Reform Part 1;Kwa nini tunahitaji mabadiliko kwenye katiba ya Nchi na katiba ya Chama

Reform Part 1;Kwa nini tunahitaji mabadiliko kwenye katiba ya Nchi na katiba ya Chama

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2021
Posts
1,250
Reaction score
3,451
Salaam kwako Tundu Lissu uko Gerezani ulipo,Sera yako au yenu Chadema imenifanya nirudie kusoma Mwalimu Julius Nyerere Epilogue of his collective work inayojulikana kama Uhuru na Umoja ili kuweza kujua ama kupata sababu ya Chadema kuja na fikra ya mabadiliko kwenye katiba ama Reformation kwenye nyanja mbalimbali katika maisha ya Mtanzania na nimeona Mwalimu Julius Nyerere akizungumzia reform kwa ukubwa zaidi akitupitisha kwenye fikra tatu,principle of change which was threefold in nature.

a. Africa(Tanzania) must change
b. The change has to be positive
c. Africans(Tanzanians) have to initiate and steer that change.

Mwalimu Julius Nyerere akizungumzia Afrika(Tanzania) kwa upana na wazungu wanasema charity begins at home hivyo basi kwenye Afrika weka Tanzania na kwenye Africans weka Tanzanians,kumbuka haya maandishi yalikuwa ni ya mwaka 1966,hivyo fikra ni za mabadiliko na nitazizungumzia kwa wakati wa sasa,fikra hizi za Mwalimu zinaweza kutuonesha ni kwa namna gani inatupasa kubadili katiba ya chama na nchi kutokana na mazingira tuliyomo,nitaeleza na mifano kadhaa kutoka Marekani ambayo ndiye baba wa Demokrasia.

Katika Makala hii tutaishi kwenye nadharia hizi za Mwalimu,Africa must change her institutions to make feasible her new aspirations; her people must change their attitudes and practices to accord with the objectives. And these changes must be positive, they must be initiated and shaped by Africa and not simply be a reaction to events which affect Africa,Niwarudishe nyuma miaka ya 1970's,1980's hadi 1990's siku ambazo hatukuweza kusoma gazeti lingine zaidi ya Uhuru,Mzalendo,Daily News na Sunday News baadae kuja gazeti la Mfanyakazi kuja kuleta faraja,Niwakumbushe nyakati ambapo 8:00 PM RTD taarifa ya habari kutoka Redio Tanzania,Dar es Salaam na ilisikilizwa na kila mmoja wetu kufuatiwa na "Ujumbe wa Leo" Nikukumbushe enzi za mabasi ya Kamata,Relwe,Moretco na kadhalika,toka enzi hizo hadi leo bado tuna fikra zile zile ilihali zama zimebadilika,tunatakiwa kubadilika kiakili,kimtazamo,kimatendo na kimaneno,Katiba ya Chama na Nchi inatakiwa iendane na mabadiliko hayo,rejea Mwalimu Julius Nyerere Uhuru na Umoja, a recurring practical theme. It is the theme of change. For Africa must change; change from an area where people (take?) out an existence and adapt themselves to their environment, to a continent which challenges the environment and adapts it to man's need.

Africa must change her institutions to make feasible her new aspirations; her people must change their attitudes and practices to accord with the objectives. And these changes must be positive, they must be initiated and shaped by Africa and not simply be a reaction to events which affect Africa,kwenye Afrika weka Tanzania.Je fikra hizo za Mwalimu kuhusu haja ya Africa na Tanzania kubadilika zimepitwa na wakati na tusiziangalie tena. Je hoja yake kuhusu haja ya Afrika and hence Tanzania kubadilika ina makosa gani?

