Mtu Fodontino
JF-Expert Member
- May 9, 2021
- 362
- 572
Pole sana mkuu hakika duniani wote wasafiri
Kwa wale mnaopenda kufurahia vifo vya wenzenu huku mkiwaita wendazao. Mjifunze kwa huyu ili kuujua uchungu halisi wa kufiwa.Ni jana tumemaliza maziko yake, alikuwa ni mtu wangu wa karibu sana kwangu kama workmate.
Kwa kipindi kifupi tulichofahamiana alikuwa ni mtu mwema kwa watu wa rika lote na ndio maana wengi tulimlilia kutoka ndani ya moyo.
Alikuwa ni mwenye kupenda kazi yake mpaka karibu na mwisho kabisa wa maisha yake japo alikuwa anatembea na tatizo kubwa mwilini mwake.
Yeye ameondoka sisi tutamsahau ila dunia haitamsahau kamwe
Funzo kwetu ingawa kazi ndio kitu kinacho tuwezesha kuishi lakini tusisahau kuujali mwili wetu.
Sikua najua kama ukiondokewa na mtu wa karibu inauma kwa kiasi hiki, naombeni dua za Rehema kwa ndugu yangu huyu
Pumzika kwa amani ndugu yangu![]()