JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 693
- 1,159
Maswali muhimu ni je, 'Reforms' zilizofanyika zinatosha?
Kwanini sauti ya pamoja ya Vyama haijasikika? Vyama vingine vinaona umuhimu wa 'reforms'? Je, Wananchi wanafahamu mabadiliko yaliyofanywa na kuyaridhia?
Kufahamu haya na mengine, jiunge nasi katika Mjadala, kupitia Xspaces ya JamiiForums, leo Mei 12, 2025 kuanzia Saa 12:00 jioni hadi 2:00 usiku.
Mwongoza Mjadala
- Masoud Kipanya
- Amani Golugwa - Naibu Katibu mkuu CHADEMA
- Issa Haji Gavu - Katibu wa oganaizesheni CCM
- Mohamed Ngulangwa - Mkurugenzi wa Habari CUF
- Deus Kibamba - Mchambuzi wa Siasa
- Janeth Rithe - Mwenyekiti wa Ngome ya Wanawake ACT Wazalendo
========================================
MAONI YA WACHANGIAJI WALIOPO KWENYE MJADALA
EUGENE KABENDERA (CHAUMMA)
"Kama Wananchi hawajakupa ridhaa ya kuongoza hata kama tukifanya Uchaguzi itakuwa tumefanya kujifurahisha tuTumeshuhudia wenzetu Kenya au Malawi wamekuwa na Uchaguzi wa Haki, Chama kilichopo Madarakani kinatolewa na kinakubali matokeo"
"Tunahitaji mabadiliko ya kweli ya Mifumo ya Uchaguzi, tunaweza kusogeza mbele Uchaguzi wakati huo tunajipanga. Hatutakiwi kurudi nyuma tulipotoka kwa Watu kuumizana"
"Kama Wananchi hawajakupa ridhaa ya kuongoza hata kama tukifanya Uchaguzi itakuwa tumefanya kujifurahisha tu"
"Tumeshuhudia wenzetu Kenya au Malawi wamekuwa na Uchaguzi wa Haki, Chama kilichopo Madarakani kinatolewa na kinakubali matokeo"
"Tunahitaji mabadiliko ya kweli ya Mifumo ya Uchaguzi, tunaweza kusogeza mbele Uchaguzi wakati huo tunajipanga. Hatutakiwi kurudi nyuma tulipotoka kwa Watu kuumizana"
YUKAPA (Mdau)
"Makamishna na Maafisa wa juu wengine wa Tume ya Uchaguzi wasichaguliwe na Rais, kuwepo na mchakato mwingine wa kuwapata ili kuondoa Mazingira ya upendeleo"
"Jeshi la Polisi halitakiwi kuhusishwa katika hatua kadhaa za ndani ya Uchaguzi ili kuondoa Mazingira ya kupendelea upande fulani, lakini pia Vyombo vya Habari virushe taarifa kwa usawa, zinavyofanya kwa Chama tawala zifanye pia kwa Vyama vingine"
"Kuhusu mchakato wa Uchaguzi, kwa sasa hivi Tume na Wananchi hatuzungumzi Lugha moja, huo ndio ukweli"
"Kuna wakati niliwahi kumshirikisha Baba yangu ambaye aliwahi kuwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya, akaniambia ‘Mwanangu acha acha’"
"Akasema kama nataka kujihusisha na Siasa, niende CCM lakini Vyama vingine Mazingira siyo rafiki"
"Vijana wengi ukiwauliza kwanini hawapigi kura au hawashiriki katika mchakato wa Uchaguzi watakwambia “Kwanini niende kupiga kura wakati mshindi anajulikana?" Hiyo ni hatari sana kwa Demokrasia"
"Makamishna na Maafisa wa juu wengine wa Tume ya Uchaguzi wasichaguliwe na Rais, kuwepo na mchakato mwingine wa kuwapata ili kuondoa Mazingira ya upendeleo"
"Jeshi la Polisi halitakiwi kuhusishwa katika hatua kadhaa za ndani ya Uchaguzi ili kuondoa Mazingira ya kupendelea upande fulani, lakini pia Vyombo vya Habari virushe taarifa kwa usawa, zinavyofanya kwa Chama tawala zifanye pia kwa Vyama vingine"
TRAVELLER VOMAN (Mdau)
"Kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025, tunaona Watu ambao wanaenda kusimamia Uchaguzi huo wengi wao ni wale ambao ni Wateule wa Kiongozi wa Nchi"
"Tume Huru ya Uchaguzi inajiita ipo huru lakini Vyama na Wananchi hawaoni huo uhuru wenyewe, hali hiyo inakera na inaweza kufanya Mtu au Watu waone hawapo sehemu sahihi"
"Tuna ulazima wa kufanya mabadiliko ya kweli, Nchi yetu ina wasomi wengi ambao wanaweza kushiriki katika kuiwezesha Nchi kuzungumza Lugha moja"
MICHAEL ENOCK (Mdau)
"Uchaguzi Mkuu wa 2010 na 2015 kuna Vyama vya Upinzani vilifanikiwa kuingia kwa wingi Bungeni, tunatakiwa kujiuliza kwa hali hiyo tatizo ni Kanuni au Vyama?"
