Ripoti: Kituo cha ITV kimeongoza kwa kuwa na watazamaji wengi zaidi nchini

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,292
Kituo cha ITV kinachomilikiwa na kampuni ya IPP Media Group kwa mara nyingine tena kimeongoza kwa kuwa na watazamaji wengi zaidi miongoni mwa vituo vya runinga nchini.

Kwa mujibu wa data za robo ya mwisho ya mwaka 2015 na robo ya kwanza ya mwaka 2016 kutoka kwenye kampuni ya utafiti wa vyombo vya habari Geo Poll yenye makao yake nchini Marekani, kituo hicho kilichukua asilimia 20 ya watazamaji (audience share) katika miezi minne ya mwisho (October – December) ya mwaka 2015 na kushuka kwa 2% katika kipindi cha miezi minne ya kwanza ya mwaka 2016 (January – April), kwa kuwa na asilimia 18.
Clouds TV imeendelea kufanya vizuri pia kwa kukamata nafasi ya pili kwa kuwa na 17% katika robo ya nne ya mwaka jana huku ikipanda kwa 2% katika robo ya kwanza mwaka 2016 hadi kufikisha 19%.
Ripoti hiyo imeonesha pia kuwa EATV imefanya vizuri katika robo ya kwanza mwaka huu kwa kuwa na 16%.

Vituo vilivyofuata ni pamoja na TBC 1, Star TV, Channel 10, TV1, TBC 2. Vingine vikiwemo Azam TV, Mlimani TV, Capital TV na vingine vimeonekana kufanya vibaya kwa kugawana 1% tu iliyosalia, kwa mujibu wa ripoti hiyo.
Kwa upande wa ratings, East Africa TV na TV1 ziliongeza katika robo ya kwanza huku ITV ikipoteza ratings kwa kiwango kikubwa. “TBC1 and Channel 10 have also dropped in their ratings in Q1,” inasema ripoti hiyo.

RADIO

Kwa upande wa vituo vya redio, Clouds FM bado imeendelea kuwa kinara kwa kuvuta 28% ya wasikilizaji katika robo ya mwisho 2015 huku ikipoteza 2% katika robo ya kwanza mwaka huu na kuwa na 26%.

TBC Taifa imeonesha kufanya vizuri kwenye robo ya kwanza mwaka huu kwa kuwa na 13% ikifuatiwa na Radio Free Africa iliyong’ang’ania kwenye 10% huku Radio One na TBC FM zikifuatia. Habari njema kwa EFM ambayo hadi sasa bado inasikika Dar es Salaam na Pwani pekee ambayo imeendelea kufanya vizuri kwa kuwa na wastanii wa 5.5% mbele ya East Africa Radio, Times FM na Capital FM.

xGTV1.jpg.pagespeed.ic.1OrUlZBdDn.jpg
xGTV2.jpg.pagespeed.ic.FrzmKmbn6s.jpg
xGT-Radio-1.jpg.pagespeed.ic.qpkqZ3rACE.jpg
xGT-Radio-2.jpg.pagespeed.ic.tSs4j7u0iO.jpg
 
Kwa mujibu wa data za robo ya mwisho ya mwaka 2015 na robo ya kwanza ya mwaka 2016 kutoka kwenye kampuni ya utafiti wa vyombo vya habari Geo Poll yenye makao yake nchini Marekani, kituo hicho kilichukua asilimia 20 ya watazamaji (audience share) katika miezi minne ya mwisho (October – December) ya mwaka 2015 na kushuka kwa 2% katika kipindi cha miezi minne ya kwanza ya mwaka 2016 (January – April), kwa kuwa na asilimia 18.
Licha ya kwamba bado kituo hicho kinaongoza kwa kuwa na Watazamaji wengi Tanzania, vile vile kimeshuka chini ukilinganisha na mwaka jana. Jisomee hapa GeoPoll Mobile Survey Research Blog
xGTV1.jpg.pagespeed.ic.rYYjosmtZ0.webp

Top TV Stations in Kenya and Tanzania, Q4 2015
 
Hapo babu kahonga mihela ili kuwekwa kwenye takwimu huu mchezo kauanza muda sana,itv kwa vipindi gani mpaka iangaliwe san?ukiondoa habar tena za kitaifa tu
 
Hapo babu kahonga mihela ili kuwekwa kwenye takwimu huu mchezo kauanza muda sana,itv kwa vipindi gani mpaka iangaliwe san?ukiondoa habar tena za kitaifa tu
Heti kahonga
Si na nyie mnamahela mngehonga na nyie tbc yenu iwe hapo itv ilipo
 
Kwanza ITV kuna vipindi gani vya maana vya kuangalia zaidi ya taarifa ya habari?
Nafikiri umeitaja taarifa ya habari kuwa ya maana, pasi na shaka basi kuna vituo vingine ambavyo taarifa zao za habari si za maana
 
Hiyo clouds Na eatv sababu ya vijana wanaofuatilia muziki lakini hakuna cha maana.
 
Hiyo clouds Na eatv sababu ya vijana wanaofuatilia muziki lakini hakuna cha maana.
Ni kweli mkuu, lakini hayo ni mafanikio maana taste ndiyo inayovutia watazamaji wa aina mbalimbali, nafikiri kuna haja kwa vyombo vya habari kugusa kila rika katika mgawanyo wa vipindi ili kujizolea mashabiki na hatimaye kuwavutia advertizers
 
Back
Top Bottom