Nionavyo mimi fikra za Mwalimu kuhusu kubadilika kwa Tanzania bado zina nguvu kubwa.Kwakweli Watanzania tukitaka maendeleo ya kweli tunahitaji kubadilika,tubadilike na tuachane na ubinafsi,huu ndiyo ugonjwa unaotumaliza waafrika(watanzania),tuiache ile dhana ya kudhani kuwa uongozi ni ulaji wako wewe na mkeo,wanao na jamaa wengine wa karibu,Mali ya Umma ni kufuja tu kwani una hasara nayo gani.Ubinafsi ndiyo ugonjwa wetu mkubwa sisi Watanzania.Ubinafsi ndiyo umetufanya tuwe waroho wa madaraka,tuwe wadhulumaji,tuwe na chuki sisi kwa sisi na hivyo tuuane hovyohovyo,tuwe mafisadi,tuwe wazembe katika majukumu mbalimbali tuliyokabidhiwa etc etc hivyo kutufanya tuendelee kuwa masikini wa kutupwa mpaka leo hii pamoja na rasilimali zote tulizojaaliwa na mwenyezi Mungu,Kwa leo Watanzania wenzangu wito wangu ni huo,katika nafasi yoyote ile uliyonayo,shughuli yoyote unayojishughulisha nayo tafadhali achana na ubinafsi kuanzia sasa,jitoe haswa kwa faida ya jamii yetu yote ya Tanzania na siyo kwa faida ya mkeo,wazazi,watoto na jamaa peke yao,Pumzikeni kwa Amani Hayati Edward Moringe Sokoine,Pumzika kwa Amani Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere,Pumzika kwa Amani Hayati Rais John Pombe Joseph Magufuli.

-Kwa nini tunahitaji badiliko kwenye katiba ya Chama na Nchi.

Tanzania haiwezi kubadilika just for the sake of kubadilika bila muongozo maalum ambao ni katiba ya Chama na Katiba ya Nchi,na hili litawezeshwa kutoka kwa viongozi wake au kutoka kwa wananchi wake,sasa kama haya maneno ya Mwalimu ni ya kweli, basi Tanzania ilitakiwa kuwapa wananchi wake nafasi ya kuweka mandate kwa viongozi wake of exactly what kind of change wanataka, that has not been the case so far,

Iwapo kuna kiongozi anataka kuleta mabadiliko lazima aweke muongozo unaokubalika kwa maana ya kufanya badiliko kwenye Katiba,na ni lazima kiongozi huyo awaulize wananchi wanataka nini,lakini maneno matupu ya change tu au kwa amri ya Rais tu kitu fulani kifanyike na kisiwekwe kwenye katiba hayawezi kutusadia kitu,Hayati Rais Magufuli alifanya sana kusaidia wanyonge na walioonewa na kuweka mashinikizo ya uwajibikaji kwenye Mashirika ya Umma lakini alipokufa hata vyeti feki waliomba kurudi tena kazini kwa sababu Rais Magufuli hayupo tena,Mao, George Washington, na wengineo hawapo tena, lakini tizama system zao zinaendelea kuongoza nchi zao imara zaidi kupitia katiba imara waliyoiweka na mabadiliko yaliyofanyika kuelekea ubora zaidi kwa manufaa ya Mataifa yao,hii inatufundisha kwamba binadamu ana tabia ya kuwa-comfortable mahali alipo,sasa kumbadili ni lazima utumie sheria, au siasa,lakini change! change! change! itasaidia nini,kama tunataka kuondoa ubinafsi dawa ni kuruhusu utawala wa sheria uchuke mkondo,lakini hatuwezi kutegemea waa-Watanzania kubadilika ghafla na kuacha ubinafsi.

Mawazo ya Mwalimu Julius Nyerere yanatupa mwanga mkubwa sana katika kila hatua tunayopiga kama Taifa la Tanzania lakini a change of what na under what conditions au under who's expense? Pumzika kwa Amani Le Mutuz ulichampion jambo hili kwa ukubwa sana miaka ya 2008 kwenye Jamii Forum,Heshima mbele Mkuu.

Kwenye Maandishi ya kitabu cha Uhuru na Umoja,Mwalimu Julius Nyerere alisema vizuri kiprophetically ( I use the term rather liberally) kuwa Bara letu kwenye bara tuweke nchi yetu lazima ibadili mtazamo na vitendo vyake.Ukiangalia hili ndilo ambalo wengi tunalijadili hasa tunapoangalia mapungufu ya Viongozi wetu n.k tunasema tunataka tubadilike,tunasema tubadili attitudes zetu na matendo yetu,ili tufikie malengo (objectives) ya kujenga taifa la kisasa na la watu wenye kufurahia Taifa lao,Tunasema tunataka tubadilike.Tunapozungumzia kuzingatia misingi ya utawala wa sheria, kuwa na maadili n.k tunachosema ni kuwa vitu hivyo havipo sasa na tunataka tubadilike.Hivyo tunakubaliana na Mwalimu kuwa we need to change our "attitudes and practices to accord with the objectives." Kuna ubaya gani katika ukweli huu mwingine kuwa kama kweli tunataka kufikia malengo yetu hatuna budi kubadilika? Hakuna Kiongozi Mkuu aliyeonesha hadi hivi sasa ndiyo maana tunaona watu kama Tundu Lissu akishika hatamu na watu watamuelewa kwa sababu ni takwa la nyakati,na suluhisho ni kukaa nae mezani na ikiwezekana kufanya hayo mabadiliko ya katiba ya nchi na tume ya uchaguzi.

