Researchers :Shambulio la VIRUS duniani (wanacry ransomware) NORTH Korea yahusishwa....

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,722
Watafiti wa mambo ya kimitandao wanasema shambulio la kimitandao lililoathiri nchi zaidi ya 150 duniani linaweza kuwa lilifanywa na Pyongyang au Kuna watu wameiframe ionekane wao ndio wahusika.

Wachambuzi wa usalama wanasema Kuna ufanano wa codes Kati ya Ransomware na virus waliowahi kutengenezwa na Hackers wa North Korea.

Mtafiti wa usalama mitandao kutoka Google Neel Mehta alieleza.

Hata hivyo watafiti wa Kaspersky wanasema ni mapema kuihusisha North Korea kwa sababu mtu mwingine anaweza kubadili codes zifanane na zinazokisiwa kuwa ni za North Korea.

Japo tuhuma hizi hazina ushahidi wa kutosha lkn Makampuni makubwa ya kiusalama mitandaoni Russian multinational cybersecurity and Antivirus provider, Kaspersky lab bado wanafikiri inawezekana.

Microsoft wao wamesema moja kwa moja shambulio hilo litakuwa limeanzia kwa US intelligence services.

Tupo tunaohisi wenda ni muendelezo wa fitna za US kwa North Korea
Tupo tunaohisi wenda North Korea kupitia kikosi chake cha kijeshi cha Hackers Bureau 121 kimefanya yao.


Karibu kwa maoni....
Rejereo

WannaCry ransomware shares code with North Korea-linked malware – researchers
 
Team kipanki tupo juuu!!

hehhehee wao wana vifaru, submarines lakini sisi tunawapiga kwa kirusi mmoja tu na wanabaki mdomo wazi!!

NB: Ni muda ambao tanzania badala ya kuwekeza kwenye kujipiga vichwa matofali tuwekeze kwenye utaalamu wa computer! kuliko kuwategemea polisi wanaotishia wananchi SMG tuwekeze kwenye cyber army!
 
Hakuna vita mbaya kama ya cyber maana wanavuruga mipango yote fikiria unaibiwa tech,uliyoiwekeza kwa zaidi mrefu.
Shambulio hili ni tafadhali kwa nchi yetu, sio lazima Kila kitu kiwe digital, unakuwa digital ni vizuri kuwe na manual /mechanical back up. Mfano Tanesco ikawa na mtambo yote digital na scada zake. Likitokea shambulio la mtandao umeme unaweza kukatika nchi nzima hadi jamaa waamue. Badala yake kukiwa na back up ya manual operation Nahisi ipo umeme unarudi.
Wanaoelewa zaidi Kuna vitu vingi sio lazima viwe computer based 100 Bila alternative...
 
Putin amesema kwamba shambulio hilo litakua limefanywa na nchi za magharibi. Nkorea atengeneze kirusi halaf akipeleke China au Russia?!... Uliona wap...
 
Team kipanki tupo juuu!!

hehhehee wao wana vifaru, submarines lakini sisi tunawapiga kwa kirusi mmoja tu na wanabaki mdomo wazi!!

NB: Ni muda ambao tanzania badala ya kuwekeza kwenye kujipiga vichwa matofali tuwekeze kwenye utaalamu wa computer! kuliko kuwategemea polisi wanaotishia wananchi SMG tuwekeze kwenye cyber army!
Mkuu NK hawezi kufnya hivi vitu hii ni backdoor ya US intell. Agencies ili kuonesha kuwa NK ni hatari by the way naona Pentagone anaelekea kupata sababu ya kumwaga damu Pyongyang...Juzi tu CIA waliripotiwa kuhack Banking system ya dunia but huwez kuwakamata hii naifananisha ya fake event ya sept 11 eti Osma kagonga ghorofa hii ilikuwa Afghan achapwe sasa NK atashambuliwa na mataifa mengi kumbe sio yeye.....Na kama ni yeye basi sio good hacker maana a good hacker must be invisible sasa ukikamatwa wewe ujuwe huwezi kuhack yaani unahack in two mins wazee washajua codes unazotumia kuhack this is childish.
 
Ukitazama kwa jicho la kipekee utaona kuwa operating systems za kimarekani kama Windows ndo zimekuwa attacked na hii Trojan ya wannacry........
Target nadhani ilikuwa Windows regardless to where it is highly used. CIA wana ukaribu wenye kutia shaka na Google pamoja na Microsoft products ndo maana kama ni kweli N.K wamehusika basi wamegusa penyewe.
 
Kwanza tuwekane sawa hapa. Huyu wanacry ni trojan, worm, virus, auuu!!!!? Maana kinachofanyika hapa ni mtu anateka mfumo halafu anakutaka mwenye mfumo umlipe hela au utekeleze masharti fulani ndio auachie mfumo wako.
Pia aina hii ya utekaji sio ngeni, nadhani imeanza mwaka Jana ambapo baadhi ya hoteli ziliwahi kutekwa kwa kushikilia mfumo wa milango ambapo aliyekuwa ndani hakuweza kutoka na aliyekuwa nje hakuweza kuingia hadi watekaji walipolipwa hela.
Sasa kusema kwamba ni NK inaleta ukakasi kidogo maana uhuni huu unafanywaga na wachina, wamarekani na warusi. Kwa NK, mmmh. Sidhani
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom