuta wengi tumesikia sikia juu
juu tu kama amekamatwa na polisi na yupo kule
kwenye kituo kidogo kwa kosa la kumsababishia
mkewe kifo jambo hilo ni kweli kwa maelezo
ambayo tumeletewa na mwanamke
huyu,,alimuonesha mama coolin.
“ ambayo yeye aliyapata toka kwa daktari walivyo
kwenda jioni hii kwa ajili ya kupeleka chakula na
hata waliweza kushuhudia maiti ya mama davidi
ikipelekwa sehemu maaulumu ili kuuhifadhi mwili
huo, mpaka taratibu zitakapo kamilika na kwenda
kuchukuliwa kwa ajili ya mazishi” alizungumza
mzee nyomolage ambaye alichaguliwa kuwa
mwenyekiti wa kikao hicho kutokana na ukaribu
alio kuwa nao kwa mzee kazinge.
“na kama mnavyo jua ndugu yetu mzee kazinge
tumeishi nae hapa kwa miaka mingi sana na hana
ndugu hapa na hakuna anayejua mawasiliano yao
jambo tunalo lijua sisi in kuwa wazazi wake
walikuwa wanaishi mkoani tanga na walisha faliki
muda mrefu hivyo sisi ndio tumekuwa ndugu zake
hatuna budi kubeba majukumu haya ili
tumpumzishe mkewe mahali salama hata uko
atakapo kwenda basi ahisi kweli alikuwa anaishi
na binaadamu na sio watu na sasa nafikiri kikao
kimeanza rasmi tuweze kusikia mawazo yenu
tuyapatie ufumbuzi kwa haraka” hayo yalikuwa
maneno ya mzee nyomolage ambaye alizidi
kuonesha utu kwa familia ya mzee kazinge.
Kidole cha kwanza kilikuwa ni cha mama coolin
ambaye alianza kwa kuchangi yanayo hitajika
hospitali, alijifikicha macho yake kwanza na sauti
iliyo karibia kukauka kutokana na kulia sana
ilianza kuzungumza,,,,,
“jamani wakati tunampeleka mgonjwa hospitali
hatukuweza kulipa chochote kile in msaada tu
tulifanyiwa na yule daktari kutokana na hali ya
marehemu ilivyo kuwa mbaya hivyo kuna kiasi cha
fedha tunadaiwa ndipo pia tunaweza kuchukua
mwili wa marehemu”wazo hilo la mama coolin
lilisikilizwa na ufumbuzi ukatolewa na mtu
akateuliwa kwenda kukusanya michango kwa
waliohudhulia msibani.
“pia me nafikiri tungeweza kwenda kuomba ili hata
mzee kazinge aje kumzika mkewe na kuona nana
na familia yake huku akisindikizwa na akari nahisi
tuna weza kukubaliwa kwa hili maana si mnajua
kule alipo anaweza asitoke mpaka siku ya kwenda
mahakamani na nchi yetu mnaijua hii sio chini ya
miaka mitatu utasikia bado wapo kwenye
uchunguzi” hilo lilikuwa wazo la mzee kombo.
Mawazo hayo yalijadiliwa na kupatiwa ufumbuzi na
baadhi ya watu walichaguliwa ambao kesho ikifika
salama basi watajigawa wengine watakwenda
kulipia gharama za matibabu na kuuchukua mwili
wa marehemu ambapo hata bajeti ya jeneza ilisha
pigwa kutokana na kiasi cha michango kilicho
patikana jioni hiyo iliyokuwa inaelekea magharibi
na wengine watakwenda kuonana na mkuu wa
kituo cha polisi ili mzee kazinge aweze kwenda
kuhudhulia mazishi ya mkewe na kwenda kuwaaga
familia yake na watakao baki watabaki kuchimba
kaburi ambalo david alipendekeza lichimmbwe
nyuma ya nyumba yao, na muda wa mazishi
ulipendekezwa utakuwa na saa kumi na nusu jioni
na watu wakatangaziwa yote yaliojili kwenye kikao
hicho.
Mpaka kikao kinaisha watu waliweza kula kisha
kila mmoja kujichukulia nafasi kwenye turubai na
kuweka ubavu wake na wengine wakiendelea
kuombeleza.
***************************
Sauti zile za mapambio zilizo kuwa zinaimbwa na
wana mama ziliweza kuwaamsha walio lala pale
nje kwenye maturubai na kuwa fanya waanze pilika
pilika za kujiandaa ili kila mmoja ashike njia ya
kwenda sehemu husika kukamilisha mambo
aliyokuwa amepangiwa ndani ya saa kuminambili
hiyo asubuhi,
Baada ya wote kukusanyika safari ikaanza
kuelekea kituo cha polisi na hospitali, kwa bahati
nzuri wote wakawa wamefanikiwa wale wa
hospitali kuupata mwili wa marehemu na
kuuhifadhi kwenye jeneza ambalo wali linunua nje
ya hospitali karibu na jengo la kuhifadhia maiti
kisha kurudi nao nyumbani na wale wa kituo cha
polisi waliambiwa abaki mmoja ambaye watarudi
wote ma gari la polisi mpaka kwenye mazishi.
Ilipofika mishale ya saa tisa maandalizi ya
kuuwaga mwili wa marehemu yaka andaliwa na
mapambio yakaanza kuimbwa na wanakwaya
ambao walialikwa na padri nae akawa anafungua
biblia yake kutafuta maandiko matakatifu ambayo
ataweza kuyasoma kwenye hadhara hiyo iliyo
kusanyika msibani hapo na baada ya muda
aliweza kuyapata na kwaya ikasimama na
maandiko matakatifu ya kaanza kusomwa,,,,,,,
“kwa jina la baba na la mwana, alitoa ishara ya
msalaba kisha kuendelea,hakika kila mpandaji
mazao atavuna kile alicho kipanda na bwana
mungu wetu leo amevuna kwenye familia hii ya
mzee alfredy kazinge ili kukamilisha kazi yake
kutokana na tukio hili na maana ya sisi
kukusanyika hapa ili tujifunze kuwa na sisi siku
moja tutalala hapa mbele na kusomewa kama
huyu marehemu ndugu yetu magrety john
tumuombe bwana mungu wetu atuepushe na
madhambi ambayo tuna yafanya amina”
padri alimaliza kutoa neno na funzo kwa walio hai
ili waweze kujifunza kupitia mwili wa magrety
ambao uliwekwa mbele pamoja na picha yake
kubwa aliyo kuwa ameipiga enzi za uhai wake,
wakina david pamoja na wadogo zake walinyolewa
vipala kama wafiwa na kuvaa nguo zao nyeusi
kisha kuketi kwenye viti vya mbele ambavyo
viliandaliwa na kutazama jeneza lala mama yao.
Padri aliweza kutoa ruhusa ya kuungalia mwili wa
marehemu magrety kwa mara ya mwisho ili
kuelekea kwenye njia ambayo inaweza kumpeleka
motoni au peponi kutokana na matendo aliyo kuwa
anayafanya enzi za uhai wake.
Watoto wa marehemu waliweza kushikiliwa katika
kipindi hicho kigumu cha kuuaga mwili wa mama
yao kipenzi, hasa david ambaye alikuwa anafikilia
mambo mengi kama mzigo ambao alio achiwa wa
kulea familia akiangalia ndio kwanza ametoka
kumaliza kidato cha sita na matokeo hayajatoka
na kazi hana jambo hilo lilimuongezea sana
sononeko moyoni mwake,
Waliomshikilia waliianza kushindana nae nguvu
alipo nga’ang’ania kwenye mwili wa mama yake
huku akiushika kwenye paji la uso na kuutikisa
huku akiuuambia,,,
“mama amka mama mi najua umelala tu mama
yangu amka basi utuone wanao tunavyo hangaika
na machozi kututoka kwa huzuni unayo tuachia”
maneno hayo yaliwafanya hata walio mbali
kusogea eneo ambalo walilo kuwa wanaagia mwili
huo baada ya kusikia sauti ya david ikiongea na
maiti tena kwa masikitiko.
ghafla vumbi na upepo mkali ukaanza kutanda
eneo hilo na hali ya hewa ikaanza kubadilika,
mbigu juu ikaanza kuwa nyeusi kutokana na
mawingu yalio kuwa yameanza kutawala ikabidi
zoezi la kuaga lisitishwe na watu wakabeba jeneza
kuelekea nyuma ya nyumba ambapo ndipo kaburi
lilipo chimbwa na hapo watu wakatumbukia ndani
ya kaburi kulipokea jeneza hilo na wengine
wakibaki juu kulishusha kwa kamba ambayo
ilipitishwa pembezoni mwa jeneza hilo.
“baada ya zoezi hilo kukamilika watu walio kuwa
ndani ya kaburi walitoka kisha padri akasoma
harakaharaka kisha kuchukua udongoulio kuwa
kwenye chepeo na kuanza kuumimina juu ya
jeneza hilo ambalo lilishwa tumbukizwa kwenye
kaburi na kumalizia na maneno haya,,,,
“wewe in vumbi na utarudi kuwa vumbi jina la
bwana lihimiliwe” sauti za watu zilisikika zikijibu
amin.
Kisha chepeo lenye udongo kugeuzwa kwa david
naye akachota udongo kabla hajaweka udongo tu
kwenye kabuli alishtushwa na sauti ya gari
lililokuwa linakuja kwa kasi eneo la kaburi hilo
lakini kabla halija simama alimuona baba yake
akiwa na pingu mkononi akiruka kwenye gari kabla
hata ya askari kushuka kwenye gari hilo la polisi
na kuanza kukimbia huku akilalamika kwa sauti
akimuomba magrety amsubiri, lakini kila mmoja
hakuamini kwa alicho kisikia maskioni mwake in
baada ya kusikia mlio wa risasi aliyo pigwa mzee
kazinge na askari aliye dhani kuwa anataka
kutoroka kupitia umati ule wa watu david
hakukubali
Aliuchukua ule msalaba alio kuwa ameushika mtu
aliye mpokea wakati yeye akiweka udongo kwenye
kaburi na ndio ikawa silaha yake, alimtazama yule
askari aliye mpiga risasi ya mguu mzee kazinge na
kuaanza kumfuata kwa kumkimbilia alipomsogelea
alinyakuwa ule msalaba kwa kunguvu zake zote
iliampige nao kichwani lakini jambo hilo
halikufanikiwa baada ya askari wenzie kuudaka
msalaba huo na kumshika david kwa kumbana
mikono yake kwa nyuma,,
Uso wa david uliiva kwa hasira kila alipofikiria jinsi
mama yake alivyo patwa na umauti na matatizo
yalio mpata baba yake, kiukweli mambo hayo yote
yaliweza kumpunguzia david moyo wa ubinaadamu
na maneno yalioufanya mioyo ya maskari wale
kupanda kooni lakini wakuwa na lakufanya,,,
“mtu malize wote sasa si ndio kazi yenu inavyo
watuma kupiga risasi ovyo kwa wananchi wenu?
“elimu yenu inawasaidia nini sasa hakuna mncho
kumbuka juu ya wananchi zaidi ya kuwapa kesi
hata kama hawana hatia nimalizeni kama mnajua
sana kupiga risasi ni uweni nasema piga hiyo risasi
yako mbona unachelewa, fikirieni in mzigo gani
nilio kuwa nao hii yote imesababishwa na nyinyi
kuto kuwa makini na kufuatilia mambo kwa undani
zaidi.”
Malumbano yaliendelea na baadhi ya watu hawa
kujua lakufanya kutokana na mshtuko wa risasi na
zile vulugu zilizo kuwa zinaendelea pale kaburini,
wengine walikimbia kwa kuhofia maisha
yao,mtawanyiko huo wa watu walishindwa kuelewa
mzee kazinge yuko wapi na hali yake ikoje,
Kumbe baada ya kupigwa risasi ile ya mguu pale
alipokuwa ameangukia aliweza kujivuta taratibu
mpaka kwenye kaburi la mkewe na kujitupa mle ili
wazikwe wote maana alihisi anastahili kufa kwa
mateso anayo yapata kwa miaka yote tena bila
sababu ya msingi.
Watu walirudishwa tena mahali pale lilipo kaburi la
mama davidi baada ya manyunyu ya mvua kuanza
hata davidi aliachiwa na wale askari, hapo ndipo
walipo gundua kuwa mzee kazinge yupo mle ndani
ya kaburi,,,,,
“jamani hii familia kama mungu haioni vile in
misuko suko kila kukicha eeh mungu wasaidie
hawa,,
“Mmh inatia huruma kwa kweli watazame watoto
wake walivyo kuwa na huzuni “
Hayo maneno yaliwatoka watu tofauti katika eneo
hilo na wakati huo wakina mzee nyomolage
walitumbukia ndani ya kaburi na kumtoa mzee
kazinge, taarifa ziliweza kuwafikia mapaparazi
ambao walitoka kwenye kwenye vituo tofauti
tofauti kama vile redio,magazeti na hata wale wa
televisheni ili kukusanya habari hiyo amabayo
walijua kuwa lazima itawapatia pesa ya kutosha
kutokana na uzito watukio hilo picha nyingi
zilipigwa ili kupendezesha magazeti..
Padri aliamrisha wazike maana mvua ilianza kuwa
kubwa watu walimfukia mama david kwa haraka ili
mvua ile iliyo kuwa inanyesha isije ikaleta balaa
lingine wakashindwa kuufukia mwili wa marehemu
magrety.
David alilia sana maana hakuamini kama mama
yake ndio safari yake imefika mwisho,
Wale askari walimshikilia mzee kazinge ambaye
alikuwa anavuja damu kwenye mguu ule ulio kuwa
umepigwa risasi, mama muksini nae hakuwaacha
watoto wake nisha na dasoni.
