Amatagaimba
Member
- Oct 19, 2016
- 5
- 3
CRONOC 7
richard MWAMBE
01
N
DANI YA CHUMBA CHENYE GIZA sauti za watu wawili tu zilikuwa zikisikika, kilikuwa ni aina fulani ya kikao cha siri ambacho hakuruhusiwa mtu mwingine kuingia. Kila mmoja hakumwona mwenzake isipokuwa alisikia tu sauti ya mazungumzo yake.
“Unanihakikishia kuwa kesho nitasikia kitu?” mmoja aliuliza.
“Bila shaka, maadam nimefika nitaifanya kazi vyema, lakini mpango ni uleule,” yule mwingine alisikika akimjibu huyo aliyeuliza.
“Mmmm, ok! Sasa kama nilivyokwambia, kila kitu utakikuta kule hotelini, hakikisha unakamilisha mapema kwani ni swala lisilotakiwa uzembe, uzembe wako ni mauti yako”.
“Yeah! Nimekuelewa, aliyekuunganisha nami anajua uwezo wangu, na nina uhakika hata wewe utakubali”
“Good! Kazi njema,” wakaagana.
Kilichofuata hapo ilikuwa ni sauti tu ya mlango ukifungwa upande ule wa pili na mara taa kali zikawaka, zilizomfanya yule mtu aliyebakia kufinya macho na kisha tarataibu aliyafungua na kujikuta hayuko peke yake aliangaza macho huku na kule akawaona watu wengine watatu; wawili wanaume waliojazia vyema vifua vyao wakiwa wamevalia suti safi nyeusi na mmoja mwanamke aliyezibana nywele zake kisogoni, mrefu lakini si mwembamba sana, muonekano wake ulionesha kuwa ni mwanamke mjanja na asiyeogopa kitu, alivaa suti nyeusi ya kiume iliyomkaa vyema mwilini mwake.
“Muandaeni…” akawaambia wale vijana nao wakatoa soksi jeusi na kumvika kichwani, kisha wakamkamata huku na huku na kumtoa ndani ya lile eneo.
Hakuleta tabu kwani alijua wazi kuwa hiyo ndiyo njia ya kuingia na kutoka katika eneo hilo na ndivyo alivyoletwa mahali hapo.
WESTLAND – NAIROBI
SUBARU FORESTER nyekundu ilikunja kulia na kuiacha barabara ya kwenda Nakuru, ikapita katika barabara mbovumbovu, katikati ya majengo kadhaa ya ghorofa, baada ya majumba kama manne hivi ilisimama mbele ya jumba moja la ghorofa tano.
“Piiiii! Piiiii!” honi ya gari hiyo ilipigwa mbele tu ya lango kubwa lililo upande wa nyuma wa jengo hilo. Sekunde kadhaa tu lile lango likafunguka taratibu lakini aliyelifungua hakuonekana. Ile gari ikaingia ndani ya wigo na kupotelea uvunguni mwa lile jengo ambapo palikuwa na maegesho ya gari za wateja.
Milango ikafunguliwa, vijana wale wawili wenye suti wakateremka na kumfungulia mlango mtu wao. Yule mwanadada aliyekuwa nyuma ya usukani akashuka pia na kusimama nje.
“Tumefika!” akawaambia na wale jamaa wakamtoa lile soksi usoni na kijana huyo akawa huru.
“Nifuate!” yule mwanamke akamwambia huyo kijana naye akamfuata nyuma wakati yule mwanadada akiwa mbele.
Baada ya ngazi kadhaa waliibukia ndani ya jengo lile, akafungua mlango na kuingia mahali palipoonekana kama sehemu ya kumpumzikia ambapo palikuwa na makochi kadhaa, meza ndogo iliyotengenezwa kwa kioo kizito juu na chini kulikuwa na sanamu ya mfano wa nge mkubwa aliyekibeba kile kioo cha juu kwa mkia wake.
“301,” akamwambia mhudumu naye akamkabidhi funguo yule dada. Wakafuatana mpaka kwenye mlango wa chumba hicho.
“Una saa arobaini na nane tu za kumaliza kazi,” akamwambia yule mtu. Hakujibu kitu akatikisa kichwa tu na yule mwanadada akaondoka zake.