"Naona ni ngumu 'Reforms' (Mabadiliko) kufanyika kwa muda huu, kwani kipindi kile Wapinzani wanapata nafasi nyingi Bungeni ilikuwaje? Kwanini tusijiulize kama wakati ule waliweza kwanini wakati huu hawawezi"
"Tunaweza kusubiri Mwakani kwa ajili ya mabadiliko yanayozungumzwa, Nchi haiongozwi na Watu wachache, hatutengenezi 'Reforms' (Mabadiliko) kwa kuangalia Vyama vya Upinzani au Chama Tawala, tunafanya hivyo kwa ajili ya Watanzania wote"
"Sipingi 'Reforms' za Uchaguzi kufanyika ndani ya Miezi minne lakini hii Nchi ni kubwa sana, tunaenda kugusa vitu vya muhimu sana, haiwezekani tukakurupuka na kufanya maamuzi kwa faida ya Watu wachache, Mabadiliko yanahitaji muda"
BELVA 0.0 (Mdau)
"Nilikuwa naangalia Barabara fulani imeharibika Mitaa ya Mwenge (Dar), nikamuuliza Mkazi wa pale kama anamfahamu Diwani wake, akasema hamjui. Hiyo ilionesha kuna Watu wanaingia Madarakani kwa nguvu ya ushawishi wa Watu au nguvu fulani ambayo siyo ya Wananchi"
"Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Mwaka 2024 umeonesha jinsi ambavyo mambo hayakuwa ‘fair’, hali hiyo ni kama imewakatisha tamaa Wananchi kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 kwa kuamini yatakuwa yaleyale. Kwa sasa hali ilivyo, Mpiga Kura una Haki ya kupiga Kura lakini hauna Haki ya kumchagua Kiongozi unayemtaka"
"Kuna namna nyingi za kufanya mgomo, mfano mimi sitapiga Kura katika Uchaguzi wa 2025, ikiwa kuna wengi kama mimi ambao hawatapiga kura, Viongozi watakaochaguliwa wataona wazi wameshinda nafasi lakini wao sio chaguo la Wananchi"
MALIMA TOGA (Mdau)
"Kuna kitu tunaona ni kidogo lakini ni kikubwa, Watanzania tunatakiwa kuelewa kuhusu umuhimu wa Uchaguzi, Haki ya kushiriki Uchaguzi, tukitambua hayo tutatambua Kiongozi bora ni yupi"
STEPHEN (Mdau)
"Tanzania ni Nchi huru, tuna nafasi ya kufanya maamuzi tunayotaka, kusema Mabadiliko yote ya Uchaguzi yafanyike kwa wakati mmoja hicho kitu hakiwezekani"
JOVINE AMBROSET (Mdau)
"Serikali isikilize maoni ya Wananchi hata kama itatokea Uchaguzi unatakiwa kupelekwa mbele, kwani hatuwezi kuingia katika Uchaguzi huku kukiwa na malalamiko mengi"
TUWA (Mdau)
"Inavyoonekana Mtaani Wananchi hawaelewi Mabadiliko ambayo Serikali imesema imeyafanya, kama wamefanya basi wamekusanyika wao na kusema tumefanya hiki na hiki ambacho Wananchi hawakioni"
"Ilivyo sasa Mpiga Kura anaenda kupiga Kura lakini anakuwa na mashaka kuwa Kura yake itakuwa na mabadiliko yoyote katika Uchaguzi? Hiyo inasababisha Wananchi tutamani kuona Kura inakuwa na thamani kama inavyotakiwa"
'Reforms' zinazosemwa zimefanyika hazigusi Wananchi moja kwa moja, zinawagusa wale wenye maslahi nazo"
DR. KING (Mdau)
"Tume Huru ya Uchaguzi haipo huru kwa kuwa naona ina uhusiano na Vyama au chama ambacho ni wazi ni jambo gumu Mtu kukandamiza kwake, kuna Watu ambao wao Tume ni kama nyumbani kwao"
"Changamoto hiyo inawaumiza wengine na upande mwingine inawafurahisha"
CAEJAY (Mdau)
"Moja ya athari za mifumo ya Uchaguzi ni kuona Bunge linavyoendeshwa, limekuwa likijadili mambo ya Kisiasa na hakuna nguvu ya Wananchi"
"Ujio wa uhitaji mabadiliko ya Mifumo ya Uchaguzi unawafungua Wananchi kuwa kile walichokuwa wakikifanya wakati wa Uchaguzi kwa kupanga foleni ni kama maigizo"
"Wagombea fulani katika Uchaguzi wanaweza kushinda kwa huruma ya Walioshika madaraka na sio kwa Kura halali zilizopigwa, mifumo iliyopo inaweza kuwapa nafasi wale wenye madaraka waamue “tumpe huyu ushindi na huyu tusimpe"
SHIIJ.M (Mdau)
"Nilishiriki katika Uchaguzi wa 2020 nilipata nafasi ya kukutana na Wadau ambao walinielezea jinsi wizi wa Kura unavyofanyika, nimeshuhudia mwenyewe na sio kwa kusimuliwa"
"Nilishiriki katika Uchaguzi wa 2024 kulikuwa na mazingira ambayo yalionekana kukibeba chama kimoja kutoka kwa Wakala niliyemkuta katika Kituo nilichoenda"
"Kama hakutakuwa na mabadiliko ya mifumo ya Uchaguzi inavyoonekana Mwaka 2025 tunaweza kuwa na Uchaguzi wa ovyo zaidi"