Ripoti ya ajali MV spice

Shega H

Member
Jun 26, 2011
9
3
Ripoti ajali ya meli yatolewa Zanzibar
19 Januari 2012 17:58
Serikali ya Zanzibar leo imetoa ripoti ya uchunguzi
wa kuzama kwa meli ya MV Spice Islander hapo
Septemba 10, 2011 eneo la Nungwi, Kaskazini mwa
kisiwa cha Unguja.
Aliyetoa ripoti hiyo kwa niaba ya serikali alikuwa
katibu kiongozi, Abdulahamid Yahya Mzee baada
ya kupokelewa na Rais wa Zanzibar Dr Ali
Muhammed Shein Novemba 30 mwaka jana kutoka
kwa Jaji Abdulhakim Ameir aliyeongoza jopo la
watu 10. Yahya akielezea sababu zilizogunduliwa
na tume kuwa chanzo cha kuzama kwake ni kujaza
abiria kupita kiasi, mizigo kuwekwa vibaya, matatizo
ya kiufundi yaliofanya kiwango cha upakizi
kisijulikane, kuingia maji na uzembe wa nahodha
kutoomba msaada. Pia imetoa hesabu ambayo
sasa itakuwa rasmi ya watu waliopotea na
waliozama ambapo inasimama kuwa 1370. Tume
imesema abiria waliopakiwa katika meli hiyo
walikuwa 2,470 wakati uwezo wake ulikuwa ni
watu 620 ikiwa ni karibu kidogo ya mara nne zaidi
ya uwezo wake. Tume imesema ubovu wa meli
hiyo ulijulikana tokea mwezi Julai, miezi miwili kabla
ya kuzama kwake kutokana na ukaguzi uliofanywa
na taasisi ya usalama wa bahari Sumatra, lakini
bado meli hiyo ilipewa leseni.
Taarifa imesema kuna mnyororo mrefu sana wa
watu waliokuwa na dhamana lakini walishindwa
kufanya wajibu wao kuanzia maafisa wa meli hiyo,
maafisa wa bandari na pia maafisa kama vile wa
polisi na taasisi ya kukusanya mapato TRA, ambao
wanatuhumiwa kupokea fedha na kupenyeza
abiria. Tume hiyo imependekeza watu kadhaa
washtakiwe na imetaja makosa iliyoona
yanawahusu na polisi waliwatia mbaroni watu
kadhaa sku ya Jumatano katika kutekeleza hilo.
Watu muhimu watakaoshtakiwa ni pamoja na
Abdula Muhammed mrajis wa meli, Haji Vuai Ussi
mkurugenzi wa usafiri wa baharini, Juma Seif
mkaguzi wa meli na wamiliki watano wa kampuni
za Visiwani Shipping na Al Gubra Marine Services.
Pia nahodha Abdullah Kinyaiite anatakiwa
kushtakiwa lakini serikali alikiri katibu kiongozi
hajulikani alipo na tume haikusema yuhai au la.
Jana polisi ilitia kishindo mji wa Zanzibar kwa
kamata kamata ya watuhumiwa hao, lakini
haikujulikana iwapo leo walipelekwa mahakamani
au la au ni lini taratibu zitakamilika na kusomewa
mashtaka yao. Mwandishi wetu wa Zanzibar Ally
Saleh amesema ripoti hiyo pia inataja orodha ya
watu ambao wameonekana wanafaa kuchukuliwa
hatua za kinidhamu na mmoja wao ni mkurugenzi
wa shirika la bandari Mustafa Aboud Jumbe
ambaye kama wengine wataondoshwa sehemu
zao za kazi mara moja.
Kwa bahati meli hiyo ilikuwa imewekewa bima
isipokuwa bima hiyo haitahusu mizigo kwa sababu
eneo hilo halikuwa limekingwa, lakini bima hiyo
itasaidia kulipa jamaa za watu waliofariki dunia na
tume imependekeza angalau kiwango cha shs
10,000 ,000 kwa kila mtu aliyefariki dunia kwa
maana ya pia waliopotea. Pia serikali imesema
itazigawa kwa waathirika na jamaa waliofiwa fedha
zote zilizokusanywa ikiwa ni michango mara
taratibu zitapokamilika lakini kazi hiyo sasa ni rahisi
kwa vile orodha kamili na iliyohakikiwa
imeshapatikana. Serikali imesema ripoti hiyo
itachapishwa kwa uwazi na ukamilifu na kuweza
kusomwa na kila mtu ikiwa na pamoja na kwenye
mtandao.

swali la kujiuliza ni kwanini mapendekezo ya tume hayafanyiwi kazi ikiwa nchi inapenda kuundia matatizo tume?
mfano tume ya tuhuma za Jairo ilitoa mapendekezo lukuki lakini.............
 
Back
Top Bottom