Kwenye Maandishi ya Uhuru na Umoja,Mwalimu hapa anaonesha wazi kuwa Afrika inaweza kuchagua watu wengine waamue mabadiliko ndani yake au yenyewe ibadilike yenyewe,kwenye Afrika weka Tanzania kwamba Watanzania wenyewe waamue hatma ya maisha yao na kiasi cha mabadiliko wayatakayo,Leo hii tunapozungumzia mabadiliko wengi tutachukia na kukasirishwa wakija wazungu na kutuambia tufanye hivi au vile kwa vile wanaamini hivyo ni vitu vizuri kwetu.

Wengi tutaona tumetukanwa na kudharauliwa kama Wamarekani wakija na kusema "badilisheni Katiba yenu", fanyeni hivi au vile,tawezekana wakawa wanasema kweli lakini yawezekana wengi tungependa kuona kuwa ni sisi wenyewe tunaamua nini tunachotaka,Sasa kwa Mwalimu kusema "Afrika(Tanzania) must initiate and shape" these changes kuna makosa gani hapo? Je tunataka wengine watubadilishe katiba na sisi tuwe wajibuo yale yafanywayo na wengine? Naamini hakuna aliyeonesha ubaya wa wazo hilo.

Nimalizie part hii lakini si mwisho fikra kutoka kwenye maandishi ya Uhuru na Umoja aliyoandika Hayati Baba wa Taifa,Mwalimu Julius Nyerere,Ni kweli tunaweza kukaa na kusubiri mabadiliko yatokee, au tunaweza kushiriki katika mabadiliko hayo.Hayati Mugabe alishindwa kubadilika na alibadilishwa na nguvu zilizo nje ya uwezo wake.

Mwalimu Julius Nyerere aliona mbali na aliona kuwa kuna mabadiliko yanakuja mbele yake inevitable change maana vijana wa mwaka 1950's 1960's si wale vijana wa 1980's na mazingira ya 1950's 1960's si yale ya 1980's hivyo basi Mwalimu Nyerere akaamua kuyawahi,kwa jinsi nilivyomjua Intellectual Mwalimu Julius Nyerere asingeweza kuendelea kukaa madarakani kwa sababu intellectually he could see the upcoming change and he could not stop it.Ndio maana akaamua kukaa pembeni na kujaribu kuyaelekeza yaende vizuri,Leo hii tunazungumzia hali ya kisiasa nchini bila kukiri kuwa uamuzi wa Mwalimu kung'atuka ulikuwa ni uamuzi wa kijasiri sana na ulisaidia sana kulipeleka Taifa letu kwenye mabadiliko badala ya kusubiri nguvu za nje kutubadilisha kama yaliyomkuta Hayati Rais Kibaki wa Kenya.

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.

-Bachelor of business administration in international business

-Master of Leadership and Management.

Recent Publications;-
-Assessment on the effects of microfinancing on Poverty reduction.
 
CCM na hasa Samia hawakuelewi kabisa mleta mada.
 
REFORM PART 2:KWA NINI TUNAHITAJI MABADILIKO KWENYE KATIBA YA NCHI NA KATIBA YA CCM.

Leo 15:10hrs 27/04/2025

Waswahili ndio waliosema kuwa "kwanini tuandikie mate wakati wino upo" na ndio hao hao waliosema "kwanini tugonganishe mawe, wakati kibiriti kipo" (well that is my own saying ama Wahenga Saying). Ni wakati sahihi sasa wa kutumia Fikra za Mwalimu Julius Nyerere tukiziangalia upya zitatuonesha mwanga wa wapi tunataka kwenda. Mara nyingi hata hivyo kuna watu ambao wanapinga fikra hizo (hata kama hawazijui) na kutoa madai lukuki juu ya "Mwalimu alisema nini".

