Ripoti juu ya muungano na serikali ya umoja wa kitaifa(gnu) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ripoti juu ya muungano na serikali ya umoja wa kitaifa(gnu)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by pinguli, Oct 25, 2011.

 1. p

  pinguli Senior Member

  #1
  Oct 25, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 122
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  "....RIPOTI iliyohuishwa ya Mpango wa Afrika Kujitathmini Kiutawala Bora (APRM) Tawi la Tanzania, imeonesha kuwa tangu ulipomalizika mgogoro wa kisiasa Visiwani mwaka 2010, juhudi madhubuti zimeonekana katika kuboresha misingi ya utawala bora Zanzibar. Hayo yalielezwa wakati wa semina ya watendaji wa APRM Tanzania na Makatibu Wakuu wa wizara mbalimbali za Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar iliyofanyika visiwani humo. Akizungumza katika semina hiyo, Katibu Mtendaji wa APRM Tanzania, Rehema Twalib aliwaeleza watendaji hao kuwa kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (GNU) kulikotokana na juhudi za viongozi wenyewe wa ndani ya nchi kuumaliza mpasuko wa kisiasa wa miaka mingi, ni suala lililoainishwa katika Ripoti ya APRM kuwa jambo zuri la kuigwa na nchi nyingine za Afrika zenye migogoro ya ndani. Hata hivyo, alisema ripoti hiyo imeainisha kuwa kuna tatizo la uelewa mdogo kuhusu uendeshaji wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa miongoni mwa watendaji wa kada za chini wa vyama na serikalini na akasisitiza kuwa wadau wengi wa masuala ya utawala bora wamependekeza kuanzishwa mikakati kukuza uelewa juu ya utendaji kazi wa GNU. Katika ripoti hiyo mpya ya hali ya utawala bora nchini, utafiti wa APRM umetaja pia kuwa Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar uliozaa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 1964 na ambao umedumu kwa zaidi ya miaka 45, ni mfano mzuri wa kuigwa wa namna Muungano wa nchi mbili unavyoweza kudumu kwa mafanikio. katika ripoti hiyo, Tanzania imetajwa kufanya kazi nzuri ya kuwa msuluhishi wa migogoro miongoni mwa majirani zake kama vile Burundi, Rwanda, Comoro na Kenya..."
  Haya kimsingi ni mambo makubwa na ya kujisifu katika duru za siasa za kimataifa na kitaifa, bahati mbaya hatuyafahamu katika uhalisia wake na badala yake tumekuwa tukizungumza juu ya upande mmoja wa makosa ya viongozi na watawala bila kupima na mafanikio yao kiutawala. Ikiwa tutakuwa tayari kuyajua haya na kuyafuatilia tunaweza kujadili matatizo yetu rationally na kujipatia ufumbuzi wa kudumu.
   
 2. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #2
  Oct 25, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kumbukeni mgogoro wa zanji ulianza kabla hata ya mzee mchonga hajatutoka lakini pamoja na kuwa yeye ndo muanzilishi wa muungano hakufanya juhudi zozote za kuumaliza ila alienda kusuluhisha wahutu na watusi, hiki ni kitu ninachokikumbuka juu ya mgogoro wa zanji. Na hapa tu ndo ninapomuonaga Kikwete ana mengi ya kukumbukwa. najua mavuvuzela ya chadema yatakuja kuniponda ila daima nitasema ukweli, uongo kwangu mwiko.
   
Loading...