Mzizi wa Mbuyu
JF-Expert Member
- May 15, 2009
- 7,472
- 7,275
Hivi lengo la makusanyo lkinapangwa vipi? Maana tusiwe tunasifiana kwa kuvuka malengo kumbe tumeweka malengo ya kuruka sufuria wakati tulikuwa na uwezo wa kuruka pipa au hata simtank lita 10,000!
Ni sawa na kujisifu umefaulu mtihani ulioutunga mwenyewe
Hivi lengo la makusanyo lkinapangwa vipi? Maana tusiwe tunasifiana kwa kuvuka malengo kumbe tumeweka malengo ya kuruka sufuria wakati tulikuwa na uwezo wa kuruka pipa au hata simtank lita 10,000!
Wewe umenikuna katika post yako mama!hayo maswali yako mengi ndio majibu!Natamani januari kuwe na bunge jipya la bajeti then tuweke malengo ya kukusanya trilioni 5 kwa mwezi!Kama bil 80 zimepigwa kwa siku chini 2 (achana na ambazo hazijastukiwa) vipi kwa mwezi!?
Kweli kabisa. maana hawa jamaa kila mwaka tunaambiwa wamevuka malengo. Sasa kama kila mwaka tunavuka malengo, kwa nini hatupigi hatua ya kuonekana?Uko sawa kabisa mkuu ni kweli kuwa malengo yanaweza pangwa ya chini strategically kuwafanya waTanzania wawe myopic. Kumbe badala ya kuweka malengo kwenye bil 5 ingewezekana kabisa yakawa bil 10
Uko sahihi kabisa. Kigezo kikuu cha kukusanya mapato kinapaswa kuwa pato la taifa. Kiwango kilichowekwa kitaalamu kwa kuzingatia mazingira ya hapa kwetu ni kukusanya kodi isiyopungua 25% ya pato la taifa (GDP). Hivyo mwaka huu TRA ingepaswa kukusanya angalau Shs 22tri/- (pato la taifa mwaka huu litakuwa Sh 90tri). Kuweka lengo kiduchu la kukusanya mapato (Sh 12tri au 13% ya GDP) kama ilivyo sasa ni sehemu ya ufisadi wa kitaasisi unaoliangamiza hili taifa. Kwa kuzingatia hii hesabu ni kwamba tabaka la mafisadi (watawala ndani) wamejiwekea lengo la kupora Sh 10tri/- mwaka huu kupitia tax fraud!!
Hilo ndo tatizo ninaloliona hapa kwetu. Watu wanajiwekea low targets. Wanakusanya ziada wanatafuna halafu wanajisifia, na wanasifiwa na viongozi wakubwa kuwa wamevuka malengo. wanaongezewa na marupurupu kama zawadi kwa "kazi nzuri". mwisho wa siku matunda ya kuvuka malengo hatuyaoni, tunazidi kuchechemea mwaka hadi mwaka.Mkuu Utotole,hii ni moja ya "comment" bora zaidi kwa leo.
Wanaopanga "lengo" ndio hao hao wanaokusanya,je wakisema lengo ni bil.900 kwa mwezi kumbe hali halisi walitakiwa wakusanye bil.1500 kwa mwezi,hizo nyingine zinaingizwa mifukon mwao,nani anajua na nani anahoji na kuchukua hatua?
Walio chini yake wamemuangusha!
You have a point man.Walikuwa wanaweka very low target na kujisifia wamefikia lengo.
Hivi lengo la makusanyo lkinapangwa vipi? Maana tusiwe tunasifiana kwa kuvuka malengo kumbe tumeweka malengo ya kuruka sufuria wakati tulikuwa na uwezo wa kuruka pipa au hata simtank lita 10,000!
Hiyo ishu ya kusema waliochini yake wamemuangusha ndio sipendi kuisikia kabisa!!!...Hata kwa jk ilikuwa hivyo hivyo, mkuu usipokuwa mfuatiliaji waliochini yako watapiga dili tu, mbona kwa magufuri tunaona hadi wakuu wa wilaya wanaiga mkuu anachokifanya?..
Nani anaweza kujiwekea malengo asiyoweza kuyafikia?That is also my question....
Kuna kuweka standard za chini ili ku forge mafanikio...
Je hiyo ndio ilikuwa optimum capacity?
Hivi lengo la makusanyo lkinapangwa vipi? Maana tusiwe tunasifiana kwa kuvuka malengo kumbe tumeweka malengo ya kuruka sufuria wakati tulikuwa na uwezo wa kuruka pipa au hata simtank lita 10,000!
Uko sahihi kabisa. Kigezo kikuu cha kukusanya mapato kinapaswa kuwa pato la taifa. Kiwango kilichowekwa kitaalamu kwa kuzingatia mazingira ya hapa kwetu ni kukusanya kodi isiyopungua 25% ya pato la taifa (GDP). Hivyo mwaka huu TRA ingepaswa kukusanya angalau Shs 22tri/- (pato la taifa mwaka huu litakuwa Sh 90tri). Kuweka lengo kiduchu la kukusanya mapato (Sh 12tri au 13% ya GDP) kama ilivyo sasa ni sehemu ya ufisadi wa kitaasisi unaoliangamiza hili taifa. Kwa kuzingatia hii hesabu ni kwamba tabaka la mafisadi (watawala ndani) wamejiwekea lengo la kupora Sh 10tri/- mwaka huu kupitia tax fraud!!
Hiyo taarifa tunaipata baada ya jipu kutumbuliwa? wakome kabisa waliwahi kunitoza kodi ya computa yangu used nilikwenda kumtembelea rafiki yangu ZANZIBAR akanipeleka MWANAKWEREKWE nikanunua ka koputa nilipofika badari ya DAR niligombaniwa kama mpira wa kona wakati ni komputa ya matumizi yangu tuu na zaidi sidhani kama koputa inalipiwa kodi.