ITAENDELEA
 
SEHEMU YA TISA
Hayo maneno yaliwatoka watu tofauti katika eneo
hilo na wakati huo wakina mzee nyomolage
walitumbukia ndani ya kaburi na kumtoa mzee
kazinge, taarifa ziliweza kuwafikia mapaparazi
ambao walitoka kwenye kwenye vituo tofauti
tofauti kama vile redio,magazeti na hata wale wa
televisheni ili kukusanya habari hiyo amabayo
walijua kuwa lazima itawapatia pesa ya kutosha
kutokana na uzito watukio hilo picha nyingi
zilipigwa ili kupendezesha magazeti..
Padri aliamrisha wazike maana mvua ilianza kuwa
kubwa watu walimfukia mama david kwa haraka ili
mvua ile iliyo kuwa inanyesha isije ikaleta balaa
lingine wakashindwa kuufukia mwili wa marehemu
magrety.
David alilia sana maana hakuamini kama mama
yake ndio safari yake imefika mwisho,
Wale askari walimshikilia mzee kazinge ambaye
alikuwa anavuja damu kwenye mguu ule ulio kuwa
umepigwa risasi, mama muksini nae hakuwaacha
watoto wake nisha na dasoni.
Upepo ulizidi na mvua ikawa kubwa na weusi ulio
sababishwa na mawingu ukawa umetawala kijijini
hapo na bahati nzuri zoezi la mazishi likawa
limeisha japo kwa shida watu walitawanyika
kuikimbia mvua ile, askari nao wakataka kuondoka
na mzee kazinge lakini mzee kazinge aliomba
azungumze na wanae hasa david ndipo alipoitwa
david baada ya mama muksini kuondoka na kina
nisha kwa kuwa wale ni watoto na hali ile ya hewa
ingeweza kuwaletea homa,
”David mwanangu hakika umeelewa binaadamu
walivyo naomba ujifunze kupitia matatizo haya
penda kuwa mtu wa kusikiliza na kuongea kidogo
tu ili uweze kuwajua wabaya wako, usiwe na
papala kutaka kupata mali zako fuatilia taratibu
iliuweze kukamilisha ushahidi utakao weza
kuwarudisha tena nyinyi katika maisha mazuri
ambayo mwanzo mimi nilikuwa naishi, sasa
nakuruhusu nenda mjini karudishe mali zako wewe
na wadogo zako nakukabidhi famulia hii uilee kadri
utakavyo weza ili wasije kupata machungu zaidi
pale watakapo tukumbuka sisi na ukifika huko
mtafute yule mama anayeitwa magdalena ambaye
aliniambua kuwa anaushaidi utakao weza
kurudisha mali zenu nakutakia kazi njema na
maisha mema uwezekano wangu wa kutoka
gerezani ni mdogo sana kwaheri mwanangu
wasalimie wanangu waambie nawapenda sana”
Alipo maliza tu kusema askari nao wakamkokota
mpaka kwenye gari lao kisha kuondoka nae david
hakuwa na cha kufanya zaid ya kuangalia tu lile
gari huku moyo wake ukiwa umesha badilika kuwa
wa simba kwa yeyote atakaye leta mchezo na
familia yake. Mvua ile kubwa iliyo kuwa
inamnyeshea ilikuwa in kama vipande vya barafu
ambavyo vina peperushwa na upepo hakujali
jambo ilo mpaka watu wazima walipo kwenda
kumtoa pale kwenye ile mvua kwa nguvu,
Akili ya david ilikuwa imesha changanyikiwa kwa
matukio ambayo yamemtokea mfululizo tena
yalikuwa chini ya umri wake lakini hakuwa na budi
kukubaliana nayo ili ajue wapi anaanzia, mpaka
pilika pilika zote zinaishia ilikuwa tayari
imeshatimia mishale ya saa kumi na mbili jioni,
hivyo kutpokana na ile mvua wengi walikwenda
majumbani kwao ila wale walio kuwa karibu na
familia ile ndio walio baki kwa kina david kuwa
fairiji kama vile mama coolin, mama muksini kina
mzee nyomolage na wengine,
Baada ya siku tatu swala la msiba likawa limeisha
kilicho baki ilikuwa in kujua kuwa wata wasaidia
vipi wale watoto hasa nisha na dasoni amabo
walikuwa wadogo maana david anakabiliwa na
majukumu mazito ya kutaka kurudisha haki ya
familia yake.
Mama muksini hakuchoka alijitolea kuwa chukua
na kuwalea lakini akasema kwa sasa mume wake
hayupo yupo safari kwa muda wa miezi sita sasa
maana anafanya kazi katika mbuga za wanyama
hivyo huchukua muda mrefu mpaka kurudi lakini
kwa sasa hana muda atakuwa amerudi baada ya
siku kama nne hivi mbele hivyo atazungumza nae
ili ajue na yeye atalipokea vipi na kama atalikubali
jambo hilo basi atakaa nao na kujitahidi kuwa
somesha mpaka pale mungu atakapo wasaidia
kupata kazi yao.
Wote walikubaliana juu jambo hilo david alikuwa
hana chakusema zaid ya kuwasikiliza tu japo
kichwani mwake alikuwa anaonekana kufikiria
jambo fulani ambalo hakutaka kuliweka wazi kwa
wakati huo mbele ya hadhara ile ya watu wake
wakaribu,
Sikuzilikatika na bwana wa mama muksini akawa
karejea kutoka ile safari yake aliyo kuwa
amekwenda alipo fika tu nyumbani kwake
aliwakuta kina nisha na dasoni wana jilia chakula
cha mchana jinsi alivyo kuwa na roho mbaya baba
ya huyu japo alizipata taarifa za msiba na
matatizo waliyo yapata watoto hao alidiliki
kumuita mke wake na kumuuliza swali mbeye ya
watoto hao mke wangu kituo hiki cha kulelea
watoto yatima kimesajiliwa lini maskini wa mungu
nisha alipaliwa na chai kusikia maneno yale ya
kejeli
“mume wangu maneno gani hayo unazungumza
mbele ya hawa watoto ndio kwanza umetoka
safari si ungepumzika kwanza kisha tuyazangumze
vizuri’?mama muksini alimwambia mumewe
Ghafla mama muksini kalamba kibao cha uso aja
kaa sawa kasukumwa aelekee chumbani, nisha
kuona vile akanyanyuka na kumshika mkono
dasoni wakakimbia mama muksini alipo taka kuwa
fuata mumewe akamzuia na kumpa maneno ya
vitisho,,,
“kama utathubutu kutoa mguu wako hapa ndani
na kuwafuata wale watoto jua kwamba ndio
umevunja pingu tulio funga mimi na wewe,
nimekaa mimi na wewe miaka kibao hapa hata
kusema mume wangu leo nimejisikia kichefuchefu
hakuna halafu unataka kuniletea vipaka vyako
hapa ndani baradhuli mkubwa wewe”
Mama muksini matumaini yake ya kutaka kuwalea
kina nisha yaligeuka na kuwa fadhaa, kilio
kikamsindikiza mpaka chumbani na huko kukawa
hakuna neno walilo kuwa wanazungumza zaidi ya
mumewe kumsema tu kwa kujichukulia maamuzi
kama yeye ndie mtafutaji.
Nisha akawa anamkimbiza dasoni waelekee
nyumbani kwao lakini hakika mwenyezi mungu in
mkubwa na alipangalo yeye hakuna anayeweza
kulipangua na watu wanaweza kushilikisha
maamuzi yake na uchawi kama tatizo likielemea
kwenye famila moja wakati,
Walipo kuwa kwenye mwendo huo ambao
ulisababishwa na kitendo kilichofanywa na mume
wake mama muksini cha kuongea kauli za
kuwanyanyapa watoto wale na kumpiga mkewe
kwa sababu yao kiliwafanya kutokuwa makini
wakati wakikimbia maana machozi pia yalikuwa
yanawatoka kwa hasira punde si punde sauti
iliyokuwa inaomba msaada ilisikika,,,,
“mama nakufaaaaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!!!”
Hapohapo na sauti za vioo vya gari lile kubwa lililo
kuwa limepakia viazi vilisikika vikivunjikavunjika,
watu wengi walionekana kukimbilia eneo lile
kutaka kujua nini kilichotekea huko.
“”ajali jamani ajali mungu wangu ni wakina nani
hawa” watu walikuwa wanazungumza
Baada ya watu kuwa wengi na kulizunguka gari lile
lililo ingia mtaloni na kuona maiti ya mtoto mmoja
wakiume baadhi ya watu walio kuwa wamemjua
mtoto huyo waliangua kilio papo hapo na kila
mmoja yalimtoka mengi mdomoni,,,,
“Kijiji hiki kina wachawi sana wamewakosea nini
familia hii ni juzi tu tumetoka kumzika mama yao
leo mtoto huyu naye ameaga dunia”
“Maskini dason ameaga dunia bila hatia”
“Nani ameaga dunia? Mtu mmoja aliuliza alihisi
kama amesikia vibaya vile,
“ ni dasoni mtoto wa mzee kazinge”
jamaa yule alivyosikia vile alitimua mbio kumfuata
david nyumbani kwao na alifika haraka sana
maana hapakuwa mbali sana na ajali ilipo kuwa
imetokea, alinzaa kugonga huku akihema,
“david david david!!!!
Kila alipo kuwa anaita akawa hajibiwi akaamua
kuchungulia dirishani hakuamini alicho kiona kitu
alicho kuwa anataka kukifanya david,,,,,
We david nakuomba usijiue rafiki yangu, nakuomba
sana sio kitu kizuri unachotaka kuki fanya kwa
wakati huu fikiria wadogo zako, kwanza mguu huu
nimekuja kwako kunatatizo limewapata wadogo
fanya haraka twende acha hicho unacho taka
kukifanya hakina faida nakuomba…
David aliachia kikombe kile kilichokuwa na maji
machache na kuzimwaga dawa zile zilizo kuwa
mchanganyiko kwa mshangao baada ya kusikia
wadogo zake wamepatwa na tatizo, alizubaa kwa
muda na kukurupuka kufungua mlango kisha
kutoka nje yule jamaa akampokea mlangoni na
kuanza kukimbia nae mpaka kwenye tukio lile
Alifika pale na kuukuta mwili wa mtoto mdogo
umefunikwa na kanga alipo ufunua alimkuta
dason,,
Maskini wa mungu david alilia kama mtoto mdogo
vile, makamasi yalishuka mpaka mdomoni mwake
ghafla akamkumbuka nisha,,
“Nisha wangu yuko wapi jamani”
“ nisha dada uko wapi njoo dada umejificha
wapi”??
david akawa anaita huku anazunguka kila upande
watu hawana la kufanya maana wengine wakujua
kama watoto hao wapo wawili ila baadhi ya watu
walio kuwa wana mjua wakawa wazunguka
kwenye majani kumsaidia kutafuta na wengine
wakajumuika pia,,,
“jamani kuna mtoto wa kike huku ila bado
anahema” mzee mmoja alifanikiwa kumuona nisha.
David ilimbidi aelekee kule alipofika alimkuta nisha
kaumia vibaya baada ya vioo vile kumchana
mgongoni na vingine kung’a ng’ania mwilini
mwake watu hawakua na muda wa kupoteza
wakamkimbiza nisha hospitali na kumuacha david
pale na maiti ya dasoni.
Tarifa ziliwafikia kina mama muksini na mumewe
hofu ikatanda kwao, mzee nyomolage naye
aliyekuwa shambani kwake aliweza kupata taarifa
hizo naye aliwahi kufika kwenye tukio ambapo
alikuta polisi wameshafika pale wakifanya taratibu
zao ambapo iligundulika kuwa na dereva wa gari
hilo naye amefariki dunia.
Hivyo polisi walitoa agizo kuwa wanandugu waka
zike maiti ya mtoto huyo dason maana ilikuwa
imeharibika vibaya na isingeweza kukaa
mudamrefu ingeaza kutoa harufu,
Hawakua na budi kufanya hivyo taratibu zote
zilifuatwa kaburi lilichimbwa pembeni ya mama
david na david kwa mara ya pili alibeba msalaba
wa mdogo wake.
Dasoni alifukiwa akawa amemfuata mama yake
mbele za haki yani ikawa pigo ndani ya pigo.
David alizidi kuisha kiafya kutokana na mambo
yalio kuwa yanamkabili na hakuwa na msaada wa
maana japo alishukuru kwa moyo waliouonesha
kina mzee nyomolage juu yake,
Usiku na mchana ulipokezana na siku zikasogea
nisha naye akawa ametolewa hospitali na kupewa
taarifa juu ya kifo cha dasoni kiukweli alilia kama
msiba ulikuwa unaanza upya vile.
Wazee walikaa kikao nakulijadili swala la msiba
ulivyo mfika dason hali ya kuwa alikabidhiwa
mama muksini. nisha ilimbidi kueleza kilichotokea,
na ndipo wanakijiji wakafikia muafaka kuwa
watamtenga mume wake na mama muksini.
Wakati kikao kilipo kuwa kinakaribia mwisho
alikuja afisa mmoja ambaye alijitambulisha na
kusema kuwa ametoka mahakama ya wilaya
akawapa barua kuwa mzee kazinge atafikishwa
mahakamani kesho hivyo wanaombwa familia yake
kufika huko
Wazee hao waliipokea barua na kuisoma na muda
uliwaonesha kuwa saa saa tatu asubuhi
wanahitajika kwenda kusikiliza hukumu ya alfredi
kazinge katika mahakama hiyo ya wilaya
****************
Adhana ya saa kumi na moja alfajiri iliyokuwa
inawakumbusha waislamu kwenda kufanya ibada
iliweza kumuamsha david toka usingizini na
kuegemea mto ulio kuwa kitandani na kuonekana
akitafakari jambo fulani hivi ambalo liliweza
kumyanyua pale kitandani na kuelekea chumbani
kwa wazazi wake.
