Ripoti ajali ya meli yatolewa ZanzibaR!!!

Pindima

JF-Expert Member
Aug 16, 2011
347
81
Serikali ya Zanzibar leo imetoa
ripoti ya uchunguzi wa kuzama
kwa meli ya MV Spice Islander
hapo Septemba 10, 2011 eneo la
Nungwi, Kaskazini mwa kisiwa
cha Unguja.
Aliyetoa ripoti hiyo kwa niaba ya
serikali alikuwa katibu kiongozi,
Abdulahamid Yahya Mzee baada
ya kupokelewa na Rais wa
Zanzibar Dr Ali Muhammed
Shein Novemba 30 mwaka jana
kutoka kwa Jaji Abdulhakim
Ameir aliyeongoza jopo la watu
10. Yahya akielezea sababu
zilizogunduliwa na tume kuwa
chanzo cha kuzama kwake ni
kujaza abiria kupita kiasi, mizigo
kuwekwa vibaya, matatizo ya
kiufundi yaliofanya kiwango cha
upakizi kisijulikane, kuingia maji
na uzembe wa nahodha kutoomba
msaada. Pia imetoa hesabu
ambayo sasa itakuwa rasmi ya
watu waliopotea na waliozama
ambapo inasimama kuwa 1370.
Tume imesema abiria
waliopakiwa katika meli hiyo
walikuwa 2,470 wakati uwezo
wake ulikuwa ni watu 620 ikiwa
ni karibu kidogo ya mara nne
zaidi ya uwezo wake. Tume
imesema ubovu wa meli hiyo
ulijulikana tokea mwezi Julai,
miezi miwili kabla ya kuzama
kwake kutokana na ukaguzi
uliofanywa na taasisi ya usalama
wa bahari Sumatra, lakini bado
meli hiyo ilipewa leseni.
Taarifa imesema kuna mnyororo
mrefu sana wa watu waliokuwa
na dhamana lakini walishindwa
kufanya wajibu wao kuanzia
maafisa wa meli hiyo, maafisa
wa bandari na pia maafisa kama
vile wa polisi na taasisi ya
kukusanya mapato TRA, ambao
wanatuhumiwa kupokea fedha na
kupenyeza abiria. Tume hiyo
imependekeza watu kadhaa
washtakiwe na imetaja makosa
iliyoona yanawahusu na polisi
waliwatia mbaroni watu kadhaa
sku ya Jumatano katika
kutekeleza hilo.
Watu muhimu watakaoshtakiwa
ni pamoja na Abdula Muhammed
mrajis wa meli, Haji Vuai Ussi
mkurugenzi wa usafiri wa
baharini, Juma Seif mkaguzi wa
meli na wamiliki watano wa
kampuni za Visiwani Shipping na
Al Gubra Marine Services. Pia
nahodha Abdullah Kinyaiite
anatakiwa kushtakiwa lakini
serikali alikiri katibu kiongozi
hajulikani alipo na tume
haikusema yuhai au la. Jana
polisi ilitia kishindo mji wa
Zanzibar kwa kamata kamata ya
watuhumiwa hao, lakini
haikujulikana iwapo leo
walipelekwa mahakamani au la au
ni lini taratibu zitakamilika na
kusomewa mashtaka yao.
Mwandishi wetu wa Zanzibar Ally
Saleh amesema ripoti hiyo pia
inataja orodha ya watu ambao
wameonekana wanafaa
kuchukuliwa hatua za kinidhamu
na mmoja wao ni mkurugenzi wa
shirika la bandari Mustafa
Aboud Jumbe ambaye kama
wengine wataondoshwa sehemu
zao za kazi mara moja.
Kwa bahati meli hiyo ilikuwa
imewekewa bima isipokuwa bima
hiyo haitahusu mizigo kwa
sababu eneo hilo halikuwa
limekingwa, lakini bima hiyo
itasaidia kulipa jamaa za watu
waliofariki dunia na tume
imependekeza angalau kiwango
cha shs 10,000,000 kwa kila mtu
aliyefariki dunia kwa maana ya
pia waliopotea. Pia serikali
imesema itazigawa kwa
waathirika na jamaa waliofiwa
fedha zote zilizokusanywa ikiwa
ni michango mara taratibu
zitapokamilika lakini kazi hiyo
sasa ni rahisi kwa vile orodha
kamili na iliyohakikiwa
imeshapatikana. Serikali
imesema ripoti hiyo itachapishwa
kwa uwazi na ukamilifu na
kuweza kusomwa na kila mtu
ikiwa na pamoja na kwenye
mtandao.
Alamisha hii
 
