Jaman naomba kujua kama huu ni utaratibu wa serikali au ni vipi katika kupata cheti cha mtoto, wakati napeleka docs kwaajili ya kupata cheti hakukua na mahali jina limekosewa,kila kitu kilikuwa sawa naa hata fumu nilipewa ilijazwa vizuri cha ajabu cheti kimetoka majina yamekosewa wakati nawaeleza kupata suluhu nikaambiwa kama nataka yarekebishwe basi nitoe 6500 then nisubiri ndani ya wiki moja,sasa yani kukosea wakosee wao then mimi nilipie makosa ya hii ni haki kweli?? Ni manispaa ya ubungo tu au ni manispaa zote?? Na je hivi ndivyo serikali yetu inavyopata fedha?