Aliwasha mshumaa ili aweze kupata mwanga kisha
kufungua sanduku dogo ambalo lilikuwa
limewekwa chini ya uvungu wa kitanda na kutoa
baadhi ya makaratasi ambayo yalikuwa na picha
ndogo ya mzee kazinge kwa juu upande wa kulia.
Aliyangaalia kwa makini maelezo yale ambayo
yalikuwa yanaonesha uhitimu wa chuo kikuu cha
biashara ambacho alisoma mzee kazinge, kisha
akatoa albamu ya picha na kuanza kuzitazama
moja baada ya nyingine alitoa tabasamu kidogo
baada ya kuona picha ya baba yake kwa mavazi
ya kizamani aliyokuwa amevaa lakini hali hiyo
ilibadilika ghafla baada ya kuona picha aliyo piga
baba yake na marehemu mama yake siku ya ndoa
yao,
David hakusita kupeleka kiganja chake cha mkono
kwenye sura ya marehemu mama yake nakuanza
kukizungusha juu ya picha hiyo, alikumbuka
upendo wa marehemu mama yake tangu alivyo
kuwa hai mpaka umauti unamfika hivyo
aliinyakuwa picha hiyo mpaka kwenye mdomo
wake na kumpa busu la heshima mama yake na
baada yapo akatoa ishara ya msalaba
iliyomaanisha pumzika kwa amani.
Alizibeba baadhi ya picha kama kumbukumbu na
kuelekea chumbani kwa nisha, aliufungua mlango
taratibu bila kuingia ndani akawa anamwangalia
mdogo wake kipenzi aliye bakia, alihuzunika baada
ya kutupa macho kwenye kitanda cha pembeni
ambacho alikuwa analalia marehemu dason, david
alishindwa kuvumilia aliufunga ule mlango kisha
kuelekea chumbani kwake.na kuziweka zile picha
kwenye mkoba wake na kutoka nje kuandaa
kifungua kinywa cha asubuhi ili waweze kuelekea
mahakamani muda utakapo wadia.
ITAENDELEA
 
SEHEMU YA KUMI NA MOJA
Ndipo mpiga debe huyo alipo ongozana nao na
kuelekea kwenye stendi kubwa ya mabasi
yaendayo mikoani na kuwafikisha mpaka kwenye
basi la abood liliokuwa mbioni kuondoka na alipo
pewa chake akaondoka zake, david alikata tiketi za
watu wawili yeye na mdogo wake kisha wakaingia
kwenye gari na kutafuta siti zao kwa kuuliza uliza,
watu wengi walionekana kuwashangaa kutokana
na muonekeno wao maana tumeshazoea kuwa kila
tunaposafiri basi lazima tupendezze lakini kina
david walikuwa kama vile wanakwenda shambani
kwa kwa ajili ya kilimo kutokana na kukurupuka
kwao.
Honi ya kujiandaa ilipigwa na baada ya dakika
chacbe tu gari ikaanza kuchanja mbuga kuiacha
morogoro mjini na kuelekea dar es salaam, nisha
alionekana kufurahia safari hiyo maana hakuwahi
kupanda gari tangu alipoanza kujitambua kwa kiasi
fulani.
David nae aliegemea kwenye siti akiutafuta usingizi
huku mawazo hayakuacha urafiki na kichwa chake,
hakika mwendo wa gari hilo ulikuwa in mkubwa
sane hata abiria waliokuwa na roho nyepesi
walianza kupiga kelele kumuomba dereva apunguze
mwendo lakini hata ivyo ikawa kazi bure kwao na
mwendo huo ulio anzia saa mbili asubuhi mjini
morogoro uliweza kuwafikisha jijini dar es saalam
saa tano asubuhi hivyo waliweza kutumia muda
wa masaa matatu tu mpaka kufika hapo..
Abairia wakaanza kushuka kwenye basi hilo na
kulakiwa na ndugu zao waliokuja kuwa pokea,,kina
david nao walishuka na kuanza kushikana mikono
kwa hofu maana sifa za jiji hilo waliweza kuzisikia
kupitia vyombo mbalimbali vya habari hivyo david
ilimbidi awe makini kidogo, alisimama pembezoni
mwagari hilo akitafakari pakwenda alipopata wazo
la kutaka kutoka kwanza mle nisha alimwambia
david,,
“kaka nimesahau mkoba wangu kwenye gari mle
ndani”
“Aah nisha nawewe mbona mzembe hivyo?
Aliongea kwa kuchukia david maana aliona kama
anamchanganya hivi ndipo alipo muacha nisha
pale nje nayeye kuelekea ndani ya gari kuufuata
ule mkoba, alipofika kweli alifanikiwa kuukuta sasa
wakati anatoka alihisi kama amepatwa na upofu
hivi kutokana na kutomuona nisha pale nje alipo
muacha na kila alipo jaribu kuwauliza wale
walikuwa nae karibu walimjibu hawaju pia wapo
waliomtukana na kumpa maneno ya kejeli,,,
“we vipi umesikia sisi tumekuja kulinda watu hapa
embu chukua time bwana unatuzingua tu hapa”
David aliweza kuwashtua watu kwa kelele alizo
kuwa anapiga kumuita nisha huku akikimbia kimbia
ndani ya stendi hiyo kama mtu aliye pandwa na
maleria kichwani vile machozi yalimtoka lakini
hakuna hata binaadamu mmoja aliye thubutu
kushiriki huzuni na matatizo yalio mpata hapo la
kupotelewa na dada yake.
Kule kuchanganyikiwa alitoka mpaka ndani ya ile
stendi ya ubungo na kuanza kuparamia watu ovyo
kumuulizia mdogo wake lakini mbuzi wa masikini
hazai na kama akizaa huzaa dume basi ndicho
kilicho mkuta david baada ya kumparamia mama
mmoja hivi kwa ghafla na kuweza kumshtua yule
ama kinywa chake kilitoa sauti,,,
“mwiziiiiiiiiiiiii huyooooooooo jaman anataka
kunibia mwizi!!!!!!!!!!! Mwizi!!!!!!!!!!!!!!!”
Yale mayowe yaliokuwa yanapigwa na yule mama
yaliweza kukusanya kundi kubwa la watu wenye
silaha ya kila aina walio beba matofali, wengine
walikuja na matairi maskini david wa watu kila
alipotaka kutafuta njia ya kulikimbia kundi lile
kubwa la watu nafasi alikosa kilio cha hofu
kilimtokaaa
“Jamani sio mwizi mimi mnisamehe jamani
tafadhalini naombeni mnielewe”
kutokana na kulalamika kwa david baadhi ya watu
waliokuwa wana utu waliweza kuhisi yawezekana
kweli sio mwizi hivyo wakawa wanaanza
kumtetea,,
“mwacheni jamani embu tumsikilize mliona wapi
mwizi aliyekuwa amekubuu analia kama mtoto
msije mkauwa mtu asiye na hatia”
Wenye roho mbaya wakawa wanataka
kuwajumuisha wale waliokuwa wanamtetea david,,,
“ Haiwezekani wamezoea hawa nyie huyu
mwenzenu mnashilikiana nae”
Wakawa wanawavuta vuta na wale jamaa, zogo lile
kubwa lilimfanya askari wa barabarani aliye karibu
kusogea eneo lile na kujitahidi kuwazuia kitendo
cha kutaka kujichukulia sheria mkononi
“embu subirini kwanza jamani huyu kashafika
kwenye mikono ya sheria hakuna tatizo”
askari yule akawa anawatuliza raia wale wenye
asila kali kisha kuuliza wakati akiwa amemshika
david aliyekuwa anajitazama tazama michubuko
michache aliyeipata na machozi kumtoka,,,,
“yuko wapi aliye ibiwa? Afande aliuliza
“mimi ndiye aliyekuwa anataka kuniibia” yule
mama alijitokeza
“kwahiyo ajakuibia ila alikuwa anataka kukuibia?
Afande alimuuliza yule mama
“ndiyo”alimjibu
Askari yule alimwangalia david na kumkuta na
mkoba wa kike ameushika mkononi kisha kuuliza
tena,,,,
“Na huu mkoba wa nani?
Kabla david hajajibu sauti za watu waliokuwa
wanalazimisha kumtoa david kwa yule afande
wakawa wanasema maneno mengi sane tofauti,,,,
“huo atakuwa kashamliza mtu huyu mwangalie
macho yake yenyewe yamekaa kiwizi wizi”
“Oya mbona tunamchelewesha huyo tumuue”
Zogo likataka kuanza tena ndipo yule afande
akamwambia yule mama amfuate kuelekea ndani
ya stendi ambapo kuna kituo kidogo cha polisi na
huko kila mmoja alitoa maelezo yake lakini ya
david yalionekana kuto kusikilizwa hivyo alipelekwa
mahabusu na alikaa huko kwa muda wa miezi
mitatu mpaka alipotoka baada ya kuonekana
upande wa mashtaka hakuna ushirikiano hivyo
jarada lake likafungwa..
************************************
Mawazo mazito yaliyo kuwa yanachanganya akili
na ubongo wa david yalimfanya kudhohofika
sana,kiasi kwamba hata ukimtazama hutamani
kurudia,mara nyingi alikuwa mtu wa kurandaranda
mitaani kana kwamba kuna kitu cha thamani
anakitafuta kwenye maisha yake,
hakuna aliye jua david anasumbuliwa na nini
kutokana na kukaa kimya muda wote.kipindi hicho
jua lilikuwa kali sana watu wengi wa jijini dare s
salaam walionekana kutembea na miamvuli na
nguo zao zilikuwa nyepesi kutokana na
joto,wengine waliketi kwenye migahawa wakipata
vinywaji baridi kupoza koo zao, hata wasichana
warembo na kina mama walipumzika ndani ya
saluni waki jipamba na wengine kufanya umbea
kama ilivyo kawaida ya wanawake.
Ndani ya saluni moja iliyopo manzese iliyo
tambulika kwa jina la “mwanamke urembo”mwana
mama mmoja aliyekuwa amevaa dela jeupe lenye
nakshi zinazo ng’a akitengenezwa nywele zake
huku akipiga domo ghafla alisikika
“ yesu wangu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!”
Nini tena? Madada wa mle ndani waliuliza
lakini bila kutoa jibu alinyanyuka aliko keti na
kukimbilia nje huku akionekana kushangaa kila
upande wa eneo lile,wale madada pia walimfuata
na kumuuliza tena,
“vipi shoga mbona unatutisha? Halafu cheki
unavyo hema haraka kuna nini?
“mmh acheni tu nilivyo kuwa pale kwenye kioo
kuna kijana nimemuona akipita kwa nje lakini sina
uhakika kama ni yeye maana david ninaye mjua
pamoja na familia yake hawezi kuwa katika hali ile
niliyo muona,yupo mchafu mchafu pia amekonda
sana sijui amepatwa na nini?
“ Chaajabu nafika nje simuoni yani kama kumwaga
maji ardhini kipindi cha kiangazi ndivyo david
alivyotoweka
”
“.pole mama Victoria huenda ukabahatisha
kumuona tena siku nyingine”
,wanawake wenzie walikuwa wakimpatia moyo wa
kutokata tama.
Safari ile ya david ya kurandaranda mitaani
alijikuta akitokea magomeni ambao walikuwa
wakiishi zamani,kabla ya kuhamia gairo mjini
morogoro,
bila kutegemea david katikati ya barabaraa alijikuta
akisimama huku macho yake yakitazama nyumba
moja ya kifahari iliyoko mbele yake
,ile hamadi gari aina ya” opa” lipo miguuni kwa
david liki mpigia honi,pipipiiiiiiiiiiiiiiiiiii iliapishe
barabarani lakini david hakusikia kutokana na
kupigwa na butwaa kwa alicho kiona mbele yake,,,
kelele za watu zilisikika,,,,,,
“mtumeeeeeee!!!!!!!!!!!!!!!,mamamaaaaaaaaaa!!!!!!!
mungu wanguuuu!!!!!!,”
zote hizo zilikuwa juu ya david kunusurika
kugongwa na gari.hapo ndipo dereva wa gari hilo
alipoteremka na kuanza kumtoa david barabarani
huku akimsukuma na kumpa maneno yaliyo
karaisha moyo wa david,,
“we kijana unaleta pombe mpaka barabarani au
bangi zenu mnazo vuta na jua hili zina wazingua
kama wazazi wako wameshindwa kukulea sisi
tutakunyoosha ----- we huku akiendelea
kumsukuma”
hatimaye david akadondoka chini,akawa
anamtazama dereva huyo kwa hasira, alitamani
kumrarua rarua kama simba mwenye njaa
akimkamata swala,lakini david aliamua
kunyanyuka kwa upole na dereva kuishia zake.
David aliendelea kuingalia nyumba hiyo kwa huzuni
huku akiwa anasonga taratibu kuelekea pembezoni
mwa nyumba hiyo ambako kulikuwa na mti
mkubwa wenye kivuli na hewa safi kisha kuketi
mahali hapo.
mawazo ya david yalimrudisha sikiu chache
zilizopita na kuhisi kwamba mbele ya macho yake
kwenye ile nyumba ya kifahari kuna watoto wawili
dason na nisha ambao walikuwa wadogo zake
vipenzi wakicheza juu ya nyasi zilizo ng’a
kutokana na rangi yake ya kijani,
jicho lililojaa huruma na majonzi likaanza kutoa
mchozi taratibu huku sauti ya chini ikisikika
kugugumia
”mhmhmhmhmh”
kama unavyojua damu ni nzito kuliko maji david
alishindwa kuisaliti nafsi, sauti ya david ilisikika
mtaa mzima ikiita nishaaaaaaaaa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!,
hata ndege waliokuwa juu ya ule mti mkubwa
waliruka na pia watu waliokuwa wakipita
kandokando ya barabara shingo zao zilionekana
kugeuka huku na kule kwa shauku ya kutaka kujua
sauti ile ya huzuni na majonzi ilikuwa inatokea
wapi
David aliendelea kulia kwa uchungu bila majina ya
wadogo zake vipenzi dason na nisha kukauka
mdomoni mwake.aliketi mahali hapo mpaka kiza
kikaingia,alipigwa na baridi la usiku na kung’atwa
na mbu,
hatimaye david kwenye mikono ya askari
waliokuwa doria usiku ule wa manane,hakuna
msaada alioambulia zaidi ya kipigo kutoka kwa
askari hao wakizani kuwa ni kibaka,shati lake lenye
rangi ya kijivu lililowa damu hata mguu wake
wakushoto uliteguka kutokana na kupigwa virungu
vya ugoko,alipelekwa mpaka kituo cha polisi
kilichopo hapo magomeni bila kupewa huduma
yoyote ya kwanza, siku hiyo david hakulala kabisa
kutokana na maumivu makali aliyo ya pata.
