RENAMO: Hatutambui matokeo

Yericko Nyerere

Platinum Member
Joined
Dec 22, 2010
Posts
17,027
Reaction score
20,518
Chama cha upinzani nchini Msumbiji kimesema hakitayapokea matokeo ya uchaguzi yanayotarajiwa kutangazwa jumatano ya wiki ijayo.

Mpaka asubuhi hii matokeo yaliyokwisha tangazwa ni 24.58% ya kura zote, Nyusi anamzidi Dhlakama kwa 63.02% dhidi 29.42%. Simango ana 7.56%.

Kumekuwa na dosari nyingi ikiwemo udanganyifu, vitisho vya dola, watu wengi kukosa haki ya kupiga kura kwa sababu lukuki zinazotolewa na mamlaka, na ucheleweshaji wa matokeo bila sababu za msingi. Hii inapelekea kusema uchaguzi haukuwa huru na haki

Nimezungumza na Dhlakama anasema hataki kurudi mstuni, lakini uhuru wa Wanamsumbiji ikibidi utatafutwa mstuni tena.


Source: BBC

http://www.bbc.co.uk/swahili/habari/2014/10/141017_renamo_msumbiji
 

Attachments

  • _78296491_024333363-1.jpg
    33.5 KB · Views: 218
  • _78226776_024324837-1.jpg
    33.3 KB · Views: 219
waacha waje kuchukua rasili mali zao bado hazijaisha...
 
Afrika bwana, mtu akishndwa uchaguz hatak kukubari matokeo. ningekua huko ningeshauri dhlakama adakwe hrk acje jaa mc2ni
 
waacha waje kuchukua rasili mali zao bado hazijaisha...
Tanzania tujiandae kwenda kukomboa msumbiji mda si mrefu, hao jamaa si walikuwa msituni hao? na kuna gesi imepatikana nyingi kuliko ya tz tena ipo kaskazini ambako ndiko chama pinzani cha msituni kimetawala, wazungu hawawezi kufadhili silaha hao jamaa warudi msituni kweli? hapo Tanzania lazima tujiandae kwenda kusaidia ndugu zetu wa msumbiji kama ilivyo kawaida yetu. tuikomboe kama tulivyoikomboa comoros futa kabisa waleta fujo nchini.
 

Waache wachukue gesi yao ndiyo yunachokitaka ... wazungu.wanachochea mambo mengi wauze silaha viwanda vinadoda kule
 
Hii imeshakuwa kawaida kwa nchi zetu Kama majirani zetu wakenya nakumbuka mwai kibaki aliapishwa na tochi fastafasta Na yule jaji akasema amelazimishwa .
 
Afrika bwana, mtu akishndwa uchaguz hatak kukubari matokeo. ningekua huko ningeshauri dhlakama adakwe hrk acje jaa mc2ni

Akubali vipi wakati anajua wanechakachua?
Km hiv wengine wanataka ht kubadirisha katiba waendelee kutawala!
Kwanini watu wakubali kirahisi tu?
Taratibu kitaeleweka tu hakuna marefu yasiyokua na ncha
 
asili ya renamo ni utawala wa ian smith na makaburu enz enzi hizo wakijaribu kuzuia frelimo isiondoshe ukoloni msumbiji. sio rahisi wananchi wa msumbiji kukabidhi dola kwa alphonso dhlakama
 
Watanzania hamna sababu za kuja kuikomboa Msumbiji kwa kuwa Msumbiji ni nchi huru inayoongozwa kidemokrasia,hivyo basi kama Dhlakama anataka kufa kama mjusi basi ajaribu kuingia tena msituni,ujue huyu jamaa hata kampeni alichelewa kuanza kwa kuogopa kutoka kule alikojificha(Gorongosa)kwa kuhofia kuwa mzee Guebz angemchinjilia mbali,mpaka pale mabalozi wa Italia na Ureno ndio waliokwenda kumtoa!
Kwa sasa Dhlakama hana jipya,matakwa yote ya chama chake cha Renamo yameshakubaliwa na kutambuliwa na serikali ya Frelimo na wanamgambo wote wa Renamo wamesamehewa kwa mauaji waliyoyafanya,kwahiyo labda atawapata machizi ndio watakaomuunga mkono.
Nalog off
 
RENAMO ni kama NCCR mageuzi ya Mrema ya those days ambapo alikuwa anasukumwa na wananchi lakini leo kwishney...

Kuna kaka amefanya PhD yake kuhusu political parties Msumbiji...nimemsikia mara kadhaa aki present kazi yake...

Yes hakuna level playing field lakini RENAMO wamesha poteza support ya wananchi...

Nadhani kwa Africa chama kikishindwa kuchukua nchi wakati kimeshaini...chance ya kuendelea ku shaini inaporomoka...

Na migogoro ndani ya vyama vingi vipya inafanya vyama vikongwe viendelee tuuuu...yani Afrika nchi nyingi kuna one party
dominance...

FRELIMO haijachukua supporters wa RENAMO, ime maintain ila RENAMO wamepoteza supporters...well sipendi siasa hivyo sina more details nilijikuta nakuwa forced kusikiliza presentations zote za huyu mkaka...kumpa shavu tu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…