Riwaya: Dunia Tambara Bovu

Riwaya: Dunia Tambara Bovu

Hyungnim

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2016
Posts
301
Reaction score
484
*JINA LA RIWAYA: DUNIA TAMBARA BOVU*

*MWANDISHI: (HYUNGNIM)*

Ulikuwa usiku adhimu kupata kutokea kwa mabanati na majamali ya nguvu.Jiji la Bujumbura lilitoa mng'aro uliopambizwa na taa kubwa zikizonasa ktk majengo mazuri ajabu na kufanya nakshi Fulani hivi ya kuvutia.

Nyakati hizi za saa sita usiku kuelekea saa saba ni kama Bujumbura ilikuwa inakucha!shamrashamra,pilikapilika na mishemishe za kila aina zilipeta!ulikuwa usiku jina na sio kwa uhalisia.Baada ya mihangaiko ya kutwa kujipatia kipato wengi walijitoma ndani ya kumbi za starehe kupoza koo na kupata burudani ya warembo wa mji!sina hakika kama na wasichana na mabinti wengine wajuvi wa mji walienda kuzipoza hisia kali za huba au kujipatia faranga kwa 'wanaume wakarimu'.
Miaka hii ya 1982 hali ya uchumi haikuwa imara ktk mataifa mengi ya kiafrika.Biashara haramu za ngono zilifanyika!kete za bangi,mirungi na heroine zilikuwa bidhaa muhimu sokoni.ulanguzi ulikithiri na hivyo biashara za magendo zikashika hatamu lakini jambo la kutia huzuni ni kuwa wengi wa waliopata faida kupitia deal hizo hawakukumbuka kulipa kodi!wakajineemesha wenyewe na kuipa serikali kisogo...jamani Bujumbura...
Mjomba Ufuta Hajiwa mnyakyusa kutoka Mbeya naye alijitoma ktk klabu mojawapo ya usiku.Kwa taaluma alikuwa kachero,sijui nini kilimtoa Dares salaam na kumsokomeza Bujumbura!
Akiwa ndani ya suruali njiwa iliyopambizwa na shati pana la mikono mifupi aliingia ukumbini kwa mwendo wa kijamaa hivi ishara ya mtu wa shamba.Alisogea karibu na jukwaa na kuchagua kiti kimojawapo kisha akaketi.Akayaelekeza macho jukwaani kupata burudani ya wanenguaji wa kike.
pumzi zikaanza kumkosea adabu na kutosikilizana.Macho yake yalitua kwa mnenguaji wa kurundi aloitwa chelina mahewa.Chelina alijinyonganyonga na kuupindapinda mgongo kwa hali ya ulegevu huku macho kayaelekeza kwa kachero Ufuta Hajiwa.Kachero wa watu akazidi kuchachawa.Akajaribu kupoteza fikra ovu kwa kuangalia pembeni lakini tamaa haikumuacha.moyo ukataka kuendelea kukodolea maungo mwanana ya chelina.
Hakika kachero huyu alipatikana kwani sasa akaanza kushuhudia eneo la kifuani kwa mrembo chelina likichezacheza.Naam kifua ambacho kifungamanishwa na maembe madogo mawili mabivu tena mororo lakink yalofichwa ndani ya kitambaa kidogo laini.
'Kachero' akang'ata meno na kuyakereza huku akitoa sauti fulani zisizo dhahiri alilalama ' aiiii naaam kenn taya' mawazoni mwake akalaumu uchoyo wa chelina.kwanini asitupilie mbali kile kitambaa kilichotupiwa kifuani?hakika shetani alikuwa kibaruani.Maungo yakamchemka,jasho likamchuruzika na kutoa harufu kali na ya kuudhi, tena akahamanika.Akili ikapotoka na taratibu akakwea ngazi ili akamvae Chelina huku shati kalichomoa toka kwenye suruali asijeumbuka kwani maungi hayakusikilizana.
wakati hayo yakiendelea ukumbini humo binti mmoja wa kirundi alijongea kumfuata mzee mmoja aloitwa Vugwa.Baada ya ugumu wa kazi ya kuendesha tekisi(teksi) anaamua kuburudika nyumbani kamuacha mkewe mama franko.Binti anamkalia mzee huyu mapajani,zee la watu linaguna na kugumia kwa maraha.binti anambusu mfululizo kisha anamwambia ninunulie fanta,mzee anakataa huku akidai hali ya maisha haijatengamaa.Mabishano yanaibuka binti akilaumu ubanizi wa mzee huyo kwani fanta iligharimu shilingi nane tu.Anamlazimisha basi amlipe fedha kichele kwa huduma maridhawa ya kumbusu alompatia.Mzee Vugwa anakataa huku akidai huo ni unyonyaji wa kibepari huku akidai yeye ni mjamaa.
Zogo linaibuka kati ya binti huyo na mzee huyo.watu wanasogelea na kuliacha jukwaa likiwa na chelina na kachero.
ghafla taa zinazimwa na milipuko ya risasi inasikika.....
 
poa shunie ngoja niweke sawa mambo
 
Kwa hiyo unasubiria Episode 15 ambaye ilikuwa itoke ijumaa?
mm nipo whatsap kwenye group nilijua unaniuliza hela ya mwezi huu tupo episode ishirini na kitu
 
Hii Riwaya nouma!

Yaani episode one tuu inaanza na mambo ya valentine..

Ikifika episode ya 10 sasa itakuwa je?
 
Mkuu mbona kiduchu hivi, na itakuwa inatoka kila ck au
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom