Ripoti maalum; Ajali za Bodaboda,Dar.

samsun

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2014
Posts
7,386
Reaction score
5,971
Inakadiriwa kuwa kati ya mwaka 2014 hadi june 2015,ajali za Bodaboda zipatazo 10,351 na kusababisha majuruhi 10,079 na kusababisha vifo vipatavyo 514. Huku ikielezwa kuwa sababu kuu ni speed na kutokuwa makini barabarani.




Tunajua kuwa hali ya maisha ni ngumu na kila mtu anatafuta namna ya kujikwamua kutokana na hali ngumu lakini kuweni makini.




Hivi ni kweli hatuwezi kupunguza hizi ajali za Bodaboda kama sio kuzimaliza kabisa.




Kwani kuvaa helmet na kudhibiti ubebaji wa abiria haiwezekani ......... kama vipi tuzuie kabisa biashara ya bodaboda maana inatuachia VILEMA wengi mno ambao wanakuwa tegemezi wakati wao ndio walikuwa wanategemewa.





Serikali fanyeni kitu kwa hili janga.

 
Nimewahi kushuhudia ajali moja ya Bodaboda,

ni kumbukumbu mbaya sana
kuwahi kuiona kwa macho

wote walifariki pale pale!
 
Hii report nina shaka nayo,miaka minne vifo 514?!!tu sio kweli kuna repoti ilitoka mwezi wa kwanza kuwa kwa wastani pikipiki zinaua watu watatu kwa siku, na hata juzi tu kuna report imetoka kuwa ndani ya miezi miwili vifo vitokanavyo na pikipiki ni 147.!!
i
 
Ni kweli mkuu nimekosea mwaka ni 2014 - JUNE 2015.
 
Kuna ajali nilishuhudia dereva wa bodaboda alishamisha scania lililokuwa limebeba cement hadi ile scania ikatolea nje ya kingo za barabarani!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…