Black Star 23
Tariq Haji
06240659
Katika chumba viongozi, huyu mshiriki hahitaji kushiriki mzunguko wa pilialiongea mmoja kati ya viongozi wasimamizi wa mzunguko huwo. Artif, mimi naungana nawewe hapo. Black Star naamini
ndio jina lake.
Kwa alichoonesha mzunguko kwa kwanza, naamini kabisa hakuna hata mmoja kati ya waliobaki mwenye uwezo wa kusimama nae ulingo aliongea msimamizi mwingine. Umenena vyema Franklin, mwiteni mmiliki wake tumlipe na kumpa kadi ya kuendelea mzunguko wa tatu mwezi ujao aliongea Montana Kris.
Don Pizallo akapewa taarifa za kuitwa katika chumba cha wasimamizi, akalipwa dola milioni moja na pamoja na kadi ya kuendelea na mzunguko wa tatu ambao utafanyika mwezi unaofata.
Akapokea mzigo huwo na kuondoka, tumepokea ujumbe kutoka kamati kuu, mpambanaji anaemilikiwa na Don Pizallo, Black Star amepita bila kushiriki mzunguko wa pili. Hivyo hata shiriki mzunguko huu badala yake atashiriki moja kwa katika mzunguko wa tatu ambao utafanyika mwezi ujao aliongea
MC.
Fahad akatoka chumba cha kusubiri na kuelekea nje kabisa ya uwanja, akamkuta Don Pizallo akimsubiri. Umefanya vyema kijana wangu, japo sura yako inaonesha kutoridhika kabisa. Ni kweli kabisa, pambano lilikuwa rahisi sana. Hakuna hata mmoja alienichemsha damu yangu leo.
Natumai kuwa mzunguko wa tatu nitakutana na upinzani mkali sana aliongea Fahad akiingia ndani ya gari. Don Pizallo akaingia upande wa pili na safari ya kurudi hotelini ikaanza. Ukiwa unasubiri mzunguko wa tatu, unakusudia kufanya nini.
Nataka niende nyumbani kuwasalimu wazazi, nitarudi ikiwa imebakia wiki moja kuelekea mzunguko wa tatu.
Sawa, hakuna shida. Achana vijana wangu wakuandalie mpango mzima wa safari, utaondoka kesho kutwa ila uwe makini sana. Nina uhakika kuwa kuna watu wameanza kukufutilia maisha yako mpaka sasa aliongea Don Pizallo.
Wafanye tu hivyo lakini wakijichanganya na familia yangu watakumbana na kiama alijibu na kukunja sura. Don Pizallo alihisi kubanwa na pumzi, AURA alijisemea kichwani.
Siku tatu baadae.
Ndege ya shirika la ndege la Ethiopia inakanyaga ardhi Tanzani katika uwanja wa taifa wa Hayati Baba wa Taifa, Julius Nyerere. Katika mlango VIP Fahad akatoka akiwa na begi lake la mgongoni.
Alitoka mpaka sehemu ya kusubiri Mizigo, akatoa maelekezo ipelekwe nje ambako alitafuta dereva wa taxi na kuipakia. Akamueleza sehemu ya kwenda, dereva huyo akaweka gia na kuondoa gari.
Siku nyingi, mnaendeleaje nyumbani alijisemea na kushusha pumzi. Baada ya safari ndefu, hatimae akawasili nyumbani kwake.
Mlinzi aliekuwepo akamsaidia mizigo na kuipeleka ndani, za siku nyingi Msola aliongea Fahad.
Nzuri tu bosi, pole kwa safari alijibu.
Ahsante, kwa wiki tatu utapumzika nyumbani na familia yako aliongea Fahad na kumkabidhi bahasha. Si pesa nyingi lakini nina imani zitakusukuma kwa siku hizi chache aliongea. Msola akipokea bahasha hiyo, wala hakuifunguwa.
Akaaga na kuondoka, Fahad akaelekea chumbani kwake na kupanga vitu vyake. Na kwa sababu tayari kiza kilishaanza kuingia, akafunga funga milango na kuingia chumbani kwa ajili ya kuupitisha usiku huwo.Ila kabla hajalala akafungua dirisha na kuliacha wazi kisha akazima taa nda kukaa kwenye kiti. Huna haja ya kujificha akaongea bila kuwasha taa.
Kimya! narudia tena, huna haja ya kujificha. Sitaki nikuone sura ila kama una jambo unataka kusema ni vyema ukafanya hivyo. Nimechoka nataka nipumzike. Bosi wangu anahitaji ujiunge na kampuni yake, atakulipa mara tano kuliko anavyokulipa Don Pizallo aliongea mtu aliekuwa gizani upande wa pili.
Nashukuru kwa ofa yako lakini bahati mbaya sina muda wa kubadilisha bosi. Nenda kamwambie, ikitokea akapambana na bosi wangu basi alete mpiganaji wake mkali na hodari kuliko yeyote. Akinipiga ndio nitajiunga ne. Nimemaliza na unaweza kuenda, ukiongea neno moja tu roho yako.
Siku ya pili mapema asubuhi, Fahad alitoka na kupelekea madukani kwa ajili ya kutafuta simu na laini kwa ajili ya mawasiliano. Alipomaliza harakati zake akatafuta mgahawa na kupata kifungua kinywa kisha akarudi nyumbani.
Baada ya kupumzika kidogo, akawasha ile simu na kuweka laini. Akaingiza tarakimu kadhaa na kupiga. Iliita lakini haikupokewa. Alipoona hivyo akafahamu kuwa mtu anayetafuta huenda akawa kwenye kikao. Baada ya dakika kama kumi hivi, akaingia bafuni na kujimwagia maji kisha akavaa suti na kutoka.
Alipohakikisha maandalizi yamekamilika akatoka na kuelekea ofisini kwa mzee Abedi. Hakutoa taarifa, alitaka kumfanyia Surprise. Baada ya mwendo wa nusu saa akawasili nje ya jengo kubwa. Akaingia sehemu ya maegesho na kuegesha gari. Akashuka na kuelekea ndani ya jengo hilo.
Habari ya saa hizi dada alimsalimu mwanamke alimkuta mapokezi. Nzuri nikusaidie nini alijibu na kumuangalia. Naweza kumuona mzee Abedi aliongea kwa sauti ya chini.
Una miadi nae
Hapana, ila we mwambie tu mtu wa miezi sita amekuja
Samahani kaka, kama huna miadi nae, ni vyema ukaondoka au ukaweka miadi. Lakini kwa leo nafasi haitakuwepo labda kesho aliongea mwanamke huyo na kubenuwa midomo.
Asante kwa maelezo yako, kama hutojali naweza kulifahamu jina lako aliongea tena kwa sauti ya chini. Yule bidada akamuangalia Fahad kwa macho yaliojaa kiburi, akasonya. Jina langu la kazi gani aliongea kwa sauti kubwa kiasi cha watu waliokuwa karibu na mapokezi kusikia. Mlinzi aliyekuwa karibu na hapo akafika, kuna nini akauliza. Mtoe huyu kaka nje, ananipotezea muda wangu tu alifoka.
Yule mlinzi akageukia Fahad na kutaka kuongea lakini midomo ikashindwa kutamka maneno aliyokusudia. Akataka kuongea jambo jingine, Fahad akaweka kidole mdomoni kisha akaongea, fanya kazi yako. Akameza funda kubwa la mate, kijasho chemba kikaanza kumchuruzika. Wewe si nimekwambia mtoe akafoka na kusimama. Akatoka sehemu ya ndani na kwenda kumshika mkono Fahad kwa ajili ya kumtoa.
Huna haja ya kunivuta, mimi ni mtu mzima, nitaondoka mwenyewe aliongea na akmshika mkono na kuutoa. Kisha akageuka na kuanza kuondoka. Tajiri akasikia sauti nzito ikitokea nyuma yake, mbona unaondoka ile sauti ikaendelea.
Nimeambiwa niondoke, na ndio maana naondoka alijibu akigeuka. Nani alokwambia uondoke aliuliza mzee huyo kwa hasira. Mzee Mussa punguza jazba, nina uhakika aliesema hivyo alikuwa anatimiza majukumu yake tu aliongea na kutabasamu kisha akaendelea isitoshe sikuwa na miadi ya kumuona bosi.
Bosi gani huyo, nani aliesema mwenye kampuni anahitaji kuweka miadi ya kuonana na bosi alifoka kisha akaelekea mapokezi. Naomba kitabu cha wageni muhimu akaongea. Yule bidada akakiweka mezani kitabu alichoambiwa.
Mzee Mussa akakifunguwa, ukurasa wa kwanza tu wa kitabu hicho kulikuwa na picha kubwa ya Fahad. Wewe, umeiona hii picha aliongea akmgeuzia kitabu. Yule mwanamke macho yakamtoka, na wakati huwo ndipo alipotambuwa kama kibarua kimeota nyasi. Mzee Mussa, usifanye kitu chochote aliongea Fahad, akamuangalia yule mwanamke na kutabasamu kisha akaondoka na mzee Mussa.