Ndani ya chumba hicho kulikuwa na kitanda kimoja kikubwa, meza ndogo na sofa moja la kutosha mtu mmoja. Akavua koti lake na kulitupa kitandani kisha akaliendea jokofu dogo lililowekwa kwenye kona ya chumba hicho, alipofungua akatoa chupa kubwa ya pombe na kuiondoa kizibo. Hakuhitaji bilauri, akapiga mafunda mawili ya haraka na kuirudisha.
Kabla hajafanya lingine lolote mlango wake ukagongwa, akasita kidogo, lakini hakuwa na wasiwasi. Alipofungua mlango akagongana macho na na mwanadada mweusi wa rangi, mfupi aliyejaa mwili, mapaja yake yaliyojaa vema yalionekana kukaa vyema ndani ya suruali aliyoivaa.
“Mzigo wako!” akamwambia huyo kijana. Naye akaupokea na yule mwanadada akaondoka zake.
Akiwa ameketi juu ya kitanda hicho, alilifungua kasha lile dogo na ndani yake kulikuwa na bahasha, akaichana na kutoa picha mbili zilizowekwa pamoja. Akaichukua ya kwanza na kuiangalia kwa makini, ilikuwa picha ya mtu, mwanaume, lakini ilionekana sura tu na pembeni yake ikaonekana nusu yaani pasipoti. Mtu yule alikuwa ni Muhindi, mnene na shingo yake ilipambwa kwa mkufu mzito wa dhahabu. Akaigeuza nyuma ile picha ilikuwa nyeupe tu kama ilivyo picha nyingine zote.
Akachomoa ya pili, nayo ilikuwa ya mwanaume Muafrika, kwa kumtazama alikuwa na umri kama wa miaka hamsini hivi, akazitazama zile picha kama zina uwiano wowote, haikuwa hivyo. Alipoking’uta ile bahasha kikadondoka kidubwasha cha kusikilizia masikioni, kidogo kama punje ya indi, akakigeuzageuza kisha akakipachika sikioni na kubofya kitufe chake cha kusikilizia.
“…Mr. Kolbas, picha namba moja ni ya Zuganji Kumeil, anapatikana huko North Kinangop, anaishi katika jumba lake kubwa lililotengwa na mji kabisa, ana wafanyakazi wasiopungua hamsini ndani na nje. Kuingia katia jumba hilo unatakiwa kutumia akili ya ziada, mtu huyu anatakiwa kuuawa bila kuulizwa swali lolote…”
Alipomaliza kusikiliza hayo akaiweka pembeni ile picha, mara akasikia sauti ya toni ikishiria kuna ujumbe mwingine.
“…Mr. Kolbas, picha ya pili ni Bwana Patrick Njuwe, yeye anapatikana Mombasa, nyumba yake kubwa na ya kisasa inapatikana katika mwambao wa bahari opposite na Mombasa Resort, anatakiwa kuuawa bila kuulizwa swali. Lakini hivi tunavyoongea yupo Nairobi amefikia katika hoteli ya Casablanca. Hakikisha unafuata maelekezo kama utakavyokuwa unayapata. Kumbuka una saa arobaini na nane tu kukamilisha hayo mauaji…kazi njema sana!”
Ile sauti ikakatika na hakukuwa na nafasi ya kuuliza swali wala kuulizwa. Akakichomoa kile kidubwasha chake na kukirudisha katika ile bahasha, kisha akavua saa yake pamoja vikorokoro vingine akaingia maliwato kujiweka sawa tayari kwa kibarua alichopewa.
NORTH KINANGOP
TOYOTA HILUX liliegeshwa nyuma ya jumba la kisasa lililojengwa katikati ya shamba kubwa. Umbali wa kutoka katika jumba hilo mpaka ile ya jirani ilikuwa kama kilomita moja au moja na nusu hivi. Ukiangalia kwa macho ya haraka haraka utajua tu kuwa waishio hapo wote ni mabepari maana hakuna kumsalimia mwingine wala kuombana chumvi.
Mlango wa gari ukafunguliwa na kijana mmoja aliyevalia nadhifu kabisa akateremka na kuufungua mlango wa pili; mtu mmoja, mnene, akateremka, mweupe mwenye nywele ndefu zilizomwagika mabegani. Akiwa anatembea kwa msaada wa fimbo akavuta hatua huku akisindikizwa na kijana yule mpaka ndani.
Sebule kubwa iliyosheheni kila kitu ilimlaki, naye akajibwaga juu ya kochi moja sebuleni hapo. Mtumishi wa ndani aliyejua wajibu wake akamletea kinywaji haraka.
