RITA wameanza...

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Mamlaka ya Usajili wa Vizazi na Vifo almaarufu kama RITA wameanza kusimamia mavazi ya heshima kwa wateja wa ofisi zao za Dar es Salaam. Getini,pale Dar es Salaam,wanaovaa mavazi yasiyo na staha( ima wanawake au wanaume) hawaruhusiwi kuingia kwa ajili ya kuhudumiwa katika Ofisi zao.Askari yuko makini na mavazi kwelikweli. RITA wameanza,nani atafuata?
 
Ujinga wa Mtanzania, badala ya kuboresha huduma kwa wananchi, mnalazimisha wananchi waboreshe mavazi ndo wahudumiwe....aaggggggggghhhhhhhhhhhhhhhh!!!!!!!!!!!!!
 
Safi sana hii. huduma zao pia zimeboreshwa, kupata cheti si zaidi ya wiki moja baada ya maombi.
 
..nilipokuwa Likizo mwenyewe nimetinga kaptura yangu na sandoz na Tshirt nafika pale askari ananizuia kuingia eti mavazi hayaruhusiwi mxiiiiiii
 
Wezi wakubwa hao wameshindwa kuboresha huduma wanaboresha mavazi,walarushwa hao wanakuzungusha na cheti chakuzaliwa ,na kwa taarifa yao hawana lao ,its planned vyeti vitolewe tu mara mtu anapozaliwa ,nilikuwa hospitali moja wakapewa hiyo taarifa wacha wafurahie wewe.waboreshe huduma sio mavazi ,its out of their business.MWISHO WAO UNATABIRIKA KAMA WA CCM,VYETI VITATOLEWA NA MAHOSPITALI KWISHNEY YAO,
 
Nilikuwa na Tangazo la dogo nikaenda pale wananiambia kitabu hakijaja toka kwa hospital dogo alipozaliwa wakati iyo hospital iko almost opposite na jengo lao!
Wako bize na mambo yasiyo ya msingi huduma kwanza wazee!
 
Hao RITA hao siku yao inakuja tena ya kwao haihitaji kusubiri katiba mpya,bila kitu kidogo utasumbuliwa mpaka utajuta kuzaliwa wakati ushazaliwa unafuatilia cheti.Waboreshe huduma mavazi wawaachie ile kamati ya waziri Nchimbi hahahaha hata sijui wamefikia wapi wale jamaa wa mavazi ya taifa.Kweli TZ kama Hollywood kila siku kuna movie mpya inachomoza
 
Back
Top Bottom