Mchumba
JF-Expert Member
- Jul 27, 2012
- 280
- 262
SEHEMU YA KWANZA
Roletha, mtoto mdogo sana wa miaka 7 anayeishi na baba yake tu ambaye ni mgonjwa mahututi wa kansa ya utumbo mwembamba, anapitia machungu mazito ya maisha katika umri wake huu, machungu ambayo hata mtu mzima hawezi kuyahimili.
Pamoja na kuwa mama yake mzazi yupo hai na ni mzima wa afya, Roletha anageuka kuwa ndiye mama na mlezi wa baba yake ambaye kutwa anashinda kitandani kuuguza ugonjwa wake.
Kutokana na ugumu wa maisha na mabalaa mengine, anajikuta anakosa fursa ya kwenda shule , pamoja na kukosa fursa hiyo lakini anakuwa na uwezo wa kusoma, kuandika pamoja na uelewa mzuri wa hesabu.
Fuatilia Riwaya hii ya kusisimua ya maisha ya mtoto huyu.
==============================================
“sasa baba kwanini usiende Hospital ?” lilikuwa ni swali la Roletha kwa baba yake ambaye alikuwa hoi kitandani kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa kansa ya utumbo mwembamba.
“mwanangu Hospitali nimekwenda mara nyingi sana, sitakiwi mimi inatakiwa fedha !” baba yake na Roletha alitoa jibu hilo kwa mwanaye huku akihangaika kujigeuza pale alipokuwa amelala.
“duh hivi madaktari ni wachache hospitalini baba ! hatuwezi kumpata ambaye siku hiyo atakuwa hana kazi tumuombe akutibu ?” Roletha aliendelea kumuhoji baba yake huku akijisikia huruma sana kwa jinsi alivyokuwa amedhoofu.
“walaaa wakati wewe unawaza kumpata daktari mmoja, kuna wagonjwa wengine kama mimi wamezungukwa na madaktari zaidi ya saba mwanangu !” Roletha kila mara alipokuwa akisikia majibu hayo kutoka kwa baba yake alizidi kujisikia uchungu sana moyoni mwake.
“sasa baba mwisho utakuwa ni upi, kama hali yenyewe ndio hii ?” Roletha alihoji huku akijikaza asitoe machozi mbele ya baba yake.
“hahaha mwanangu ! ndio unataka hadi kulia, ntapona tuu ! mbona we ukiumwa kichwa au tumbo huwa unapona mwenyewe, kwanini nisiwe mimi mwanangu ?” baba yake alijaribu kumfariji mwanae kwa kumuongopea kwamba ugonjwa wake ni wakawaida tu kama yalivyo magonjwa mengine, wakati siku zote alikuwa akijua yupo kitandani akisubiri muujiza wa Mungu au kifo chake tu.
“haya baba mimi nakupenda sana, basi tulale !” baada ya jibu hilo Roletha alimuomba baba yake walale kwa kuwa giza, usiku ulikuwa ushatamalaki, na bila kinyongo baba yake alikubaliana na mwanaye.
Roletha na baba yake walikuwa wakilala katika chumba kimoja, hii ilitokana na umasikini mkubwa waliokuwa nao, kwani hata nyumba waliyokuwa wakiishi ilikuwa na vyumba viwili tuu, yaani sebule ambayo ilikuwa haina kitu na zaidi ikifanyika kama jiko na chumba hicho walichokuwa wakilala, nyumba yenyewe hiyo ilikuwa ni hisani tu ambayo baba yake na Roletha alipewa na boss wake kajieneo wakati hali yake ya ugonjwa ikianza kumvaa.
Sababu ya kupewa ilikuwa ni kwamba mwenye eneo hilo aliamua kuuza eneo lake hivyo alijikuta akishikwa na imani na kuamua sehemu ndogo ya eneo hilo kumuachia ndugu huyo na hayo ni baada ya kufanya kazi ya ulinzi kwake kwa muda mrefu.
Kila mara ulipofika usiku wa manane baba yake na Roletha alikuwa akishtuka usingizini na kulia sana huku akimtizama mwanaye, swali kubwa lililokuwa likimtesa kichwani mwake ni, ni nini hatima ya mwanaye baada ya kifo chake ?
Aliamini kwa ugonjwa aliokuwa nao ni lazima tuu atakufa, ikiwa wenye fedha wanashindwa kumudu vipi yeye masikini tena na hospitali washamwambia amechelewa !
Wakati huo akikumbwa na hali hiyo pia mwanaye alipokuwa akishituka naye alijikuta akiikumbwa na hali hiyo hiyo huku akijutia, umasikini na hali ya baba yake, na kila mtu alikuwa akijitahidi kujificha ili tuu kutokumfadhaisha mwenzie.
Roletha pamoja na utoto wake alikuwa ashazoea kukaa njaa na siku akishiba basi chakula ni uji kama si uji basi watashindia chai na siku kitu hali ikiwa njema basi chakula kizuri ni ugali na dagaa wa uswahilini ambao washakaangwa ili kusevu matumizi mengine ya kupika.
Shughuli kuu aliyokuwa akiifanya Roletha ni kuomba omba ndipo aendeshe maisha yake na ya baba yake, pamoja na yote hayo Roletha na baba yake walikuwa wametengwa na majirani kama ujuavyo masikini hana rafiki.
Na sababu ya kutengwa ilikuwa ni familia ambayo haishiriki shughuli za kijamii, kama misiba, harusi nk.
Japokuwa sababu ilikuwa ni ufukara uliokubuhu lakini watu hawakuwaelewa na kuwashutumu kwamba ni watu ambao hawatoi hata michango ya misiba wakati wao wanaishi, lakini si hivyo tuu majibu ya Roletha pia watu wengi walikuwa hawapendezwi nayo, hakuwa na jeuri bali alikuwa ni mtoto ambaye ana uwezo wa kujenga hoja kiasi kwamba hata mtu mzima ukajikuta unabaki mdomo wazi.
Laiti angekuwa ni mtoto wa tajiri basi angeonekana kama ana akili sana ila kwa kuwa ni mtoto wa fukara alionekana ni mtoto jeuri na mwenye kiburi.
Tatizo kubwa la Roletha lilikua anazijua haki zake lakini ukweli ni kwamba Roletha alikuwa na heshima pia alikuwa ni mtoto ambaye hawezi kutukana hata kwa kusema mjinga.
Baba yake ilikuwa ni kila siku ambayo anaachiwa uhai alikuwa akiitumia kumfundisha mwanaye kujiamini, kuelewa, kujihami, kujali na kuilewa dunia na mambo yake yote, masomo hayo japo yalikuwa ni zaidi ya umri wa Roletha lakini yalikuwa ni zaidi ya masomo ya elimu ya kawaida.
Roletha pia alikuwa na kichwa kizuri kunasa mambo, alikuwa na uwezo akasikia kitu na akakirudia kukisema kama kilivyo bila ya kuacha hata neno moja.
Huyo ndio Roletha mtoto mzuri kuanzia sura, fikra na muonekano tatizo lake ni moja tuu anaishi katika maisha ambayo ni magumu pasina mfano.
Watoto wa mtaani kwao walizoea kumuita "ombaomba ombaomba hilo!", lakini kila walipomuita hivyo wala hakujisikia vibaya zaidi ya kucheka tu huku akiwajibu majibu ambayo wenzie hao walikuwa wanashindwa kuelewa kutokana akili zao kuwa changa,
“hamjawahi kuomba, sijawahi kwenda shule nani ana faida ikiwa hamjui hata kuumba silabi” mara zote Roletha alikuwa ajibu hivyo bila kujali makelele ya kuzomewa na watoto wa mtaani, pamoja na hayo hakupenda jambo hilo amueleze baba yake kwa kuwa alijua akimwambia litamfanya azidi kujisikia hovyo zaidi kwa yale ambayo mwanaye anakumbana nayo atokapo nyumbani.
Hatimaye kama utaratibu wa siku ulivyo giza lilikuwa linatokomea na mapambazuko ndio yakawa yanaanza, Roletha akiwa bado katika usingizi mzito, baba yake alikuwa akifungua macho huku akimshukuru Mungu kwa kumuamsha salama kwani kila mara alipokuwa akilala hofu yake ilikuwa ni kama ataiona kweli siku inayofuata.
“Roletha…… Roletha…. Roletha amka mwanangu ?” baba alikuwa akimuamsha mwanaye kwakuwa kulikuwa kumekucha.
“mmmmh !” Roletha alikuwa akiamka huku akijinyosha kutokana na uchovu wa usiku kucha.