Asubuhi ilipofika askari waliokuwa zamu usiku ule
walipeleka ripoti kwa mkuu wa kituo
ikiambatanishwa pamoja na majina ya
watuhumiwa hao.,Afande cris ambaye alikuwa
mkuu wa kituo alipopitia taarifa hizo anakuta jina
la “david kazinge” alihisi kama analifahamu jina
hilo hasa la kazinge, ndipo alipo muita afande juma
na kumwambia…..
”nenda kawatoe watuhumiwa wote walio kamatwa
usiku na wapange foleni mara moja sawa?
“Sawa afande”,
afande juma alifuata agizo hilo bila kipingamizi
alielekea mahabusu na kuwaamrisha watoke nje
“haya haya toka haraka na panga foleni mara moja
huku akiwapiga na virungu migongoni”
.baada ya zoezi hilo kukamilika afande cris aliitwa
nakuanza kuwatazama watuhumiwa usoni kwa
makini huenda akabahatisha kumjua david
kazinge,akawa anakwenda anarudi anakwenda
anarudi mwishowe aliweka kirungu begani kwa
kijana mmoja na kumuuliza kwa ukali,,,,,
” wewe ndiye david kazinge?
Sauti yenye kutetemeka ikiambatana na woga
ilijibu,,,,,
” ndi ndio mimi afande” david alijibu
.”haya nifuate ofisi kwangu”alimueleza david
.afande cris alikuwa ametangulia na david nyuma
akimfuata huku akichechemea,walipo fika ofisini
afande cris aliketi, david akawa amesimama moyo
wake ulikuwa na hofu kwakuwa hakujua kwanini
yupo pale.
ndipo afande cris alipo muamuru kukaa,,,
” hey! david alishtuka,
“unaweza kukaa”,alipo keti akawa anamtazama
afande cris atazungumza nini,,
.
“ Wewe ni mtoto wa mr.kazinge ambaye alikuwa
anafanya kazi benk ya nmb? afande alimuuliza
swali david
David alikubali,
Jesus Christ!!,afande alishangaa na kuuliza,,,,
“Ina maana baba yako hajatoka gerezani mpaka
leo?
Bila kujibiwa aliendelea,,,,
“Kwa hali uliyonayo ni dhahiri umekosa mahitaji
muhimu kwa muda mrefu”
“,kwa hiyo kwasasa mnaishi wapi wewe na family
yako na imekuaje mpaka wewe kuwepo hapa
kituoni?
Afande criss alimuuliza david huku akionekana
kuguswa sana na hali ya david
. Macho ya david yalionekana kumwangalia afande
criss kwa huruma na mdomo wake ukionekana
unataka kujibu lakini aliishia kutaja,,,,
” fa, fa fa!!!!”
ghafla akadondoka chini na kupoteza fahamu papo
hapo.
Afande chriss alishtushwa sana na kitendo kile
ndipo alipo waita maafande wenzie kisha kumbeba
kwenye gari ya polisi na kumu waisha hospitali
iliyopo hapo magomeni.
*************************
Upande wa mama victoria ambaye alimuona david
kule saluni, alionekana kukosa amani tangu alipo
muona david,
alijikuta akifikiria mambo mengi sana hasa ukweli
na siri nzito alio nayo ndani ya moyo wake,
alitamani kuonana na familia ya kina david ili
awaelezee juu ya ukweli huo lakini hakupata nafasi
hiyo maana hakujua wapi wanapatikana,
baada ya kufikiri kwa muda mrefu alipata wazo la
kuwatafuta bila kujua wapi anaanzia...
ITAENDELEA
 
Kazi nzuri willy shusha vitu mana muda unaelekea kwisha wakifurushi
 
SEHEMU YA KUMI NA MBILI
Upande wa mama victoria ambaye alimuona david
kule saluni, alionekana kukosa amani tangu alipo
muona david,
alijikuta akifikiria mambo mengi sana hasa ukweli
na siri nzito alio nayo ndani ya moyo wake,
alitamani kuonana na familia ya kina david ili
awaelezee juu ya ukweli huo lakini hakupata nafasi
hiyo maana hakujua wapi wanapatikana,
baada ya kufikiri kwa muda mrefu alipata wazo la
kuwatafuta bila kujua wapi anaanzia...
Muda ulikwenda masaa yalikatika, kule hospitalini
david alionekana kupata fahamu baada ya kupewa
huduma nzuri katika hospitali hiyo,wakati huo
afande criss alikuwa katika dirisha la muhasibu
akilipia bili ya matibabu,
,saa ambayo anajirejesha hodini alimkuta david
akijitahidi kujiinua pale kitandani,tabasamu
lilionekana kwenye uso wa afande criss baada ya
kuona hali ya david inaendelea vizuri,
ndipo alipo msogelea na kumshika kichwani huku
akimwangalia usoni na kumwambia maneno ya
faraja,,,
”David mwanangu pole sana ninachokuomba kuwa
na amani kwenye moyo wako,
Hutorudi tena kituoni tutaenda kuishi wote sawa”?
David alitingisha kichwa kukubali.
Afande criss alipomaliza tu kuongea sauti ya dokta
ilisikika,
”Unaendeleaje david”?
”Nzuri tu dokta namshukuru mungu,”
Baada ya mazungumzo na david dokta akawa ana
ongea na afande criss,
”Afande,,.mgonjwa wako hana tatizo kubwa ila
kilichokuwa kina msumbua ni msongo wa mawazo
yaliyo ambatana na njaa ambayo yalipelekea
mzunguko wa damu kuwa mdogo ndio maana
alipoteza fahamu hivyo chukua cheti hiki ukanunue
hizi dawa zita msaidia na sasa mnaweza
kwenda.dokta alitoa ruhusa.
Bila kupoteza muda safarari ya kuondoka ikaanza
wakiwa na gari ile ya polisi,afande cris alimpeleka
david hotelini kisha kumpitisha dukani na
kumnunulia nguo kadhaa za kuanzia,
Walifika mabibo external ambapo afande cris
alikuwa akiishi,
David alkaribishwa vizuri nyumbani kwa afande cris
lakini ukimya wa nyumba hiyo ulimfanya david
kuuliza,,,
”mkeo na watoto zako wako wapi?
Afande cris alitabasamu kidogo kutokana na swali
ambalo david amemuuliza kisha kumjibu,,
”tume tengana muda mrefu sasa na hapa naishi
mwenyewe tu kwakuwa na wewe upo basi angalau
nyumba itakuwa imechangamka”
David alionekana kutoamini ukarimu alio kuwa
ameoneshwa na afande cris kwa muda mfupi,
Alitaka kumuuliza maswali mengi zaidi lakini
alikumbuka usemi wa baba yake kuwa
”usimuamini yoyote yule pia penda kuwa mtu wa
kusikiliza na kusema kidogo tu ili upate kujua
mengi zaid.”
Hivyo david akafunga kinywa chake na kuendelea
kusikiliza afande criss akizungumza tu;
********************************
Mwaka huo ulikatika na david akawa amesha
mueleza afande criss yote yalio mkuta na juhudi za
kumtafuta nisha zikawa zinaendelea ila
hakumwambia swala la ushahidi kuhusu
mwanamke ambaye baba yake alimwambia akifika
mjini amtafate na afande criss kumuahidi kuwa
atakuwa nae bega kwa bega mpaka atakapo
fanikiwa kupata mali zake,,
Siku moja ya mapumziko mishale ya saa mbili
usiku wakati taarifa ya habari inatangazwa waziri
wa elimu alitangaza kuwa matokeo ya kidato cha
sita sasa yapo hewani na kiwango cha ufaulu
kimeongezeka kwa asilimia 65 toka yale ya awali
yalio kuwa na asilimia43,
Taarifa hizo zilimshtuwa sana david maana na
yeye alikuwa anahusika katika mtanange huo
Hivyo afande cris naye hakuchelewa akaenda
kuchukua laptop yake na kuanza kutafuta namba
ya mtihani ya david ambayo alimueleza tayari,
Nyuso za furaha zilionekana usoni kwa kila mmoja
baada ya kuona matokeo ya david kuwa amefaulu
kwa kupata daraja la pili hasa yale masomo yake
ya sayansi,
Lakini ghafla tu furaha ya david ilikatika na afande
cris alimuuliza,,,,
”vipi david hukuridhika na daraja ulilo pata? Swali
hilo david hakujibu na mchozi mwembamba
ukaanza kumtoka,
Afande criss ilibidi amuulize tena,,,
”David mwanangu tatizo nini embu niweke wazi
basi?
Ndipo alipo nyakuwa kinwywa chake na kusema,,,,,
”nafanikio haya madogo nilitamani wangekuewepo
familia yangu hapa lakini sina jinsi”’
Afande cris alizidi kumpa maneno ya kiume david
na kumueleza jumatatu wataenda morogoro mpaka
gerezani alipo mzee kazinge na atapata
kuzungumza naye david jicho lilimtoka------------
Ile siku iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu ya
kwenda kijijini kwa kina david ikawa imewadia,
david alionekana kubadilika kutokana na siha nzuri
ya uso aliokuwa nao kutakata na maji yale ya
chumvi ndani ya jijini lenye kila aina ya ufuska na
wingi wa watu jiji la dar es saalam,
Afande cris kazi yake ilikuwa kuachia tabasamu tu
kwa david maana alikuwa kanyonga tai ya
kiuutuuzima shati lake la mikono mirefu renye
rangi ya zambarau lilijitosheleza vizuri ndani ya
suruali ile nyeusi achia mbali kile kizibao
kilichoendana na rangi ya suruali,
Nywele zake alizofuga kiasi na kuzitana vizuri
zilizidi kung’aa hasa kutokana na mafuta maalumu
kwaajili ya nywele, hakika shida ndizo zilizo kuwa
zinauficha ushababi wa david lakini kwa hali ya
sasa hakuna mwanamke ambaye akaambiwa lugha
ya ushawishi wa kimapenzi akakataa kwanza ni
lazima huyo mwanamke atapata uwoga kwa
kutojiamini kusimama na david,
Afande cris na david waligonisha matabasamu yao
kisha kupanda kwenye ile mazda yenned namba za
usajiri Tz6210, kisha mafuta kukolezwa safari
kuelekea morogoro, foleni ile ya pale maeneo ya
kimara mpaka mbezi kwa msuguli iliwapotezea
kama dakika 45 hivi walipo imaliza mazda ikawa
imepamba moto,,
Injini ya gari ile iliweza kuwatunzia heshima yao
kwa kutowasumbua njiani mpaka walipo kuwa
wanaingia kwenye ardhi ile yenye sifa ya kuwa na
udongo mwekundu na kunyimwa bahari, hiyo ni
ndani ya milima ya uluguru Morogoro
Hapo morogoro mjini waliweza kupumzika kwenye
bar moja inayoitwa makuti
Kupata vinywaji na chakula kupoza njaa kidogo
baada ya kuwa wametembea njiani kwa muda usio
pungua masaa matau hivyo walikuwa wanatoa
uchovu wa safari hiyo,
Wahudumu waliokuwa wana wahudumia
walitamani kwenda kwenye meza hiyo mara kwa
mara kutokana na mvuto wa david japo mwenyewe
aliweza kujua kuwa wasichana hao walikuwa
wanajigonga gonga kwake lakini kwa upande wake
hakujali yani kama moyo wake wa upendo ulipigwa
kufuli na matatizo yalio kuwa yana muandama kwa
muda mrefu,
Hapo ilikuwa sio mwisho wa safari walikuwa na
saa moja na nusu hivi mpaka kufika gairo kijijini
kwa kina david hivyo walivyo maliza kula na
kunywa mazda ikawashwa upya na kuchukua
barabara inayoelekea dodoma ili waweze kufika
gairo eneo maarufu kwa ulimaji wa viazi vitamu,
Ndani ya saa saba na mchana wakawa wapo ndani
ya kijiji cha gairo, watu wengi walianza kulishanga
lile gari lilikuwa linaelekea nyumbani kwa kina
david maana palionekana kuwa kimya kwa muda
mrefu sana, majani mengi yaliota kuzunguka ile
nyumba ambapo ilikuwa in dalili tosha kwamba
kulikuwa hakuna mtu,
Jambo hilo pia lilimshangaza david sana yani,
hakujua kwa nini pale nyumbani pako vile,iliwabidi
washuke haraka na david akaanza kugonga lile
geti,,,,,
“mzee nyomolage, mzee nyomo lage!!!!!!!!!!!!!!!!!!!,
lakini kimya kilizidi na mwangi ndio uliokuwa
unamjibu kama yeye alivyokuwa anaita,
Lakini punde tu kuna mmama mmoja hakuwa
mbali na pale akawa anawapigia kofi kama ishara
na kuwaoneshea mkono kama ishara ya kuwaita,
afande cris alimtazama na david kisha wakaelekea
kule alipo yule mama,
Walivyofika yule mama aliwaomba waelekee
nyumbani kwake ambako kulikuwa si mbali sane
na pale na huko aliwakalibisha na kuanza
kuzungumza,,,,
“david baba yani mmekuwa maarufu kijiji kizima
hakuna asiyejua habari zenu ,hakuna asiyetoa
chozi kwa ajili yenu kila mtu anawa hurumia
nyie!!!!!!!