When the TANU National Executive Committee met in Arusha January 26-29 1967 it turned out to be a stormy session. At this meeting Nyerere proposed that Ujamaa become the official policy of the government.This made Hayati Nyerere,Kambona na Kawawa to go into private session,The result was that the Arusha Declaration was adopted,Nimewakumbusha jambo hili ili kupata picha ya takwa la wakati husika,kwa wakati huo ilihitajika sana nchi iendeshwe kijamaa ili kuepusha mabeberu yaliyotaka kutuletea matabaka ya matajiri na wanyonge na kuujenga ubepari kati ya Watanzania,pili nimeongelea TANU kama chanzo cha badiliko la sera na katiba,hivyo basi badiliko la katiba ya Chama na katiba ya Nchi yote yanahitaji takwa la nyakati husika ili kuepusha Ufisadi,na kuongeza uwajibukaji kwa Mali ya Umma,tukumbuke tupo zama za AI,kizazi hiki cha AI ni tofauti na kizazi cha 1970's kwa hiyo takwa la kurekebisha katiba ni lazima ili kuepusha kuivunja katiba kwa kisingizio cha AI.

Suala la katiba iliyobora ni la Msingi sana kwa maana nchi itajiendesha hata Rais akiwa darasa la pili,Mfumo hauwezi kumletea kila mwananchi faida, lakini angalau unampa kila mwananchi nafasi ya kujaribu, badala ya viongozi tu na watoto wao, na wafanya biashara za viongozi hao hao wanaolilia ujamaa, huku wakituchezea wananchi,Sasa hivi China awarudii maneno ya Mao,ila wanatekeleza pamaoja na modifications nyingi walizoziweka on it,kumbuka Ping, alikuwa ni mfuasi wa karibu wa Mao, Chuo-en lai, kina Hua-guofeng, wale walikuwa wafuasi wa karibu na Mao, na wote walikuwa wtu makini wenye mawazo very independent, na hata ukisoma vitabu vya China, utaona kuwa hawakusita hata siku moja kumwambia ukweli Mao, the matter of fact kuna wakati hata walimpunguzia madaraka, walipooona anaanza kukosa muelekeo!

fikra nzuri ziko huru na vitendo vya mtu au watu wengine. Mtu akisema "ukijumlisha mbili na mbili unapata nne" siyo tu anatoa wazo lakini ana articulate ukweli fulani. Lakini mtu huyo huyo akiamua kwenda pembeni na kumdanganya mtu kuwa mbili na mbili ni sita, kitendo chake hicho ni kiovu lakini ukweli alioutoa unasimama wenyewe.Kuna fikra ambazo inachukua muda kupata mtekelezaji na kuna fikra ambazo hata mtu mwenyewe aliyezitoa anashindwa kuzitekeleza. Lakini huu ni ukweli wa wanafalsafa wengi siyo wafalme. Aristotle , Plato, Thomas Aquinas na wengine wametoa mchango mkubwa sana katika uelewa wetu wa maadili, utawala na uchumi, lakini mawazo yao yalibakia vitabuni hadi pale walipopatikana watu walioamua kuyafanyia kazi kweli.

Tuangalie fikra katika substance yake. Mawazo hutangulia vitendo, lakini fikra hutangulia vitendo vikuu. Sasa, tuangalie hizo fikra tuone ubaya wake kwamba tuzibadilishe inapobidi ili kupata badiliko bora,fikra ni independent of time,zipo fikra nyingi nzuri kwa maslahi ya taifa,(mf. kutoa elimu bure,matibabu,ujamaa,kutenganisha siasa/uongozi na biashara,njia za uchumi kuwa chini ya serikali,etc) falsafa binafsi ya Nyerere ambayo ni kutopenda maisha ya juu na/au kufaidika kupitia mali ya umma,(rejea Mkapa na mtaji wa masikini au Sumaye:Ukitaka mfanyabiashara mambo yako yakinyookee),Ubaya wa watu binafsi kumiliki njia kuu za Uchumi, fikra bora zitalindwa na katiba bora,Mao, George Washington, na wengineo hawapo tena, lakini tizama system zao zinaendelea kulinda nchi dhidi ya viongozi wote wabaya.