Baada ya kuamka kama ilivyokuwa kawaida yake baada ya kuosha uso wake, alichukua kiporo chake cha uji na kunywa kisha safari ya kuelekea katikati ya mji ikawa inaanzia hapo kwani huko ndiko alikokuwa akikutumia kama ofisi yake kwa ajili ya kuomba.
“badae baba ! uji wako nimekuachia mi naenda !” Roletha kila asubuhi alikuwa akitumia lugha hiyo kwa baba yake utafikili anakwenda kazini vile, huku baba yake kila akisikia kauli hiyo moyo wake ukimuuma sana na akijisikia hata shida kujibu kauli ile ya mwanaye.
“Mungu akulinde mwanangu, usichelewe kurudi ikifika saa tisa na nusu anza kurudi, pia kuwa makini na pikipiki sawa” Roletha alikuwa ni msikivu sana pia alikuwa na uwezo hata wa kumsoma mtu kwa muonekano wake na kuweza kutambua nini kinachomsibu.
“niko makini baba ! usiumie sana haya yataisha siku moja” ndio lilikuwa jibu la mtoto huyo kisha akafungua mlango na safari ikaanzia hapo.
Hiyo ndio ilikuwa ratiba ya kila siku ya mtoto huyo, akiwa na safari hiyo alikuwa akikutana na makundi ya watoto wenzie wengi wakielekea shule, na hapo ndipo alipokuwa akikutana na kadhia ya kukashifiwa pia kutukanwa.
“ahaa ombaomba !” ilikuwa ni sauti ya mtoto mmoja katika ya kundi akiwa anaelekea shule.
“unapenda ehee twende tukaombe wote basi” Roletha alijibu huku akitabasamu na kumtizama mtoto mwenzie huyo.
“we kijinga nini ! nani akaombe, ntakuzaba !” mtoto huyo alikuwa akiongea huku akimsogelea Roletha.
“basi nisamehe kaka !” Roletha alijaribu kujitetea kwa kuwa alijua mwenzie tayari amekasirika.
“nani kaka ako nani !” Roletha kabla hajajibu lolote mkono wa mtoto yule ulikuwa ushatua shavuni kwake, kiasi kwamba alijikuta akiona nyota maana mtoto yule alikuwa amemzidi sana kimuonekano alikuwa ni kama mtoto wa darasa la nne hivi.
“ubabe na shule wala haviendani, nenda kawaulize waliomaliza wababe wao wa enzi hizo walipo !” Roletha alitoa kauli hiyo kisha akaendelea na safari yake huku machozi yakiwa yamemlenga na hasira ikiwa imemkaba na kujaza kifua, hata hivyo mtoto yule hakutosheka alichokifanya ni kumuongeza kumpiga mtama mmoja na Roletha alipoinuka alimsindikiza na kibao, mtoto wa watu wala hakujibu kitu zaidi ya kuendelea na safari yake tuu huku moyoni akitamka maneno ambayo yalikuwa ni kama laana kwa mtoto yule aliyekuwa akimpiga.
“Eeehe Mungu kama kweli upo na umtizame huyu hapa hapa duniani kabla ya siku ya mwisho” Roletha alikuwa akiwaza hayo huku akijifuta chozi ambalo alishindwa kustahimili kulivumilia.
Njia nzima mtoto Roletha hakuwa mwenye furaha zaidi ya kutembea akiwa na masononeko pamoja huzuni, na alikuwa akitembea umbali mrefu sana kwani nyumba yao ilikuwa nje ya mji na sehemu aliyokuwa akitakiwa kufika kila siku ni katikati ya mji ambapo ilikuwa ni zaidi ya kilometa 8.
Tofauti na watu wengine walivyokuwa wakifikiri kwamba mtoto huyo alikuwa akikaa chini na kuomba au kuvizia magari na kuomba, haikuwa hivyo Roletha alikuwa akikusanya watu na kuanza kufanya mambo ambayo watu walikuwa wakistaajabu na wakati wakimshangaa alikuwa anaweka kopo lake na kutaka asaidiwe.
Kwa mfano watu walikuwa wakistaajabu kuona mtoto mdogo akijieleza kuwa ana uwezo wa kusoma, na kweli wakiandika kitu alikuwa anasoma tena bila ya kutetereka, si hivyo tuu Roletha alikuwa akiwashangaza watu pia alipokuwa akijipambanua kwamba ana uwezo hata wa kuimba tebo, na watu walikuwa wakifikili labda kama kanatania hivi ! walipojaribu kuchagua tebo ambazo ni ngumu kwa rika lake kama tebo ya tisa mtoto alikuwa anaimba tu huku watu wakipiga makofi utafikili wanasikiliza hutuba ya mwanasiasa.