Maneno hayo bado yakawa yanamuweka katika
wakati mgumu sane david na afande criss
walishindwa kumuelewa yule mama alikuwa ana
maana gani ilibidi david ambembeleze azungumze
kitu ambacho wanaweza wakamuelewa,,
“mama tafadhali in yale yale au kuna mengine
yametokea maana hali ya nyumbani kwetu
sijaielewa!!!, wakati naondoka tulimuacha mzee
yomolage pale nyumbani lakini tunafika kuna
onesha hakuna dalili zozote zile za kuwepo na mtu
wala vitu ndani kwa kuwa ule mwangi nilikuwa
nausikia kama vile nyumba ipo tupu nakuomba
mama tueleze ukweli mzee nyomo lage yuko
wapi?????
David sasa hali ikaanza kubadilika kwake na
machozi kuonekana kulenga lenga kwake hapo
afande cris kama mtu mzima naye alichukua nafasi
ya kuzungumza na yule mama iliawaeleze hali
halisi iliyo tokea ndipo yule mama ikabidi awaeleze
kilichotokea,,,,,
“ilikuwa ni siku moja ililyokuwa na mvua kiasi
ambapo watu wengi walikuwa wakipishana
kuikimbia mvua ile kuelekea ma kwao nami nikiwa
mmoja wao niliyekuwa naikimbia ile mvua kuja
nyumbani kwangu, sasa wakati na pita nilisikia
kelele mle ndani kwenu zikijibizana na sauti
niliyoweza kuitambua ni ya mzee nyomolage
ikilalamika kujibu maswali ila ile iliyokuwa inauliza
sikuweza kuitambua,,,,,
“watoto wa alfred wako wapi wewe mzee eeh?
Kunamtu alikuwa anauliza kwa ukali sane
“Sijui mimi jamani walipoenda, nimewatafuta sana
kila kijiji lakini sikuwapata na ukweli sijui
watakuwa kijiji gani kwa sasa” mzee nyomolage
nilimsikia akijibu swali hilo kwa sauti ya machozi
tena nikasikia sauti za watu wengine zikimuuliza
swali hilohilo la kuwaulizia nyinyi,,
Ghafla niliwaona watu ambao walikuwa wamejazia
wasio pungua watatu na mmoja aliyekuwa amvaa
suti na miwani ya kitanashati wakitoka mle ndani
na kupanda kwenye gari kisha kuishia punde tu
alitoka mzee nyomolage na kutimua mbio kuelekea
kusiko julikana mpaka leo hii hatuji kama mzima
au amekufa,
Wanakijiji ambao nao walipata kuliona tukio hilo
kwa mbali kama mimi niliye jibanza kwenye mti
kushuudia tukio hilo tuliaandamana mpaka kwenye
serikali ya kijiji na kutaka swala hili lifatile kisheria
kuna tatizo gani mpaka familia hii inyanyasike kiasi
hiki na yote hayo yalibebwa na tukio zito ambalo
tulipata kusikia kwamba na baba yako mzee
kazinge amefariki huko akiwa gerezani na kuzikwa
na serikali baada ya kukosa ndugu,,
hicho ndicho kilichotokea yani mungu ashukuliwe
kuwaepusha wewe na nisha katika tatizo hili
yawezekana kizazi chenu kingeishia siku ile kama
nanyi mngekuwepo,,
***********************
Maneno hayo yalimfanya afande criss alijisikia aibu
sana kwakuwa na yeye in mmoja katika vyombo
vya dola na baada ya david kushikwa na hasira na
kulalamaika kwa kilio ambacho alikuwa anailaumu
serikali nzima.,,
Afande cris alizungumza na yule mama na
kushukuru kwa ujumbe ambao walimpatia kisha
kumbembeleza david anyamaze iliwajue wanaanzia
wapi kulifatilia tatizo hilo,,
Baada ya kuwaza na kuwazua afande alitoa wazo
waende kwanza shuleni kwako alikosoma david
wakachukue vyeti vyake vya form six lakini kabla
hawajaelekea huko afande alimuuliza swali yule
mama,,
“sasa mbona na ule mlango umefungwa in nani
aliyeufunga na wakati mzee nyomolage alikimbia?
“ni mimi ndie niliyempa kufuli mwenyekiti alipokuja
kuhakikisha na serikali ya kijiji baada ya kusikia
mzee nyomolage amekimbia hivyo funguo zingine
ni nazo mimi kama mnazihitaji naweza kuwapatia”
afande cris alizihitaji ili wakaangalie usalama wa
mle ndani,
Zoezi hilo lilifanyika wakawa wamekwenda mle
ndani na kwa bahati nzuri vitu muhimu walivikuta
kama vile picha na vyeti vya kidato cha nne vya
david na walikwenda shule wakapatiwa vyeti vya
kidato cha sita na siku hiyo wali lala kwa huyo
mama na asubuhi yake safari ya kwenda gerezani
kutaka kujua kilichomuua mzee kazinge ni nini na
swala hilo afande cris kuahidi kuwa atalifatilia-
Ndami ya david alikuwa anaona kama wanachelwa
vile kufika kule gerezani, mawazo ya hasira
yalikuwa yanakuja kichwani mwake juu ya afande
criss kuona ndio wale wale tu kama maaskari
wengine, uso uliiva kwa hasira kila akifikiria
matukio yaliokuwa yanaongozana,afande crss nae
alisha gundua gadhabu anayo ipata david kwa
wakati ule hivyo alijitahidi kuendesha gari hilo kwa
mwendo kasi mpaka lilipo wafikisha salama
kwenye kwenye gereza alilokuwa amefungwa
afande mzee kazinge,
Walifika getini na kufuata utaratibu wa
kujiandikisha jina lako, mahali unapoishi na mtu
unayekwenda kumtazama,. Swala hilo halikuwa
gumu kwako, walijiandikisha lakini ujanja
alioutumia afande criss ulikuwa wahali ya juu sana
alimnong’oneza david sikioni kisha matokeo ya
yale aliyo mwambia kwa siri yalikuwa ni haya,,
Kwakuwa afande criss alikuwa in mtu mzima pia
hakuvaa kipolisi alikwenda kama raia wa kawaida
hivyo yeye aliandika anakwenda kwa mkuu wa
gererza na divid aliangalia jina moja la juu baada
kama ya majina matano hivi akaliandika kuwa
anakwenda kumuona mtu yule kumbe hata kumjua
hamjui ila lengo lilikuwa in kutaka kuonana na
wafungwa angalau anaweza akapata chochote kitu
juu ya kifo cha baba yake..
ITAENDELE
 
SEHEMU YA KUMI NA TATU
Kwakuwa afande criss alikuwa in mtu mzima pia
hakuvaa kipolisi alikwenda kama raia wa kawaida
hivyo yeye aliandika anakwenda kwa mkuu wa
gererza na divid aliangalia jina moja la juu baada
kama ya majina matano hivi akaliandika kuwa
anakwenda kumuona mtu yule kumbe hata kumjua
hamjui ila lengo lilikuwa in kutaka kuonana na
wafungwa angalau anaweza akapata chochote kitu
juu ya kifo cha baba yake..
Walivyo maliza wote walitoka kwa pamoja na kila
mmoja alikwenda kwenye upande wake lakini
afande alizi kumsisitiza david awemakini katika
uulizaji wake, na yeye alikwenda kuonana na mkuu
wa gereza na maongezi yao yakaanza baada ya
kuwa amefika ndani ya ofisi,,,
“habari ya kazi mheshimiwa? Afande criss
alimsalimia yule mkuu wa kituo
“salama tu habari yako na wewe?
“Namshukuru mungu niko salama:” afande criss
alijibu
“Mmmh nikusaidie nini? Ule mkuu wa kituo
alimuuliza afande criss
“mheshimiwa mimi ni ndugu yake na marehemu
alfred kazinge ila sikuwepo hapa nchini kwa muda
kidogo na nimekwenda nyumbani kwake kule gairo
sikufanikiwa kuikuta hata familia yake zaidi ya
kukuta makaburi mawili la mwanane na mkewe na
taarifa za majonzi ambazo zimenifanya nije hapa
hivyo nilikuwa napenda kujua ndugu yangu alikufa
kwa ugonjwa gani na wapi alipo zikwa”
Jicho lilimtoka yule mkuu wa kituo na kuanza
kukuna kichwa akitafuta jibu la kumpatia afande
criss na baada ya kujishauli kwa muda kidogo
aliweza kumwambia ,,,
“kwanza pole sana kwa msiba ulio kupata na hata
hivyo kifo chake kimetuhudhunisha sana hapa
gerezani alfred alikuwa na ucheshi sana kila
mmfungwa alikuwa nanamtania lakini kumbe
ucheshi huo tulishindwa kuutambua mapema kuwa
alikuwa ameanza kuchanganyikiwa mpaka siku
moja walipo kuwa wanafanya usafi mdogo wa
gereza hili kulimalima na kufyeka majani alijaribu
kuchukua kifaa kimoja na kutaka kujiua lakini
wenzie walimuwahi na kumpeleka gerezani na
baada ya siku tatu hivi alikutwa amekufa pembeni
ya pembeni ya kuuta wa gereza ambapo wenzio
walikuwa wanalima na uchunguzi wa polisi
ulipofanyika tuligundua kuwa amekufa kwa sumu
na wala hatujua aliitoa wapi naa kuuamua kuinywa
hivyo ndivyo tulivyo mpoteza alfred kazinge”
Pumnzi ndefu ilishuka kwa afande criss na
kumwangalia yuke mkuu wa gereza aliyekuwa
anajiangaisha pale kwenye kiti huku akionekana
akili yake haipo sawa na kisha kumuuliza tena,,,,,
“Na alizikwa na nani?
“Serikali ndio ilimzika baada ya kuwa hakuna
ndugu hata mmoja aliyekuja”
Kwa maelezo aliyo sema yule mkuu wa gereza na
kutokana na uzoefu wa kazi yake ya kipolisi afande
criss aliweza kugundua kuwa kuna kitu kinafichwa
pale basi hakutaka kupoteza muda alimshukuru
yule mkuu wa gereza na kumuaga kuwa
anaondoka basi walipeana mikono kisha afande
criss kutoka nje,.
Na upande wa david yeye alilitumia jina lilelile
ambalo aliiandika kwenye kile kitabu na kuitiwa
yule mfungwa mwenye jina la frank mgaya ambaye
au kwa jina lake la utani walikuwa wanamuita sir/
side in kutokana na ucheshi aliokuwa nao. Na
kuanza kuonge nae,,
“samahani sana kaka najua hunijui na wala mimi
sikujui lakini niliweza kupata jina lako pale kwenye
kitabu cha wanao wasili na ombi langu kubwa
ambalo kama utanisaidia basi mimi kuanzia leo
nitakuw anakuja kukusalimia na kukuletea
chochote ambacho utakuwa uanataka kutoka nje”
david alizungumza,
Yule jamaa frank mgaya aliposikia maswala ya
kuleteana vitu hakutaka kulemba akijiweka vizuri
kutaka kusikiliza hilo jambo amabalo anataka
kuambiwa na david ndipo alipomuuliza,,,
“ namjua alfred kazinge ambaye sasa in
marehemu?
Frank kabla hajajibu alikuwa kama amelisahau jina
hilo hivyo akawa kama nanjaribu kulikumbuka hivi
ndipo na yeye akamuuliza swali david iliapate
uhakika,,,,
“umesema kuwa sasa in marehemu?
“ndiyo” david alimjibu na ndipo yule mfungwa frank
alipokuwa amekumbuka na kumwambia,,
“aaah nimekumbuka ungesema Bob “k” ndio jina
mbalo kila mmoja alikuwa analijua hapa kutokana
na kule kudata kwake na mambo aliyokuwa
anayafanya kwani wewe nani yako? Frank
alimuuliza david
“ni baba yangu mzazi”
“Sasa rafiki yangu ulikuwa wapi mpaka baba yako
anakufa kinyama na kuzikwa na wafungwa kama
vile mbwa yani dah kiukweli bob k alichofanyiwa
lilikuwa sio jambo la kiuungwana kabisa wengi
walishuhudia tu mazishi yake lakini wachache ndio
ulishuudia kifo chake na mimi in kiwepo yani kama
unamungu sana kukutana na mimi yani” frank
alimwambia david na david sasa akaa mkao wa
kula kusikiliza kilicho tokea baada ya kumuiliza
ilikuwaje,,,,,,,,,,,,
“siku moja tulikuwa tumetoka kumaliza usafi
tukawa tuna kula na ukweli mzee wako alikuwa
ameanza kuchanganyikwa bila watu wengi kujua
kwakua alikuwa anaucheshi sana lakini hata hivyo
kuna baadhi ya mambo alikuwa anayafanya lazima
mtu ushtuke kidogo kuwa huyu mtu hayupo sawa
sasa tulipokuwa tunaendelea kula tukaona kuna
watu kama wanne hivi wamekuja mmoja akiwa
mevaa suti nyeusi na wengine walikuwa wamejazia
jazia hivi na bob k yeye alikuwa amejitenga na sisi
ambao tulikuwa karibu na eneo lile lakini ili kuwa
si rahisi kutuona, basi wale jamaa walionekana
kuelekezwa na askari alipo kuwa bob k na
wakafika mpaka pale na kumzunguka wakijifanya
wanacheka nae kumpa mikono ilikutengeneza
uhalisia wa udugu,
lakini bob k alipigwa na butwaa kumuangalia yule
jamaa aliye kuwa amevaa suti nyeusi kisha
kujipiga piga kichwani kulazimisha kukumbuka kitu,
wakati tukio hilo la bob k kupigwa na butwaa
mmoja kati ya wale akatoa kitu kwenye koti lake
na kuweka kwenye chakula cha bob na mwingine
akampiga na gazeti kichwani na kuliacha pale
kisha kuondoka zao na baada ya muda tu ndipo
tuliposikia bob k amefariki dunia na ukweli hakuna
hata mmoja aliyejitokeza kufuatilia swala hili ila
nimeshangaa sana unasema wewe mwanae na
ulikuwa wapi siku zote?