Mwalimu alizungumzia "the extension of all African citizens of the requirements of human dignity" na anasema wazi kuwa mapinduzi ama (mabadiliko hayo) yana lengo moja nalo ni "the extension of all African citizens of the requirements of human dignity". Je, haikuwa lengo la uhuru na utaifa wetu kuwa na sisi tuwe na utu na heshima kama ya wanadamu wengine? Je halikuwa lengo na limebakia lengo kuwa tuweze kujichagulia viongozi wetu na kuamua hatima ya maisha yetu? Sasa kuna ubaya gani kwa Mwalimu kusema kuwa mabadiliko haya lazima yatupeleke kwenye lengo moja nalo ni "extension of all Africans citizens of the requirements of human dignity"? ambalo lilikuwa ni takwa la wakati ule!? Hakuna aliyeonesha wapi Mwalimu amekosea kwenye hilo. Hakuna.

-Mwalimu hakuahidi luninga kwa kila mtu, hakuahidi maisha Rais, hakuahidi "maisha bora kwa kila Mtanzania" na wala hakuahidi kuwa njia ya kufikia maendeleo na mafanikio itakuwa ni nyepesi na isiyohitaji watu kuhangaika. Mwalimu hakuwa mtu wa kufikirika kuwa maneno matamu basi ndiyo huliwa. Alitambua kuwa kujenga Taifa siyo lele mama; Angeweza kutoa ahadi ya "maziwa na asali" kwenye hiyo nchi ya ahadi. Hakufanya hivyo. Alituambia mapema kabisa kuwa "the task is a big and complicated one".

-Fikra ya "the task before is big and complicated one"?. Hakuna mtu aliyeonesha kuwa "the task should be small one and uncomplicated one".

Mwalimu Julius Nyerere aliweza kuona matokeo ya maamuzi yake na kwa mbali anaweza kuyaona katika fikra na kufanya mabadiliko,Mwalimu aliona ugumu wa maamuzi mengine na alituambia mapema kabisa kuwa yawezekana katika kujenga hili Taifa tutakutana na maamuzi ambayo yana "involve the clashes of principle". Huu ni ukweli. Leo hii tunashindwa kuchagua nini cha kufanya kwa sababu tumepoteza principles zenyewe na hatuna cha kushilikia au pa kuanzia. Kuna makosa gani katika kutambua kuwa katika kufanya maamuzi huko mbeleni tunaweza "kugonganisha kanuni" mbalimbali na maslahi mbalimbali? Hakuna aliyeonesha ubaya wa kauli hiyo ya Mwalimu,Hivyo takwa la mabadiliko linahitajika kwa kila nyakati.

Ametoa mfano ambao kwa wengine naona umewapita kwa haraka. Katika kujenga Taifa na unakutana na migongano ya principle hauna budi kuchagua. Nitatoa mfano. Baada ya matukio ya Septemba 11 Marekani ilijikuta inagonganisha principles mbili ambazo zimelijenga Taifa hilo; Usalama wa nchi na Uhuru wa kila mtu (security and individual liberties). Sasa walipokuwa wanajaribu kuja na sheria ambayo ingeweza kuwasaidia baadaye (positive change) wakajikuta na jukumu "big and complicated one".

Matokeo yake ni kupitishwa kwa sheria ya "Patriotic Act" ambayo ilikuwa inajaribu kutafuta uwiano wa mambo haya mawili katika kujaribu kuja na sheria nzuri. Hadi leo hii karibu miaka nane baadaye bado wanahangaika kutafuta "balance" ya clashing principles.

Sasa, kuna makosa gani katika kauli ya Mwalimu kuwa tunaweza kujikuta tunagonganisha principles? Hakuna mtu aliyeonesha mapungufu ya kauli hiyo ya Mwalimu zaidi ya watu kuleta hadithi na stori za maisha yao. (If you have noticed I have not interjected my own experiences.. nimezaliwa, nimesoma, na kukulia katika Tanzania hiyo hiyo ya Mwalimu.. lakini sijengi hoja kupitia mwanga wa hisia, kumbukumbu na vionjo vyangu; najenga hoja kwa kutumia intellectual argument).

Muda wa mabadiliko unapofika na "jinsi ilivyo" lazima tubadilike na ilibidi tubadilike. Lakini ni sisi wenye kusimamia mabadiliko hayo,Wakati mwingine mabadiliko yataudhi watu wachache au kusababisha usumbufu lakini kutofanya mabadiliko kwa kuogopa usumbufu ni woga.