Tunashuru kwa taarifa.Hebu tujulishe ni kiasi gani cha pesa watapewa walioumia na waliosalimika.
 
Waziri anayehusika pia akamatwe, sijaona ni wapi wanamtia nguvuni!! alitakiwa ajiuzuru tokea kipindi kile lakini akakaa kimya.
 
Wakimchukulia hatua stahili Mustafa Aboud Jumbe, tutaanza kuamini kidogo kuwa Utawala wa Sheria kwa kila mmoja unawezekana
 
Waziri anayehusika pia akamatwe, sijaona ni wapi wanamtia nguvuni!! alitakiwa ajiuzuru tokea kipindi kile lakini akakaa kimya.

Rais Amani Karume alishasema kwamba hatuna utamaduni wa kuwajibishana, sasa kujiuzulu ni sawa, lakini tegemea kutokee kwa "kudra" tu.
 
Word has it, waziri husika ni kutoka CUF
Word has it ndio nini Gaijin, kila waziri anajulikana anahusika na nini, na ripoti imetoka watu wametajwa, sasa word has it tena who has the word? hahaha....

By the way, kwenye swala la insurance wanasema Bima italipa kwa waliofariki. My question is unapokata bima ya chombo cha biashara the first thing wanataka kujua ni unasafirisha watu wangapi chombo kikijaa. Ili wajue wakidhurika wote liability yao bima ni shilingi ngapi. Sasa kama meli ni ya watu 620 halafu ukapakia watu 2,470 na katika hao Mungu alikuwa anawapenda zaidi 1,370 akawaulia baharini, hapo Bima itakubali kulipa kwa watu wote hao kweli? Ningependa bima ikatae kulipa hii bili, walipe wenye kampuni wenyewe, mali zao zipigwe mnada!
 
Word has it ndio nini Gaijin, kila waziri anajulikana anahusika na nini, na ripoti imetoka watu wametajwa, sasa word has it tena who has the word? hahaha....

By the way, kwenye swala la insurance wanasema Bima italipa kwa waliofariki. My question is unapokata bima ya chombo cha biashara the first thing wanataka kujua ni unasafirisha watu wangapi chombo kikijaa. Ili wajue wakidhurika wote liability yao bima ni shilingi ngapi. Sasa kama meli ni ya watu 620 halafu ukapakia watu 2,470 na katika hao Mungu alikuwa anawapenda zaidi 1,370 akawaulia baharini, hapo Bima itakubali kulipa kwa watu wote hao kweli? Ningependa bima ikatae kulipa hii bili, walipe wenye kampuni wenyewe, mali zao zipigwe mnada!

Ilikuwa ni words in the streets, manake Tanzania taarifa hazina kawaida ya kuwekwa nakala mtandaoni, na hivyo sina source ya maandishi

Juu ya hivyo taarifa zinasema kuwa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano ya Zanzibar inaongozwa na Hamad Masoud Hamad kutoka Chama cha Wananchi- CUF

Haingii maanani kuwa meli izame kwa uzembe kisha bima iwalipe. Iendeleze uzembe wa mtu mwenginekwa kuingia hasara!
 
Back
Top Bottom