“Nilikuwa shuleni”: david alimjibu kwa mkato na
kuonekana kutafakari jambo hivi kisha kumuuliza
tena yule mfungwa,,
“hilo gazeti liliandikwa nini”
Kiukweli mimi sikufanukiwa kuliona ila waliokuwa
zamu kufanya usafi kule kwenye ofisi ya mkuu wa
gereza waliliona na kuja kusema kuwa bob k
alikuwa na matatizo sane ya kumpoteza mkewe
sijui nini mambo mengi sana si alikuwa nakaa
gairo?
“ndiyo”
“Basi mle pia waliandika baada ya washkaji
wengine waliokuwa wanatokea huko kulala mika
kuwa wamempoteza ndugu yao wa kutoka kijijini
kwako”
Wakati maongezi yakiendelea muda wao ukawa
umeisha hivyo yule mfungwa alirudishwa gerezani
na david alimpatia dole kuwa usijali tuko pamoja
kisha david kuondoka na alipofika nje alikutana na
afande criss wakawa wanaelekea kwenye geti
kubwa la kutokea nje lakini wakati wanaenda
afande criss aligundua kuwa amesahau funguo
npale kwenye meza ya mkuu wagereza ilimbidi
arudi moaka kule na alipo fika mlangoni alimsikia
yule mkuu wakituo akiongea na simu iliyomshtua
afande criss-Baada ya kusikia manane haya,,,,,,
“ee bwana ule mpango umeharibika kuna,,,,,,,!!!!!!!”
wakati hajamalizia kusema kuwa kuna nini kuna
askari alikuwa anapita pale nje alihisi kama afande
cris ametega sikio ndipo alimpomhtua kwa
kumwambia,,,,
””nikusaidie nini mzee wangu?afande criss
alijiumauma na kusema,,,,
“asanate sana kjiana naingia humu sema nilisahau
in mlango gani hivyo nikawa anafananisha hii sauti
lakini sasa nimegundua kuwa ni humu
ninakotakiwa kuingia”
Yule askari alistupa macho yake juu ya mlango wa
mkuu wa gereza na kukuta kibao kimeandikwa
“ofisi ya mkuu wa gereza” kisha akarudisha macho
yake kwa afande criss ambaye naye hakutaka
kupoteza muda akausukuma ule mlango bila
kubisha hodi na kuingia mle ndani,
Mkuu wa gereza aliposikia mlango wake
unafunguliwa alikata ile simu haraharaka na
kujifanaya anatafuta baadhi ya nyaraka pale juu ya
meza yake na afande criss naye akajifanya kama
hakusikua hata neno moja ambalo lita mfanya
ajaue pakuanzia. Alimuomba ladhi yule mkuu wa
gereza kwa kuingia bila kubisha hodi na kuchukua
funguo zake na kutoka zake huku akiwa na jambo
kichwani na kumuachia maswali yule yule mkuu
wa gereza aliyokuwa anajiuliza na kujipa majibu
yasio kuwa na uhakika,,,,
Alitoka njee kabisa na kuungana na david kisha
kuanza safari ya kuelekea ndani ya jiji la dar es
salaam. Ndani ya gari walitumia umbali huo
mpaka kufika dar es salaam kwa kuambizana kila
mmoja alichokipata walivyo jigawa iliwajue wapi
pa kuanzia,
Maelezo ya david yalimpa afande criss uwanja
mkubwa sane wa kufikiria nini afanye ili wa weze
kukamilisha ushahidi bila ya kujua kuwa kuna mtu
ambeye david alimsikia kuwa anaushahidi ambao
ungeweza kuwasaidia lakini naye pia hakusema
jambo hilo kwa afande criss akihisi asije
akamfanyia kama yale ya aliyofanyiwa marehemu
baba yake na helman,
Safari ilizidi kunoga kwa kila mmoja kutoa wazo
lake juu ya swala hilo mpaka walipofika jijini na
moja kwa moja gari ilianza kukataa mitaa na
kuelekea nyumbani kwa afande criss, kila mmoja
alikuwa amechoka kutokana na uzito wa jambo
hilo akifikiria ni wapi pakuanzia maana kama
utakurupuka unaweza kufungwa wewe ndivyo
afande criss alivyokuwa anawaza,,,
Afande criss alimuangalia david ambaye
aliyeonekana kuchoka zaidi hasa kwa mawazo ya
jinsi babaye alivyo uwawa kikatili na kuzikwa kama
mbwa lakini hakuna mtu aliye jali wala kufatilia
swala hilo ndipo afande criss alipo mwambia david
ampatie vile vyeti vyake vya form four na form six
kisha akaanza kuviangalia kwa makini na
kugundua kuwa katika somo la hesabu pia david
alifanya vizuri amabalo linaweza kumpa fursa ya
yeye kusomea kitu ambacho yeye alikuwa
anakifikiria ilikiweze kuleta urahisi katika uchunguzi
wake,
Afande cris alimuita david ambaye alikuwa mbali
kimawazo na kumwambia,,,,
“david kuna wazo nimelipata!”
“Lipi hilo? David aliuliza na kukaa mkao wa kula
“embu somea shahada ya mambo ya
kibiahara”afabde criss alimwambia, lakini david
alionekana kupinga
“kwa nini afande mimi nina ndoto zangu za kutaka
kuja kuwa daktari bingwa wa moyo iliniuma sane
mama yangu alipokufa kwa ugonjwa huo hivyo
inanibidi nisomee udaktari ilinije kushuhudia
mgonjwa anakufa kwa ugonjwa wa moyo mbele
yangu, mimi siwezi kusome hayo maswala ya
kibiashara afande” david alikataa katakata lakini
afande criss ndipo alipoamua kumuelewesha na
kumfafanulia vizuri zaidi,,,,,,,,,
“david sikia in kwambie kumbuka kuwa baba yako
alikuwa anafanya kazi benk maana yake alisomea
maswala ya kibiashara hivyo na marafiki wake
wengi in lazima watakuwa in wafanya biashara
hata matatizo yake yametokana na fedha za benki
ambazo in za biashara kwa hiyo sasa wewe
ukisomea maswala hayo in rahisi kuwajua watu
wengi waliokuwa wanafanya biashara na baba
yako, matajiri wengi utawajua na huenda huko
ukapata wapi helmani anapatika na nina uhakika
yeye kukukumbuka sio rahisi kwa kuwa umekuwa
sana na mpaka utakapo maliza masoma yako
utazidi kuwa mbaba na mimi nitakuwa nimepata
baadhi ya vitu katika uchunguzi wangu
umenielewa?’
David alionekana kufikiria swala hilo na kuona
limemuingia akilini na kuona kweli linaweza
kuwapa nafasi ya pakuanzia na urahisi wa kumjua
helman anapopatikana, hivyo david alikubaliana na
ushauri wa afande criss, na afande criss
alinyanyuka alipoketi na kumpiga kofi la pongezi
begani kwake kisha kuelekea chumbani kwake,,
Baada ya siku kadhaa kukatika afande criss kumbe
alifanya mawasiliano nchi moja ya jirani hapo
rwanda na nakupata chuo cha kibiashara ambacho
ndicho alichoprndrkrza david akasome na david
alikubali hilo na mipango ya safari ikawa
imeandaliwa na david akaelekea huko na atakaa
kwamuda wa miaka minne bila kurudi nchini
tanzania,,
Chuoni huko david alipokelewa vizuri na baadhi ya
wanafunzi wa kirwanda ambao kiswahili kwao
ilikuwa ni tatizo kidogo na gata kama
wakizungumza kuna utoauti na watanzania hivyo
wengi wao walipenda kuzungumza kingereza na
lugha ya kwako,
Maisha ya david yalianza kubadilika chuoni hapo
baada ya kumpata rafiki mmoja wa kiume alieitwa
gozbety lakini yeye alikuwa anapenda kujiita
gozbety CT 234 ambaye ni mwenyeji wa hapo hapo
rwanda, siku moja walipokuwa wanapata chakula
cha mchana katika mgahawa wa hapo chuoni
kwako na kupeleka kufikia katika mazungumzo
yaliomfanya david kushikilia kijijo cha chakula kwa
muda kidogo bila kukipeleka mdomoni Baada ya
kumuuliza,,,,,
“kwanini unajiita gozbety CT 234? Gozbety
alimwangalia david kwa makini sana kisha
kumueleza,
ITAENDELEA
 
SEHEMU YA KUMI NA NNE
Maisha ya david yalianza kubadilika chuoni hapo
baada ya kumpata rafiki mmoja wa kiume
alieitwa
gozbety lakini yeye alikuwa anapenda kujiita
gozbety CT 234 ambaye ni mwenyeji wa hapo
hapo
rwanda, siku moja walipokuwa wanapata chakula
cha mchana katika mgahawa wa hapo chuoni
kwako na kupeleka kufikia katika mazungumzo
yaliomfanya david kushikilia kijijo cha chakula
kwa
muda kidogo bila kukipeleka mdomoni Baada ya
kumuuliza,,,,,
“kwanini unajiita gozbety CT 234? Gozbety
alimwangalia david kwa makini sana kisha
kumueleza,
“david rafiki yangu jina hili lina silinzinto sana
ambayo inazidi kuniumiza na kunifanya kuwa
mkiwa kwa muda sasa na hapa nikimaliza
masomo yangu nitaelekea tanzania huko kuna
baba yangu mdogo ni tajiri sana na ana
makampuni yake ya kibiashara pia nitasikitika
kukuacha hapa chuoni rafiki yangu
nilitamanikama
wote tungekuwa tunamaliza mwakani lakini wewe
bado unamika miwili mbele lakini usijali ukifika
tanzania tutatafutana tu”
Maneno hayo yalikuwa yanaongelewa kwa lugha
ya kingereza na kuchanganya na kiswahili kidogo
yaliendelea kuwapotezea muda hapo mgahawani
lakini david alikuwa na shauku ya kutaka kujua
kwanini anajiita CT 234 ndipo alipo muuliza
tena,,,,
“gozbety hujaniambia kwa nini unanjiita jino hilo
bado na lina siri gani?
Gozbety alicheka na kumwambia mbona
unaonekana unashauku ya kutaka kujua sane
david?, usijali nitakwambia tu rafiki yangu japo
sijawahi kumwambia mtu yoyote yule kwenye
maisha yangu hata mpenzi wangu mwenyewe
hajui
ila“Ninachokuomba iwe siri yako maana kama
huyo baba yangu mdogo akijua kuwa
nimemueleza
mtu juu ya siri la jina hili anaweza kunifanya kitu
kibaya kwa kuwa si baba yangu mdogo wa
kuzaliwa na baba yangu hapana, ila nimetokea
kumuheshimu kutokana na baba yangu mzazi
kufanya kazi kwake kwa muda mrefu japo
mwanzoni sikujua kuwa wanafanya kazi gani
kutokana na umri wangu kuwa mdogo lakini
baada
ya kukua na kujitambua nilielezwa na watu kuwa
baba yangu alikuwa anafanya kazi ya ujambazi
na
akakamatwa huko tanzania,
“Lakini siwezi kuamini maneno ya watu sana na
kuacha kumuamini yule aliyekuwa karibu na baba
yangu na kufanyanae kazi kwa muda mrefu
maana
yeye alinimbia kuwa walikuwa wanafanya
biashara
yakuuza magari yaliokuwa yamesha tumika kwa
muda mchache na kuyauza kwa watu hivyo baba
yangu kazi yake ilikuwa ni kuyasambaza sehemu
mbalimbali,
“Siku moja baba yangu alipokuwa anajiandaa
kutaka kuyasafirisha magari bandalini ndipo polisi
wakazingira nyumba yake na kuingia ndani
kuanza
kukagua na hatimaye walikuta bunduki kama tano
hivi na risasi kazaa hicho ndicho kilicho
msababisha akamatwe, na nilipomuuliza baba
yangu huyo mdogo zile bunduki zilitoka wapi
aliniambia kuwa kuna rafiki yao mmoja ambaye
alikuwa nafanya kazi benki ndiye aliyetuma watu
kuzipeleka pale baada ya kushindwana bei katika
gari moja zuri aina ya masidinzi benzi na
kutoleana maneno ya kashfa mbele za watu hivyo
rafiki yao yule hakupenda kuzalilishwa mbele za
watu akaamua kumuabisha kwa aina hiyo ili baba
yangu aonekane jambazi
“na kuhusu jina hili la CT 234 nimeliweka kama
kumbukumbu ili hata watoto wangu watakapo
zaliwa waweze kukumbuka kwa urahisi maana
litakuwa linatamkwa na wengi bila ya watu hao
kujua lina maana gani, hii herufi C ni jina la baba
yangu mzazi lina maana ya Cholo na T ni
Tanzania na hiyo namba 234 ni namba ya usajiri
ya ufungwa wa baba yangu huko tanzania, hivyo
ndivyo nilivyo amua kuweka kwamfumo huo hata
watoto wangu wakiulizwa huko baadae
watasema”
babu yetu alikuwa anaitwa cholo alifungwa
tanzania kwa namba yake 234 hivyo ndivyo
nilivyo
amua kuweka”
“baba yangu aliweza kufungwa tanzania japo ni
raia wa rwanda ni kutokana na huyo baba yangu
mdogo kufanya mipango ya kumsajili kama raia
wa tanzania kwa kuhonga pesa haraka haraka ili
kesi isiwe kubwa na isiweze kumuingiza na yeye
kama jambazi kwa kumuajili raia wa rwanda bila
kibali chochote kile.
“Kiukweli rafiki yangu david inaniuma sana kila
nikikumbuka alichofanyiwa baba yangu na huyo
jamaa wao wa benki nilitamani kumjua japo jina
tu
lakini baba yangu mdogo hakuniambia kwa
wakati
huo alinificha kutokana na jazba niliyokuwa nayo
ambayo ingenipelekea kushindwa kusoma na
kudili
kumfanyia kitu kibaya jamaa huyo yeye na familia
yake maana imenifanya nimeishi maisha ya bila
baba kwa muda mrefu,,
Gozybety alipomaliza kueleza siri ya jina lake kwa
david alishangaa kumuona david jicho limemuiva
na kuwa jekundu mchozi mwembemba ukimtililika
huku misuli ya kwenye mikono yake ikiwa
imekaza
kama mtu anayejiandaa kupigana lakini alijitahidi
kujizui kuonesha fadhaa yake pale baada ya
kukumbuka maneno ya marehemu baba yake
yaliokuwa yanasema….
“utulivu wako ndio utakao kufanya ujue mengi na
kuzipata mali zako”
Japo alijitahidi kujizuia lakini jina la cholo ndilo
lilikuwa linaelea ndani ya kichwa chake maana
analijua vizuri ni mmoja wa watu walio panga
mpango wa baba yake kufungwa kwa mara ya
kwanza na ndio matatizo mengine yakaanza
kuongozana lakini alicho ambiwa na gozbety
kuhusu kufungwa kwa baba yake mzazi cholo,
anaona kinataka kumuangamiza yeye na wakati
waliofanya ubaya ni wao,
akafikiri kwa muda na kutaka kujua huyo baba
yake mdogo wa tanzania ni nani ili apate uhakika
juu ya cholo anayezungumziwa yule ambaye
alikuwa anashirikiana na adui yake mkubwa
helman ambaye amemfanya mpaka kupoteza
ndoto
zake za kuwa daktari na kusomea maswala ya
kibiashara ili ampate kwa urahisi au mwingine?
Alipokuwa anataka kumuuliza Gozbety jina la
baba
yake mdogo huyo wa tanzania walikatishwa na
mayowe yaliokuwa yanapigwa na wanafunzi hapo
chuoni wakilalamika kuwa bweni la wasichana
linawaka moto,
wote walikurupuka na kwenda kusaidia huko,
watu
walionekana kuchanganyikiwa,wengi walikimbia
mahali pasipo julikana wengine walikuwa
wanataja
majina ya watu waliokuwa wapo ndani ndipo
gozbety aliposikia jina la mpenzi wake ambaye
alikuwa anaitwa Segito kuwa yupo ndani na moto
unazidi kuongezeka,
Nguvu ya mapenzi ikamsukuma gozbety kukimbia
na kuingia mle ndani ya bweni ili ikiwezekana
amuokoe mpenzi wake lakini kwa bahati mbaya
alizidiwa na moshi mle ndani alipoteza maisha na
hiyo baada ya kuwa uchunguzi umefanyika na
kugundua kuwa katika watu sita walioaga dunia
na
ajali hiyo ya moto mmoja alikuwa ni mwanaume
aliye kwenda kuwasaidia ambaye alitambulika
kwa
jina la gozbety,
Kifo cha gozbety kilichukua sura mpya kwenye
moyo wa david maana alikuwa bado anahitaji
kujua mambo mengi sana kupitia yeye hasa
kutaka
kuhakikisha kuwa helman ndiye baba mdogo wa
gozbety?
Taratibu za mazishi zilifanyika kwa wanafunzi
waliopoteza maisha na ajali hiyo ya moto, wageni
wengi walihuzulia msiba huo akiwemo rais wa
nchi
hiyo paul kagame akiambatana na wanae, msiba
huo ulihuzunisha wengi sana maana ulikuwa ni
waghafla,
kwa kuwa ajali haina kinga basi ilibidi
wakubaliane
na tukio hilo la moto ambao chanzo chake
kilikuwa
ni shoti ya umeme,
siku zilikatika baada ya wanafunzi kupata
mapumziko mafupi ili ikiwezekana waweze
kupunguza mawazo ya tukio hilo lakini david
hakurudi tanzania alipata hifadhi kwa rafiki
mwingine ambae hawakuwa karibu sana ila
walifahamiana kutokana na kusoma kozi moja,
muda ukawa umewadia wa kurudi chuoni na
walikuta mambo yamebadilika kiasi fulani baada
ya yale majengo yalio kuwa yameungua
kurekebishwa na kupakwa rangi upya,wengi
walifurahi kukutana kwa mara nyingine na
kusimuliana mambo mengi ya mtaani kwao, hasa
yalikuwa maswala ya kimapenzi ndio yaliochukua
nafasi kubwa katika maongezi yao,
Lakini david muda mwingi alikuwa kimya sana na
nakujitenga na wenzie, hali hiyo kuna watu
walikuwa wanahisi analinga na kujisikia sana hata
wengine walidriki kusema ile sababu ambayo kila
mtu wa kutoka nchi nyingine anapokuwa kwenye
nchi ya wenyeji huonekana wa thamani sana
hivyo
utanzania wa david pia ulimuongezea umaharufu
chuoni hapo.
Madada wengi walimpenda kwa ukimya wake huo
na walitamani kuwa naye kwakuwa hawakuwahi
kusikia kuwa anamahusiano ya kimapenzi na
msichana yoyote yule chuoni hapo japo kwa uzuri
alionao na weusi wake ulio kuwa una waka waka
na kumeremeta, wapo waliojipeleka wenyewe
lakini
david aliwajibu kwa ustaarabu wa hali ya juu hata
kama walikataliwa lakini walijisikia fahari kukaa
nae,
Siku moja usiku david alikaa kwenye kitanda
chake
huku wengine wakiendelea na maongezi ya hapa
na pale, wenye kuongea na simu na wapenzi wao
waliongea na wenye kurudia kusimulia lile tukio la
moto lilivyotokea waliendelea kusikitika,
Utulivu wa david pale juu ya kitanda ulimfanya
kuanza kufikiria vitu vingi sana alimkumbuka sana
mdogo wake nisha hakujua kama yuko hai au
amekufa,alitamani kuwahi kurudi tanzania
iliakafanye harakati za kujaribu tena kumtafuta
maana alimtafuta mara ya kwanza bila mafanikio,
Lakini maneno aliyokuwa ameyazungumza
marehemu gozbety yalichukua utawala kwenye
kichwa chake aliyatafakari kwa kina sana na
kujiuliza maswali mengi ambayo alipata majibu
baada ya kuchekecha akili na kulinganisha
matukio
akajua kabisa kuwa huyu baba yake mdogo wa
marehemu gozbety ni helma tu hakuna mwingine,
Alijaribu kufikiria tena kwanini maelezo yake
gozbety yaonekane ni yakutaka kulipa kisasi kwa
familia yake akahisi kuwa ni dhahili helman
amenywesha sumu ya maneno ili apate usaidizi
wa kutaka kuendelea kuingamiza familia yake na
hapo aliapa kwa sasa yuko tayari kufa au
kufungwa, popote atakapo kutana na helman na
kumjua basi kitakachotokea hapo itakuwa habari
ya kusikitisha tanzania nzima na haitosahaulika
kamwe,
Mawazo hayo yalimsindikiza mpaka akapitiwa na
usingizi, alipoamka mida ile ya saa mbili asubuhi
akaangalia ratiba yake na kuona kuwa anakipindi
majira ya saa nne ndipo alipo jiandaa na
kuchukua
vifaa vyake na kuelekea kwenye darasa moja
ambalo lilikuwa halina mtu yoyote yule ili
akajisomee wakati anasubiria kipindi, ukimya wa
darasa lile ulimridhisha david na kwenda kukaa
kwenye kona kabisa ya darasa maana alikuwa
hapendi kelele wala kujichanganya na wenzie
kutokana na matatizo aliyo nayo hivyo aliogopa
siku moja asije akayasema mbele za watu na kila
mtu kujua kilichompata na kuwa mada chuoni
hapo,
Alipo kuwa akiendelea kujisomea ghafla alishtuka
alipohisi kama kuna mtu amepita kwa kasi nje,
alipepesa macho yake kutazama ni nani huyo
aliyepita lakini hakufanikiwa kumuona,ndipo
alpoendelea kujisomea,
Ndani ya muda huo mchache masikio ya david
yaliweza kusikia sauti nyembamba ya mtoto wa
kike ikitokea nje ya dirisha ambalo lilikuwa karibu
na yeye, sauti hiyo kwa mara ya kwanza iliweza
kumvutia david japo bado hajafanikiwa kumuona
kwa sura na kikubwa na kilichomshngaza ni
kusikia akilia kuyalalamikia mapenzi tena kwa
lugha ya kiswahili fasaha kabisa ambapo
hajawahi
kumsikia mtu yoyote yule akizungumza kiswahili
fasaha hata kama baadhi ya wa nyaruanda
wengine chuoni hapo walikuwa wanajaribu jaribu
ila kiswahili hicho kilikuwa ni tofauti kabisa hivyo
masikio yake akayatega kusikiliza maneno
haya,,,,,,,,
“hii ni sayari gani jaman kila siku watu wanalia
nimekosa nini mimi? Au sikustahili kuishi kwenye
sayari hii ya mapenzi mbona niliingia kwa furaha
na ninatoka kwa machozi,kumpenda kwangu
naonekana malaya leo,sioni faida ya kuishi ni
bora
kupoteza maisha kuliko kuishi kwenye sayari
isiyokuwa na upendo na mimi”
Maneno hayo dada huyo alikuwa akiyazungumza
huku machozi yakimtoka alijutia kupenda sana
mpaka kufikia kuchukua maamuzi ya kutaka
kujiua
na hilo ndilo swala david lililomfanya kunyanyuka
pale alipokuwa amekaa na kutoka nje kuifuta
sauti
ile nzuri iliyokuwa ina yalalamikia mapenzi kwa
lugha ya kiswahili,
Alipofika alimkuta msichana huyo amejiinamia
chini akizidi kulia kwa uchungu alisimama kwa
sekunde hivi akitafakari ataanza vipi
kumuongelesha yule mdada na yeye mazoea na
wasichana hana lakini alipo kuwa anajifikiria yule
dada pale chini alihiisi kuwa kunamtu kasimama
mbele yake, alipo nyakuwa kichwa chake na
kugundua kuwa yule mtu aliyesimama ni
mwanaume alimrukia na kuanza kumpigapiga na
mikono yake laini huku akimwambia,,,,
“ I hate boys just leave me alone please, I hate
you
go,”( tafadhali naomba uniache mwenyewe
nawachukia wavulana, nakuchukia nenda)
dada huyo alizidi kumpigampiga david huku
akirudia maneno hayo kwa lugha ya kingereza
bila
kujua anaye mwambia lugha hiyo naye anajua
kiswahili kama yeye alivyo kuwa ana lia kwa
lugha
ya kiswahili,
ITAENDELEA
 
SEHEMU YA KUMI NA TANO
“ I hate boys just leave me alone please, I hate
you
go,”( tafadhali naomba uniache mwenyewe
nawachukia wavulana, nakuchukia nenda)
dada huyo alizidi kumpigampiga david huku
akirudia maneno hayo kwa lugha ya kingereza
bila
kujua anaye mwambia lugha hiyo naye anajua
kiswahili kama yeye alivyo kuwa ana lia kwa
lugha
ya kiswahili,
David alikuwa akimtazama tu jinsi alivyokuwa
anampiga piga na kufikiri huenda yule dada naye
anamawazo kama yake kuwa hapo chuoni hakuna
mtu anayejua kiswahili kwa kutokana na wengi
wao walikuwa ni wanyaruanda na kutoka mataifa
mengine ambayo yanazungumza kiingereza, lakini
akajikaza na kumuuliza swali kwa kiswahili,,,,,
“Dada unamatatizo gani yanayokusumbua mpaka
unataka kujiua?
Ghafla tu yule dada alijikuta kaacha kumpiga na
kumsukuma david na kuanza kuduwaa kwa
alichokisika maskioni mwake kwa lugha ya
kiswahili ndipo na yeye alipomuuliza swali david
huku akitetemeka maana alihisi kama anaota
vile,,,,,,,
“we, we ni mtanzania??
