zubedayo_mchuzi
JF-Expert Member
- Sep 2, 2011
- 4,873
- 1,221
- Thread starter
-
- #21
Lengo la kununua mbuzi wakati tunaweza nunua tembo....
Kwahyo zile bil 80 inakuwaje?
naona un bashiri mapungufuHizo ni changamoto, kama angeliweza kutupa ufafanuzi labda tungelielewa vizuri. Huenda ikawa ndio pungufu kwenye asilimia 97.6, i.e. 2.4%!
Hii pesa bado ni ndogo ukilinganisha na wizi unaofanywa bandarini! Haya malengo bado hayashabiani na kiasi halisi kinacho patikana hapo!Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekusanya jumla ya shilingi trilion 3.77 kuanzia mwezi Julai hadi Oktoba 2015 ambayo ni sawa na asilimia 97.6. ya lengo la makusanyo ya sh trilioni 3.87 ikiwa ni jitihada za TRA kutekeleza mkakati wa serikali ambao unaitaka kukusanya Ths . Trililioni 12.3 kwa mwaka wa fedha 2015/2016.
Kwa mujibu wa Kamishna Mkuu wa TRA Rished Bade, mwezi Julai TRA ilikusanya kiasi cha shilingi bilioni 849,582.9 ambacho ni asilimia 99.4 ya lengo la kukusanya shilingi bilioni 854,922.9.
Mwezi Agosti TRA ilikusanya kiasi cha shilingi bilioni 890,536.7 ambacho ni asilimia 101.5 ya lengo la kukusanya shilingi biilioni 876,974.2 .ambapo mwezi Septemba jumla ya shilingi trilioni 1.07 zilikusanywa ikiwa ni asilima 91.7 ya lengo trilioni 1.16 kwa mwezi mwezi Oktoba TRA iilkusanya shilingi bilioni 970,089.6 ikiwa ni asilima 99.3 ya lengo la kukusanya shilingi bilioni 976,441.5.
Taarifa ya mwenendo wa makusanyo ilipitishwa na Bodi ya Wakurugenzi ya TRA katika kikao cha bodi kilichofanyika jana tarehe 10 Novemba 2015 katika ofisi za makao makuu ya TRA? amesema Bw. Bade.
Mafanikio katika makusanyo haya yametokana na mikakati madhubuti iliyowekwa na mamlaka baada ya kusaini mkataba na Waziri wa Fedha ambapo Kamishna Mkuu alisaini mkataba na kila Mkuu wa Idara na wakuu wa Idara kusaini mikataba na wafanyakazi walioko chini yao ili kila mfanyakazi kuwajibika ipasavyo.
Wito wa TRA ni kwa mfanyabiashara na wadau wote wa kodi kutimiza wajibu wao wa kulipa kodi kwa hiari ili kuchangia pato la taifa.
Sambamba na hilo TRA imepokea kwa furaha sana wito wa Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli wa kuhimiza ukusanyaji wa mapato bila woga na bila kumwonea mtu.
Pamoja Tunajenga Taifa Letu
Rished Bade
KAMISHNA MKUU
http://www.tra.go.tz/index.php/about-tra/465-taarifa-ya-makusanyo-ya-kodi
Kama makusanyo yako almost asilimia 100 na ukwepaji kodi ni mkubwa hivyo kuna shida zifuatazo:-
1. Wakadiriaji malengo hawaitendei haki nchi hii kwa kutoa malengo ya chini sana
2. Wakadiraji kodi wanashirikiana na wakwepa kodi
3. Wanaoweka viwango vya ukusanyaji wanashirikiana na wanaokwepa kodi. Lengo tupige makofi kuwa compliance ni 100% huku tunaibiwa. (Staili ya kuuma na kupuliza)
Kuna mambo hayako SAWASAWA somewhere??? Huwezi kuvuka malengo na kujipongeza wakati tumeibiwa mpaka basi!!!
Queen Esther
billion 80+offence+penalties=?????
swali haliwezekani.
Chukua like ✅kabah
That is also my question....Hivi lengo la makusanyo lkinapangwa vipi? Maana tusiwe tunasifiana kwa kuvuka malengo kumbe tumeweka malengo ya kuruka sufuria wakati tulikuwa na uwezo wa kuruka pipa au hata simtank lita 10,000!