“Niitie Morio,” akamwambia mtumishi wake na yule mwanadada akaondoka zake na baadaye akaja kijana mmoja, mkubwa kwa umbo, akaingia na kusimama mbele ya tajiri huyo.
“Yes Sir!” akaitika.
“Keti,” akaambiwa.
“Sikiliza Morio, nimetoka mjini kwenye ishu muhimu, hali si shwari sana. Imegundulika kuna mchezo mchafu unatunyemelea. Sina imani na mtu awaye yote. Kumbuka wewe ndiye nakutegemea sana kwenye swala la ulinzi, hakikisha hakuna mgeni anayeingia hapa bila taarifa na kama hamumjui apekuliwe vya kutosha, na isitoshe mtamkaribisha kwenye sebule namba moja nami nitaongea naye kwa kutumia VC. Lakini kama mtu ambaye ni wa karibu sana, ni mimi tu wa kutoa ruhusa, sawa?”
“Sawa!” Morio akajibu na kuondoka pale sebuleni.
Moja kwa moja alizunguka kwenye kona zote ambazo vijana wake wa ulinzi waliweka kambi na kuwapa mikakati ya kuwa makini katika hilo. Kamera za usalama ‘CCTV’ nazo zikategwa vyema, na watu katika chumba cha kuziongoza walikuwa makini kutazama kila kona ya jumba hilo na mipaka yake huko shambani. Zaidi ya hapo Morio aliongeza doria katika viunga vyote vya shamba lile na kila mmoja alikuwa na silaha iliyo kamili yenye magazine iliyoshibishwa sawasawa.
***
Usiku wa siku hiyo Kolbas alitoka hotelini na kurandaranda mitaani huku akiwa na silaha yake kwa maana alijua muda wowote anaweza kujikuta katika hali isiyo ya kawaida ama ya kushambulia au kushambuliwa.
Katika tembea tembea yake alijikuta ananasa katika ukumbi mkubwa wa disco uliosheheni watu wa kila aina. Kwa hatua ndogo ndogo akaukaribia na kupokelewa na warembo waliovalia kibiashara; wengine walikuwa wakivuta sigara na wengine wakiendelea kuwang’ang’aniza wanaume wawachukue usiku huo, japo kwa pesa kidogo.
“Hello puppy!” ilisikika sauti moja ya kike nyuma yake. Alipogeuka alikutana na moshi uliopulizwa kwa umahiri usoni mwake, akakohoa kidogo kisha akamtazama mwanamke huyo mshumami.
“Unasemaje?” akauliza.
“Aaah hilo si swali la wanaume,” yule mwanamke akamwambia, “wapaswa kuuliza, huduma ni shin’ ngapi,” akaongeza kusema kisha akaipachika tena sigara yake kinywani na kupiga pafu mbili za maana.
“Kwani huduma wanalipia hapa au wanalipia mlangoni…?”
Yule mwanadada akawageukia wenzake huku akionesha uso wa dharau kidogo.
“Hili vipi ka’ fala!” akajisemea.
“Mbona unaonekana kama sio mwanaume wewe,” akaendelea kusema na kisha ghafla akaupeleka mkono wake na kukamata dhakari ya Kolbas na kuiachia, “kumbe ipo,” akamwambia. Kolbas akamkamata mkono yule mwanamke na kuondoka naye eneo lile wakapotelea gizani.
“Naweza kumuona Shakila?”
“Hata usingeuliza, lazima ningempa taarifa ya uwepo wako,”
“Kwa nini?” Kolbas akauliza.
“Ndiyo utaratibu wa kazi yetu,” akamjibu huku akimpulizia moshi wa sigara na kuondoka zake. Dakika chache baadae, mwanamke mwingine akafika eneo lile akiongozana na yule wa kwanza. Hakuuliza kitu, akamtazama Kolbas juu mpaka chini, akamkamata mkono na kuongozana naye nje.
“Napenda watu kama ninyi, tutakunywa pombe, tutacheza muziki na nitakuhitaji kwa usiku mzima,” akamwambia akiwa kambana ukutani huku akihisi chuchu zilizochongoka za mwanamke huyo zikimchoma kifuani mwake.