David alitingisha kichwa kukubali kuwa ndio yeye
ni mtanzania, lakini kukubali kule kulimfanya
david
kuchanganyikiwa kwa muda ndipo alipo chukua
maamuzi ya kugeuka nyuma na kuondoka kwa
mwendo wa haraka kuelekea bwenini kwao,
alifika
na kujitupa kwenye kitanda hata dhana zake
alizobeba kwa ajili ya kujisomea aliziacha kule
kule
darasani,
Yule dada alibaki akijiuliza maswali na kuonesha
hali ya kutoamini kwa alicho kisikia na kukiona
mbele yake hivyo mawazo yale ya mapenzi
aliyokuwa nayo mwanzo na tukio hilo
lilimuongezea msongo wa mawazo kwa muda
huo
mchache, alidondoka palepale chini na kupoteza
fahamu, watu waliokuwa karibu na maeneo yale
walishtushwa na kile kishindo na kuanza kuelekea
kule sauti ya kishindo ilipotokea na kumuona yule
dada kadondoka chini na damu zikimtoka puani,
Walimbeba juujuu na kumuwaisha kwenye
zahanati
ya chuo hiko, wauguzi walimpokea kwa haraka
na
kumlaza kwenye kitanda kisha kumuongezea maji
ambayo yaliweza kusaidia kurudisha fahamu yake
kwa haraka zaidi,
marafiki zake hawakuwa mbali kutaka kujua hali
ya
rafiki yao inaendeleaje baada ya kupata taarifa
kwa wanafunzi walio mbeba hivyo wakawa
wanamfariji na kujaribu kumchekesha kwa vituko
vya hapa na pale ilimradi aweze kupoteza
mawazo
aliyo kuwa nayo maana walishajua kuwa huyu
atakuwa kapoteza fahamu baada ya kutendwa na
mpenzi wake aliyekuwa anaitwa Emmanuel
Regan,
Kichwa cha david kikawa kimeongeza wazo
lingine
la kuwaza, aliifikiria sana ile sauti ya yule dada
japo ilikuwa na majonzi lakini bado ilizidi kuvutia,
aliutafakari ule ufupi wake kiasi aliokuwa nao
ambao ulimfanya david kuachia tabasamu la
upendo hapo kitandani alipokuwa,
Alivuta picha na kujiuliza swali,vipi kama ataweza
kumkumbatia msichana huyo mwenye muanya
kwa
juu na aliye kata nywele zake kiasi ambazo
zilikuwa zina ng’aa kutokana na weusi wake
ambao ulizidi kufanya ile rangi yake ya usoni
inayotaka kufanana na maji ya kunde kuonekana
zaidi ni nini kitatokea?
jibu la kimahaba na bashasha likaja akilini mwake
na kujijibu
“ Ni dhahili ataweza kusikia mapigo ya moyo
wangu yanavyodunda kwa haraka zaidi kwa ajili
yake”
Mawazo hayo yalimfanya david kuchelewa kipindi
darasani, na siku hiyo ikawa imepote bule,
Siku iliyofuata yule dada akawa ameruhusiwa
kule
zahanati kwa kuwa tatizo lake halikuwa kubwa
sana na kikubwa alichoshauriwa ni kupunguza
mawazo,
David alionekana kwenye viunga vya maua chuoni
hapo akizunguka zunguka kujaribu kumtafuta yule
dada ambaye hakujua atampata vipi maana
hakuwa na chochote ambacho kingeweza
kumrahisishia kumpata kama vile jina hata
mchepuo aliokuwa anasoma,
Wahenga walisema mola hamtupi mja wake
usemi
huo uliweza kumsaidia david,baada ya kumtafuta
dada huyo kwa muda mrefu bila mafanikio
akaamua kutaka kujirejesha bwenini kupumzika
alipokuwa anataka kuchukua njia ambayo itamtoa
mazingira yale ya chuoni na kumfikisha bwenini
alimuona yule dada akiwa wanabadirishana
namba
simu na msichana mwenzie ili amuelezee jinsi
mpenzi wake Emmanuely regan alivyo mtenda,
david hakuremba alijibanza kwenye mti uliokuwa
karibu na kumvizia yule dada amtajie mwenzie
namba zake,
Yule dada alipokuwa anazitaja namba zake
ambazo ni +250768000092, masikio ya david
yakayapa ushirikiano mzuri vinganja vyake na
kuanza kuziandika kwenye simu yake, basi wale
madada walipomaliza kubadirishana namba kila
mmoja akachukua njia yake bila kujua kama kuna
mtu ambaye alikuwa amejificha jirani yao,
Tukio hilo lilizidi kumuongezea david furaha na
kutaka kusahau kama anamatatizo makubwa, ali
zihifadhi namba kwenye simu yake na kuipa jina
la
Qeen tz, maana alikuwa hamjui jina lake,
Shughuli za masomo ziliendelea kwa furaha siku
hiyo kwa david na alitamani usiku ufike haraka ili
aweze kujaribu bahati yake kwakuwa huyo dada
alikuwa katoka kwenye maumivu siku mbili
nyuma
hivyo alihisi lazima kutakuwa na ugumu wa hali
ya
juu,
Ombi lake lilifanikiwa jua lilielekea magharibi na
sauti za mbu zikawa zinamsumbua david wakati
akiweka chandalua chake vizuri, kisha kuchukua
mto na kuegesha kichwa chake kwa juu na
kuanza
kubonyeza vitufe kulitafuta jina la Qeen tz,
alipolipata akabonyeza kitufe cha kijani ambacho
kina ruhusu simu kutoka au kupokea wakati
ikiingia na baada ya kuweka skioni kuzikiliza
kama
inaita alijibiwa,,
“simu unayopiga kwa sasa inatumika jaribu tena
baadae”
ujumbe huo ulibadilisha sura ya david na furaha
yake kutaka kupotea, alijaribu zaidi ya mara nne
lakini jibu likawa ni lilelile mpaka alipokata tamaa
na kunza kusinzia ghafla alishtushwa na wimbo
mfupi ulikowa unaashiria kuwa kuna ujumbe
umeingia ambao na kuaza kujibizana lakini lugha
iliyokuwa inatumia hapo ni kiingereza,
“mambo? Ndio ujumbe ulio ingia kwenye simu ya
david na akanza kuuijibu,
“poa”
“Sijui mwenzangu nani maana hii namba in ngeni
kwangu” yule dada aliuliza
“mimi ni mtu mwenye pendo wa kweli ninaye toka
kwenye sayari ya kufuta mchozi na kuwa patia
furaha wenye majonzi kama wewe” alionge david
“Mmh wewe mbona unanichanganya na majibu
yako namba yangu amekupa nani kwanza?
Aliuliza
yule dada
“Kuna ubaya nikiwa nayo” david naye alimuuliza
swali
“Hapana ila lazima tujuane kwanza na najue
namba yangu umepata wapi kama hivyo siwezi
kukaa na namba mpya kwenye simu bila kuijua
sawa eeh” yule dada alivyojibu tu ule ujumbe
ilionekana wazi amekasirika ndipo david alimpo
mjibu,,,
“sikuzote hakuna upendo wa zamani kwa
mwanamke unaye mpenda jinsi namba yangu
ilivyokuwa mpya kwako ndivyo mimi nitakavyo
kuwa mpya ndani ya moyo wako kama utaruhusu
kupokea pendo langu kama unavyo pokea ujumbe
wangu”
david aliona bora afunguke kwa staili ya
kumuweka
kwenye mabano yule dada wa katanzania,
na kweli yule dada alizidi kuchanganyikiwa
maana
majibu aliyokuwa anayapokea kwa david
hakuwahi
kuyasikia kwa mwanauume yoyote yule ndipo
alipomuomba kesho asubuhi waonane kwenye
kiunga kimoja cha maua kilicho karibu na jengo
kuu la ofisi za chuo hiko david alikubali lakini
akamuuliza tena swali yule dada,,
“unaitwa nani lakini maana jina lako limejificha
ndani ya moyo wangu na alitaki kutoka kwa kuwa
onaonekana umechukia na macho yangu
yanausumbu moyo kutaka kuona jina lako kwa
mara nyingie huenda nilikuwa na kosea hata
katika
kuliandika katika kitabu changu cha matukio
ambapo jina lako ndilo lililofungua ukurasa wa
kwanza wakitabu hicho ila hata kama nilikuwa
nakosea lakini jina lako ni zuri sana tafadhali
naomba unitumie jina lako iliniliandike vizuri
kwenye kitabu changu”
David aliona yule dada kasha chukia na
maaongezi
yalikuwa yanakaribia kuisha kwa muda ule na jina
alikuwa bado halijui ndipo alipoamua kutumia
ujanja huo kana kwamba alikuwa analifahamu
tangu zamani ila alikuwa analikosea katika
kuliandika,
Ndege mjanja huna kwenye tundu bovu yule dada
akaingilia kwenye mtego huo na akatuma jina
lake
akihisi tayari lina fahamika kwa mtu anaye
jibizana
nae akasema,,
“Jina langu linaandikwa hivi Victoria”
David baada ya ujumbe huo aliokuwa anausubiria
kwa hamu kuingia na kuusoma alifurahi sana
mpaka wenzie mle ndani wakawa wanashangaa
huyu jamaa siku zote huwa kimya vipi leo mbona
amekuwa na furaha ya ajabu sane lakini david
aliendelea kugeuka geuka na kuliangalia lile jina
mara kwa mara kisha kujifunika shuka ili apate
usingizi mapema kesho iwahi kufika------- Miale
ya jua iliyo kuwa inapenya dirishani iliweza
kumfanya david afunue shuka na kuchungulia nje
na kuona wanafunzi wenzie wakiendelea na usafi
wa nguo zao siku hiyo ya jumamosi ambayo
wengi
walikuwa hawana vipindi japo wachache walikuwa
navyo,
Alifumba macho yake na kuanza kusali
kumshukuru mungu wake kwa kumuamsha
salama
kisha kunyanyuka kitandani na kutandika vizuri
na
safari ya kuelekea bafuni ikafuata,
Ndani ya muda mchache akawa kasha maliza
kujianda na kuelekea kwenye mgahawa wa chuo
kujipatia kifungua kinywa,
marashi aliyo yapaka david yalikuwa na harufu
nzuri sana yalionekana kama yanaendana na
nguo
zake alizovaa asubuhi hiyo,ilikuwa ni pensi
nyeupe
na singrendi nyeupe yenye picha kubwa yakuvutia
na zile sendro zake nyeupe,
Wengi alio pishana nao waligeuka kumtazama
kwa
muonekano mzuri aliokuwa nao david, acha
baadhi
ya wavulana wenzie waliokuwa wanamsimamisha
kuulizia jina la marashi aliyo yapaka maana
yalionekana kuwavutia sana,
Alifika mgahawani hapo na kuagiza vitafunwa
pamoja na chai ya maziwa akajipatia na kushiba
vizuri kisha kuondoka, kurudi bwenini, kila alipo
pita au kukaa mahali popote pale basi akiondoka
ni lazima aache mada kwa watu,
walimzungumzia kwa mengi mazuri na mabaya,
japo sifa nyingi nzuri alikuwa anazipata kutoka
kwa wasichana, wavulana wengi walikuwa
wanamchukia kutokana na baadhi ya wasichana
waliokuwa wanatongozwa wengi wao walikuwa
wana sema kuwa wanawachumba tayari
naukiwauliza walikuwa wana mtaja david hivyo
kitendo hicho kilikuwa kina wakera sana,
david alifika kitandani kwake na kuchukua simu
yake ambayo alisahau kutoka nayo, alipoiangalia
akakuta ujumbe mpya kutoka kwa victoria
uliomuomba ifikapo saa saba mchana wakutane
kwenye mgahawa wa chuo kupata chakula cha
mchana na waweze kufahamiana kwa sura
maana
victoria alikuwa hajui kama anayetaka kuonana
naye walisha wahi kukutana na akazimia kwa
kutoamini kumsikia mtu akizungumza kiswahili
chuoni hapo,
******************************
Kila mmoja wao alionekana kuwa na shauku ya
kutaka kuonana na mwenzie japo victoria alikuwa
katoka kuumizwa lakini alivutika na maneno
aliyokuwa anatumiwa na david kwenye simu,
Muda uliobaki kabla ya kukutana waliweza
kuutumia kufanya shughuli zao za hapa na pale
mpaka kijua kilipokuwa kikali na kukili kuwa sasa
ni muda muafaka wa kwenda kukutana,
David alijipigilia jinsi nyeusi na tisheti jeupe
ambalo halikuwa na doa hata ya andishi moja na
chini kuvaa kiatu ambacho kiliendana na rangi ya
tisheti lake,
weusi wake mzuri wenye kuwaka waka ulizidi
kuonekana kutokana na nguo ile nyeupe
aliyokuwa
amevaa, alipojihakikishia kuwa yuko sawa na
hana
tatizo lolote lile basi hakuwa na budi kuanza
safari
yake ya kuelekea kuonana na mtoto mzuri victori,
Moyo ulikuwa una mdunda david maana hajawahi
kuongea na mwanamke ana kwa ana kuhusiana
na
mapenzi hivyo alihisi atakuwa na wakati mgumu
sana siku hiyo,
Alipokuwa anaukaribia mlango wa kuingia ndani
ya
mgahawa huo alisikia sauti ambayo ndiyo
ilimfanya mapaka kuchukua maamuzi ya kutoa
hisia zake za moyoni, ikizungumza na simu
Alipogeuka nyuma waligongana macho kwa
macho,
victoria alidosha pochi yake chini kwa mshtuko
na
david ilibidi azuge kama ndio alikuwa anatoka mle
ndani ya mgahawa hivyo alimpita na kurudi alipo
tokea,
victoria aligeuza shingo yake kumtazama david
ambaye alikuwa anaishia basi akabaki kuvuta
pumzi ndefu ambayo ile harufu ya marashi
aliyopaka david kuingia kwa wingi puani mwake,
Akili ile ya mahaba ilipomtoka victoria alishtuka
kuona baadhi ya watu wakimtazama na wengine
kucheka kwa kitendo alichokuwa anakifanya,
aliinama na kuokota pochi yake kisha kuingia mle
mgahawani huku akiwa anahema kwa haraka,
aliketi kwa muda kumsubiri mtu aliyekuwa na
ahadi naye bila kujua mtu mwenye ndiyo david
aliye pishana nae,aliendelea kusubiri lakini bila
mafanikio,maana david hakurudi tena muda huo,
Hivyo victoria naye ikabidi aondoke kwa hasira
kwa kufanywa kama mtoto mdogo mgahawi
pale,lakini furaha ilikuwa inakuja kila alipokuwa
anakumbuka jinsi david alivyompita na kuacha
harufu nzuri ya marashi,
********************
Siku kama hiyo ya jumamosi chuoni hapo kuna
kuwa na disko ndani ya ukumbi wa chuo na
baadhi
ya wanafunzi huwa wanachaguliwa kucheza
nyimbo za aina mbalimbali ilikuonesha uwezo
wao
na vipaji vyao,
Rafiki zake na victoria waliweza kugundua kuwa
victoria ameanza kumpenda david hivyo walianda
mpango na kuongea na wanachumba wenzie na
david kuwa itakapofika muda wa kucheza basi
david acheze na victoria na wengine waliobaki
watacheza na wao,
ITAENDELEA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom