Report ya milipuko ya mabomu Mbagala iko wapi?

Manyanza

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
9,481
14,339
Baada ya tukio la jana katika kambi ya Jeshi Gongo la Mboto nimeona ni vyema tukiliangalia na hili ....................
April mwaka 2009 ulitokea mlipuko wa mabomu katika kambi ya Jeshi la Wananchi kambi ya Mbagala, na baada ya tukio hili viongozi wanaohusika na dhamana ya majeshi na ulinzi.. waliahidi kwamba hali hiyo haitatokea tena... na ikaundwa kamati maalum ya kufuatilia chanzo cha lile tukio na amiri jeshi mkuu (JK) akaagiza ukaguzi wa mabomu katika kambi zote za jeshi nchini je hili lilitekelezwa? au ilikuwa ni danga toto na kupunguza machungu ya wananchi waliopoteza mali, ndugu na jamaa zao

Jamani mimi naomba mwenye report ya Mbagala anifahamishe au aiweke hapa jamvini ... ni hayo tu

Poleni sana watanzania wenzangu mlioondokewa na ndugu na jamaa zenu na wale wote waliopoteza mali zao....
 
namhala RIPORT anayo Mkwere ila kuipata mpaka Salma aruhusu....
 
Taarifa mimi ninayo, ni PM nikupatie.
Mkuu, heshima kwako
Kama kweli unayo tunaomba uiweke hapa kwani sio siri, mabomu hayakulipuka kwa siri na yaliondoa uhai wa ndugu zetu tuliowapenda na kuwahitaji. Weka hiyo ripoti mkuu.

Hizi kauli za tume au tukio kutojirudia tena ni namna tu ya kuwafariji kijinga wafiwa na wahanga wa matukio kama haya, nafikiri tunahitaji zaidi ya tume au ripoti ili kuweza kumaliza matatizo ya namna hii.
 
Wazee mimi naona Tanzania tumeweka siasa na propaganda kama vipaumbele vyetu namba moja. Mabomu ya Mbagala yalipotokea ilitakiwa mtu angalau mmoja tu ajiuzulu lakini hicho hakikutokea...kwa ahadi kuwa tukio kama hilo lisingetokea tena hapa Tanzania. Gongolamboto limetokea!....Na mpaka leo hii hatujasikia mtu yeyote yule angalau akigusia tu kuwa huenda atajiuzulu kwa tukio la kufyatuka mabomu kujirudia....Hii ndio Tanzania na hivyo ndio vipaumbele vyetu...Mungu bariki!
 
Nchi inaongozwa kimaigizo na Mafisadi kwa kuwa wanaongoza wafu:roll: Hata Kuchukuwa hatua za kuandamana tunaogopa tunabaki kulalamika JF
 
pole kwa woote mliopoteza ndg na jamaa ktk janga la mabomu!! mungu awatie nguvu pia uvumilivu. tumwombe mwenyezi mungu awalehemu ndugu zetu waliotangulia mbele ya haki!. Amen
 
Back
Top Bottom