Moja kwa moja alipelekwa mpaka katika ofisi yake, katika kampuni hiyo Fahad alikuwa ndio mtu wa juu kabisa. Akiwepo yeye hata baba ake hushuka cheo na kuwa cheo cha chini. Subiri katika ofisi yako, mzee yupo kwenye kikao.
Atatoka muda si mrefu aliongea mzee Mussa. Ahsante sana, ni matumaini yangu uko salama lakini. Maana wala hatujapata muda wa kuulizana hali aliongea Fahad na kutabsamu. Mi nashukuru Mungu, naendelea vizuri sema tu, kipidni cha nyuma nilipata ugonjwa kidogo ila sasaniko vizuri aliongea mzee huyo.
Nafurahi kusikia hivyo aliongea Fahad na kuinuka, akaelekea dirishani na kufunguwa mapazia kwa ajili ya kuruhusu mwanga wa jua. Unahitaji kinywaji chochote, nipatie chai tu ya tangawizi aliongea na kurudi kwenye kiti chake. Mzee Mussa akatoka na kumuacha Fahad peke yake, pasi na kuwa nyumbani. Bado alihisi kuna kitu anakikosa moyoni mwake. Alitoa simu yake na kutaka kupiga lakini alifahamu kabisa isingewezekana.
Baada ya dakika kama kumi hivi mzee Mussa akarudi akiwa na kikombe vikombe pamoja na chupa ndogo ya chai. Akaweka mezani na kumimina chai, akamsogezea kikombe kimoja. Wakati wanapata chai wakawa wanaongea mambo mbali mbali kuhusu kampuni. Nusu saa baadae mlamgo ukafunguliwa, mzee Abedi akaingia akiwa anahema. Alikuwa haamini macho yake, miezi sita kwakem ilikuwa kama miaka.
Fahad ni wewe baba au macho yang yananidanganya aliongea mzee huyo huku machozi yakijenga michirizi mashavuni mwake. Ni baba, awe Fahad yupi kama sio jembe lako alionge akitabasamu. Hivi ni miezi sita au miaka, katika kipindi hiki mwanangu umekuwa sana aliongea na maneni hayo yalimshtuwa sana Fahad. Kwa duniani kweli ana miaka ishirini kama awali lakini katika ulimwengu wa Dao tayari alishfika miaka ishirini na sita.
Hapana baba ni miezi sita tu alijbu na kwenda kumkumbatia mzee huyo. Nashukuru mungu umerudi salama japo nafahamu kama hutokaa sana aliongea Mzee Abedi. Wakakaa katika ofisi hiyo na na kuongea, bila kushughulika na saa.
Walishtushwa na alarm ya saa sita, vipi utakwenda nyumbani leo, au bado kidogo aliuliza mzee Abedi. Kama ulivyosema baba, mimi sina muda mrefu. Nitakuwepo kwa wiki mbili tu kisha nitaondoka tena aliongea Fahad.
Mi naelewa na sitaki kuingia wala kuuliza majukumu yako, kwasababu ya wewe leo ndio familia yetu ina uwezo angalau wa kusimama. Hivyo mi nakuombea kwa mungu chochote kile unachofanya kifanikiwe aliongea mzee Abedi. Leo tutaenda wote nyumbani aliongea Fahad wakitoka katika ofisi hiyo, walipofika tu mapokezi. Nataka kuongea na yule binti pale, naomba mnipe kama dakika tano aliongea na kuondoka.
Yule binti alivyoona Fahad anakwenda upande wake akaanza kutetemeka. Alikuwa ameshika kopo la sharubati akajikuta likimponyoka, pasi na watu walivyotegemea Fahad akaliwahi na kulidaka. kuwa makini aliongea na kutabasamu. Naomba unisamehe kwa tabia yangu ya awali aliongea akikwepesha macho. Usijali, ila siku nyingine jaribu kuwa mpole zaidi.
Jaribu kumuhudumia kila mtu kwa usawa aliongea na kumkabizi kopo lake la sharubati. Akarudi alipokuwa mzee Mussa na baba ake. Wakatoka katika jengo hilo, nje wakaachana na mzee Mussa. Wao wakatumia gari ya mzee Abedi na kuondoka.
Kilele cha Mlima Sumeru
Kikao cha miungu kumi na mbili kilikuwa kinaendelea, mjadala mkubwa ilikuwa jinsi ya kuiangamiza moja kwa mbili ngome ya Asura. Mimi nasema hivi, huyo mtoto niachieni mimi lazima nikumute aliongea Masya. Kwanini tukuachie wewe wakati ulitulia kipindi anaiangsha moja ya vitongoji vyao.
Kama mungu umeshindwa kutekeleza majukumu yako ipasavyo. Wewe unasema hivyo kama nani, huna hata nchi moja ambayo ipo vizuri katika nchi zako. Kazi yako nikujificha mapango na kujilimbikizia mali tu. Mabishano makali yalizuka kati ya Anubis na Masya.
Nyamazeni Indra alinguruma mpaka kusababisha tetemeko, samahani mfalme tumepitiwa tu aliongea Anubis na kuinamisha kichwa. Tulizeni jazba, kumbukeni tumekubaliana tumuache kwa miaka ishirini kabla ya kumshambulia aliongea. Ndio wengine wakajibu kwa pamoja, na hivyo ndivyo tutakavyofanya aliendelea kuongea.
Manchotakiwa kufanya ni kuwanoa vijana wenu wote, nakusudia wa pande zote mbili. Nimeshaikisha habari kwa mlinzi wa bahari saba, nina uhakika Mfalme Zeusi kashazipata habari pia aliongea Indra na kuachia tabasamu. Kama hatuwezi kumshambulia huku, basi tutamuua akiwa katika ulimwengu wake huko huko.
Hahaha! Kweli mnamuogopa kijana mdogo tu, pamoja kuwa na akili za kujiita miungu. Sikuwa nimekosea kusema kuwa nyinyi ni binaadamu ambao muko na uwezi kidogo zaidi ya binadamu wengine sauti ilisikika chumba kizima.
Asura Indra aliongea kwa hasira, punguza jazba Indra, nimekuja kuwasalimu tu. Hicho ni kivuli changu tu aliongea Asura akiwa anatembea taratibu kuelekea alipo Indra. Ukipiga hatuwa moja tu nakuuwa aliongea Sun Wu Kong. Umesikia wapi kivuli kikafa, acha upuuzu wewe ngedere kauli hiyo ikamkera sana Sun Wu Kong.
Unakasirika nini sasa, kwani wewe sio ngedere. Kajiangalie kwenye kioo halafu ndio uje hapa kutema cheche. Kwasasa nipo hapa hapa kuwapa taarifa tu, Black Star ni silaha ya mwisho nitakayoitengeza. Hiyo ni nyota inayokula mwangaza ili kuishi, kama jina lake linavyojisema.
Huyu ndio mwisho wa uwepo wenu, nawaonya tu hakuna binadamu wa kawaida atakaemuweza hata wale ambawo mnasema mumewabariki kwa kuwawezesha kutumia nguvu zenu katika mapambano. Ishini vizuri maana siku zenu za mwisho zinakaribia alimaliza kuongea na kutoweka.
Ndoto za mwenda wazimu hizo aliongea Kaminotore, Indra alikuwa kimya akimumunya maneno ya Asura. Mpaka kuwapa ujumbe huwo ni wazi kuna mambo bado hawayajui, Black Star ni nani ndio swali lililokuwa linazunguka kichwani mwake. Na kwanini katokea upande wa pili, inafahamika kama Dunia ina kiwango kidogo sana cha Qi ambacho hakiwezi hata kumfikisha mtu DAN ya tatu katika Martial Art.
Anubis, si una ndugu zako ambao wanaishi Egypt aliongea Indra na kumuangalia, ndio wapo. Waambie wamfatilia Black Star, wasiache jiwe bila kufukuliwa. Watafute asili yake, nina wasiwasi kuna kitendawili kikubwa hapa. Na tusipokuwa makini, nina hofu tutakuwa hatarini alisisitiza. Sawa mkuu nitawafikishia ujumbe alijibu Anubis. Kikao kiliendelea huku kila mtu akipewa jukumu lake. Kikao kikaisha na wote wakatawanyika isipokuwa mmoja tu.
Mtukufu mfalme nikusaidie kazi gani aliongea akiinamisha kichwa, nguo yake ikaachanikika sehemu ya kiuno na mikia tisa ikajitokeza. Kuna kazi yangu nataka unifanyie, Kitsubi aliongea Indra na kusimama, maneno yako ni amri kwangu mtukufu mfalme aliongea Kitsubi kwa unyenyekevu wa hali ya juu.
Nahitaji usafiri mpaka upande wa pili na ufanye kila liwezekanalo upate taarifa kuhusu Black Star. Nimesikia, nitaondoka punde tu nitakapomaliza akageuka na kugeukia kiumbe kinachofanana na bweha ila chenye mikia tisa na kupotea.
**********