Lakini siku ambazo mambo kama hayo hayakujipa ilikuwa inambidi aingie naye tu mtaani kuomba kama watoto wengine, na huko ndiko alikokuwa akizidi kuumia sana na kuhisi watoto wenzie wote nao wana shida zinazowakabili kama yeye.
Ilipokuwa imefika mida ya saa tisa Roletha kama kawaida yake ilikuwa ni muda wa kurudi nyumbani, na wakati huo alianzisha safari yake kama kawaida japokuwa alikuwa na fedha hakufikilia kupanda gari kwa kuwa alijua hata fedha aliyonayo haimtoshi kabisa.
Alipokuwa amekaribia mitaa ya nyumbani kwao alipitia dukani na kununu unga, na baada ya hapo alipita sehemu akanunua mkaa kisha safari ya kuelekea nyumbani kwao ikawa imepamba moto huku akifurahi kweli kwamba anakwenda kukutana tena na baba yake !
Ghafla furaha yake ilingia dosari baada ya kukutana tena na mtoto yule yule ambaye asubuhi ya siku hiyo alimpa kipigo, hakuogopa alichokifanya ni kuongoza mbele tuu huku mtoto yule akimzuia kwa mbele kama anataka kumfanyia ukorofi vile, na kweli ndio ilikuwa nia yake alipofika jilani tuu alianza kumzingira kama mtu anayemzuia kupita hivi ?
Roletha wala hakusema kitu zaidi zaidi ya kuhama pande na mtoto yule akizidi kumzingira tu, baada ya kuhangaishana kwa muda mrefu mtoto wa watu masikini alijitahidi kutumia nguvu ili kupenya lakini hakuweza kufanikiwa kwa kuwa mkubwa wake alikuwa na nguvu zaidi, katika purukushani za hapa na pale mwishoe unga aliokuwa ameshika mtoto yule ulimwagika wote baada ya mfuko aliobebea kupasuka.
Roletha alijikuta akishikwa na hasira na alimtizama mtoto yule takribani kwa dakika mbili na baada ya hapo alimng’ata mtoto Yule kwa nguvu sana huku akikaza sawasawa meno yake bila kujali kipigo alichokuwa anapokea huku mgongoni, na vile tumeno twake tulivyokuwa tumechongoka mtoto aliyekuwa ameumwa alipiga kelele sana ! kiasi kwamba mpaka mama yake anafika pale tayari damu zilikuwa zikimvuja mwanaye.
Mama yule kuona tuu mwanaye yuko vile wala hakutaka kuuliza alichokifanya ni kumkamata mtoto wa watu na kuanza kumtandika makofi, huku akimuagiza mwanaye akalete kiboko, Roletha kuwa ombaomba ilikuwa akihesabika kama mtoto mtukutu sana, mpaka kiboko kinafika pale Roletha alikuwa kimyaa wala hakuwa na la kusema lolote na mama yule alianza kumshushia viboko mfululizo utafikiri anapiga paka mwizi vile.
Roletha alikuwa na uchungu sana alimatamani alie kwa sauti ili naye baba yake asikie aje kumnasua pale ! lakini baba yake ndio huyo hata akiamka anaweza tumia nusu saa kufika pale, mama yule alipohakikisha fimbo ile imepasuka pasuka kidogo ndio moyo wake ukaridhika na kumuachia Roletha, hata hivyo mtoto wa watu hakuhangaika kukimbia zaidi zaidi alipoachwa ndio kwanza alianza kujiokotea mkaa wake ili tuu ukawasitili na baba yake, huku kila bonge aliloinua juu akililipa kwa chozi lake lililokuwa likidondoka chini na baada ya hapo safari ya kuelekea nyumbani ikaanza huku Roletha akiongea peke yake kwa jinsi alivyokuwa amechanganyikiwa na kipigo kile.
“Hivi kweli ameshindwa hata kuona unga uliotapakaa mahali pale ! basi sawa nimekosea mimi ! lakini ananipigaje vile kweli ameshindwa hata kunitizama kwa umri !” Roletha alikuwa akiongea peke yake huku akivuja machozi tuu katika mashavu yake na akielekea nyumbani kwao.
Itaendelea.....