Leo, US na nchi nyingi bado zinafanya mabadiliko na watu wanasumbuka kidogo lakini wanajifunza kuishi nayo. Kuna mabadiliko kadhaa ya sheria mbalimbali n.k na watu wanatakiwa kuadjust. Sisi tunaogopa kubadilika kwa sababu tuko kwenye comfort zones zetu,lakini utaona kuwa watu hapa wanataka mabadiliko katika Tanzania lakini hawatuambii ni usufumbufu na shida gani zinaweza kutokea kwa wananchi tukileta mabadiliko? Tukitunga sheria ambazo zitasababisha usumbufu kwa watu je tuzipitishe?

Kwa mfano, tukipitisha sheria inayosema kuanzia sasa hadi ndani ya miaka kumi ijayo, nyumba zote za Tanzania ni lazima ziwe aidha za matofali ya kuchoma au ya sementi na ziwe zimeezekwa mabadi au vigae. Lengo likiwa ni hatimaye kuondokana na nyumba za udongo na makuti na mitete! Je sheria kama hiyo ni nzuri au kwa vile itasababisha usumbufu basi tusifanye hivyo?

Vipi tukisema kuwa Jiji la Dar linahitaji mifereji mipya ya kupitisha maji yatuwamayo na kuyapeleka baharini. Katika kufanya hivyo kuna majengo na nyumba ambazo itabidi zivunjwa ili kulitengeneza jiji la kisasa; je tufanye hivyo licha ya usumbufu kwa wakati na wananchi wa Dar. Wanaoogopa usumbufu watasema "hapana" tusiwasumbue watu. Lakini leo hii hata Marekani wanafanya mambo hayo tena kwa sababu za kiuwekezaji kupitia sheria kama za "eminent domain" ambazo hata Tanzania tunazo na zimewekwa kwenye mikataba ikiwemo ya migodini

-Views zetu zinatakiwa zibadilike due to circumstances where/when needed.

Mwalimu aliongea kwa falsafa kubwa sana na kuigeuza kuwa vitendo,akina Lee Kuan Yewe wa Singapore walikuwa na falsafa kama za Nyerere nao walikwenda hatua 100 zaidi mbele kwa kugeuza Hotuba zao za majukwaani kuwa Shughuli halisi za uchumi,kama kuna mtu anataka kudumisha Fikra za Mwalimu Nyerere asituletee hotuba atupe mkakati kamili wa kiuchumi unao tafsiri Fikra hizo,kunukuu na kupamba maua maneno ya mwalimu na kujidai kuenzi fikra za Mwalimu Nyerere bila kutoa maana halisi ya kiuchumi inayoweza fanyiwa kazi na wananchi walio wengini upuuzi na ni mambo yaliyo pitwa na wakati,tunataka Tafsiri halisi ya Fikra hizo katika nyanja zote za Maendeleo na uchumi wa nchi.

-"We prefer to participate in the shaping of our own destiny, and we believe that we have the resolution and the ability to overcome difficulties and build the kind of society we want." J. Nyerere

China wana kitu kimoja muhimu sana alichokiweka Mao, nacho ni heshima kwa sheria, pamoja na mengine yote mazuri yao, cha muhimu kuliko yote wanaheshimu sheria, kiongozi akiiba ni risasi mbele ya umma, that helps a lot kwenye utekelezaji wa sera, badala sisi umeharibu hapa kwenye uwaziri unaenda kuwa balozi nje, sasa unashangaa kwa nini tuko hapa au ujamaa umeshindwa? Enzi zile watoto wote wa wananchi ni kusoma bongo tu, isipokuwa watoto wa viongozi kusoma nje, sasa unashangaa kwa nini sasa wanakuwa viongozi wetu kama baba zao?

Nimalizie kwa kusema,Mwalimu alisema mabadiliko hayana budi yawe mazuri,kwa maana kubadilika kuelekea ubaya si mabadiliko tunayoyataka,alichosema na ambacho kinashuhudiwa na wachangiaji wengi hapa ni kuwa tubadilike kuelekea upande chanya. Tunapoangalia historia yetu na kuona mapungufu ya viongozi waliotutangulia tunaona ipo haja ya kubadilika. Kubadilika huko siyo kurudia kanuni, na mifumo ambayo imeonekana imefeli au ilikuwa na kasoro kubwa lakini ni kubadilika kufuatia kitu kilichobora zaidi.

Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of business administration in international business

-Master of Leadership and Management

Recent Publications;-
-Assessment on the effects of microfinancing on Poverty reduction.
 
Back
Top Bottom