Ridhwani: Viongozi wa CCM hawawajibiki
*Asema tatizo ni kukwepa lawama
*Atamani CCM ya Mwalimu Nyerere
*Amsifu Mzee Msekwa kwa ukomavu
*Azungumzia sakata la malipo ya Dowans
Na John Daniel
Miezi michache baada ya kumalizika uchaguzi mkuu Oktoba mwaka jana, Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Baraza Kuu la Umoja Wa Vijana CCM, Bw Ridhwani Kikwete, amesema hali ndani ya chama hicho si shwari kutokana na viongozi wake kushindwa kutim,iza wajibu wao kw akukwepa lawama.
Akizungumza na gazeti hili wiki hii katika mahojiano maalum, Bw Ridhwani ambaye pia ni motto wa mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete alitaja mambo mengine yanayotishia mustakbali wa chama hicho kuwa ni ubinafsi na kushuka kwa nidhamu ndani ya chama.
Alisema kutokana na hali ilivyo sasa ndani ya chama hicho anatamani CCM ingekuwa ile aliyoiacha Baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere. "Katika kampenmi za mwaka jana nilijifunza mambo mengi mazuri, lakini kikubwa zaidi ni kwamba chama CCM kinahitaji mabadiliko makubwa, nawaomba sana viongozi watusaidie wanapeleka wapi nchi? Watusaidie sisi vijana," alisema Bw Kikwete.
Aliendelea; "Mfano rahisi wakati tunaanza kazi ya kuzunguka nchi nzima, yalikuwa ni mamauzi ya UVCCM na tulikuwa na makundi manne moja likiongozwa na Makamu wa UVCCM, Beno Malisa, lingine Katibu Martine Shigela na lingine bwana Mfaume. Lakini baadaye yalianza maneno oooh chama kimebinafsishwa, hakuna hata kiongozi mmoja aliyesimama kutoa ufafanuzi huo wa kweli, matokeo yake wananchi wakajenga dhana mbaya, sasa hii tunaelekea wapi?" alihoji.
Ni ndefu na hawa jamaa hawajaweka mtandaoni nimebidi kuichapa upya na sina muda wa kuimaliza wengine saidieni