Sio hivyo mkuu. Hii nchi imekubuhu kwa ukwepaji wa kodi na nakumbuka Basil Mramba alifanya kazi kubwa sana kutambua wigo wa kodi na kuingiza walipa kodi zaidi kupitia mfumo wa TIN. Hadi sasa wanasema kama mfumo wa kodi ungelikuwa wa haki na usawa ingeliwezekana kabisa VAT kuwa 12%, PAYE 6% na walipaji kuwa na moyo zaidi wa kulipa kwa hiari.naona un bashiri mapungufu
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekusanya jumla ya shilingi trilion 3.77 kuanzia mwezi Julai hadi Oktoba 2015 ambayo ni sawa na asilimia 97.6. ya lengo la makusanyo ya sh trilioni 3.87 ikiwa ni jitihada za TRA kutekeleza mkakati wa serikali ambao unaitaka kukusanya Ths . Trililioni 12.3 kwa mwaka wa fedha 2015/2016.
Kwa mujibu wa Kamishna Mkuu wa TRA Rished Bade, mwezi Julai TRA ilikusanya kiasi cha shilingi bilioni 849,582.9 ambacho ni asilimia 99.4 ya lengo la kukusanya shilingi bilioni 854,922.9.
Mwezi Agosti TRA ilikusanya kiasi cha shilingi bilioni 890,536.7 ambacho ni asilimia 101.5 ya lengo la kukusanya shilingi biilioni 876,974.2 .ambapo mwezi Septemba jumla ya shilingi trilioni 1.07 zilikusanywa ikiwa ni asilima 91.7 ya lengo trilioni 1.16 kwa mwezi mwezi Oktoba TRA iilkusanya shilingi bilioni 970,089.6 ikiwa ni asilima 99.3 ya lengo la kukusanya shilingi bilioni 976,441.5.
Taarifa ya mwenendo wa makusanyo ilipitishwa na Bodi ya Wakurugenzi ya TRA katika kikao cha bodi kilichofanyika jana tarehe 10 Novemba 2015 katika ofisi za makao makuu ya TRA? amesema Bw. Bade.
Mafanikio katika makusanyo haya yametokana na mikakati madhubuti iliyowekwa na mamlaka baada ya kusaini mkataba na Waziri wa Fedha ambapo Kamishna Mkuu alisaini mkataba na kila Mkuu wa Idara na wakuu wa Idara kusaini mikataba na wafanyakazi walioko chini yao ili kila mfanyakazi kuwajibika ipasavyo.
Wito wa TRA ni kwa mfanyabiashara na wadau wote wa kodi kutimiza wajibu wao wa kulipa kodi kwa hiari ili kuchangia pato la taifa.
Sambamba na hilo TRA imepokea kwa furaha sana wito wa Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli wa kuhimiza ukusanyaji wa mapato bila woga na bila kumwonea mtu.
Pamoja Tunajenga Taifa Letu
Rished Bade
KAMISHNA MKUU
Tanzania Revenue Authority - Taarifa ya makusanyo ya kodi
Uko sahihi kabisa. Kigezo kikuu cha kukusanya mapato kinapaswa kuwa pato la taifa. Kiwango kilichowekwa kitaalamu kwa kuzingatia mazingira ya hapa kwetu ni kukusanya kodi isiyopungua 25% ya pato la taifa (GDP). Hivyo mwaka huu TRA ingepaswa kukusanya angalau Shs 22tri/- (pato la taifa mwaka huu litakuwa Sh 90tri). Kuweka lengo kiduchu la kukusanya mapato (Sh 12tri au 13% ya GDP) kama ilivyo sasa ni sehemu ya ufisadi wa kitaasisi unaoliangamiza hili taifa. Kwa kuzingatia hii hesabu ni kwamba tabaka la mafisadi (watawala ndani) wamejiwekea lengo la kupora Sh 10tri/- mwaka huu kupitia tax fraud!!
Tusubiri taarifa ya mwaka ujao
tutalinganisha....