“Mh, uuuuuuh!” akashusha pumzi, “haina shaka, cash ya Kenya, shilingi elfu kumi …”
“Hata ukitaka Dollar au Paundi utapata!” akamwambia na kutoka naye mpaka katika mlango wa ukumbi huo. Ndani yake dansi zito lilikuwa linaendelea, siku hiyo mwanamuziki kutoka Kongo Tabu Ley alikuwa akitumbuiza, watu walisheheni katika Dance Floor, wakajichanganya na kuendelea kuruka mangoma ya muziki huo.
♫….Muzinaaaaaaa…
Mu zina di tata e di mwana
e di Mpemve Santu,
Mu zina di tata zambi ooo, mu zinaaa….♪
Wimbo huo uliwafanya watu wajimwage sawasawa katika ukumbi huo, Kolbas na yule mwanadada nao walikuwa katikati ya watu wakiyarudi mangoma.
“Nimechoka mpenzi!” Shakila akamwambia Kolbas.
“Twende tupumzike”.
Wakatoka na kupanda ngazi kadhaa, viti viwili vilivyojitenga kwenye kona viliwakaribisha nao wakaketi juu yake. Kolbas akaangalia saa yake, tayari ilikuwa saa tano usiku. Wakaagiza vinywaji na kuendelea na mazungumzo, kila alipokumbuka kuwa ana saa arobaini na nane moyo wake ulimshituka na kwenda mbio.
“Unaitwa nani?” Shakila akauliza.
“Kolbas,”
“Umenijuaje mimi mpaka ukaniulizia moja kwa moja?” Shakila akauliza huku akimtazama kwa macho makali yaliyokuwa yakibadilikabadilika rangi kadiri ya taa za ukumbi huo zilivyobadili rangi.
“Sifa zako zinavuma kama pepo za Magharibi, nikiwa Antananarivo niliambiwa kuwa nikifika hapa nikutafute wewe kwani ni mwanamke wa pekee mwenye utamu wa kila namna, nami sikusita. Ndiyo wewe Shakila?”
“Yeah, ndiyo mimi,” Shakila akamjibu, “umekuja kibiashara?”
“Bila shaka! Tena siyo moja, na ni za pesa nyingi. Unaweza kunipa usiku wako mmoja?” Kolbas aliongea huku akimshika mwanamke huyo viganja vya mikono yake pale mezani.
“Ndiyo kazi yangu, utapata kila utakacho, usiku mzima ni Dola 100 za Kimarekani, lakini sintoweza kwani nina miadi saa nane za usiku na kibopa mwingine,” akatulia na kumwangalia kijana huyo, “nitakupa saa tatu tu lakini nitakupa huduma kubwa ya dola hizo hizo 100,” Shakila akatangaza dau kwa kubadili ukubwa wa huduma.
“Usijali, nitakupa hata zaidi ya hizo, na ukiifanya kazi yangu utafaidika zaidi, mimi ndiyo Kolbas,” akajitapa mbele ya mwanamama huyo aliyeonekana yuko tayari kwa kila kitu. Shakila hakuwa msichana mdogo kama wengine, yeye ni mwanamke haswa ambaye angeweza hata kukaa ndani kama mama.
“Unamfahamu Patrick Njuwe?” akamwuliza Shakila.
“Patrick Njuwe?...”
“Ndiyo! Wa Mombasa…”
“Aaaaa namjua sana yaani. Nani asiyemjua Patrick? Mzee wa totoz, kasambaza virusi kila kona, ana pesa, hana pa kuzipeleka, kahonga magari, majumba, ni Mungu mtu,” Shakila akamwambia Kolbas.
“Ninahitaji kumwona”.
“Una shida naye gani? Maana si mtu wa kufikiwa ovyo,”
“We niambie nitampataje hata kama ni kwenda Mombasa usiku huu tutaondoka mi na wewe kumfuata huko aliko, na nitakupa pesa iliyotakata.” Kolbas akatangaza dau baada ya kujikuta kuwa yuko karibu na Patrick kwa kuketi na mrembo huyo ambaye analijua windo lake ndani - nje.
Shakila alinyamaza kwa nukta kadhaa akifikiri jambo, “haina haja kwenda Mombasa,” akamwambia, na kauli hiyo iliamsha hisia na akili za Kolbas.
“Ati?” akauliza.
<<<<<<<<<
PAKUA 'HADITHI APP' KATIKA SIMU YAKO YA MKONONI UBURUDIKE NA RIWAYA HII NA NYINGINE NYINGI SASA
HADITHI APP ... INAKULETEA MAKTABA KIGANJANI MWAKO